Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Yehova. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Yehova. Onyesha machapisho yote

4/14/2019

Kujua madhumuni na Umuhimu wa Kila Moja ya Hatua Tatu za Kazi ya Mungu

II. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Hatua Tatu za Kazi ya Wokovu wa Mungu kwa Wanadamu

2. Kujua madhumuni na Umuhimu wa Kila Moja ya Hatua Tatu za Kazi ya Mungu

(1) Lengo na umuhimu wa kazi ya Mungu katika Enzi ya Sheria
Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ambayo Yehova Alifanya kwa Waisraeli ilianzishwa miongoni mwa binadamu mahali pa asili pa Mungu hapa ulimwenguni, pahali patakatifu ambapo Alikuwepo. Hii kazi Aliiwekea mipaka miongoni mwa watu wa Israeli tu. Kwanza, hakufanya kazi nje ya Israeli;

3/30/2019

1.Kwa nini Mungu huitwa majina tofauti katika enzi tofauti? Ni nini umuhimu wa majina ya Mungu?

IV. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Hatua Tatu za Kazi ya Mungu na Majina Yake

1. Kwa nini Mungu huitwa majina tofauti katika enzi tofauti? Ni nini umuhimu wa majina ya Mungu?

Maneno Husika ya Mungu:
Unapaswa kujua kuwa Mungu mwanzoni hakuwa na jina. Yeye Alichukua tu jina moja, au majina mawili, ama majina mengi kwa sababu Alikuwa na kazi ya kufanya na Alikuwa na jukumu la kumsimamia mwanadamu.

12/27/2018

Ni jinsi gani Mungu anayepata mwili ili kufanya kazi ya hukumu huimaliza imani ya wanadamu katika Mungu asiye yakini na enzi ya giza ya utawala wa Shetani?

Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Kupata Mwili kwa Mungu

9. Ni jinsi gani Mungu anayepata mwili ili kufanya kazi ya hukumu huimaliza imani ya wanadamu katika Mungu asiye yakini na enzi ya giza ya utawala wa Shetani?

Aya za Biblia za Kurejelea:
"Na itatimia katika siku za mwisho, kwamba mlima wa nyumba ya Yehova utawekwa imara juu ya milima, na utainuliwa juu zaidi ya vilima; na mataifa yote yatamiminika kwenda kwake. Na watu wengi wataenda na kusema, Njoo, na hebu twende juu ya mlima wa Yehova, kwa nyumba ya Mungu wa Yakobo;

11/15/2018

Swahili Christian Movie "Kutamani Sana" (3) - Nani Atanyakuliwa Kwanza Wakati Bwana Atakaporudi?

Wengi wa wale wanaomsadiki Bwana wanasadiki kwamba mradi tu wajitolee, wajitumie, na kutia bidii, bila shaka watakuwa miongoni mwa wale wa kwanza kunyakuliwa. Lakini je, kuna msingi wowote wa haya katika maneno ya Bwana? Bwana Yesu alisema, "But many that are first shall be last; and the last shall be first" (Mathayo 19:30). "Kondoo wangu huisikia sauti yangu" (Yohana 10:27). Ni wazi kwamba kama mtu anaweza kunyakuliwa au la kunaamuliwa na kama ataisikia sauti ya Bwana. Wale wanaoisikia kwanza sauti Yake na kukubali kuonekana Kwake na kazi ni wanawali wenye hekima, na watakuwa wa kwanza kunyakuliwa.

9/11/2018

"Jina la Mungu Limebadilika?!" (3) - Umuhimu wa Jina la Mungu💗😇


"Yehova" na "Yesu" yalikuwa ni majina ya Mungu katika Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema, na imetabiriwa katika Ufunuo kuwa Mungu atakuwa na jina jipya katika siku za mwisho. Ni kwa nini Mungu anaitwa kwa majina tofauti katika enzi mbalimbali? Majina haya mawili ya "Yehova" na "Yesu" yana umuhimu gani? Video hii fupi itakusaidia kukutatulia fumbo hili.

Yaliyopendekezwa : Umeme wa Mashariki Hutoka wapi? Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu

8/12/2018

Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili

Sura ya 5 Ukweli Kuhusu Mungu Kupata Mwili

5. Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili

Maneno Husika ya Mungu:
Kupata mwili mara ya kwanza kulikuwa kumkomboa mwanadamu kutoka katika dhambi kupitia mwili wa Yesu, hivyo, Aliokoa mwanadamu kutoka kwa msalaba, lakini tabia potovu ya kishetani ilibaki ndani ya mwanadamu. Kupata mwili mara ya pili si kwa ajili ya kuhudumu tena kama sadaka ya dhambi ila ni kuwaokoa kamilifu wale waliokombolewa kutoka kwa dhambi. Hii inafanyika ili wale waliosamehewa wakombolewe kutoka kwa dhambi zao, na kufanywa safi kabisa, na kupata mabadiliko ya tabia, hivyo kujikwamua kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza na kurudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu. Hivyo tu ndivyo mwanadamu ataweza kutakaswa kikamilifu. Mungu Alianza kazi ya wokovu katika Enzi ya Neema baada ya Enzi ya Sheria kufika mwisho.

7/15/2018

Trela ya Filamu ya Kikristo "Yule Anayeshikilia Ukuu Juu ya Kila Kitu" | Kutoa Sheria🎬👏



🎉🎉🎉🎉🎉🎉**********🎊🎊🎊🎊→→*******👏👏👏


Amri na sheria ambazo Yehova Mungu aliwapa Waisraeli hazijakuwa na athari kubwa sana kwa sheria ya binadamu tu, lakini pia zimetekeleza jukumu muhimu katika kuanzishwa na utengenezwaji wa ustaarabu wa kimaadili na taasisi za kidemokrasia katika jamii za binadamu. Filamu ya Kikristo ya muziki—Yule Anayeshikilia Ukuu Juu ya Kila Kitu—hivi karibuni itaonyesha ukweli wa kihistoria!

Sikiliza zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, Chanzo cha Mafanikio ya Umeme wa Mashariki 

7/08/2018

Kwa Nini Mungu Anaitwa kwa Majina Tofauti katika Enzi Tofauti?

Sura ya 2 Ukweli wa Majina ya Mungu

2. Kwa Nini Mungu Anaitwa kwa Majina Tofauti katika Enzi Tofauti?

Maneno Husika ya Mungu:
Katika kila enzi, Mungu Anafanya kazi mpya na huitwa kwa jina jipya; Je, anawezaje kufanya kazi sawa katika enzi tofauti? Itakuwaje Yeye kugandamana na yale ya zamani? Jina la Yesu lilichukuliwa kuwa la kazi ya ukombozi, hivyo bado Yeye Anaweza kuitwa kwa jina moja wakati Atarudi katika siku za mwisho? Je, bado Yeye Atafanya kazi ya ukombozi? Ni kwa nini Yehova na Yesu ni kitu kimoja, ilhali wanaitwa kwa majina tofauti katika enzi hizi tofauti? Je, si kwa sababu enzi za kazi Yao ni tofauti? Jina moja linawezaje kumwakilisha Mungu kwa ukamilifu wake?

7/02/2018

Mwenyezi Mungu Ndiye Bwana Yesu Aliyerudi

Sura ya 1 Mwenyezi Mungu Ndiye Mungu Mmoja wa Kweli Ambaye Aliumba Kila kitu

2. Mwenyezi Mungu Ndiye Bwana Yesu Aliyerudi

Maneno Husika ya Mungu:
Baada ya kazi ya Yehova, Yesu Alipata mwili ili Afanye kazi Yake miongoni mwa wanadamu. Kazi Yake haikutekelezwa kivyake, ila ilijengwa juu ya misingi ya kazi ya Yehova. Ilikuwa kazi ya enzi mpya baada ya Mungu kukamilisha Enzi ya Sheria. Vivyo hivyo, baada ya kazi ya Yesu kukamilika, Mungu bado Aliendeleza kazi Yake ya enzi iliyofuata, kwa sababu usimamizi wote wa Mungu huendelea mbele siku zote. Enzi nzee ikipita, itabadilishwa na enzi mpya, na mara tu kazi nzee imekamilika, kazi mpya itaendeleza usimamizi wa Mungu. Kupata mwili huku ni kupata mwili kwa Mungu mara ya pili kufuatia kukamilika kwa kazi ya Yesu.

5/29/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Fumbo la Kupata Mwili (4)

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Fumbo la Kupata Mwili

    Mnapaswa kujua kuhusu hadithi ya ndani na uumbaji wa Biblia. Ufahamu huu haushikiliwi na wale ambao hawajakubali kazi mpya ya Mungu. Wao hawajui. Waelezee mambo haya ya kiini, na hawatakuwa pamoja nawe wenye kushikilia sana elimu ya vitabuni na sheria kuhusu Biblia. Wao huchunguza kwa uthabiti kile ambacho kimetabiriwa: Kauli hii imeshatimia? Kauli ile imeshatimia? Kukubali kwao injili ni kwa mujibu wa Biblia;

5/14/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Asili na Utambulisho wa Mwanadamu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Asili na Utambulisho wa Mwanadamu

Kwa kweli, hawajasikitika, na wamekuwa wakitazama kile ambacho kimefanywa kwa miaka elfu sita iliyopita mpaka leo, kwa kuwa Sikuwaacha. Badala yake, kwa sababu mababu zao walikula tunda kutoka kwa mti wa ujuzi wa mema na maovu lililotolewa na yule mwovu, waliniacha kwa ajili ya dhambi. Mema ni Yangu, wakati maovu ni ya yule mwovu ambaye hunihadaa kwa ajili ya dhambi. Mimi Siwalaumu mwanadamu, wala Siwaangamizi kwa ukatili au kuwatolea kuadibu kusiko na huruma, kwani uovu haukuwa wa wanadamu kiasili.

5/13/2018

Matamshi ya Mungu | Majani Yaangukayo Yatakaporudi kwa Mizizi Yake Utajuta Maovu Yote Ambayo Umefanya

Mwenyezi Mungu alisema, Nyote mmeshuhudia wenyewe kazi ambayo Nimefanya miongoni mwenu, ninyi wenyewe mmesikia maneno ambayo Nimenena, nanyi mnajua mtazamo Wangu kuelekea kwenu, kwa hiyo mnapaswa kujua kwa nini Ninafanya kazi hii miongoni mwenu. Nitawaambia ukweli—ninyi ni vifaa tu vya kazi Yangu ya ushindi katika siku za mwisho; ninyi ni vyombo vya kupanua kazi Yangu miongoni mwa nchi za Mataifa. Mimi huzungumza kupitia kwa udhalimu wenu, uchafu wenu, upinzani na uasi wenu ili kupanua bora zaidi kazi Yangu ili jina Langu lienee miongoni mwa nchi za Mataifa, yaani, kuenea miongoni mwa nchi yoyote nje ya Israeli.

5/12/2018

Umeme wa Mashariki | Umuhimu wa Kuukoa Uzao wa Moabu

Umeme wa Mashariki | Umuhimu wa Kuukoa Uzao wa Moabu

    Mwenyezi Mungu alisema, Katika miaka hii miwili hadi mitatu ya kazi, kile kilichopaswa kutimizwa katika kazi ya hukumu iliyofanyika juu yenu kimetimizwa kimsingi. Watu wengi wamesahau matarajio na kudura yao ya baadaye. Hata hivyo, inapotajwa kuwa ninyi ni uzao wa Moabu, wengi wenu huchukizwa sana—nyuso zenu hubadilika, vinywa vyenu hupinda, na macho yenu hukodolea. Hamuwezi kabisa kuamini kwamba ninyi ni uzao wa Moabu. Moabu ilifukuzwa hadi nchi hii baada ya kulaaniwa. Ukoo wa wana wa Moabu umerithishwa mpaka leo, na ninyi nyote ni uzao wake. Hakuna kitu ambacho Ninaweza kufanya—nani aliyekusababisha uzaliwe katika nyumba ya Moabu? Ninakuhurumia na Siko radhi uwe hivi, lakini ukweli hauwezi kubadilishwa na watu.

5/11/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ufahamu wako wa “Baraka” ni Upi

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ufahamu wako wa “Baraka” ni Upi

Ingawa wale waliozaliwa katika enzi hii wametiishwa chini ya upotovu wa Shetani na mapepo wachafu sana, pia ni kweli kwamba wanaweza kupata wokovu mkuu kutokana na upotovu huu, hata mkubwa kuliko mifugo wanaotanda milima na tambarare na mali nyingi ya familia ambayo Ayubu alipata, na pia ni zaidi ya baraka ambayo Ayubu alipokea ya kumwona Yehova baada ya majaribu yake. Ilikuwa tu baada ya Ayubu kupitia jaribio la kifo ndipo angeweza kuyasikia maneno ya Yehova na angeweza kusikia sauti Yake ya mshindo kutoka mawinguni. Hata hivyo, hakuuona uso wa Yehova na hakujua tabia Yake. Kile Ayubu alipata kilikuwa tu mali ya kimwili ambayo hutoa furaha za mwili na watoto wazuri mno katika miji jirani pamoja na ulinzi kutoka kwa malaika wa mbinguni.

4/30/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Fumbo la Kupata Mwili (3)

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Fumbo la Kupata Mwili (3)

    Wakati ambapo Mungu huitekeleza kazi Yake, Yeye haji kujishughulisha katika ujenzi wowote au mabadiliko; Yeye huja kutimiza huduma Yake. Kila wakati Anapopata mwili, ni kwa ajili tu ya kufanikisha hatua ya kazi na kuifungua enzi mpya. Sasa ni Enzi ya Ufalme, na mwanadamu ameingia katika zoezi la ufalme. Hatua hii ya kazi si kazi ya mwanadamu au ya kumfanya mwanadamu mkamilifu kwa kiasi fulani; ni kuimaliza sehemu ya kazi ya Mungu. Kazi Yake si kazi ya mwanadamu na si kumfanya mwanadamu mkamilifu kwa kiasi fulani kabla ya kuondoka duniani; ni kutimiza huduma Yake kwa ukamilifu na kuimaliza kazi ambayo Anapaswa kuifanya, ambayo ni kutengeneza mipango ya kufaa ya kazi Yake duniani, na hivyo kupata kutukuka.

3/28/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kuhusu Majina na Utambulisho

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Yesu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kuhusu Majina na Utambulisho

    Iwapo unataka kufaa kwa ajili ya matumizi na Mungu, lazima uijue kazi ya Mungu; lazima uijue kazi Aliyofanya awali (katika Agano Jipya na la Kale), na, zaidi ya hayo, lazima uijue kazi Yake ya leo. Ndiyo kusema, ni lazima uzitambue hatua tatu za kazi ya Mungu ya zaidi ya miaka 6,000. Ukiulizwa ueneze injili, basi hutaweza kufanya hivyo bila kuijua kazi ya Mungu. Watu watakuuliza yote kuhusu Biblia, na Agano la Kale, na nini Yesu alisema na kufanya wakati huo. Watasema, “Mungu wenu hajawaeleza haya yote? Kama Yeye (Mungu) hawezi kuwaeleza ni nini hasa yanayoendelea kwa Biblia, basi Yeye si Mungu;kama Anaweza, basi tumeamini,” Mwanzoni, Yesu alizungumzia sana Agano la Kale na wanafunzi Wake. Kila kitu walichosoma kilitoka Agano la Kale;

3/19/2018

Uchaguzi Kutoka kwa Vifungu Vitatu vya Neno la Mungu juu ya “Maono ya Kazi ya Mungu”

1. Yohana alianza kueneza injili ya ufalme wa mbinguni miaka saba kabla ya ubatizo wa Yesu. Kwa watu, kazi aliyoifanya ilionekana kuwa juu zaidi ya kazi ya baadaye ya Yesu, ilhali yeye alikuwa, hata hivyo, nabii tu. Hakufanya kazi au kuzungumza ndani ya hekalu, lakini katika miji na vijiji nje yake. Hii alifanya, bila shaka, miongoni mwa taifa la Wayahudi, hasa wale waliokuwa maskini. Ni mara chache ambapo Yohana alitangamana na watu kutoka ngazi za juu za jamii, na alieneza injili miongoni mwa watu wa kawaida wa Yudea tu ili kuandaa watu wema kwa Bwana Yesu, na kuandaa maeneo yafaayo Kwake kufanya kazi.

3/13/2018

📖🤲🙂Watu Waliochaguliwa Nchini China Hawawezi Kuwakilisha Kabila Lolote la Israeli

Mwenyezi Mungu alisema, Nyumba ya Daudi ilipokea ahadi ya Bwana, na ilikuwa ni familia iliyopokea urithi wa Yehova. Ilikuwa kwa asili moja ya makabila ya Israeli na ilikuwa ya watu waliochaguliwa. Wakati huo, Yehova aliamuru sheria iwepo kwa Wana wa Israeli kuwa Wayahudi wote waliokuwa wa nyumba ya Daudi, wale wote waliozaliwa katika nyumba hiyo wangepokea urithi Wake. Wangepokea sehemu mia kwa moja na kupata hadhi ya wana wa kiume wazaliwa wa kwanza. Wakati huo, wao ndio waliokuwa wameinuliwa zaidi miongoni mwa Waisraeli wote—walikuwa na cheo cha juu zaidi miongoni mwa familia zote za Israeli, na walimhudumia Yehova hekaluni moja kwa moja, kama wamevaa kanzu za ukuhani na mataji.

2/19/2018

Mwanadamu Anaweza Kuokolewa Tu Katikati ya Usimamizi wa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Kila mtu anahisi kuwa usimamizi wa Mungu ni wa ajabu, kwa sababu watu wanafikiri kuwa usimamizi wa Mungu hauna uhusiano wowote na mwanadamu. Wanafikiri kuwa usimamizi wa Mungu ni kazi ya Mungu pekee, shughuli za Mungu, na hivyo wanadamu hawajali kuhusu usimamizi wa Mungu. Kwa njia hii, kuokolewa kwa wanadamu kumekuwa kusiko yakini na kusiko dhahiri, na kumebaki tu maneno matupu. Hata kama mwanadamu anamfuata Mungu ili aokolewe na aingie katika hatima inayopendeza, mwanadamu hajishughulishi na jinsi ambavyo Mungu Hutekeleza kazi Yake. Mwanadamu hashughulishwi na Anachokipanga Mungu na anachopaswa kufanya ili aokolewe.

2/05/2018

Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (3)

Mwenyezi Mungu alisema, Matokeo ya kutimizwa kutoka kwa kazi ya kushinda kimsingi ni kwa ajili ya mwili wa mwanadamu kuacha kuasi, yaani, ili fikira za mwanadamu zipate ufahamu mpya wa Mungu, moyo wake umtii Mungu kabisa, na aamue kuwa wa Mungu. Jinsi ambavyo mwenendo wa mtu ama mwili wake unavyobadilika haiamui ikiwa ameshindwa. Badala yake, ni wakati ambapo fikira zako, utambuzi wako, na ufahamu wako unabadilika—yaani, ni wakati mielekeo yako yote ya kifikira inabadilika—ndipo huwa umeshindwa na Mungu. Ukiamua kutii na kupata fikira mpya, pale ambapo huingizi mawazo na nia zako katika maneno na kazi ya Mungu, na wakati ubongo wako unaweza kufikiri kwa njia ya kawaida, yaani, unapoweza kujitolea kwa Mungu kwa moyo wako wote—huyu ni mtu aliyeshindwa kabisa.