Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Hatima-ya-Binadamu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Hatima-ya-Binadamu. Onyesha machapisho yote

4/08/2018

Kifo: Awamu ya Sita | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Maisha

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kifo: Awamu ya Sita

    Baada ya mahangaiko mengi na masikitiko mengi, na kuvunjwa moyo kwingi, baada ya furaha nyingi na huzuni nyingi na baada ya misukosuko ya maisha, baada ya miaka mingi sana isiyosahaulika, baada ya kutazama misimu ikipita na kujirudia, mtu hupita kwenye kiungo muhimu sana cha maisha bila ya arifa, na kwa ghafla tu mtu anajipata kwenye miaka yake ya kufifia. Alama za muda zimejichora kotekote kwenye mwili wa mtu: Mtu hawezi tena kusimama wima, kichwa cha nywele nyeusi kinageuka na kuwa cha nywele nyeupe, macho maangavu na mazuri yanabadilika na kuanza kufifiliza na kuwa na wingu mbele yao, nayo ngozi laini, yenye unyumbufu inageuka na kuwa na makunyanzi na madoadoa.

11/14/2017

Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake

Umeme wa Mashariki,Yesu,Kanisa la Mwenyezi Mungu
Umeme wa Mashariki | Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake
    Kwanza, hebu na tuuimbe wimbo wa kumsifu Mungu: Wimbo wa Ufalme (I) Ufalme Umeshuka katika Ulimwengu
   Kisaidizi ala cha muziki: Watu wanashangilia Mungu kwa furaha, watu wanamsifu Yeye, sauti zisizohesabika zinaongea kuhusu Mungu mmoja wa kweli, ufalme umeshuka ulimwenguni.
    1. Watu wanashangilia Mungu kwa furaha, watu wanamsifu Yeye, sauti zisizohesabika zinaongea kuhusu Mungu mmoja wa kweli, watu wasiohesabika wanaangalia matendo Yake. Ufalme umeshuka ulimwenguni, na mtu wa Mungu yu tajiri na mwenye ukarimu, tajiri na mwenye ukarimu.
Ni nani asiyeshangilia kwa haya (ni nani asiyeshangilia kwa haya)? Ni nani asiyecheza kwa haya (ni nani asiyecheza kwa haya)? Zayuni (Zayuni), Zayuni (Zayuni), inua bango lako la ushindi ili kusherehekea Mungu!