Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Israeli. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Israeli. Onyesha machapisho yote

7/29/2018

Neno la Mungu "Ngurumo Saba Zatoa Sauti - Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni"


Neno la Mungu "Ngurumo Saba Zatoa Sauti - Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni"

Mwenyezi Mungu alisema, "Wakati nuru ya Mashariki inapong’aa polepole tu ndipo giza kote duniani litaanza kugeuka na kuwa nuru, na hapo tu ndipo mwanadamu atatambua kwamba Nilishatoka Israeli zamani na Nimeanza kuchomoza upya Mashariki. Niliwahi kushuka Israeli na baadaye Niliondoka kutoka huko, Siwezi tena kuzaliwa Israeli kwa mara nyingine, kwa kuwa kazi Yangu inauongoza ulimwengu mzima na, zaidi ya hilo, umeme unamulika moja kwa moja kutoka Mashariki kwenda Magharibi.

7/10/2018

Nia ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Sura ya 3 Ukweli Kuhusu Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

2. Nia ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Maneno Husika ya Mungu:
Mpango Wangu mzima wa usimamizi, mpango ambao una urefu wa miaka elfu sita, unashirikisha hatua tatu, au enzi tatu: Enzi ya Sheria mwanzoni; Enzi ya Neema (ambayo pia ni Enzi ya Ukombozi); na katika siku za mwisho, Enzi ya Ufalme. Kazi Yangu katika enzi hizi tatu hutofautiana katika maudhui kulingana na asili ya kila enzi, lakini katika kila hatua huambatana na mahitaji ya mwanadamu—au, kwa usahihi zaidi, inafanywa kulingana na ujanja ambao Shetani hutumia katika vita Vyangu dhidi yake. Madhumuni ya Kazi Yangu ni kumshinda Shetani, ili kudhihirisha hekima Yangu na kudura, kufichua ujanja wote wa Shetani na hivyo kuokoa wanadamu wote, wanaoishi chini ya miliki yake.

3/13/2018

📖🤲🙂Watu Waliochaguliwa Nchini China Hawawezi Kuwakilisha Kabila Lolote la Israeli

Mwenyezi Mungu alisema, Nyumba ya Daudi ilipokea ahadi ya Bwana, na ilikuwa ni familia iliyopokea urithi wa Yehova. Ilikuwa kwa asili moja ya makabila ya Israeli na ilikuwa ya watu waliochaguliwa. Wakati huo, Yehova aliamuru sheria iwepo kwa Wana wa Israeli kuwa Wayahudi wote waliokuwa wa nyumba ya Daudi, wale wote waliozaliwa katika nyumba hiyo wangepokea urithi Wake. Wangepokea sehemu mia kwa moja na kupata hadhi ya wana wa kiume wazaliwa wa kwanza. Wakati huo, wao ndio waliokuwa wameinuliwa zaidi miongoni mwa Waisraeli wote—walikuwa na cheo cha juu zaidi miongoni mwa familia zote za Israeli, na walimhudumia Yehova hekaluni moja kwa moja, kama wamevaa kanzu za ukuhani na mataji.

1/15/2018

002 Mungu Ameleta Utukufu Wake Mashariki

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,nyimbo

Wimbo wa Maneno ya MunguMungu Ameleta Utukufu Wake Mashariki 

I
Mungu aliipa Israeli utukufu Wake
kisha Akauhamisha mbali na pale,
na kuwaleta Waisraeli na kuwaleta watu wote Mashariki.
Mungu amewaelekeza wote kwenye mwanga
ili waweze kuungana tena na kuwa pamoja na mwanga,
wasilazimike kuutafuta tena, kuutafuta mwanga.

9/16/2017

Umeme wa Mashariki | Ukaribisheni Urejeaji wa Bwana Yesu | Sifa na Ibada "Mungu Ameleta Utukufu Wake Mashariki"


Mungu Ameleta Utukufu Wake Mashariki


Mungu aliipa Israeli utukufu Wake kisha Akauhamisha mbali na pale,

na kuwaleta Waisraeli na kuwaleta watu wote Mashariki.

Mungu amewaelekeza wote kwenye mwanga

ili waweze kuungana tena na kuwa pamoja na mwanga,

wasilazimike kuutafuta tena, kuutafuta mwanga.