Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kidini-na-Haki. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kidini-na-Haki. Onyesha machapisho yote

7/12/2018

Kusudio na Umuhimu wa Kila Mojawapo ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Sura ya 3 Ukweli Kuhusu Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

3. Kusudio na Umuhimu wa Kila Mojawapo ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ambayo Yehova alifanya kwa Waisraeli ilianzisha mahali pa Mungu pa asili miongoni mwa binadamu, ambapo pia palikuwa pahali patakatifu ambapo Alikuwapo. Aliwekea kazi Yake mipaka kwa watu wa Israeli. Mwanzoni, Hakufanya kazi nje ya Israeli; badala yake, Aliwachagua watu Aliowaona kuwa wa kufaa ili kuzuia eneo la kazi Yake. Israeli ni mahali ambapo Mungu aliwaumba Adamu na Hawa, na kutoka katika mavumbi ya mahali hapo Yehova alimuumba mwanadamu; mahali hapa pakawa kituo cha kazi Yake duniani. Waisraeli, ambao walikuwa wa ukoo wa Nuhu na pia wa ukoo wa Adamu, walikuwa msingi wa kibinadamu wa kazi ya Yehova duniani.

12/08/2017

Swahili Christian Movie Trailer | "Nyendo za Mateso ya Kidini Nchini China"


Kanisa la Mwenyezi Mungu | Swahili Christian Movie Trailer | "Nyendo za Mateso ya Kidini Nchini China"

Tangu kilipokuja mamlakani katika China Bara mnamo mwaka wa 1949, Chama Cha Kikomunisti cha China kimekuwa hakikomi katika mateso yake kwa imani ya kidini. Kwa wayowayo kimewashika na kuwaua Wakristo, kuwafukuza na kuwadhulumu wamishonari wanaofanya kazi nchini China, wakachukua ngawira na kuchoma nakala nyingi za Biblia, wakafunga kabisa na kubomoa majengo ya kanisa, na bila mafanikio wakajaribu kukomesha makanisa yote ya nyumbani. Miaka ya hivi karibuni pia imeona sera za serikali ya CCP zikianzishwa kwa kiwango kikubwa kwa lengo la "Usimilishaji " wa Ukristo. Maelfu ya misalaba ya makanisa yamevunjwa, majengo mengi ya kanisa yambomolewa, na idadi kubwa ya Wakristo katika makanisa ya nyumbani wamekamatwa na kuteswa.