Hadithi ya 2. Mlima Mkubwa, Kijito Kidogo, Upepo Mkali, na Wimbi Kubwa
Mwenyezi Mungu alisema, Kulikuwa na kijito kidogo kilichotiririka kwa kuzungukazunguka, hatimaye kikawasili chini ya mlima mkubwa. Mlima ulikuwa unazuia njia ya kijito hiki, hivyo kijito kikauomba mlima kwa sauti yake dhaifu na ndogo, "Tafadhali noamba kupita, umesimama kwenye njia yangu na umenizibia njia yangu kuendelea mbele." Basi mlima ukauliza, "Unakwenda wapi?" Swali ambalo kijito kililijibu, "Ninatafuta makazi yangu." Mlima ukasema, "Sawa, endelea na tiririkia juu yangu!" Lakini kwa sababu kijito kilikuwa dhaifu sana na kichanga sana, hakukuwa na namna kwake kutiririka juu ya mlima mkubwa hivyo, hivyo hakikuwa na uchaguzi bali kuendelea kutiririka chini ya mlima...
Upepo mkali ukavuma, ukiwa umekusanya mchanga na vumbi kuelekea ambapo milma ulikuwa umesimama. Upepo ukauungurumia mlima, "Hebu nipite!" Mlima ukauliza, "Unakwenda wapi?" Upepo ukavuma kwa kujibu, "Ninataka kwenda upande ule wa mlima." Mlima ukasema, "Sawa, kama unaweza kupenya katikati yangu, basi unaweza kwenda!"