Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mungu. Onyesha machapisho yote

7/12/2018

Njoo Mbele Ya Mungu Mara kwa Mara

Chukua fursa unapokuwa na wakati, keti kimya mbele ya Mungu.
Soma neno Lake, jua ukweli Wake, rekebisha makosa na dhambi ndani yako.
Majaribu huja, yakabili; ijue nia ya Mungu na utakuwa na nguvu.
Mwambie ni vitu gani unavyokosa, shiriki ukweli Wake kila mara.
Roho yako ina furaha unapomwabudu Yeye.
Njoo mara kwa mara mbele ya Mungu, usipinge tena.
Kujali kwako mwili, kunamuumiza Yeye sana.

7/03/2018

Mimi Sistahili Kumwona Kristo

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Wakristo
๐ŸŒป๐ŸŒป๐ŸŒป๐ŸŒป๐ŸŒป๐ŸŒป๐ŸŒป๐ŸŒป~~~~~~~~๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ๐ŸŒบ
Huanbao    Mji wa Dalian, Mkoa wa Liaoning
Tangu kwanza nianze kumwamini Mwenyezi Mungu, daima nimewapenda wale ndugu wa kiume na wa kike ambao wanaweza kupokea huduma ya kibinafsi ya Kristo, ambao wanaweza kusikia mahubiri Yake kwa masikio yao wenyewe. Katika moyo wangu, nimewaza jinsi ingekuwa vizuri sana kama siku moja katika siku zijazo ninaweza kusikia mahubiri ya Kristo, bila shaka kumwona Yeye kungekuwa kwa ajabu hata zaidi.

6/02/2018

Usitafute Mbinu Mpya Unapomtumikia Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Wakristo
Heyi   Mji wa Zhuanghe, Mkoa wa Liaoning
Nilikuwa nimepandishwa cheo tu kuchukua jukumu la kiongozi wa kanisa. Lakini baada ya kipindi cha kazi ngumu, sio tu kuwa kazi ya kiinjili ilikuwa bila uhai kiasi, lakini ndugu zangu wa kiume na wa kike katika timu ya kiinjili walikuwa pia wakiishi katika hali hasi na ya udhaifu. Nikiwa nimekabiliwa na hali hii, sikuweza tena kudhibiti hisia zangu. Ni vipi tena ningeweza kuiamsha kazi ya kiinjili?

4/25/2018

Baada ya Kupoteza Hadhi Yangu …

 Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Wakristo

Umeme wa Mashariki | 3. Baada ya Kupoteza Hadhi Yangu …

Huimin Mji wa Jiaozuo, Mkoa wa Henan
Kila wakati nilipoona au kusikia kuhusu mtu aliyekuwa amebadilishwa naye kujisikia mwenye huzuni, dhaifu au mnunaji, na kutotaka kufuata tena, basi niliwaangalia kwa dharau. Nilidhani haikuwa kitu zaidi ya watu tofauti waliokuwa na majukumu tofauti ndani ya kanisa, kwamba hakukuwa na tofauti kati ya juu au chini, kwamba sote tulikuwa uumbaji wa Mungu na hakukuwa na sababu ya kuhuzunikia. Kwa hiyo kama nilikuwa nikiwatunza waumini wapya au kuongoza wilaya, sikuwahi kufikiri kuwa nilizingatia sana hadhi yangu, kwamba nilikuwa mtu wa aina hiyo. Singeweza kamwe kufikiri hata katika miaka milioni moja kwamba ningeonyesha tabia ya aibu kama hiyo wakati mimi mwenyewe nilipobadilishwa ...

3/09/2018

๐ŸŽฌ๐ŸŽฌMuujiza katika Msiba | Video ya Injili "Mungu Abariki"



Utambulisho

Watu mara nyingi husema kwamba "Dhoruba hukusanyika bila tahadhari na balaa huwafika watu kwa ghafula sana." Katika enzi yetu iliyopo ya kupanua kwa haraka kwa sayansi, uchukuzi wa kisasa na utajiri wa mali, maafa yanayotokea pande zote zinazotuzunguka huongeza kila siku. Tunapoligeuza na kulifungua gazeti au kuwasha TV, tunayoyaona hasa ni: vita, matetemeko ya ardhi, sunami, tufani, moto, mafuriko, ajali za ndege, maafa ya kuchimba madini, msukosuko wa kijamii, mgongano mkali sana, mashambulizi ya kigaidi nk. Yote tunayoona ni maafa ya kiasili na maafa yaliyotengenezwa na mtu. Maafa haya yanatokea mara kwa mara na yanazidi kuwa makali zaidi.

1/27/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu, Kusudi la Kuwasimamia Binadamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,Injili

Matamshi ya Mwenyezi Mungu, Kusudi la Kuwasimamia Binadamu

    Ikiwa watu wanaweza kweli kuielewa kikamilifu njia sahihi ya maisha ya binadamu na vilevile kusudi la usimamizi wa Mungu wa binadamu, wasingeshikilia mategemeo yao ya baadaye na majaliwa yao binafsi kama hazina mioyoni mwao. Wasingetamani tena kuwatumikia wazazi wao ambao ni wabaya zaidi kuliko nguruwe na mbwa. Je, mategemeo ya baadaye na majaliwa ya mwanadamu si kabisa kile kinachoitwa nyakati za sasa "wazazi" wa Petro? Yamekuwa kama tu mwili na damu ya mwanadamu.

11/25/2017

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha Kwa ajili ya Hatima Yako

Umeme wa Mashariki | Kanisa la Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha Kwa ajili ya Hatima Yako

   
      Nimefanya kazi nyingi miongoni mwenu na, bila shaka, Nimetamka mengi pia. Hata hivyo, Nahisi kwamba maneno na kazi Yangu havijatimiza lengo la kazi Yangu ya siku za mwisho kikamilifu. Maana, katika siku za mwisho, kazi Yangu si kwa ajili ya mtu au watu fulani, bali ni kwa manufaa ya kufafanua tabia Yangu asilia. Hata hivyo, kutokana na sababu nyingi—pengine ukosefu wa muda au shughuli nyingi za kazi—tabia Yangu haijamwezesha binadamu kunijua hata kidogo. Kwa hivyo, Ninasonga mbele katika mpango Wangu mpya, katika kazi Yangu ya mwisho, kufungua ukurasa mpya katika kazi Yangu ili wale ambao wanaoniona watajipiga kifuani na kuulilia na kuombolezea uwepo Wangu bila kukoma.

11/18/2017

Tofauti Muhimu Kati ya Mungu Aliyepata Mwili na Wanadamu Wanaotumiwa na Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki


Kwa miaka mingi Roho wa Mungu Amekuwa Akifanya kazi kwa kutafuta duniani. Kwa enzi nyingi Mungu Ametumia wanadamu wengi kufanya kazi Yake. Hata hivyo Roho wa Mungu bado hana mahali pazuri pa kupumzika. Kwa hivyo Mungu hupitia wanadamu mbalimbali kufanya kazi Yake na kwa kiasi kikubwa hutumia wanadamu kufanya hivyo. Yaani, katika miaka hii yote mingi, kazi ya Mungu haijawahi kusimama. Inaendelezwa mbele kupitia mwanadamu, bila kikomo mpaka siku ya leo. Ingawa Mungu Amesema na Ametenda mengi, mwanadamu bado hamjui Mungu, hii ni kwa sababu Mungu hajawahi kuonekana na mwanadamu na Yeye Hana umbo.

11/17/2017

Umeme wa Mashariki | Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,ukweli
Matamshi ya Mwenyezi Mungu - "Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea"

Matamshi ya Mwenyezi Mungu - "Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea"

Watu wengi wanamwamini Mungu kwa ajili ya hatima yao ya baadaye au kwa ajili ya starehe ya muda mfupi. Kwa wale ambao hawajapitia ushughulikiaji wowote, imani kwa Mungu ni kwa ajili ya kuingia mbinguni, ili kupata tuzo. Sio ili kufanywa wawe na ukamilifu, au kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu. Ambayo ni kusema kwamba watu wengi hawamwamini Mungu ili watimize majukumu yao, au kukamilisha wajibu wao. Mara chache watu humwamini Mungu ili waishi maisha ya maana, wala hamna wale ambao wanaamini kwamba kwa kuwa mwanadamu yu hai, anapaswa ampende Mungu kwa kuwa ni sheria ya Mbinguni na kanuni ya dunia kufanya hivyo, na ni wito wa asili wa mwanadamu.

11/15/2017

Wale wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watakubaliwa na Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Kazi ya Roho Mtakatifu inabadilika kutoka siku hadi siku, ikipanda juu kwa kila hatua; ufunuo wa kesho unakuwa hata juu kuliko wa leo, hatua kwa hatua ukikwea hata juu zaidi. Hii ndiyo kazi anayotumia Mungu kumkamilisha mwanadamu. Iwapo mwanadamu hawezi kwenda sambamba, basi anaweza kuachwa wakati wowote. Kama mwanadamu hana moyo wa kutii, basi hawezi kufuata hadi mwisho. Enzi ya kale imepita; sasa ni enzi mpya. Na katika enzi mpya, kazi mpya lazima ifanywe. Hasa katika enzi ya mwisho ambapo mwanadamu atakamilishwa, Mungu atafanya kazi mpya hata haraka zaidi.

11/14/2017

Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake

Umeme wa Mashariki,Yesu,Kanisa la Mwenyezi Mungu
Umeme wa Mashariki | Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake
    Kwanza, hebu na tuuimbe wimbo wa kumsifu Mungu: Wimbo wa Ufalme (I) Ufalme Umeshuka katika Ulimwengu
   Kisaidizi ala cha muziki: Watu wanashangilia Mungu kwa furaha, watu wanamsifu Yeye, sauti zisizohesabika zinaongea kuhusu Mungu mmoja wa kweli, ufalme umeshuka ulimwenguni.
    1. Watu wanashangilia Mungu kwa furaha, watu wanamsifu Yeye, sauti zisizohesabika zinaongea kuhusu Mungu mmoja wa kweli, watu wasiohesabika wanaangalia matendo Yake. Ufalme umeshuka ulimwenguni, na mtu wa Mungu yu tajiri na mwenye ukarimu, tajiri na mwenye ukarimu.
Ni nani asiyeshangilia kwa haya (ni nani asiyeshangilia kwa haya)? Ni nani asiyecheza kwa haya (ni nani asiyecheza kwa haya)? Zayuni (Zayuni), Zayuni (Zayuni), inua bango lako la ushindi ili kusherehekea Mungu!

11/11/2017

Upendo Halisi kwa Mungu ni wa Hiari

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mungu
Umeme wa Mashariki | Upendo Halisi kwa Mungu ni wa Hiari

Umeme wa Mashariki | Upendo Halisi kwa Mungu ni wa Hiari

Watu wote wamepitia usafishaji kwa sababu ya maneno ya Mungu. Kama sio Mungu mwenye mwili wanadamu bila shaka hawangebarikiwa kuteseka hivyo. Inaweza pia kusemwa hivi—wale wanaoweza kukubali majaribio ya maneno ya Mungu ni watu waliobarikiwa. Kulingana na ubora wa akili wa watu wa asili, mwenendo wao, mitazamo yao kwa Mungu, hawastahili kupokea aina hii ya usafishaji. Ni kwa sababu wameinuliwa na Mungu ndio wamefurahia baraka hii. Watu walikuwa wakisema kwamba hawakustahili kuuona uso wa Mungu au kusikia maneno Yake. Leo ni kwa sababu tu ya kutiwa moyo na Mungu na fadhili Zake ndio watu wamepokea usafishaji wa maneno Yake.

11/09/2017

Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mungu
Umeme wa Mashariki | Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu

Umeme wa Mashariki | Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu

Mwenyezi Mungu  alisema, Kazi ya kumsimamia mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu, na ina maana kuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu. Hatua hizi tatu hazihusishi kazi ya kuuumba ulimwengu, ila ni hatua tatu za kazi ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Kazi ya kuiumba dunia ilikuwa kazi ya kusababisha uwepo wa wanadamu wote. Haikuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu, na haina uhusiano na kazi ya kumwokoa mwanadamu, kwa kuwa dunia ilipoumbwa mwanadamu hakuwa amepotoshwa na Shetani, na hivyo hakukuwa na haja ya kutekeleza kazi ya kumwokoa mwanadamu.

11/08/2017

Umeme wa Mashariki | Sura ya 23

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu,

 Umeme wa Mashariki | Sura ya 23

 Ninapopaza sauti Yangu, macho Yangu yanapofyatua moto, Ninaitazama kwa uangalifu dunia nzima, Ninatazama kwa uangalifu ulimwengu mzima. Wanadamu wote wananiomba Mimi, wameinua macho yao kuelekea Kwangu, wakiomba Nipunguze hasira, na kuapa kutoniasi tena. Lakini haya siyo yaliyopita; bali yaliyopo kwa sasa. Ni nani anayeweza kubadilisha mapenzi Yangu? Kwa kweli sio sala katika moyo wa mwanadamu, wala maneno yanayotoka midomoni mwao? Ni nani ambaye ameweza kuishi hadi wakati huu, isipokuwa ni kwa nguvu Zangu? Ni nani anayeishi ila kwa maneno ya kinywa Changu? Ni nani asiyekaa chini ya uangalifu wa macho Yangu?

11/05/2017

Unapaswaje Kuitembea Hatua ya Mwisho ya Njia?

Umeme wa Mashariki | Unapaswaje Kuitembea Hatua ya Mwisho ya Njia?
Sasa mko kwenye hatua ya mwisho ya njia, na hii ni sehemu muhimu. Labda umevumilia mateso mengi kabisa, umefanya kazi nyingi, umetembea barabara nyingi, na umesikiliza mahubiri mengi, na haijakuwa rahisi kufika hadi sasa. Ikiwa huwezi kuvumilia mateso yaliyo mbele yako na kama unaendelea kama ulivyofanya zamani, basi huwezi kufanywa mkamilifu. Hii si ili kukutisha—huu ni ukweli. Baada ya Petro kupitia kazi ya Mungu kiasi fulani, alipata umaizi na ufahamu mwingi. Pia alielewa kiasi fulani cha kanuni ya huduma, na baadaye aliweza kujitolea kikamilifu kwa kile ambacho Yesu alimwaminia. Usafishaji mkubwa alioupokea mara nyingi ulikuwa kwa sababu katika mambo aliyoyafanya, alihisi kwamba alikuwa na deni kubwa kwa Mungu na kwamba hangeweza kamwe kumfidia, na aligundua kuwa wanadamu wamepotoka sana, kwa hivyo alikuwa na dhamiri yenye hatia. Yesu alikuwa amemwambia mambo mengi na wakati huo alikuwa na ufahamu mdogo tu.

Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Fuata Nyayo za Mungu

Umeme wa Mashariki  Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Fuata Nyayo za Mungu
Mwenyezi Mungu alisema, Sasa, mnatakiwa kufuatilia kugeuka kuwa watu wa Mungu, na mtaanza kuingia kote katika njia sahihi. Kuwa watu wa Mungu kuna maana ya kuingia katika Enzi ya Ufalme. Leo, mnaanza kwa urasimu kuingia katika mafunzo ya ufalme, na maisha yenu ya baadaye yatakoma kuwa goigoi na hobelahobela kama yalivyokuwa awali; maisha hayo ni yasiyoweza kufikia viwango vinayotakiwa na Mungu. Kama huhisi umuhimu wowote, basi hili huonyesha kwamba huna hamu ya kujiendeleza mwenyewe, kwamba ukimbizaji wako umekanganywa na kuchanganywa, na wewe ni usiyeweza kutimiza mapenzi ya Mungu.

11/03/2017

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Maneno kwa Vijana na Wazee

Umeme wa Mashariki,Wakristo,Roho Mtakatifu
Umeme wa Mashariki | Maneno kwa Vijana na Wazee

Mwenyezi Mungu alisema , Nimetekeleza kazi nyingi sana duniani na Nimetembea kati ya wanadamu kwa miaka mingi sana. Ilhali watu kwa nadra sana huwa na ufahamu wa sura Yangu na tabia Yangu, na watu wachache wanaweza kuelezea kikamilifu kazi Ninayofanya. Watu wanakosa mengi sana, daima wanakosa ufahamu wa kile Ninachokifanya, na mioyo yao daima iko tayari kana kwamba wanaogopa sana Nitawaleta katika hali nyingine na kisha kuwapuuza. Kwa hivyo, mtazamo wa watu Kwangu daima ni vuvuwaa pamoja na tahadhari kubwa sana. Hili ni kwa sababu watu wamekuja kwa wakati wa sasa bila kuelewa kazi Ninayofanya, na wao hasa hukanganywa na maneno ambayo Ninawaambia. Wao huyabeba maneno Yangu mikononi mwao, wasijue kama wanapaswa kujitahidi kuamini au kama wanapaswa kuyasahau kwa shaka. Hawajui kama wanapaswa kuyatia katika vitendo, au kama wanapaswa kungoja kuona. Hawajui kama wanapaswa kuachana na kila kitu na kisha kufuata kwa ujasiri, au kama wanapaswa kuendelea kuwa wa kirafiki na ulimwengu kama hapo awali. Ulimwengu wa ndani wa watu ni wenye utata sana, na wao ni wajanja sana.

Umeme wa Mashariki | Asili na Utambulisho wa Mwanadamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Wakristo
Umeme wa Mashariki | Asili na Utambulisho wa Mwanadamu
Kwa kweli, hawajasikitika, na wamekuwa wakitazama kile ambacho kimefanywa kwa miaka elfu sita iliyopita mpaka leo, kwa kuwa Sikuwaacha. Badala yake, kwa sababu mababu zao walikula tunda kutoka kwa mti wa ujuzi wa mema na maovu lililotolewa na yule mwovu, waliniacha kwa ajili ya dhambi. Mema ni Yangu, wakati maovu ni ya yule mwovu ambaye hunihadaa kwa ajili ya dhambi. Mimi Siwalaumu mwanadamu, wala Siwaangamizi kwa ukatili au kuwatolea kuadibu kusiko na huruma, kwani uovu haukuwa wa wanadamu kiasili. Kwa hivyo ingawa wale Waisraeli walinipigilia misumari msalabani hadharani, wao, ambao wamekuwa wanamngoja Masiha na Yehova na kumtamani sana Mwokozi Yesu, hawajasahau ahadi Yangu.

Kuijua Kazi ya Mungu Leo

Mwenyezi Mungu alisema, Kuijua kazi ya Mungu katika nyakati hizi, kwa sehemu kubwa, ni kumjua Mungu katika mwili wa siku za mwisho, kile ambacho ni huduma Yake kuu, na kile ambacho Amekuja kufanya duniani. Hapo mwanzoni Nimesema katika maneno Yangu kwamba Mungu Amekuja duniani (wakati wa siku za mwisho) ili kuweka mfano kabla Hajaondoka. Ni kwa jinsi gani Mungu Ameuweka mfano huu? Kwa kuzungumza maneno, kwa kufanya kazi na kuzungumza katika nchi nzima. Hii ni kazi ya Mungu wakati wa siku za mwisho; Anazungumza tu ili dunia iwe ulimwengu wa maneno, ili kila mtu awe amepewa na kutiwa nuru maneno Yake, na ili roho ya mwanadamu iamshwe na aweze kuona vizuri kuhusu maono yake.

11/02/2017

Umeme wa Mashariki | Hakuna Aliye wa Mwili Anayeweza Kuepuka Siku Ya Ghadhabu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mungu
Umeme wa Mashariki | Hakuna Aliye wa Mwili Anayeweza Kuepuka Siku Ya Ghadhabu
Leo, Nawaonya hivi kwa ajili ya kusalimika kwenu wenyewe, ili kazi Yangu iendelee vizuri, na ili kazi Yangu ya uzinduzi kote ulimwenguni iweze kufanyika kwa njia inayofaa na kikamilifu, ikifichua maneno Yangu, mamlaka, adhama na hukumu kwa watu wa nchi zote na mataifa. Kazi Ninayoifanya miongoni mwenu ni mwanzo wa kazi Yangu katika ulimwengu wote. Ingawa sasa ni siku za mwisho tayari, jua kwamba "siku za mwisho" ni jina tu la enzi: Kama tu vile Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema, linaashiria enzi, na linaashiria enzi nzima, badala ya mwisho wa miaka au miezi michache. Hata hivyo siku za mwisho ni tofauti kabisa na Enzi ya Neema na Enzi ya Sheria. Kazi ya siku za mwisho haifanyiki katika taifa la Israeli, lakini kati ya mataifa; ni ushindi mbele ya kiti Changu cha enzi cha watu kutoka mataifa yote na makabila yote nje ya Israeli, ili utukufu Wangu katika ulimwengu wote uweze kujaza dunia nzima.