Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Maombi. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Maombi. Onyesha machapisho yote

6/09/2019

Have You Been Rapturned? | "Kutamani Sana" | Swahili Christian Movie


         Miaka elfu mbili iliyopita, Bwana Yesu aliwaahidi wafuasi Wake: "Naenda kuwatayarishia mahali. Na nikienda kuwatayarishia mahali, nitarudi tena na kuwapokea kwangu; ili mahali nipo, muweze kuwa pia" (Yohana 14:2-3). Kwa sababu ya hili, vizazi vya waumini vimeendelea kujawa na tumaini na kushikilia maombi kwa ajili ya kutimizwa kwa ahadi ya Bwana, na kutumaini na kuomba kwamba wanyakuliwe hadi kwenye mbingu ili kukutana na Bwana na kuingia katika ufalme wa mbinguni wakati Bwana atakapokuja. Huu pia unamfafanua mhusika mkuu wa filamu, Chen Xiangguang. Ni mtafutaji mwenye shauku kubwa, anaieneza injili, na kumshuhudia Bwana ili kukaribisha kurudi kwa Bwana. Licha ya kuachishwa kazi shuleni na kushindwa kupata huruma kutoka kwa familia yake, katu hakati tamaa moyoni mwake.

4/19/2019

Wimbo wa Kuabudu | "Umuhumi wa Maombi" | How to Gain the Praise of God


Utambulisho

Wimbo wa Kuabudu | "Umuhumi wa Maombi" | How to Gain the Praise of God


Maombi ni njia moja ya mwanadamu kushirikiana na Mungu,

kuita Roho Wake na kuguswa na Mungu.

Kadiri unavyoomba zaidi, ndivyo utakavyoguswa zaidi, kuangaziwa na kuwa mwenye nguvu-nia.

Watu kama hao wanaweza kufanywa kamili hivi karibuni.

11/03/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ufafanuzi wa Tamko la Ishirini na Nane

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ufafanuzi wa Tamko la Ishirini na Nane

Hali ya watu ni kwamba kadri wanavyoelewa maneno ya Mungu kwa kiasi kidogo, ndivyo wanavyoshuku zaidi njia ya sasa ya Mungu ya kufanya kazi. Lakini hii haina athari kwa kazi ya Mungu; maneno Yake yanapofikia kiwango fulani, kwa kawaida mioyo ya watu itabadilika.

10/17/2018

Nyimbo za Kanisa | Umuhumi wa Maombi

Nyimbo za Kanisa | Umuhumi wa Maombi

I
Maombi ni njia moja ya mwanadamu kishirikiana na Mungu,
kuita Roho Wake na kuguswa na Mungu.
Kadiri unavyoomba zaidi, ndivyo utakavyoguswa zaidi, kutiwa nuru na kuwa na mawazo ya nguvu zaidi.
Watu kama hao wanaweza kufanywa kamili hivi karibuni.
Kadiri unavyoomba zaidi, ndivyo utakavyoguswa zaidi, kutiwa nuru na kuwa na mawazo ya nguvu zaidi.

9/17/2018

Ni Muhimu Sana Kutii Kazi ya Roho Mtakatifu!📝😇

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Wakristo
Xiaowei    Mji wa Shanghai
Wakati fulani kitambo, hata kama daima nilipata msukumo kiasi na fadhila wakati dada mmoja aliyeshiriki nami alishiriki nuru aliyokuwa amepata wakati alipokula na kunywa neno la Mungu, pia kila wakati nilikuwa na hisia ya muda mrefu kuwa alikuwa anajionyesha. Ningejiuliza, “Nikimjibu sasa hivi, sitakuwa nikimtia moyo? Kwa namna hiyo, sitaonekana basi kuwa duni kumliko yeye?”

4/22/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Ishirini na Nane

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

 Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Ishirini na Nane

Nilipokuja kutoka Zayuni, vitu vyote vilikuwa vimenisubiri, na Niliporudi Zayuni, Nilisalimiwa na wanadamu wote. Nilipokuja na kwenda, hatua Zangu hazikuwahi zuiliwa na vitu vilivyokuwa na uadui Kwangu, na kwa hivyo kazi Yangu iliendelea kwa utaratibu. Leo, Ninapokuja miongoni mwa viumbe vyote, vitu vyote vinanisalimu kwa kimya, kwa uoga mkuu kuwa Nitaondoka tena na Niondoe usaidizi kwao. Vitu vyote vinafuata uongozi Wangu, na vyote vinaangalia upande ulioashiriwa na mkono Wangu. Maneno ya kinywa Changu yamefanya kamili viumbe vingi na kuwaadibu wana wengi wa uasi Kwa hivyo, wanadamu wote wanaangalia maneno Yangu kwa makini, na kusikiza kwa karibu maneno ya kinywa Changu, na wanaogopa sana kupitwa na fursa hii nzuri.

4/02/2018

Umeme wa Mashariki | Kuhusu Desturi ya Sala

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Maombi

Umeme wa Mashariki | Kuhusu Desturi ya Sala

     Mwenyezi Mungu alisema, Nyinyi hamtilii maanani sala katika maisha yenu ya kila siku. Watu daima wamepuuza sala. Katika sala zao hapo awali walikuwa wakifanya tu mambo kwa namna isiyo ya dhati na kufanya mchezo tu, na hakuna mtu aliyeupeana moyo wake kwa ukamilifu mbele ya Mungu na kumwomba Mungu kweli. Watu humwomba Mungu tu wakati kitu kinawatendekea. Katika wakati huu wote, umewahi kweli kumwomba Mungu? Je, umewahi kutoa machozi ya uchungu mbele ya Mungu? Je, umewahi kujijua mwenyewe mbele ya Mungu? Je, umewahi kumwomba Mungu maombi ya kutoka?

3/04/2018

Umeme wa Mashariki | 62. Sababu ya Kweli ya Kazi Isiyofaa

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kanisa

Umeme wa Mashariki | 62. Sababu ya Kweli ya Kazi Isiyofaa
Xinyi Mji wa Xi’an, Mkoa wa Shaanxi
Katika ziara zangu za karibuni kwa makanisa, mara nyingi niliwasikia viongozi na wafanyakazi wakisema kwamba watu wengine, baada ya kuhudhuria ushirika na mimi, waligeuka hasi, wanyonge na walikosa motisha ya kuendelea kutafuta. Wengine walisema ilikuwa vigumu sana kumwamini Mungu na walimwelewa Mungu visivyo. Wengine walisema kwamba hali zao zilikuwa nzuri kabla ya wao kukutana na mimi, lakini punde tu waliponiona, walihisi shinikizo kubwa mno na wasio na raha.

2/11/2018

Neno la Mwenyezi Mungu | 34 Umuhimu na Mazoezi ya Sala

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,maombi

Neno la Mwenyezi Mungu  | 34  Umuhimu na Mazoezi ya Sala

Je, mnaomba vipi kwa sasa? Ni maendeleo kwa sala za kidini jinsi gani? Mnaelewa nini hasa kuhusu umuhimu wa sala? Je mmechunguza maswali haya? Kila mtu ambaye hafanyi sala ako mbali na Mungu, kila mtu ambaye hasali anafuata mapenzi yake; Kukosekana kwa sala kunaashiria kwenda mbali na Mungu na usaliti wa Mungu. Ni nini uzoefu wenu hasa na sala? Sasa hivi, kazi ya Mungu tayari inakaribia mwisho na uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu unaweza kuonekana kutoka kwa maombi ya mwanadamu. Je wewe hutenda vipi wakati watu walio chini yako wanakurai na kukupa sifa kwa matokeo unayozalisha katika kazi yako? Je wewe hutenda vipi wakati watu wanakupa mapendekezo? Je, wewe huomba mbele ya Mungu?

2/07/2018

54 Watu Ambao Daima Wana Mahitaji kwa Mungu Ndio wa Mwisho Kuwa Tayari Kusikia Hoja

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kumjua Mungu,
kumfuata Mungu
   Kama utajielewa, ni lazima uielewe hali yako ya kweli; jambo muhimu zaidi katika kuielewa hali yako mwenyewe ni kuwa na ufahamu juu ya fikira zako na mawazo yako. Katika kila kipindi cha muda, fikira za watu zimekuwa zikidhibitiwa na jambo moja kubwa; ikiwa unaweza kuzielewa fikira zako, unaweza kukielewa kitu kilicho nyuma yazo. Hakuna mtu anayeweza kuzidhibiti fikira na mawazo yake. Je, fikira na mawazo haya hutoka wapi? Je, ni nini kiini cha matilaba haya? Je, fikira hizi na mawazo haya huzalishwaje? Je, zinadhibitiwa na nini? Asili za fikira na mawazo haya ni nini? Baada ya tabia yako kubadilika, fikira na mawazo yako, tamaa ambazo moyo wako unatafuta na maoni yako kwa ukimbizaji, ambazo zimefanyizwa kutokana na sehemu ambazo zimebadilika zitakuwa tofauti.

1/31/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 6

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu, Sura ya 6

    Binadamu wanapigwa bumbuazi kwa sababu ya matamshi ya Mungu wanapotambua kwamba Mungu amefanya kitendo kikubwa katika ulimwengu wa kiroho, kitu ambacho mwanadamu hawezi na ambacho Mungu Mwenyewe pekee ndiye Anaweza kufanikisha. Kwa sababu hii, Mungu mara tena anawasilisha maneno ya huruma kwa wanadamu. Mioyo ya watu inapojaa ukinzani, ikishangaa: “Mungu ni Mungu asiye na huruma au upendo, lakini badala yake Mungu aliyejitolea kuwaangusha binadamu; kwa hiyo mbona Atuonyeshe huruma? Yawezekana kwamba Mungu kwa mara nyingine amehamia kwa utaratibu?”

1/24/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu, Utendaji (1)

 Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Wakristo
imani katika Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu, Utendaji (1)

Mbeleni, kulikuwa na kupotoka kwingi katika jinsi watu walipata uzoefu, na kungeweza hata kuwa kwa ajabu. Kwa sababu tu hawakuelewa viwango vya mahitaji ya Mungu, kulikuwa na maeneo mengi ambayo uzoefu wa watu ulienda kombo. Sharti la Mungu kwa mtu ni kwao kuwa na uwezo wa kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida. Njia za mtu wa kisasa kuhusiana na chakula na mavazi, kwa mfano. Wanaweza kuvaa suti na tai na wanaweza kujifunza kiasi kuhusu sanaa ya kisasa, na katika muda wao wa ziada wanaweza kuwa na kiasi fulani cha fasihi na maisha ya burudani.Wanaweza kuchukua baadhi ya picha za kumbukumbu na wanaweza kusoma na kupata kiasi cha elimu, na kuwa na mazingira mazuri kiasi ya kuishi.

11/19/2017

Kujadili Maisha ya Kanisa na Maisha Halisi

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kanisa
Umeme wa Mashariki | Kujadili Maisha ya Kanisa na Maisha Halisi
Mwenyezi Mungu alisema, Watu huhisi kuwa wao wanaweza tu kubadilika katika maisha yao ya kanisani, na kuwa iwapo hawaishi ndani ya kanisa, mbadiliko hauwezekani, kuwa hawawezi kutimiza mbadiliko katika maisha yao halisi. Mwaweza kutambua suala hili ni lipi? Nimeongea juu ya kumleta Mungu katika maisha halisi, na hii ndiyo njia kwa wale wanaomwamini Mungu kuingia katika uhalisi wa maneno ya Mungu. Kwa kweli, maisha ya kanisa ni njia ndogo tu ya kuwakamilisha watu. Mazingira ya msingi ya kuwakamilisha wanadamu bado ni maisha halisi. Hiki ndicho kitendo halisi na mafunzo halisi Niliyozungumzia, yanayowaruhusu wanadamu kutimiza maisha ya ubinadamu wa kawaida na kuishi kwa kudhihirisha mfano wa mtu wa kweli katika maisha ya kila siku. Kipengele kimoja ni kwamba mtu lazima aelimike ili kuinua kiwango chake mwenyewe cha elimu, aweze kuelewa maneno ya Mungu, na kutimiza uwezo wa kuelewa.

11/15/2017

Wale wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watakubaliwa na Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Kazi ya Roho Mtakatifu inabadilika kutoka siku hadi siku, ikipanda juu kwa kila hatua; ufunuo wa kesho unakuwa hata juu kuliko wa leo, hatua kwa hatua ukikwea hata juu zaidi. Hii ndiyo kazi anayotumia Mungu kumkamilisha mwanadamu. Iwapo mwanadamu hawezi kwenda sambamba, basi anaweza kuachwa wakati wowote. Kama mwanadamu hana moyo wa kutii, basi hawezi kufuata hadi mwisho. Enzi ya kale imepita; sasa ni enzi mpya. Na katika enzi mpya, kazi mpya lazima ifanywe. Hasa katika enzi ya mwisho ambapo mwanadamu atakamilishwa, Mungu atafanya kazi mpya hata haraka zaidi.

11/10/2017

Umeme wa Mashariki | Tabia Yako Ni Duni Sana!

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kristo
Umeme wa Mashariki | Tabia Yako Ni Duni Sana!

Mwenyezi Mungu alisema, Ninyi nyote mmeketi katika viti vya kifahari, mkiwafundisha wale wa vizazi vijana ambao ni wa aina yenu, ukiwafanya waketi nawe. Je, mngekosaje kujua kwamba wale "watoto" wenu walikuwa tayari hawana pumzi, na kwamba hawakuwa na kazi Yangu zamani? Utukufu Wangu huangaza kutoka nchi ya Mashariki hadi nchi ya Magharibi, lakini wakati utukufu Wangu huenea mpaka mwisho wa dunia na wakati unapoanza kuinuka na kuangaza, Nitaondoa utukufu wa Mashariki na kuuletea Magharibi ili kwamba hawa watu wa giza katika Mashariki ambao wameniacha Mimi watakuwa bila mwanga unaong'aa kuanzia hapo kwendelea.

11/07/2017

Umeme wa Mashariki | Dhambi Zitampeleka Mwanadamu Jahanamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,maombi
Umeme wa Mashariki | Dhambi Zitampeleka Mwanadamu Jahanamu
Mwenyezi Mungu alisema, Nimewapa maonyo mengi na kutawaza juu yenu kweli nyingi ili kuwashinda. Leo mnajihisi kustawishwa zaidi kuliko mlivyokuwa hapo zamani, kuelewa kanuni nyingi za jinsi mtu anapaswa awe, na kumiliki kiasi kikubwa cha maarifa ya kawaida ambayo watu waaminifu wanapaswa kuwa nayo. Hiki ndicho mmepata baada ya miaka mingi sasa. Mimi sikani mafanikio yenu, lakini lazima Niseme wazi kuwa Mimi pia sikani kutotii kwenu kwingi na uasi dhidi Yangu hii miaka mingi, kwa sababu hakuna hata mtakatifu mmoja kati yenu, bila yeyote kuachwa nyuma nyinyi ni watu mliopotoshwa na Shetani, na maadui wa Kristo. Dhambi zenu na kutotii kwenu hadi sasa havihesabiki, hivyo si ajabu kwamba Mimi daima Hujirudia mbele yenu. Sitaki kuishi hivi na nyinyi, lakini kwa ajili ya siku zenu za baadaye, kwa ajili ya hatima zenu, Mimi hapa Nitarudia Niliyoyasema mara nyingine tena.

11/06/2017

Kuwa Mzingatifu wa Mapenzi ya Mungu ili Upate Utimilifu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mungu,Umeme wa Mashariki
Umeme wa Mashariki | Kuwa Mzingatifu wa Mapenzi ya Mungu ili Upate Utimilifu
Mwenyezi Mungu alisema, Kadiri unavyozingatia mapenzi ya Mungu, ndivyo unavyokuwa na mzigo zaidi; kadiri unavyokuwa na mzigo, ndivyo uzoefu wako utakuwa mwingi zaidi. Unapokuwa mzingatifu wa mapenzi ya Mungu, Mungu atakupa mzigo huu, na Mungu atakupa nuru ya mambo ambayo amekuaminia. Baada ya Mungu kukupa mzigo huu, utaangalia ukweli wa kipengele hiki unapokula na kunywa maneno ya Mungu. Kama una mzigo unaohusiana na hali ya maisha ya ndugu, huu ni mzigo ulioaminiwa kwako na Mungu, na sala zako za kila siku daima zitaubeba mzigo huu. Kile ambacho Mungu hufanya kimeaminiwa kwako, uko radhi kutekeleza kile ambacho Mungu anataka kufanya, na hivi ndivyo inavyomaanisha kuuchukua mzigo wa Mungu kama wako. Wakati huu, kula na kunywa kwako maneno ya Mungu kutalenga masuala katika vipengele hivi, na utafikiri, nitayatatuaje masuala haya? Nitawaruhusu vipi ndugu kufunguliwa, wawe na furaha katika nafsi zao?

11/05/2017

Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Fuata Nyayo za Mungu

Umeme wa Mashariki  Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Fuata Nyayo za Mungu
Mwenyezi Mungu alisema, Sasa, mnatakiwa kufuatilia kugeuka kuwa watu wa Mungu, na mtaanza kuingia kote katika njia sahihi. Kuwa watu wa Mungu kuna maana ya kuingia katika Enzi ya Ufalme. Leo, mnaanza kwa urasimu kuingia katika mafunzo ya ufalme, na maisha yenu ya baadaye yatakoma kuwa goigoi na hobelahobela kama yalivyokuwa awali; maisha hayo ni yasiyoweza kufikia viwango vinayotakiwa na Mungu. Kama huhisi umuhimu wowote, basi hili huonyesha kwamba huna hamu ya kujiendeleza mwenyewe, kwamba ukimbizaji wako umekanganywa na kuchanganywa, na wewe ni usiyeweza kutimiza mapenzi ya Mungu.

11/02/2017

Umeme wa Mashariki | Hakuna Aliye wa Mwili Anayeweza Kuepuka Siku Ya Ghadhabu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mungu
Umeme wa Mashariki | Hakuna Aliye wa Mwili Anayeweza Kuepuka Siku Ya Ghadhabu
Leo, Nawaonya hivi kwa ajili ya kusalimika kwenu wenyewe, ili kazi Yangu iendelee vizuri, na ili kazi Yangu ya uzinduzi kote ulimwenguni iweze kufanyika kwa njia inayofaa na kikamilifu, ikifichua maneno Yangu, mamlaka, adhama na hukumu kwa watu wa nchi zote na mataifa. Kazi Ninayoifanya miongoni mwenu ni mwanzo wa kazi Yangu katika ulimwengu wote. Ingawa sasa ni siku za mwisho tayari, jua kwamba "siku za mwisho" ni jina tu la enzi: Kama tu vile Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema, linaashiria enzi, na linaashiria enzi nzima, badala ya mwisho wa miaka au miezi michache. Hata hivyo siku za mwisho ni tofauti kabisa na Enzi ya Neema na Enzi ya Sheria. Kazi ya siku za mwisho haifanyiki katika taifa la Israeli, lakini kati ya mataifa; ni ushindi mbele ya kiti Changu cha enzi cha watu kutoka mataifa yote na makabila yote nje ya Israeli, ili utukufu Wangu katika ulimwengu wote uweze kujaza dunia nzima.

11/01/2017

Umeme wa Mashariki | Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Kristo,Roho Mtakatifu
Umeme wa Mashariki | Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Kwa nini unamwamini Mungu? Watu wengi wanafadhaishwa na swali hili. Siku zote wana mitazamo tofauti kuhusu Mungu wa vitendo na Mungu wa mbinguni, jambo linaloonyesha kwamba wanamwamini Mungu sio ili wamtii, bali kupata manufaa fulani, au kuepuka mateso ya janga. Wakati huo tu ndipo wanakuwa watii kwa kiasi fulani, lakini utii wao ni wa masharti, ni kwa ajili ya matarajio yao wenyewe, na kushinikiziwa. Hivyo: kwa nini unamwamini Mungu? Ikiwa ni kwa ajili ya matarajio yako tu, na majaliwa yako, basi ni bora zaidi usingeamini. Imani kama hii ni kujidanganya, kujihakikishia, na kujishukuru. Kama imani yako haijajengwa katika msingi wa utii kwa Mungu, basi hatimaye utaadhibiwa kwa kumpinga Mungu. Wale wote ambao hawatafuti utii kwa Mungu kwa imani yao wanampinga Mungu. Mungu anaomba kwamba watu watafute ukweli, kwamba wawe na kiu cha neno la Mungu, na wanakula na kunywa maneno ya Mungu, na kuyaweka katika matendo, ili waweze kupata utii kwa Mungu.