Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ufahamu wako wa “Baraka” ni Upi
Ingawa wale waliozaliwa katika enzi hii wametiishwa chini ya upotovu wa Shetani na mapepo wachafu sana, pia ni kweli kwamba wanaweza kupata wokovu mkuu kutokana na upotovu huu, hata mkubwa kuliko mifugo wanaotanda milima na tambarare na mali nyingi ya familia ambayo Ayubu alipata, na pia ni zaidi ya baraka ambayo Ayubu alipokea ya kumwona Yehova baada ya majaribu yake. Ilikuwa tu baada ya Ayubu kupitia jaribio la kifo ndipo angeweza kuyasikia maneno ya Yehova na angeweza kusikia sauti Yake ya mshindo kutoka mawinguni. Hata hivyo, hakuuona uso wa Yehova na hakujua tabia Yake. Kile Ayubu alipata kilikuwa tu mali ya kimwili ambayo hutoa furaha za mwili na watoto wazuri mno katika miji jirani pamoja na ulinzi kutoka kwa malaika wa mbinguni.
Hakuwahi kumwona Yehova, na hata ingawa aliitwa mwenye haki, kamwe hakuijua tabia ya Yehova. Ingawa watu wa leo ni maskini kwa muda katika starehe za kimwili au wanapitia mazingira ya nje ya uhasama, Nimedhihirisha tabia Yangu ambayo Sikuwahi kuifunua kwa wanadamu katika vizazi vilivyopita, ambayo siku zote imekuwa siri, na miujiza Yangu kabla ya enzi kwa watu duni mno ambao pia Nimewapa wokovu mkuu, na hii ni mara ya kwanza ambayo Nimefanya hivyo. Sijawahi kufanya aina ya hii awali, na ingawa ninyi mko chini zaidi kuliko Ayubu, yale mmepata na yale mmeona yamemshinda Ayubu kwa mbali. Ingawa mmepitia kila aina ya mateso na maudhi, mateso hayo si kama majaribu ya Ayubu, lakini ni hukumu na kuadibu ambako watu wamepokea kwa sababu ya uasi na ukinzani wao, na kwa sababu ya tabia Yangu yenye haki. Ni hukumu yenye haki, kuadibu, na laana. Ayubu alikuwa mmoja wa Waisraeli, mmoja wa watu wenye haki aliyepokea upendo na rehema ya ajabu ya Yehova. Hakufanya vitendo viovu na hakumpinga Yehova; badala yake, alijitoa kwa Yehova kwa uaminifu, naye alitiishwa chini ya majaribu kwa sababu ya haki yake, na alipitia majaribu makali kwa sababu alikuwa mtumishi mwaminifu wa Yehova. Watu leo wako chini ya hukumu na laana Yangu kwa sababu ya uchafu na uovu wao. Ingawa mateso yao hayalingani kabisa na kile Ayubu alipitia wakati alipoteza mifugo wake, mali yake, watumishi wake, watoto wake, na wale walio wapendwa kwake wote, kile watu wanapitia ni usafishaji na uteketezaji mkali; kilicho kikubwa zaidi kuliko kile Ayubu alipitia ni kwamba aina hii ya jaribio haipunguzwi wala kuondolewa kwa sababu ya udhaifu wao, badala yake, ni ya muda mrefu hadi siku yao ya mwisho ya maisha. Hii ni adhabu, hukumu, laana—ni ya kuteketea bila huruma, na hata zaidi ni “urithi” wa wanadamu wa haki. Ni kile wanachostahili, na ni mahali pa maonyesho ya tabia Yangu yenye haki. Ni ukweli unaojulikana. Lakini yale watu wamepata yanapita sana yale wamevumilia sasa. Yale ambayo mmepitia ni vipingamizi tu kutokana na upumbavu, lakini mapato yenu ni mara mia zaidi ya mateso yenu. Kwa mujibu wa sheria za Israeli katika Agano la Kale, wale wote wanaonipinga Mimi, wale wote wanaonihukumu waziwazi, na wale wote wasioifuata njia Yangu lakini wanatoa sadaka zenye kukufuru Kwangu kwa ujasiri kwa hakika wataharibiwa kwa moto katika hekalu, au baadhi ya watu waliochaguliwa watawatupia mawe hadi kifo, na hata vizazi vyao vya nyumba yao wenyewe na jamaa zao wengine wa karibu watapitia laana Yangu, na katika dunia ijayo hawatakuwa huru, lakini watakuwa watumwa wa watumwa Wangu, Nami nitawaelekeza hadi uhamishoni miongoni mwa Mataifa nao hawataweza kurudi katika nchi yao. Kulingana na vitendo vyao, tabia zao, mateso yanayovumiliwa na watu leo si makubwa kama adhabu waliyopitia Waisraeli. Kusema kuwa kile mnachopitia sasa ni adhabu si bila sababu, na hii ni kwa sababu mmevuka mpaka kweli, na kama mngekuwa katika Israeli mngekuwa mmoja wa wenye dhambi milele na mngekatwa vipande vipande na Waisraeli muda mrefu uliopita na pia mngeteketezwa kwa moto kutoka mbinguni katika hekalu la Yehova. Na nini ambacho mmepata sasa? Nini ambacho mmepokea, nini ambacho mmefurahia? Nimedhihirisha tabia Yangu yenye haki ndani yenu, lakini muhimu zaidi ni kwamba Nimefunua uvumilivu Wangu kwa ukombozi wa mwanadamu. Mtu angesema kwamba yote ambayo Nimefanya ndani yenu ni kazi na uvumilivu, kwamba ni kwa ajili ya usimamizi Wangu, na hata zaidi ni kwa ajili ya starehe ya wanadamu.
Ingawa Ayubu alipitia majaribu kutoka kwa Yehova, alikuwa tu mtu mwenye haki aliyemwabudu Yehova, na hata alipokuwa akipitia majaribu hayo hakulalamika kumhusu Yeye, lakini alithamini sana kukutana kwake na Yehova. Watu wa leo hawathamini tu uwepo wa Yehova, bali humkataa, humchukia sana, hulalamika kumhusu, na hudhihaki uwepo Wake. Je, hamjapata zaidi ya kidogo? Je, mateso yenu kweli hayajakuwa makubwa sana? Je, baraka zenu hazijakuwa nyingi kuliko zile za Maria na Yakobo? Je, upinzani wenu haujakuwa hafifu? Inawezekana kuwa yale Nimehitaji kwenu, yale Nimeuliza kutoka kwenu yamekuwa makuu mno na mengi sana? Ghadhabu Yangu iliachiliwa huru tu juu ya wale Waisraeli walionipinga Mimi, si moja kwa moja juu yenu, lakini kile ambacho mmepata kimekuwa tu hukumu Yangu isiyo na huruma na mafichuzi pamoja na utakaso mkali usio na huruma. Licha ya haya watu bado wananipinga na kunikana Mimi bila hata chembe ya utii. Na hata kuna baadhi ya watu ambao hujitenga na Mimi na kunikataa; aina hiyo ya mtu si bora zaidi kuliko bendi ya Kora na Dathani wakimpinga Musa. Mioyo ya watu imekuwa migumu sana, na asili zao ni kaidi sana. Kamwe hawatabadili mienendo yao ya zamani. Wamejiweka wazi kama kahaba hadharani kwa matamshi Yangu, na maneno Yangu ni makali sana kwamba “hayana adabu”, yakiweka wazi asili za watu hadharani. Lakini watu huamkia tu kwa vichwa vyao, wanamwaga machozi machache, na kuwa na hisia za kusikitisha kidogo tu. Mara tu inapoisha, ni wakali kama mfalme wa wanyama wa pori katika milima na hawana utambuzi kabisa. Je, watu na aina hii ya tabia wanawezaje kujua kwamba wamefurahia baraka zaidi ya mara mia kuliko zile za Ayubu? Wanawezaje kugundua kwamba kile wanachokifurahia ni baraka ambazo zimeonekana katika enzi zote kwa nadra sana, ambazo hakuna mtu aliyewahi kuzifurahia awali? Dhamiri za watu zinawezaje kuhisi aina hii ya baraka ambayo hubeba adhabu? Kusema ukweli, chote Ninachohitaji kwenu ni ili muweze kuwa mifano kwa kazi Yangu na kuwa mashahidi kwa ajili ya tabia Yangu yote na matendo Yangu yote, na ili muweze kuwekwa huru kutokana na mateso ya Shetani. Lakini wanadamu daima huchukizwa na kazi Yangu na wanakuwa na uhasama kwake kimakusudi. Aina hiyo ya mtu anawezaje kutonichochea Mimi kurejesha sheria za Israeli na kuleta juu yake ghadhabu Yangu kwa ajili ya Israeli? Ingawa kuna wengi miongoni mwenu ambao ni “watiifu” Kwangu, kuna hata zaidi ambao wa namna ya “bendi ya Kora” Mara tu Nitakapoupata utukufu Wangu kamili, Nitachukua moto kutoka mbinguni na kuwateketeza hadi wawe majivu. Mnapaswa kujua kwamba Sitawaadibu watu kwa maneno Yangu tena, lakini kabla ya kuifanya kazi ya Israel, Nitaiteketeza kabisa ile namna ya “bendi ya Kora” wanaonipinga Mimi na ambao Nimewaondoa muda mrefu uliopita. Wanadamu hawatapata tena nafasi ya kunifurahia, lakini yote ambayo wataona yatakuwa ghadhabu na “moto” Wangu kutoka mbinguni. Nitafichua matokeo ya watu wote, na Nitawagawanya watu wote katika makundi mbalimbali. Nitaangalia kila tendo lao lenye uasi, na kisha kuimaliza kazi Yangu, ili matokeo ya watu yataamuliwa kulingana na uamuzi Wangu wakati wako duniani pamoja na mitazamo yao kunihusu. Wakati huo utakapofika, hakutakuwa na kitu kitakachoweza kubadilisha matokeo yao. Acha watu wafunue matokeo yao wenyewe! Acha Niyakabidhi matokeo ya watu kwa Baba wa mbinguni.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Kuhusu Sisi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni