Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Hukumu-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Hukumu-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote

10/05/2019

4. Umuhimu wa hukumu ya Mungu katika siku za mwisho unaweza kuonekana katika matokeo yaliyofanikishwa na kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho

III. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Kazi ya Mungu ya Hukumu katika Siku za Mwisho

4. Umuhimu wa hukumu ya Mungu katika siku za mwisho unaweza kuonekana katika matokeo yaliyofanikishwa na kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho

(1) Kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho inafanywa kumtakasa, kumwokoa na kumkamilisha mwanadamu, na kukiunda kikundi cha washindi
Aya za Biblia za Kurejelea:
Kwa sababu umelihifadhi neno la uvumilivu wangu, pia mimi nitakuhifadhi dhidi ya saa ya majaribu, ambayo itajia dunia yote, kuwajaribu wale waishio duniani. Tazama, nakuja kwa haraka: shikilia kwa thabiti yale uliyo nayo, ili mtu yeyote asichukue taji lako. Yule ambaye anashinda nitamfanya awe nguzo katika hekalu lake Mungu wangu, na hatatoka nje tena: na nitaandika kwake jina lake Mungu wangu, na jina la mji wake Mungu wangu, ambao ni Yerusalemu mpya, ambao hukuja chini kutoka kwa Mungu wangu mbinguni: na nitaandika kwake jina langu jipya” (Ufunuo 3:10-12).

8/02/2019

Maigizo Yaliyosimuliwa ya Hadithi za Kweli "Upendo wa Kweli wa Mungu" (Swahili Subtitles)


Maigizo Yaliyosimuliwa ya Hadithi za Kweli "Upendo wa Kweli wa Mungu" (Swahili Subtitles)


Ili kujitengenezea nafasi yake mwenyewe duniani, mhusika mkuu alilazimika kufuata mwenendo wa duniani humu, akihangaika na kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya umaarufu na hadhi. Maisha yake yalilikuwa hasa matupu na yenye maumivu. Baada ya kumwamini Mwenyezi Mungu, alipata maana ya maisha ya binadamu ndani ya maneno ya Mwenyezi Mungu, na akiwa amejawa na furaha, akamfuata Mungu na kutimiza majukumu yake. Hata hivyo, kwa sababu moyo wake ulikuwa chini ya udhibiti wa umaarufu na hadhi, katika kutekeleza majukumu yake mara kwa mara alitenda kwa mujibu wa mawazo yake mwenyewe, na alikuwa dhalimu na mwenye udikteta.

7/27/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 94

Narudi Sayuni pamoja na wazaliwa Wangu wa kwanza—kweli mnaelewa maana ya kweli ya maneno haya? Nimewakumbusha tena na tena kwamba Mimi nataka mkue haraka ili mtawale na Mimi. Je, mnakumbuka? Vitu hivi vyote vinahusiana moja kwa moja na kupata mwili Kwangu. Kutoka Sayuni Nilikuja duniani katika nyama ili Nipate kupitia nyama kundi la watu ambao ni wa akili moja na Mimi, na kisha turudi Sayuni.

7/26/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 104

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 104 


      Watu, matukio na vitu vyote nje Yangu vitakufa na kuwakatika hali ya kutokuwepo, ilhali watu, matukio na vitu vyote vilivyo ndani Yangu vitapata kila kitu kutoka Kwangu na kuingia katika utukufu pamoja na Mimi, kuingia katika Mlima Wangu Sayuni, makazi Yangu, na kuishi pamoja kwa amani nami milele. Niliumba vitu vyote mwanzoni na Nitamaliza kazi Yangu mwishowe, na pia Nitatawala milele kama Mfalme. Katikati, pia Ninaongoza na kuutawala ulimwengu mzima.

7/17/2019

Kuna tofauti ipi kati ya jinsi ambavyo Bwana Yesu alifanya kazi katika Enzi ya Neema na jinsi Mwenyezi Mungu anavyofanya katika Enzi ya Ufalme?

V. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Tofauti Kati ya Kazi ya Mungu ya Hukumu Katika Siku za Mwisho na Kazi Yake ya Ukombozi Katika Enzi ya Neema

2. Kuna tofauti ipi kati ya jinsi ambavyo Bwana Yesu alifanya kazi katika Enzi ya Neema na jinsi Mwenyezi Mungu anavyofanya katika Enzi ya Ufalme?

Maneno Husika ya Mungu:


        Wakati wa kupata mwili Kwake mara ya kwanza, ilikuwa muhimu kwa Mungu kuponya wagonjwa na kufukuza mapepo kwa sababu kazi Yake ilikuwa ni kukomboa. Ili kulikomboa kabila lote la mwanadamu, Alipaswa kuwa mwenye upendo na mwenye kusamehe. Kazi Aliyoifanya kabla ya kusulubiwa ilikuwa kuponya watu na kufukuza mapepo, ambayo iliashiria wokovu Wake wa mwanadamu kutoka katika dhambi na uchafu.

5/25/2019

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa Makanisa | Sura ya 16

Baada ya ushuhudiaji wa Mwana wa Adamu, Mwenyezi Mungu alijifichua kwetu hadharani kama Jua la haki. Haya ndiyo mabadiliko mlimani! Sasa inakuwa halisi zaidi na zaidi, na zaidi kuwa jambo la uhalisi. Tumeona utaratibu wa kazi ya Roho Mtakatifu, Mungu Mwenyewe ameibuka kutoka kwa mwili wa damu. Yeye hayuko chini ya udhibiti wa mwanadamu, wala anga, wala jiografia; Yeye huvuka mipaka ya nchi na bahari, Yeye hufika miisho halisi ya ulimwengu, na mataifa yote na watu wa jumuia zote wanasikiliza sauti Yake kwa utulivu.

4/06/2019

"Nimewahi Treni ya Mwisho" (4) : Hukumu Mbele ya Kiti Kikuu Cheupe cha Mungu Imeanza


   "Nimewahi Treni ya Mwisho" (4) : Hukumu Mbele ya Kiti Kikuu Cheupe cha Mungu Imeanza


    Unajua jinsi hukumu ya kiti cha enzi kikuu cheupe iliyotabiriwa katika Ufunuo inatimizwa? Je, hukumu ya kiti cha enzi kuu cheupe iko mbinguni, au duniani? Je, inafanywa na Mungu aliyepata mwili, au kwa Roho? Video hii fupi itajibu maswali yenu moja baada ya nyingine.
  
       Tazama Video: Filamu za Injili

              App ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

3/18/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 15

Kuonekana kwa Mungu tayari kumetokea katika makanisa yote. Roho ndiyo anayeongea, Yeye ni moto mkali, Yeye hubeba uadhama na Anahukumu; Yeye ni Mwana wa Adamu, liyevaa vazi lililofika kwa miguu, na kufungwa mshipi kwenye matiti na ukanda wa dhahabu. Kichwa Chake na nywele Zake ni nyeupe kama sufu nyeupe, na macho Yake ni kama mwale wa moto; na miguu Yake iko kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru;

3/11/2019

Matamko ya Kristo Mwanzoni—Sura ya 12

Mwenyezi Mungu anasema, “ Ikiwa una tabia ambayo si thabiti, nyepesi kuhamaki kama upepo au mvua, kama huwezi kuendelea kusonga mbele, basi fimbo Yangu haitakuwa mbali na wewe. Unaposhughulikiwa, kadiri hali ilivyo mbaya zaidi, na kadiri unavyoteswa zaidi, ndivyo upendo wako kwa Mungu unavyoongezeka, na unaacha kushikilia dunia. Bila njia nyingine, unakuja Kwangu, na unapata tena nguvu na imani yako. Ilhali, katika hali rahisi, ungeboronga.

2/26/2019

Ushuhuda wa Mkristo: Jinsi Alivyoshinda Majaribu ya Kuwa na Mpenzi wa Siri (Sehemu ya 2)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Wakristo
 
Na Xiyue, Mkoa wa Henan
Katika siku chache zilizofuata, ingawa Jingru hakuwa ameanguka katika majaribu ya Shetani na alijua kwamba hangeweza kuwa mwenzi wa Wang Wei kamwe, mkutano wake na Wang Wei jioni hiyo na ungamo lake la kweli vilirudiwa akilini mwake tena na tena kama onyesho katika filamu …
Wang Wei alipompigia simu tena, moyo wa Jingru ulishtuka kidogo, naye akajiambia: “Sote wawili hatuwezi kuwa kitu kimoja, lakini bado tunaweza kuwa marafiki wa kawaida.

1/18/2019

Swahili Gospel Movie Clip (9) - Ushuhuda kutoka kwa Kupitia Hukumu ya Mungu katika Siku za Mwisho

Swahili Gospel Movie Clip "Kutoka kwa Enzi Hububujika Maji ya Uzima" (9) - Ushuhuda kutoka kwa Kupitia Hukumu ya Mungu katika Siku za Mwisho

Katika siku za mwisho, Mwenyezi Mungu anaonyesha ukweli nchini China na anafanya kazi ya hukumu akianza na nyumba ya Mungu. Alishinda na kuokoa kundi la watu, na wao ndio ambao wamepata njia ya uzima wa milele. Je, unataka kujua jinsi ambavyo wamepitia hukumu na kuadibiwa kwa Mungu? Je, unataka kujua ni mabadiliko gani ambayo wamepitia kwa kupitia hukumu na kuadibu kwa Mungu? Unaweza kusikia kutoka kwao ukiitazama hii video fupi.

Yaliyopendekezwa: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

11/12/2018

Swahili Christian Video "Kuzinduka" | Ni nini Maana ya Uzima?


Jina lake ni Chen Xi, na tangu akiwa mtoto elimu na ushawishi wa wazazi wake na shule yake zilimfanya yeye mara zote kutaka kwa tofauti na wengine na kutafuta kuwa juu ya wengine,kwa hivyo alikuwa na bidii katika masomo yake na kutia juhudi zote. Baada ya kumwamini Mungu Chen Xi alisoma maneno ya Mungu kwa wingi na akaja kuelewa kiasi fulani cha ukweli. Aliona kuwa njia pekee inayofaa katika maisha ni kumwamini na kumfuata Mungu na kuwa mtafutaji mwenye shauku, na alijitolea kwa dhati katika kutekeleza wajibu wake.

9/02/2018

Kujua Chanzo cha Upinzani wa Watu kwa Kazi Mpya ya Mungu katika Imani Yao kwa Mungu

Sura ya 7 Vipengele Vingine vya Ukweli Ambavyo Unafaa Kueleweka Katika Imani Yako kwa Mungu

1. Kujua Chanzo cha Upinzani wa Watu kwa Kazi Mpya ya Mungu katika Imani Yao kwa Mungu

Maneno Husika ya Mungu:

Sababu kwamba mwanadamu humpinga Mungu inatoka, kwa upande mmoja, katika tabia potovu ya mwanadamu, na kwa upande mwingine, kutokana na kutomfahamu Mungu na kutoelewa kanuni za kazi ya Mungu na mapenzi Yake kwa mwanadamu. Vipengele hivi viwili vinaunganishwa katika historia ya upinzani wa mwanadamu kwa Mungu. Wanafunzi katika imani wanampinga Mungu kwa sababu upinzani kama huu uko ndani ya asili yao, ilhali upinzani dhidi ya Mungu wa wale walio na miaka mingi katika imani unatokana na kutomfahamu Mungu, kuongeza kwa tabia yao potovu.

7/26/2018

Nitalipa Upendo Wa Mungu

Nahisi furaha sana kumfuata Mungu wa matendo.
Sikufikiria kamwe kuuona uso wa Mungu.
Ni neema kubwa sana kupokea hukumu ya Mungu.
Lazima tuujali moyo Wake.
Katika uzoefu wa kazi ya Mungu, nimefurahia upendo Wake.
Kumwona Mungu akiteseka sana kwa ajili yetu,
nagundua kuwa mwanadamu amepotoshwa sana na Shetani.

7/24/2018

Umeme wa Mashariki | Ufafanuzi wa Tamko la Thelathini na Tatu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Umeme wa Mashariki | Ufafanuzi wa Tamko la Thelathini na Tatu 

Mwenyezi Mungu alisema, Kwa ukweli, kutegemea kile ambacho Mungu amefanya ndani ya watu, na kuwapa, na vilevile kile ambacho watu wanacho, inaweza kusemwa kwamba matakwa Yake kwa watu sio makubwa mno, kwamba hataki mengi kutoka kwao. Wangekosaje basi, kujaribu kumridhisha Mungu? Mungu humpa mwanadamu asilimia mia moja, lakini Huhitaji tu sehemu ndogo ya asilimia kutoka kwa watu—hii ni kuhitaji mengi sana?

7/22/2018

Kupima kwa Sura Ni Upuuzi Tu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Ushuhuda
Yifan    Jiji la Shangqiu, Mkoa wa Henan
Katika siku za nyuma, mimi mara nyingi niliwapima watu kwa sura zao, nikiwachukua watu wachangamfu, wajuzi na wambuji hasa kwa heshima sana. Niliamini kwamba watu kama hao walikuwa wa busara, hodari kwa kuwaelewa wengine na kwa ujumla wema na wakarimu. Ni juzi juzi tu, kama ambavyo uhalisi umejifichua, nimekuja kurekebisha njia hii ya upuuzi ya kufikiri.

7/13/2018

Ambua Barakoa, na Uanze Maisha Upya

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Ushuhuda

Chen Dan    Mkoa wa Hunan
Mwishoni mwa mwaka jana, kwa sababu sikuweza kuzindua kazi ya injili katika eneo langu, familia ya Mungu ilimhamisha ndugu mmoja wa kiume kutoka eneo jingine ili kuchukua kazi yangu. Kabla ya haya sikuwa nimearifiwa, bali nilisikia kwa njia isiyo ya moja kwa moja kutoka kwa dada mmoja niliyekuwa mbia naye. Nilifadhaika sana. Nilishuku kwamba mtu aliyekuwa madarakani hakuwa ameniarifu kwa kuhofia kwamba singekubali kuiacha nafasi yangu na ningeshindana.

6/16/2018

Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Unampenda Mungu kiasi gani hasa leo? Na unajua kiasi gani hasa kuhusu yote ambayo Mungu amefanya ndani yako? Haya ni mambo unayopaswa kujifunza. Mungu anapowasili duniani, yote ambayo Amefanya ndani ya mwanadamu na kumkubalia mwanadamu kuona ni ili mwanadamu atampenda na kumjua Yeye kweli. Kwamba mwanadamu anaweza kuteseka kwa ajili ya Mungu na ameweza kufikia umbali huu ni, kuhusiana na jambo moja, kwa sababu ya upendo wa Mungu, na kuhusiana na jambo lingine, ni kwa sababu ya wokovu wa Mungu;

2/25/2018

Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (4)

Mwenyezi Mungu alisema, Kukamilishwa kuna maana gani? kushindwa kuna maana gani? Ni vigezo vipi mtu anapaswa kuwa navyo ili apate kushindwa? Na ni vigezo vipi mtu anapaswa kuwa navyo ili afanywe mkamilifu? Kushinda na kukamilisha yote yanakusudiwa kumfanyia kazi mwanadamu ili aweze kurudi katika asili yake na awe huru na tabia zake potovu za shetani na ushawishi wa Shetani. Huu ushindi huja mapema katika mchakato wa kumfinyanga mwanadamu, ikiwa na maana kwamba ni hatua ya kwanza ya kazi. Kukamilisha ni hatua ya pili, au hitimisho la kazi. Kila mwanadamu ni lazima apitie hali ya kushindwa;