Ufafanuzi wa neno “Mfarisayo” ni upi? Ni mtu ambaye ni mnafiki, ambaye ni bandia na anajifanya katika kila kitu anachofanya, akijifanya kuwa mwema, mwenye fadhila, na mzuri. Je, hivyo ndivyo alivyo kwa kweli? Yeye ni mnafiki, na hivyo kila kitu kinachodhihirika na kufichuliwa ndani yake ni cha uongo, yote ni kujifanya—sio hali yake ya kweli. Hali yake ya kweli imefichwa ndani ya moyo wake; haionekani. Watu wasipofuatilia
ukweli, kama hawaelewi ukweli, basi maarifa yao ya kidini na nadharia ambazo wamepata zinakuwa nini? Je, zinakuwa maneno ya mafundisho ambayo watu huzungumzia mara nyingi? Watu hutumia haya yanayodaiwa kuwa mafundisho sahihi kujifanya na kujionyesha kuwa wazuri. Popote waendapo, mambo wanayozungumzia, mambo wanayoyasema, na tabia yao ya nje huonekana kuwa sawa na nzuri kwa wengine. Yote yanalingana na fikira na mapendeleo ya mwanadamu. Machoni pa wengine, wao ni wenye kumcha Mungu na wanyenyekevu. Wao ni wavumilivu, wastahimilivu, na wenye upendo kwa wengine. Kwa kweli, yote ni bandia—yote ni kujifanya. Kwa nje, wao ni waaminifu kwa Mungu, lakini kisirisiri, kila kitu wanachofanya ni cha uzembe. Kwa juujuu, wameacha familia zao na kazi zao, wanajitahidi kwa bidii na hujitumia—lakini kwa kweli wanafaidika kisirisiri kutoka kwa
kanisa na kuiba sadaka! Kila kitu wanachofichua kwa nje, tabia yao yote ni bandia! Hii ndiyo maana ya Mfarisayo mnafiki. “Mafarisayo”—watu hawa hutoka wapi? Je, wanajitokeza kati ya wasioamini? Wote hujitokeza kati ya wasioamini. Kwa nini waumini hawa hugeuka kuwa hivyo? Inaweza kuwa kwamba
maneno ya Mungu yaliwafanya wawe namna hiyo? Sababu ya wao kuwa namna hiyo ni hasa kwamba waliichukua njia mbaya. Wanayachukulia maneno ya Mungu kama chombo cha kujihami nacho; wanajihami na maneno haya na kuyachukulia kama mtaji wa kupata riziki, kupata kitu bila kutoa chochote. Hawafanyi chochote ila kuhubiri mafundisho ya kidini, na hawajawahi kufuata njia ya Mungu. Tabia yao inayokisiwa kuwa nzuri na mwenendo mzuri, hicho kidogo ambacho wameacha na kutumia kimelazimishwa kabisa, yote ni uigizaji tu wanaofanya. Yote ni bandia kabisa; yote ni kujifanya. Katika mioyo ya watu hawa hakuna uchaji kwa Mungu hata kidogo, na hawana hata imani yoyote ya kweli kwa Mungu. Zaidi ya hayo, wao ni wa wasioamini. Watu wasipofuatilia ukweli, watatembea njia ya aina hii, na watakuwa Mafarisayo. Je, hili silo jambo la kuhofisha?