Baada ya Liang Zhi kumwamini Mungu, bila kukoma alitafuta kwa shauku, na kujitosa katika kutimiza wajibu wake. Baada ya miaka kadhaa, alichaguliwa kama kiongozi wa kanisa. Wakati alipokuwa akitekeleza wajibu wake kama kiongozi wa kanisa, aligundua kwamba baadhi ya ndugu walikuwa na uwezo zaidi kumliko, ambayo ilimfanya asiwe na furaha kwa kiasi kwamba alikuwa na wivu kwao. Ili kuokoa uso na kulinda hali yake, alishindana nao kwa siri ili kuona ni nani aliyekuwa bora, na alikimbilia umaarufu na hadhi. Umaarufu na hadhi vilionekana kama pingu zisizoonekana zilizomfunga sana, kumnyima uhuru, kumsababisha afanye mambo kinyume na ukweli na kupinga Mungu.
Chen Dan Mkoa wa Hunan
Mwishoni mwa mwaka jana, kwa sababu sikuweza kuzindua kazi ya injili katika eneo langu, familia ya Mungu ilimhamisha ndugu mmoja wa kiume kutoka eneo jingine ili kuchukua kazi yangu. Kabla ya haya sikuwa nimearifiwa, bali nilisikia kwa njia isiyo ya moja kwa moja kutoka kwa dada mmoja niliyekuwa mbia naye. Nilifadhaika sana. Nilishuku kwamba mtu aliyekuwa madarakani hakuwa ameniarifu kwa kuhofia kwamba singekubali kuiacha nafasi yangu na ningeshindana.