Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kazi-ya-Ukombozi. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kazi-ya-Ukombozi. Onyesha machapisho yote

7/19/2019

Maonyesho ya Mungu | "Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi"



Maonyesho ya Mungu | "Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi"


Mwenyezi Mungu anasema, "Katika Enzi ya Neema mwanadamu alikuwa amepotoshwa na Shetani, na hivyo kazi ya ukombozi wa wanadamu wote ulihitaji wingi wa neema, ustahimili usio na mwisho na uvumilivu, na hata zaidi, sadaka ya kutosha kulipia dhambi za wanadamu, ili kufikia athari yake. Kile wanadamu waliona katika Enzi ya Neema kilikuwa tu sadaka Yangu ya dhambi ya binadamu, Yesu. Na walijua kwamba ni Mungu tu ndiye Anaweza kuwa mwenye huruma na uvumilivu, na waliona tu huruma wa Yesu na fadhili Zake. Hii ni kwa sababu wao waliishi katika Enzi ya Neema. Hivyo kabla ya kukombolewa, walilazimika kufurahia neema nyingi ambayo Yesu aliwapa;

7/17/2019

Kuna tofauti ipi kati ya jinsi ambavyo Bwana Yesu alifanya kazi katika Enzi ya Neema na jinsi Mwenyezi Mungu anavyofanya katika Enzi ya Ufalme?

V. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Tofauti Kati ya Kazi ya Mungu ya Hukumu Katika Siku za Mwisho na Kazi Yake ya Ukombozi Katika Enzi ya Neema

2. Kuna tofauti ipi kati ya jinsi ambavyo Bwana Yesu alifanya kazi katika Enzi ya Neema na jinsi Mwenyezi Mungu anavyofanya katika Enzi ya Ufalme?

Maneno Husika ya Mungu:


        Wakati wa kupata mwili Kwake mara ya kwanza, ilikuwa muhimu kwa Mungu kuponya wagonjwa na kufukuza mapepo kwa sababu kazi Yake ilikuwa ni kukomboa. Ili kulikomboa kabila lote la mwanadamu, Alipaswa kuwa mwenye upendo na mwenye kusamehe. Kazi Aliyoifanya kabla ya kusulubiwa ilikuwa kuponya watu na kufukuza mapepo, ambayo iliashiria wokovu Wake wa mwanadamu kutoka katika dhambi na uchafu.

7/10/2018

Nia ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Sura ya 3 Ukweli Kuhusu Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

2. Nia ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Maneno Husika ya Mungu:
Mpango Wangu mzima wa usimamizi, mpango ambao una urefu wa miaka elfu sita, unashirikisha hatua tatu, au enzi tatu: Enzi ya Sheria mwanzoni; Enzi ya Neema (ambayo pia ni Enzi ya Ukombozi); na katika siku za mwisho, Enzi ya Ufalme. Kazi Yangu katika enzi hizi tatu hutofautiana katika maudhui kulingana na asili ya kila enzi, lakini katika kila hatua huambatana na mahitaji ya mwanadamu—au, kwa usahihi zaidi, inafanywa kulingana na ujanja ambao Shetani hutumia katika vita Vyangu dhidi yake. Madhumuni ya Kazi Yangu ni kumshinda Shetani, ili kudhihirisha hekima Yangu na kudura, kufichua ujanja wote wa Shetani na hivyo kuokoa wanadamu wote, wanaoishi chini ya miliki yake.

1/16/2018

Je, Mwenyezi Mungu na Bwana Yesu ni Mungu Mmoja?

Je, Mwenyezi Mungu na Bwana Yesu ni Mungu Mmoja?

Wanadamu walipopotoshwa na Shetani, Mungu alianza mpango Wake wa usimamizi kwa ajili ya wokovu wa wanadamu. Mungu ametekeleza hatua tatu za kazi kwa ajili ya wokovu wa wanadamu. Wakati wa Enzi ya Sheria, Yehova Mungu alitoa sheria na kuyaongoza maisha ya wanadamu, Akiwafanya watu kujua kwamba wanapaswa kumwabudu Mungu, na kuwafanya wajue dhambi ni nini. Lakini kutokana na ujio wa hatua za mwisho za Enzi ya Sheria, upotovu wa wanadamu ukawa hata wa kina zaidi, na watu mara nyingi walikiuka sheria na kutenda dhambi dhidi ya Yehova.

12/09/2017

Kiini cha Mwili Ulio na Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Matamshi ya Mwenyezi Mungu
kumfuata Mungu,sauti ya Mung
Mwenyezi Mungu alisema, Mungu mwenye mwili wa kwanza Aliishi duniani kwa miaka thelathini na tatu na nusu, lakini Alitekeleza huduma Yake kwa miaka mitatu na nusu pekee ya hiyo miaka yote. Kipindi Alichofanya kazi na kabla Aanze kazi Yake, Alikuwa na ubinadamu wa kawaida. Aliishi na ubinadamu Wake wa kawaida kwa miaka thelathini na tatu na nusu. Katika miaka yote mitatu na nusu ya mwisho Alijifichua kuwa Mungu mwenye mwili. Kabla Aanze kutekeleza kazi ya huduma Yake, Alikuwa na ubinadamu wa kawaida, bila kuonyesha ishara ya uungu Wake, na ni baada tu ya kuanza rasmi kutekeleza huduma Yake ndipo uungu Wake uliwekwa wazi. Maisha na kazi Zake katika ile miaka ishirini na tisa yote ilidhihirisha kuwa Alikuwa mwanadamu halisi, mwana wa Adamu, mwili;