Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Matamshi-ya-Kristo-wa-Siku-za-Mwisho. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Matamshi-ya-Kristo-wa-Siku-za-Mwisho. Onyesha machapisho yote

12/09/2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Kumi na Sita"

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Kumi na Sita"


Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

12/01/2019

Mtu kutekeleza wajibu wake ni nini?

Maneno Husika ya Mungu:
Kutimiza wajibu wako ni ukweli. Kutimiza wajibu wako katika nyumba ya Mungu sio tu kutimiza masharti fulani au kufanya kitu unachopaswa kufanya. Ni kutimiza wajibu wa kiumbe aliyeumbwa anayeishi kati ya mbingu na dunia! Ni kutimiza majukumu na wajibu wako mbele ya Bwana wa uumbaji. Majukumu haya ni majukumu yako ya kweli. Linganisha kutimiza wajibu wa kiumbe aliyeumbwa na kuwa na upendo kwa wazazi wako—ni kipi ndicho ukweli? Kutimiza wajibu wa kiumbe aliyeumbwa ndio ukweli; ni wajibu wako unaotarajiwa kutimiza.
kutoka katika “Uhalisi wa Ukweli ni Nini?” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

11/07/2019

Sauti ya Mungu | “Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu” (Dondoo 1)


Sauti ya Mungu | “Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu” (Dondoo 1)

“Kumcha Mungu” hakumaanishi woga na hofu isiyotajika, wala kukwepa, wala kuweka umbali, wala si kuabudu kama mungu ama ushirikina. Ila, ni kutazama na kupendezwa, sifa, imani, kuelewa, kujali, kutii, kuweka wakfu, upendo, na pia ibada isiyo na vikwazo au malalamishi, malipo na kujisalimisha. Bila ya ufahamu halisi wa Mungu, binadamu hawatakuwa na kupendezwa halisi, imani halisi, kuelewa halisi, kujali halisi ama utiifu, ila tu hofu na kukosa utulivu, shaka pekee, kutoelewa, kukwepa, na kuepuka; bila maarifa halisi ya Mungu, binadamu hawatakuwa na utakatifu na malipo halisi; bila ufahamu halisi wa Mungu, binadamu hawatakuwa na ibada halisi na kujisalimisha, uabudu kama mungu upofu tu na ushirikina; bila maarifa halisi juu ya Mungu, binadamu hawawezi kutenda kulingana na njia ya Mungu, ama kumcha Mungu, ama kuepuka maovu. Badala yake, kila tendo na tabia ambayo mwanadamu anashiriki litajaa uasi na kutotii, na kumbukumbu zinazokashifu na hukumu ya usengenyaji kumhusu Yeye, na mienendo miovu inayokwenda kinyume na ukweli na maana ya kweli ya maneno ya Mungu.

11/04/2019

Matamshi ya Mungu | "Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu"


Matamshi ya Mungu | "Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu"

Tatizo la kawaida lililo miongoni mwa binadamu wote ni kwamba wao huuelewa ukweli lakini hawawezi kuuweka katika matendo. Sababu moja ni kwamba binadamu hana nia ya kulipa gharama, na sababu nyingine ni kwamba utambuzi wa mwanadamu ni duni mno; hawezi kuona zaidi ya ugumu mwingi ulio katika hali halisi ya maisha na hajui jinsi ya kutenda kwa njia inayofaa. Kwa vile mtu ana tajriba ndogo sana, mwenye uwezo wa chini, mwenye ufahamu mdogo wa ukweli, yeye hawezi kutatua matatizo yanayomkabili maishani. Anaweza tu kupiga domo kuhusu imani yake kwa Mungu, ilhali hawezi kumhusisha Mungu katika maisha yake ya kila siku. Hii ni kusema, Mungu ni Mungu, na maisha ni maisha, kama kwamba binadamu hana uhusiano na Mungu katika maisha yake. Hayo ndiyo binadamu wote wanayaamini. Aina hii ya imani kwa Mungu haitaruhusu binadamu kupatwa na kukamilishwa Naye kwa uhakika. Kwa kweli, si kwamba neno la Mungu ni pungufu, badala yake uwezo wa binadamu wa kupokea neno Lake ni duni mno. Inaweza kusemwa karibu binadamu wote hutenda kulingana na nia za Mungu. Badala yake, imani yao kwa Mungu ni kwa mujibu wa nia zao wenyewe, fikra za kidini zilizowekwa, na desturi. Ni wachache wanaopitia mabadiliko baada ya kulikubali neno la Mungu na kuanza kutenda kwa mujibu wa mapenzi Yake. Badala yake, wanaendelea katika imani yao potovu. Wakati mwanadamu anaanza kuamini katika Mungu, anafanya hivyo kwa kuzingatia sheria za kawaida za dini, na anaishi na kuhusiana na wengine kwa misingi ya falsafa yake ya maisha. Hivyo ndivyo ilivyo kwa watu tisa kati ya kila watu kumi. Ni wachache sana wanaounda mpango mwingine na kuanza mwanzo mpya baada ya kuanza kumwamini Mungu. Hakuna anayeona au kuweka katika vitendo neno la Mungu kama ukweli.

10/20/2019

Mtu anayemwamini Mungu ni lazima aweze kutambua wachungaji wa uwongo na wapinga Kristo kuiacha dini na kurudi kwa Mungu

VIII. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Kipengele cha Ukweli Kuhusu Tofauti Kati ya Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu

Aya za Biblia za Kurejelea:
“Bwana Yehova alisema hivi kwa wachungaji; Ole wao wachungaji wa Israeli wajilishao! Wachungaji hawapaswi kuwalisha kondoo? Mnawala kondoo walio wanono, na kuvalia sufu zao, mnawaua wale ambao wamenona: lakini hamwalishi kondoo. Hamjawapa nguvu wagonjwa, wala hamjawaponya waliougua, wala hamjawafunga waliovunjika, wala hamjawarudisha wale waliofukuzwa, wala hamjawatafuta wale waliopotea; lakini mmewatawala kwa nguvu na ukatili” (Ezekieli 34:2-4).
Kuweni macho dhidi ya manabii wa uongo, ambao wanawajia wakiwa wamevalia nguo za kondoo, lakini kwa ndani wao ni mbwa mwitu wakali” (Mathayo 7:15).

10/19/2019

Mtu lazima atambue tofauti kati ya Kristo mwenye mwili na Makristo wa uongo na manabii wa uongo

VIII. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Kipengele cha Ukweli Kuhusu Tofauti Kati ya Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu

3. Mtu lazima atambue tofauti kati ya Kristo mwenye mwili na Makristo wa uongo na manabii wa uongo

Aya za Biblia za Kurejelea:
Mimi ndiye njia, ukweli na uhai” (Yohana 14:6).
Huamini kwamba mimi niko ndani ya Baba, na Baba yuko ndani ya mimi? Maneno ninenayo kwenu sineni juu yangu, ila Baba aishiye ndani yangu, anazifanya kazi hizo” (Yohana 14:10).
Mimi na yeye Baba yangu tu mmoja” (Yohana 10:30).
Kwa kuwa wataibuka makristo wasio wa kweli, na manabii wasio wa kweli, nao wataonyesha ishara kubwa na vioja; ili kwamba, ikiwezekana, watawadanganya walio wateule zaidi” (Mathayo 24:24).

10/15/2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo"


Maneno ya Roho Mtakatifu | "Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo"


Mwenyezi Mungu anasema, "Ninyi mnatafuta tu uwiano na Mungu asiye yakini, na kutafuta tu imani zisizo yakini ilhali ninyi hulingani na Kristo. Si uovu wenu utapata adhabu kama ile wanayostahili waovu? Wakati uo huo, mtagundua kuwa hakuna mtu yeyote asiyelingana na Kristo atakayeepuka siku ya ghadhabu, na mtagundua ni aina gani ya adhabu italetwa juu ya wale walio katika uadui na Kristo. Siku hiyo itakapofika, ndoto yenu ya kubarikiwa kwa imani yenu katika Mungu na kupata kuingia mbinguni, yote itakatizwa. Lakini, hata hivyo, si hivyo kwa wale ambao wanalingana na Kristo. Ingawa wao wamepoteza sana, ingawa wamekabiliwa na mengi ya ugumu wa maisha, watapokea urithi wote ambao Nimeutoa kwa ajili ya mwanadamu. Hatimaye, mtaelewa kwamba Mimi tu ndiye Mungu mwenye haki, na kwamba ni Mimi tu Niliye na uwezo wa kuwachukua binadamu mpaka kwenye hatima yao yenye kupendeza."


Tufuate: Asili na Maendeleo ya Kanisa la Mwenyezi Mungu


10/14/2019

Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Unyakuo ni nini na Maana Halisi ya Kuinuliwa Mbele ya Kiti cha Enzi cha Mungu

2. Unyakuo wa kweli ni nini?

Aya za Biblia za Kurejelea:
Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha. … na wale waliokuwa tayari wakaingia ndani na yeye kwa harusi: nao mlango ukafungwa” (Mathayo 25:6, 10).
Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti yangu, na aufungue mlango, Mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na Mimi” (Ufunuo 3:20).
Andika, Wamebarikiwa wale wanaoitwa katika karamu ya arusi ya Mwanakondoo” (Ufunuo 19:9).