Neno la Mwenyezi Mungu | Sura ya 41. Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu
Je, ni vitu vipi vya asili ya mwanadamu? Unajua tu kuhusu upotovu wa mwanadamu, uasi, upungufu, dosari, fikra, na dhamira, lakini huwezi kugundua sehemu za ndani za asili ya mwanadamu—unafahamu tu safu ya nje, lakini huwezi kugundua chanzo chake. Baadhi hata hufikiri haya mambo ya juu kuwa ni asili ya mwanadamu, wakisema, “Tazama, ninaelewa asili ya mwanadamu; ninatambua ufidhuli wangu. Je, hiyo si asili ya mwandamu?” Je, haitoshi kuikubali kikanuni pekee? Ufidhuli ni kitu cha asili ya mwanadamu; huu ni ukweli kabisa. Je, kuelewa asili ya mtu binafsi ni nini? Inawezaje kujulikana? Je, inajulikana kutoka kwa vipengele vipi? Aidha, vitu hivi vinavyofichuliwa kutoka kwa vipengele hivi tofauti vinapaswaje kutazamwa kwa uthabiti? Tazama asili ya mtu kupitia shauku yake.