Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kuwasiliana. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kuwasiliana. Onyesha machapisho yote

11/15/2017

Wale wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watakubaliwa na Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Kazi ya Roho Mtakatifu inabadilika kutoka siku hadi siku, ikipanda juu kwa kila hatua; ufunuo wa kesho unakuwa hata juu kuliko wa leo, hatua kwa hatua ukikwea hata juu zaidi. Hii ndiyo kazi anayotumia Mungu kumkamilisha mwanadamu. Iwapo mwanadamu hawezi kwenda sambamba, basi anaweza kuachwa wakati wowote. Kama mwanadamu hana moyo wa kutii, basi hawezi kufuata hadi mwisho. Enzi ya kale imepita; sasa ni enzi mpya. Na katika enzi mpya, kazi mpya lazima ifanywe. Hasa katika enzi ya mwisho ambapo mwanadamu atakamilishwa, Mungu atafanya kazi mpya hata haraka zaidi.