9/30/2017

Je, Kazi ya Mungu ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania?

Umeme wa Mashariki | Je, Kazi ya Mungu ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania?
Umeme wa Mashariki | Je, Kazi ya Mungu ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania?
Kama mtu anayemwamini Mungu, inakupasa kuelewa kuwa, leo, katika kupokea kazi ya Mungu nyakati za mwisho na kazi yote ya mpango wa Mungu ndani yako, umepokea utukufu mkuu na wokovu wa Mungu kabisa. Kazi yote ya Mungu ulimwengu mzima imelenga watu wa kikundi hiki. Amejitolea kwa nguvu Zake zote na kutoa vyote kwa ajili yako; Amekurejesha na kukupa kazi yote ya Roho ulimwenguni kote. Ndiyo sababu Nasema kuwa wewe una bahati. Zaidi ya hayo, Amehamisha utukufu wake kutoka kwa Israeli, watu wake wateule, hadi kwako, ili kufanya kusudio lake lijidhihirishe kwenu kama kundi. Kwa hiyo, ninyi ndinyi mtakaopokea urithi wa Mungu, na hata zaidi warithi wa utukufu wa Mungu. Pengine utayakumbuka maneno haya: “Kwa kuwa huzuni yetu nyepesi, ambayo ni ya muda mdogo pekee, inatufanyia utukufu mkubwa na wa daima ambao unazidi kuwa mkuu kabisa.”

9/27/2017

Umeme wa Mashariki | Juu ya Hatua za Kazi ya Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu
Kutoka nje, inaonekana kwamba hatua za kazi ya Mungu katika kipindi hiki tayari zimemalizwa, na kwamba wanadamu tayari wamepitia hukumu, kuadibu, kuangamizwa, na usafishaji wa maneno Yake, na kwamba wamepitia hatua kama vile jaribio la watendaji huduma, kusafisha kwa nyakati za kuadibu, jaribio la kifo, jaribio la foili[b], na nyakati za[a]kumpenda Mungu. Ingawa watu wamepitia mateso makubwa katika kila hatua bado hawajaelewa mapenzi ya Mungu. Kama tu jaribio la watendaji huduma, kile ambacho watu walipata kutoka kwa hilo, kile walichoelewa kutoka hilo, na matokeo gani Mungu alitaka kutimiza kupitia kwa hilo—watu bado hawaelewi kuhusu masuala haya. Inaonekana kutokana na mwendo wa kazi ya Mungu, kwamba kulingana na kiasi cha sasa watu bila shaka hawawezi kuendelea.

9/26/2017

Ishini Katika Upendo wa Mungu | "Wimbo wa Mapenzi Matamu" | Best Swahili Christian Worship Song


Wimbo wa Mapenzi Matamu

Kinani mwa moyo wangu, ni mapenzi Yako. Ni matamu sana, nakaa karibu yako.

Kukutunza hukoleza moyo wangu; kukutumikia na mawazo yangu yote.

Kuongoza moyo wangu, ni mapenzi Yako; mimi hufuata nyayo zako za mapenzi.

Mimi hujisogeza kulingana na macho Yako; mapenzi yanaonyesha furaha ya moyo wangu.

Mapenzi yanaonyesha furaha ya moyo wangu.


Sasa mimi huishi katika ulimwengu mwingine, hakuna yeyote isipokuwa wewe uko nami.

Unanipenda, ninakupenda; hakuna huzuni wala sikitiko hutusumbua.

Umeme wa Mashariki | Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Mustakabali?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu
      Je, unaweza kuonyesha tabia ya Mungu ya nyakati kwa lugha inayofaa iliyo na umuhimu wa nyakati? Kupitia uzoefu wako wa kazi ya Mungu, unaweza kueleza kwa undani tabia ya Mungu? Utaielezaje vizuri, kikamilifu? Ili kupitia haya, watu wengine wapate kufahamu uzoefu wako. Utawezaje kupitisha uliyoyaona na kupitia kwa maskini hawa wa kuhurumiwa, na waumini wa kidini wa kumcha Mungu waliojitolea na waliojawa na njaa na kiu cha haki na wanaongoja uwe mchungaji wao? Ni watu wa aina gani ndio wanangoja uwe mchungaji wao? Unaweza kuwaza kweli? Je, unajua mzigo ulio begani mwako, kazi yako na majukumu yako? Hisia yako ya kihistoria ya mwito iko wapi? Utahudumu vipi kama kiongozi mzuri wa wakati unaofuata? Je, unao hisia nzuri wa uongozi? Utaeleza mkuu wa kila kitu kama nini?

9/24/2017

Umeme wa Mashariki | Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili

Umeme wa Mashariki | Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili
Umeme wa Mashariki | Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili

    Kila hatua ya kazi iliyofanywa na Mungu ina umuhimu wake mkubwa. 
Yesu alipokuja zamani, Alikuwa mwanaume, lakini Mungu anapokuja wakati huu Yeye ni mwanamke. Kutokana na hili, unaweza kuona kwamba Mungu aliwaumba mwanaume na mwanamke kwa ajili ya kazi Yake na Kwake hakuna tofauti ya jinsia. Roho Wake anapowasili, Anaweza kuchukua mwili wowote kwa matakwa Yake na mwili huo unaweza kumwakilisha Yeye. Uwe wa kiume au kike, unaweza kumwakilisha Mungu alimradi tu ni mwili Wake wa nyama. Kama Yesu angeonekana kama kike alipokuja, kwa maneno mengine, iwapo mtoto wa kike, sio wa kiume, angezaliwa kwa njia ya Roho Mtakatifu, hatua hiyo ya kazi ingekuwa imekamilika pia.

Umeme wa Mashariki | Nitampenda Mungu Maisha Yangu Yote | "Mpendwa Wangu, Tafadhali Nisubiri" (Video Rasmi ya Muziki)


Mpendwa Wangu, Tafadhali Nisubiri

Juu ya miti, nikiukwea mwezi wa amani. Kama mpendwa wangu, wa haki na mzuri.

Ee mpendwa wangu, Uko wapi? Sasa mimi nina machozi. Je, Wanisikia nikilia?

Wewe Ndiwe hunipa upendo. Wewe Ndiwe Unayenitunza.

Wewe Ndiwe unayeniwaza daima, Wewe Ndiwe unayeyatunza maisha yangu.

Mwezi, nyuma ya upande wa pili wa anga. Usimfanye mpendwa wangu asubiri muda mrefu sana.

9/23/2017

Umeme wa Mashariki | Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Injili
Mwanadamu anaelewa sehemu ndogo ya kazi ya leo na kazi ya baadaye, lakini hafahamu hatima ambapo mwanadamu ataingia. Kama kiumbe, mwanadamu anapaswa kutekeleza wajibu wa kiumbe: Mwanadamu anapaswa kumfuata Mungu kwa lolote afanyalo, na mnapaswa muendelee mbele kwa njia yoyote ambayo Nitawaambia. Wewe huna mbinu ya kufanya mipango yako mwenyewe, na huna uwezo wa kujitawala mwenyewe; yote ni lazima yaachwe kwa rehema za Mungu, na kila kitu kinadhibitiwa na mikono Yake.

Umeme wa Mashariki | Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Injili
Mwanzoni, Mungu alikuwa anapumzika. Hakukuwa na binadamu ama kitu chochote kingine duniani wakati huo, na Mungu hakuwa amefanya kazi yoyote ile. Mungu alianza tu kazi Yake ya usimamizi baada ya binadamu kuwepo na baada ya binadamu kupotoshwa. Kutoka hapa kuendelea, Mungu hakupumzika tena lakini badala yake Alianza kufanya kazi miongoni mwa binadamu. Ilikuwa kwa sababu ya upotovu wa binadamu ndipo Mungu alichukuliwa kutoka kwa pumziko Lake, na ilikuwa pia kwa sababu ya uasi wa malaika mkuu ndipo Mungu alichukuliwa kutoka kwa pumziko Lake.

9/22/2017

Umeme wa Mashariki | Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"


Yasifu Maisha Mapya

Haleluya! Twakushukuru na kukusifu Wewe!

Haleluya! Twakushukuru na kukusifu Wewe, Mwenyezi Mungu!

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu.

Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Ni neno la Mungu ambalo limenibadilisha,

kwa hivyo nina maisha mapya ya kumsifu Mungu. (Halleluya!)

9/20/2017

Tafuteni Maana ya Maisha - "Kwa Ajili ya Nani Mtu Aishi" (Video Rasmi ya Muziki)


Kwa Ajili ya Nani Mtu Aishi


I

Haikuwa wazi ni kwa ajili ya nani mtu anapaswa kuishi. Sasa nina jibu kwa hilo.

Nilikuwa naishi tu kwa ajili yangu mwenyewe, kutafuta hadhi tu na umaarufu.

Maombi kwa Mungu yaliyojaa maneno mema, lakini nikishikilia njia zangu mwenyewe katika maisha halisi.

Imani juu ya msingi wa kesho na majaliwa, sina ukweli au uhalisi.

Mila na sheria, zikifungia imani yangu; sikubaki na kitu ila utupu.

Kushindwa kuishi kama binadamu, sistahili upendo wa Mungu kwa ajili yangu.

9/19/2017

Umeme wa Mashariki | Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu kwa ajili ya Wokovu wa Mwanadamu

Kwa mwanadamu, haiwezekani kwa wana wa Moabu kuwa wakamilifu na hawajahitimu kufanywa hivyo. Wana wa Daudi, kwa upande mwingine, hakika wana matumaini na hakika wanaweza kufanywa kamili. Kwa sharti kwamba mtu ni mzawa wa Moabu, basi hawezi kufanywa kamili. Hata leo, bado hamjui umuhimu wa kazi inayofanyika miongoni mwenu; mpaka katika hatua hii ya sasa bado mnashikilia matumaini yenu ya baadaye katika mioyo yenu na hamtaki kuyaacha. Hakuna mtu anayejali ni kwa nini leo Mungu amewachagua tu—kikundi kisichostahili mno—kukifanyia kazi, hivyo je, kazi hii inafanywa vibaya? Je, hii ni kazi ya uangalizi wa muda mfupi? Kwa nini Mungu ameshuka chini bila upendeleo kufanya kazi kati yenu, ingawaje Amekuwa akijua kwa muda mrefu kwamba nyinyi ni wana wa Moabu?

Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu
Kama washiriki wa jamii ya binadamu na Wakristo wamchao Mungu, ni jukumu na wajibu wetu wote kutoa akili na mwili wetu kwa kutimiza agizo la Mungu, kwani uhai wetu wote ulitoka kwa Mungu, na upo kwa sababu ya ukuu wa Mungu. Kama akili zetu na miili yetu si kwa ajili ya agizo la Mungu na si kwa sababu ya haki ya mwanadamu, basi nafsi zetu hazina thamani kwa wale waliokufa kishahidi kwa ajili ya agizo kwa Mungu, na thamani ndogo zaidi kwa Mungu, aliyetupa kila kitu.
Mungu aliumba dunia hii, Aliumba mwanadamu huyu, na zaidi ya hayo Alikuwa msanifu wa utamaduni na ustaarabu wa binadamu wa zamani wa mataifa mengine.

9/18/2017

Umeme wa Mashariki | Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (2)

Umeme wa Mashariki | Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (2)
Umeme wa Mashariki | Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (2)
 Mlikuwa mnatafuta kutawala kama wafalme, na leo bado hamjaacha kabisa suala hili; bado unatamani kutawala kama wafalme, kushikilia juu mbingu na kusaidia dunia. Sasa, fikiria kuhusu hilo: Je, unazo sifa kama hizo? Je, huoni unakuwa mtu usiyekuwa na maana? Je, mnachokitafuta na kujitolea umakini wenu kwacho ni cha uhalisi? Hamna hata hali ya kawaida ya ubinadamu—hilo si la kutia huruma? Hivyo, leo Nazungumzia tu juu ya kushindwa, kuwa na ushuhuda, kuboresha tabia yako, na kuingia katika njia ya kufanywa kuwa mkamilifu, na kutozungumzia kitu chochote kile. Watu wengine wanaonekana kuchoshwa na ukweli usiotiwa doa, na wanapoona mazungumzo ya ubinadamu wa kawaida na kuboresha tabia ya watu, wanakuwa wabishi.

9/17/2017

Anzeni Maisha Mapya - "Nimeuona uzuri wa Mungu" (Video Rasmi ya Muziki)

Nimeuona uzuri wa Mungu

I

Nasikia sauti ijulikanayo ikiniita mara kwa mara.

Nikaamka na kuangalia kuona, ni nani aliye pale akizungumza.

Sauti yake ni nyororo lakini kali, picha Yake nzuri!

Nateseka kupigwa na kuvumilia maumivu makubwa, nikipapaswa na mkono Wake wenye upendo.

Halafu natambua ni Mwenyezi ambaye nilipigana naye.

Najichukia mwenyewe, kwa majuto makubwa, fikiria niliyoyafanya.

9/16/2017

Umeme wa Mashariki | Ukaribisheni Urejeaji wa Bwana Yesu | Sifa na Ibada "Mungu Ameleta Utukufu Wake Mashariki"


Mungu Ameleta Utukufu Wake Mashariki


Mungu aliipa Israeli utukufu Wake kisha Akauhamisha mbali na pale,

na kuwaleta Waisraeli na kuwaleta watu wote Mashariki.

Mungu amewaelekeza wote kwenye mwanga

ili waweze kuungana tena na kuwa pamoja na mwanga,

wasilazimike kuutafuta tena, kuutafuta mwanga.

9/15/2017

Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo ni Mungu Mwenyewe

    Je, unapaswa kujua nini kuhusu Mungu wa vitendo? Mungu wa vitendo Mwenyewe anajumuisha Roho, Nafsi, na Neno, na hii ndiyo maana ya kweli ya Mungu wa utendaji Mwenyewe. Kama unajua Nafsi pekee—kama unajua tabia na utu Wake—lakini hujui kazi ya Roho, au ambacho Roho hufanya katika mwili, na kuangazia Roho tu, na Neno, na kuomba mbele ya Roho, bila kujua kazi ya Roho wa Mungu katika Mungu wa vitendo, basi hii inadhihirisha kuwa humjui Mungu wa vitendo.

9/13/2017

Umeme wa Mashariki | Jinsi ya Kuujua Uhalisi

Umeme wa Mashariki | Jinsi ya Kuujua Uhalisi
Umeme wa Mashariki | Jinsi ya Kuujua Uhalisi
Mungu ni Mungu wa uhalisi: kazi Zake zote ni halisi, maneno yote Anayoyanena ni halisi, na ukweli wote Anaouonyesha ni halisi. Kila kisicho maneno Yake ni kitupu, kisichokuwepo, na kisicho timamu. Leo, Roho Mtakatifu yupo kwa ajili ya kuwaongoza watu katika maneno ya Mungu. Ikiwa watu wanatafuta kuingia katika uhalisi, basi ni lazima wauandame uhalisi, na waujue uhalisi, baadaye ni lazima wapitie uhalisi, na kuishi kwa kudhihirisha uhalisi. Kadiri watu wanavyoujua uhalisi zaidi, kadiri wanavyoweza kugundua ikiwa maneno ya wengine ni halisi; kadiri watu wanavyojua uhalisi, ndivyo wanavyokuwa na dhana kidogo z aidi; 

9/11/2017

Umeme wa Mashariki | Utangulizi

Umeme wa Mashariki | Utangulizi
Umeme wa Mashariki | Utangulizi
"Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima" ni kundi la pili la matamshi yanayoonyeshwa na Kristo. Ndani yake, Kristo Anatumia utambulisho wa Mungu Mwenyewe. Yanajumlisha kipindi cha kuanzia Februari 20, 1992 hadi Juni 1, 1992, na yana jumla ya matamshi arobaini na saba. Namna, maudhui na mtazamo wa maneno ya Mungu katika matamshi haya hayafanani kabisa na "Maneno ya Roho kwa Makanisa." "Maneno ya Roho kwa makanisa" inafichua na kuongoza tabia ya watu ya nje na maisha yao rahisi ya roho.Hatimaye, inaisha kwa "majaribu ya watendaji huduma." Hata hivyo, "Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima," inaanza na hitimisho la utambulisho wa watu kama watendaji huduma na mwanzo wa maisha yao kama watu wa Mungu.

9/10/2017

Maonyesho ya Awali ya Video za Injili | Je, Biblia ndiye Bwana, au ni Mungu? | "Bwana Wangu Ni Nani"


Liu Zhizhong ni mzee katika kanisa moja la mtaani la nyumba nchini China. Amekuwa muumini kwa zaidi ya miaka 30, na amesisitiza bila kukoma kwamba “Biblia ni ufunuo wa Mungu,” “Biblia inamwakilisha Mungu, kuamini katika Mungu ni kuamini katika Biblia, kuamini katika Biblia ni kuamini katika Mungu.” Moyoni mwake, Biblia ni kuu. Kwa sababu ya upendo na imani yake pofu katika Biblia, hajawahi kutafuta au kuitazama kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Hadi siku moja, alipowazuia waumini kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu mtandaoni, akawa na fursa ya kukutana na wahubiri kutoka katika Kanisa la Mwenyezi Mungu. Baada ya kupitia majadiliano makali kuhusu ukweli, aliweza hatimaye kuona wazi uhusiano kati ya Biblia na Mungu? Je, aliweza kusonga mbali na Biblia kuelewa kwamba Kristo ndiye ukweli, njia, na uzima? Je, atachukuliwa kwenda mbinguni mbele ya Mungu?

Umeme wa Mashariki | Neno la Mungu Humwongoza Mtu Kuishi Maisha Mapya | Maisha Yetu ya Kanisa Yanapendeza Sana

Maisha Yetu ya Kanisa Yanapendeza Sana

I
Mwenyezi Mungu mwenye mwili, tunaimba nyimbo za sifa kubwa Kwako.
Wewe hutuleta katika maisha ya ufalme.
Sisi watu wa ufalme tu katika karamu yako ya fahari,
tukifurahia maneno Yako, tukitakaswa upotovu wetu.
Neno Lako hutuongoza na sisi kukufuata kwa karibu.
Ni neema ya Mungu kwamba tabia yetu ya kishetani imetupiliwa mbali.
Sisi hufurahia neno la Mungu na kuishi maisha mapya mbele Zake.
Kutunza moyo wa Mungu, kumpenda Yeye kwa dhati, kumshukuru na kumsifu.
La la la la la ... la la la la la ...

Umeme wa Mashariki | 2. Utangulizi Mfupi Kuhusu Usuli wa Kuonekana kwa Kazi ya Kristo wa Siku za Mwisho Nchini China


China ni nchi ambamo joka kubwa jekundu hukaa, na ni mahali ambapo pamempinga na kumshutumu Mungu zaidi sana katika historia. China ni kama ngome ya mapepo na gereza linalodhibitiwa na shetani, lisilopenyeka na lisiloingilika. Zaidi ya hayo, utawala wa joka kubwa jekundu husimama ukilinda katika ngazi zote na umeanzisha ulinzi katika kila kaya. Matokeo yake, hakuna mahali pagumu zaidi ya hapa kueneza injili ya Mungu na kufanya kazi ya Mungu. Wakati Chama cha Kikomunisti Cha China kiliposhika madaraka mwaka wa 1949, imani za kidini katika China bara zilizimwa kabisa na kupigwa marufuku.

Ukaribisheni Urejeaji wa Bwana Yesu | Sifa na Ibada "Furaha katika Nchi Nzuri ya Kanaani"

Furaha katika Nchi Nzuri ya Kanaani


Nimerudi kwa familia ya Mungu, mchangamfu na mwenye furaha.
Mikono yangu imemshika mpendwa wangu, moyo wangu ni miliki Yake.
Japo nimepitia Bonde la Machozi, nimeyaona mapenzi ya Mungu.
Mapenzi yangu kwa Mungu hukua siku baada ya siku, Mungu ndiye chanzo cha furaha yangu.
Nikiduwazwa na uzuri wa Mungu, moyo wangu umeshikizwa kwa Mungu.
Siwezi kumpenda Mungu vya kutosha, nyimbo za sifa huchemka moyoni mwangu.
Nikiduwazwa na uzuri wa Mungu, nyimbo za sifa huchemka moyoni mwangu.
Siwezi kumpenda Mungu vya kutosha, nyimbo za sifa huchemka moyoni mwangu.

9/09/2017

Umeme wa Mashariki | Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli

Kazi ya siku za mwisho ni kutenganisha vitu vyote kulingana na jinsi yavyo, kuhitimisha mpango wa usimamizi wa Mungu, kwa maana muda u karibu na siku ya Mungu imewadia. Mungu huwaleta wote ambao wameingia katika ufalme Wake, yaani, wale wote ambao wamekuwa waaminifu Kwake mpaka mwisho, katika enzi ya Mungu Mwenyewe. Hata hivyo, kabla ya kuja kwa enzi ya Mungu Mwenyewe, kazi Atakayofanya Mungu si kutazama matendo ya mwanadamu wala kuchunguza maisha ya wanadamu, ila ni kuhukumu uasi wake, kwa maana Mungu atawatakasa wale wote wanaokuja mbele ya kiti Chake cha enzi.

9/08/2017

Umeme wa Mashariki | Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" (Video Rasmi ya Muziki)

Nitampenda Mungu Milele

Ee Mungu! Maneno Yako yameniongoza kurudi Kwako.
Nakubali mafunzo katika ufalme Wako mchana na usiku.
Majaribio mengi na maumivu, mateso mengi sana.
Mara nyingi nilimwaga machozi na kuhisi huzuni,
na mara nyingi nimeanguka katika mtego wa Shetani.
Lakini Hujawahi kuniacha.
Uliniongoza kupitia matatizo mengi, Umeniweka kupitia hatari nyingi.
Sasa najua ya kuwa Wewe Umenipenda.

Ee Mungu! Waniongoza kwa maisha mapya.
Nikifurahia Maneno yako, Nimeelewa mapenzi yako.
Maneno yako hunihukumu na kuniadibu, na kutakasa upotovu wangu.
Kupitia majaribio nimejifunza kukutii Wewe.
Kukua katika neno la Mungu, nimekuja kumjua Mungu.
Niko tayari kufanya wajibu wangu kwa shahidi Wako na utukufu.

9/06/2017

Umeme wa Mashariki | Mungu Amekuja Mungu Ametawala | " Kwaya ya Injili ya Kichina Onyesho la 18"


Kwaya za Injili :
1. "Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho"
2. "Mwenyezi Mungu Amekuwa Ameketi Kwenye Kiti Kitukufu cha Enzi"

1. Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho
Mungu ndiye Mwanzo, Mungu ndiye Mwanzo, Mungu ndiye Mwanzo, na tena Mwisho, na tena Mwisho, na tena Mwisho. Mungu ndiye Mpanzi, Mungu ndiye Mpanzi, Mungu ndiye Mpanzi, na Mvunaji (Mvunaji).   Mungu ndiye Mwanzo na Mwisho; Mungu ndiye Mpanzi na Mvunaji. Mungu ndiye Mwanzo na Mwisho; Mungu ndiye Mpanzi na Mvunaji. Mungu ndiye Mwanzo na Mwisho; Mungu ndiye Mpanzi na Mvunaji. Mungu Anakuwa mwili hasa kwa ajili ya kuikaribisha enzi mpya, na, kwa hakika, Anapoikaribisha enzi mpya, Atakuwa Ameikamilisha enzi ya kale wakati uo huo. Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Mataifa huabudu miungu halisi-ya muziki

Umeme wa Mashariki | Mataifa huabudu miungu halisi-ya muziki

    Wakati huu, Mungu haji kufanya kazi kwa mwili wa kiroho ila kwa ile kawaida sana. Sio tu mwili wa kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili, lakini pia mwili ambao Mungu anarudia. ... Mwili huu usio na umuhimu ni mfano halisi wa maneno yote ya kweli kutoka kwa Mungu, ambao hufanya kazi ya Mungu siku za mwisho, na maonyesho ya tabia nzima ya Mungu kwa mwanadamu kuja kujua. 
 kutoka kwa Neno Laonekana Katika Mwili
  
 Je, hukutamani sana kumwona Mungu aliye mbinguni? Je, hukutamani sana kumwelewa Mungu aliye mbinguni? Je, hukutamani sana kuona hatima ya mwanadamu? Atakueleza hizi siri zote ambazo hazijaelezwa, na hata Atakuelezea kuhusu ukweli usioelewa. Yeye ndiye lango la kuingia katika ufalme, na kiongozi wako katika enzi mpya. 
                                                                       kutoka kwa Neno Laonekana Katika Mwili

Umeme wa Mashariki | Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake

 Umeme wa Mashariki |1. Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake

Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake


Kama wale mamia ya mamilioni ya wengine wanaomfuata Bwana Yesu Kristo, tunafuata sheria na amri za Biblia, kufurahia neema tele ya Bwana Yesu Kristo, na kukusanyika pamoja, kuomba, kusifu, na kuhudumu kwa jina la Bwana Yesu Kristo—na haya yote sisi hufanya chini ya utunzaji na ulinzi wa Bwana. Mara nyingi, sisi huwa dhaifu, na mara nyingi sisi huwa pia wenye nguvu. Tunaamini kwamba matendo yetu yote yanaambatana na mafundisho ya Bwana. Na basi, ni dhahiri kwamba sisi pia tunajiamini kuwa kwenye njia ya kutii mapenzi ya Baba aliye mbinguni.

9/05/2017

Umeme wa Mashariki | Mazungumzo Mafupi Kuhusu “Ufalme wa Milenia Umefika”

Umeme wa Mashariki | Mazungumzo Mafupi Kuhusu “Ufalme wa Milenia Umefika”
Umeme wa Mashariki | Mazungumzo Mafupi Kuhusu “Ufalme wa Milenia Umefika”
  Mwenyezi Mungu alisema, Mnayaonaje maono ya Ufalme wa Milenia? Baadhi ya watu hutafakari sana kuuhusu na kusema kuwa Ufalme wa Milenia utadumu duniani kwa miaka elfu moja, hivyo basi ikiwa waumini wazee katika kanisa hawajaoa, je, wanapaswa kuoa? Familia yangu haina pesa, je napaswa nianze kutafuta pesa? … Ufalme wa Milenia ni nini? Je, mnajua? Watu ni nusu vipofu na wanapitia mateso mengi. Kwa hakika, Ufalme wa Milenia bado haujafika rasmi. Katika hatua ya kuwafanya wanadamu wakamilike, Ufalme wa Milenia ni mfano mdogo tu;