Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Yesu-Kristo. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Yesu-Kristo. Onyesha machapisho yote

8/13/2019

New Swahili Gospel Movie "Siri ya Utauwa" | Bwana Yesu Kristo Atarudi Vipi?



New Swahili Gospel Movie "Siri ya Utauwa" | Bwana Yesu Kristo Atarudi Vipi?


Lin Bo'en alikuwa mzee wa kanisa katika kanisa la nyumbani Uchina. Wakati wa miaka yake yote kama muumini, alihisi kwamba ameheshimiwa kuteseka kwa ajili ya Bwana, na alithamini kumfahamu na kumpata Bwana Yesu Kristo zaidi ya kitu kingine chochote duniani. Siku moja ya jaala, alienda nje kuhubiri na akasikia habari fulani za kushtua: Bwana Yesu amerudi katika mwili, na Yeye ni Kristo wa siku za mwisho—Mwenyezi Mungu! Lin Bo'en alikanganyikiwa. 

8/12/2018

Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili

Sura ya 5 Ukweli Kuhusu Mungu Kupata Mwili

5. Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili

Maneno Husika ya Mungu:
Kupata mwili mara ya kwanza kulikuwa kumkomboa mwanadamu kutoka katika dhambi kupitia mwili wa Yesu, hivyo, Aliokoa mwanadamu kutoka kwa msalaba, lakini tabia potovu ya kishetani ilibaki ndani ya mwanadamu. Kupata mwili mara ya pili si kwa ajili ya kuhudumu tena kama sadaka ya dhambi ila ni kuwaokoa kamilifu wale waliokombolewa kutoka kwa dhambi. Hii inafanyika ili wale waliosamehewa wakombolewe kutoka kwa dhambi zao, na kufanywa safi kabisa, na kupata mabadiliko ya tabia, hivyo kujikwamua kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza na kurudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu. Hivyo tu ndivyo mwanadamu ataweza kutakaswa kikamilifu. Mungu Alianza kazi ya wokovu katika Enzi ya Neema baada ya Enzi ya Sheria kufika mwisho.

8/11/2018

Unafaa Kutofautisha Vipi Kati ya Kazi ya Mungu na ya Mwanadamu?

Sura ya 6 Aina Mbalimbali za Utofautishaji Ambazo Unafaa Kumiliki katika Kusadiki Kwako kwa Mungu

1. Utofautishaji Kati ya Kazi ya Mungu na Ile ya Mwanadamu

Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya Mungu Mwenyewe inahusisha kazi ya wanadamu wote, na pia inawakilisha kazi ya enzi nzima. Hii ni kusema kwamba, kazi ya Mungu mwenyewe inawakilisha harakati na mwelekeo wa kazi yote ya Roho Mtakatifu, ilhali kazi ya mitume inafuata kazi ya Mungu na wala haiongozi enzi, na wala haiwakilishi mwelekeo wa kufanya kazi wa Roho Mtakatifu katika enzi nzima. Huwa wanafanya tu kazi ambayo mwanadamu anapaswa kufanya, ambayo haihusishi kabisa kazi ya usimamizi. Kazi ya Mungu ni mradi ndani ya kazi ya usimamizi. Kazi ya mwanadamu ni wajibu tu wa wanadamu kuweza kutumika na wala haina uhusiano na kazi ya usimamizi.

4/09/2018

Maono ya Kazi ya Mungu (3)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi mungu
Mwenyezi Mungu alisema, Mara ya kwanza Mungu alipopata mwili ilikuwa kupitia kutungwa mimba kwa Roho Mtakatifu, na ilihusiana na kazi Aliyokusudia kufanya. Jina la Yesu liliashiria mwanzo wa Enzi ya Neema. Wakati Yesu Alianza kufanya huduma Yake, Roho Mtakatifu Alianza kutoa ushuhuda kwa jina la Yesu, na jina la Yehova halikuzungumziwa tena, na badala yake Roho Mtakatifu Alianza kazi mpya hasa kwa jina la Yesu. Ushuhuda wa wale waliomwamini Yeye ulitolewa kwa ajili ya Yesu Kristo, na kazi waliyoifanya walifanya pia kwa ajili ya Yesu Kristo. Hitimisho Enzi ya Sheria ya Agano la Kale lilimaanisha kuwa kazi iliyofanywa hasa kutumia jina la Yehova ilikuwa imefikia kikomo. Baada ya hii, jina la Mungu halikuwa Yehova tena;

2/28/2018

Umeme wa Mashariki | Kazi na Kuingia (6)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Umeme wa Mashariki | Kazi na Kuingia (6) 

Kazi na kuingia kwa uhalisia ni vya kiutendaji na vinarejelea kazi ya Mungu na kuingia kwa mwanadamu. Mwanadamu kukosa kabisa uelewa juu ya sura halisi ya Mungu na kazi ya Mungu kumesababisha shida kubwa katika kuingia kwake. Leo hii, watu wengi bado hawajui kazi ambayo Mungu anatimiza katika siku za mwisho, au kwa nini Mungu Anastahimili fedheha kubwa kupita kiasi kuja katika mwili na kusimama na mwanadamu katika makovu na majonzi. Mwanadamu hajui chochote kuhusu lengo la kazi ya Mungu, wala kusudi la mpango wa Mungu kwa ajili ya siku za mwisho. Kwa sababu mbalimbali, watu daima wanakuwa vuguvugu katika kuingia ambako Mungu anataka na wanabakia wenye shaka[1], kitu ambacho kimeleta shida kubwa katika kazi ya Mungu katika mwili.

2/19/2018

Mwanadamu Anaweza Kuokolewa Tu Katikati ya Usimamizi wa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Kila mtu anahisi kuwa usimamizi wa Mungu ni wa ajabu, kwa sababu watu wanafikiri kuwa usimamizi wa Mungu hauna uhusiano wowote na mwanadamu. Wanafikiri kuwa usimamizi wa Mungu ni kazi ya Mungu pekee, shughuli za Mungu, na hivyo wanadamu hawajali kuhusu usimamizi wa Mungu. Kwa njia hii, kuokolewa kwa wanadamu kumekuwa kusiko yakini na kusiko dhahiri, na kumebaki tu maneno matupu. Hata kama mwanadamu anamfuata Mungu ili aokolewe na aingie katika hatima inayopendeza, mwanadamu hajishughulishi na jinsi ambavyo Mungu Hutekeleza kazi Yake. Mwanadamu hashughulishwi na Anachokipanga Mungu na anachopaswa kufanya ili aokolewe.

12/27/2017

Matamshi ya Mwenyezi Mungu, Ahadi kwa Wale Ambao Wamekamilishwa

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kanisa
ukamilifu,kukamilishwa na Mungu,watu wa Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu, Ahadi kwa Wale Ambao Wamekamilishwa

Ni njia gani ambayo Mungu hutumia kumkamilisha mwanadamu? Ni vipengele vipi vinavyojumuishwa? Je, uko tayari kukamilishwa na Mungu? Je, uko tayari kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu? Unajua nini kuhusu maswali haya? Kama huwezi kuzungumzia maarifa kama haya, basi hii inaonyesha kwamba bado huijui kazi ya Mungu na hujapatiwa nuru katu na Roho Mtakatifu. Binadamu wa aina hii hawezi kukamilishwa. Wanaweza tu kupokea kiasi kidogo cha neema ili kufurahia kwa muda mfupi na haiwezi kuendelezwa kwa kipindi kirefu. Kama mtu hufurahia tu neema ya Mungu, hawezi kukamilishwa na Mungu. Baadhi wanaweza kutoshelezwa na amani na furaha ya mwili, maisha yenye furaha bila ya dhiki au msiba, huku wakiishi kwa amani na familia zao bila ya mapigano au ugomvi.

12/12/2017

Matamshi ya Mwenyezi Mungu - Unajua Nini Kuhusu Imani?

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Yesu
imani katika Mung,watu wa Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu - Unajua Nini Kuhusu Imani?


Ndani ya binadamu, kunalo neno lisilokuwa la uhakika, ilhali binadamu hajui imani inajumuisha nini, na vilevile hajui ni kwa nini anayo imani. Binadamu huelewa kidogo sana, na binadamumwenyewe amepungukiwa sana; yeye anakuwa tu na imani ndani Yangu bila kujali na bila kujua. Ingawa hajui imani ni nini wala ni kwa nini anayo imani ndani Yangu, anaendelea kufanya hivyo kwa shauku mno. Kile Ninachomwomba binadamu, si tu yeye kuniita Mimi kwa shauku kwa njia hii au kuniamini Mimi kwa mtindo huu wa kukosa mwelekeo.

10/20/2017

Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo

Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kanisa la Mwenyezi Mungu
Umeme wa Mashariki | Wafaa Kujua Namna Ambavyo Ubinadamu Wote Umeendelea Hadi Siku ya Leo
Uzima wa kazi ya miaka 6,000 yote umebadilika kwa utaratibu kuambatana na nyakati. Mabadiliko katika kazi hii kumefanyika kulingana na hali zinazozunguka ulimwengu mzima. Kazi ya usimamizi ya Mungu imebadilika tu kwa utaratibu kulingana na mitindo ya kimaendeleo ya ubinadamu kwa ujumla; haikuwa imepangwa tayari mwanzoni mwa uumbaji. Kabla ya ulimwengu kuumbwa, au punde tu baada ya kuumbwa kwake, Yehova hakuwa amepanga bado awamu ya kwanza ya kazi, ile ya sheria; awamu ya pili ya kazi, ile ya neema; au awamu ya tatu ya kazi, ile ya kushinda, ambapo Angefanya kazi kwanza miongoni mwa kundi la watu—baadhi ya vizazi vya Moabu, na kuanzia hapa Angeweza kushinda ulimwengu mzima. Hakuyaongea maneno haya baada ya kuumba ulimwengu; Hakuyaongea maneno haya baada ya Moabu, wala hata kabla ya Lutu. Kazi yake yote ilifanywa bila kupangwa. Hivi ndivyo hasa kazi Yake nzima ya usimamizi ya miaka elfu sita imeendelea; kwa vyovyote vile, Hakuwa ameandika mpango kama huo kama Chati ya Muhtasari wa Maendeleo ya Ubinadamu kabla ya kuumba ulimwengu. Katika kazi ya Mungu, Anaeleza moja kwa moja Yeye ni nani;

10/16/2017

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | ” (Video za Kikristo)

Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa


I

Nilitaka kulia lakini hakuna mahali palihisi sawa.

Nilitaka kuimba lakini hakuna wimbo ulipatikana.

Nilitaka kuonyesha upendo wa kiumbe aliyeumbwa.

Nikitafuta juu na chini, lakini hakuna maneno yangeweza kusema,

yangeweza kusema jinsi hasa ninavyohisi.

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu.

9/11/2017

Umeme wa Mashariki | Utangulizi

Umeme wa Mashariki | Utangulizi
Umeme wa Mashariki | Utangulizi
"Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima" ni kundi la pili la matamshi yanayoonyeshwa na Kristo. Ndani yake, Kristo Anatumia utambulisho wa Mungu Mwenyewe. Yanajumlisha kipindi cha kuanzia Februari 20, 1992 hadi Juni 1, 1992, na yana jumla ya matamshi arobaini na saba. Namna, maudhui na mtazamo wa maneno ya Mungu katika matamshi haya hayafanani kabisa na "Maneno ya Roho kwa Makanisa." "Maneno ya Roho kwa makanisa" inafichua na kuongoza tabia ya watu ya nje na maisha yao rahisi ya roho.Hatimaye, inaisha kwa "majaribu ya watendaji huduma." Hata hivyo, "Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima," inaanza na hitimisho la utambulisho wa watu kama watendaji huduma na mwanzo wa maisha yao kama watu wa Mungu.