Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Usomaji-wa-Matamshi-ya-Kristo-wa-Siku-za-Mwisho. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Usomaji-wa-Matamshi-ya-Kristo-wa-Siku-za-Mwisho. Onyesha machapisho yote

11/03/2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | “Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni” (Dondoo 1)

 Maneno ya Roho Mtakatifu | “Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni” (Dondoo 1)

      Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu mwenye mwili Anaitwa Kristo, na Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe. Basi iwe ubinadamu Wake au uungu, yote hujiwasilisha kwa mapenzi ya Baba wa mbinguni. Kiini cha Kristo ni Roho, yaani, uungu. Kwa hivyo, chemichemi Yake ni ile ya Mungu Mwenyewe; Dutu hii haitapinga kazi Yake Mwenyewe, na Yeye hangeweza kufanya kitu chochote kinachoharibu kazi Yake Mwenyewe, wala milele Yeye kutamka maneno yoyote ambayo yanakwenda kinyume na mapenzi Yake Mwenyewe. Kwa hiyo, Mungu mwenye mwili kamwe hangefanya kazi yoyote ambayo inasumbua usimamizi Wake Mwenyewe. Hili ndilo ambalo binadamu wote wanapaswa kuelewa. Kiini cha kazi ya Roho Mtakatifu ni kuokoa binadamu na ni kwa ajili ya usimamizi wa Mungu Mwenyewe. Vile vile, kazi ya Kristo ni kuokoa binadamu na ni kwa ajili ya mapenzi ya Mungu. Kutokana na kwamba Mungu Anapata mwili, Anatambua dutu Yake ndani ya mwili Wake, kama kwamba mwili Wake ni wa kutosha kufanya kazi Yake. Kwa hivyo, kazi zote za Roho wa Mungu zinabadilishwa na kazi ya Kristo wakati wa kupata mwili, na kwenye msingi wa kazi zote wakati wa kupata mwili ni kazi ya Kristo. Haiwezi kuchanganyika na kazi yoyote ile kutoka enzi nyingine yoyote. Na kwa kuwa Mungu Anakuwa mwili, Yeye Anafanya kazi katika utambulisho wa mwili Wake; kwa kuwa Yeye hukuja katika mwili, kisha Yeye humaliza katika mwili kazi hiyo Anayoazimia kufanya. Iwe ni Roho wa Mungu au ni Kristo, wote ni Mungu Mwenyewe, na Anafanya kazi hiyo Anayoazimia kufanya na hufanya huduma hiyo Anayopaswa kufanya.”

Kujua zaidi:Asili na Maendeleo ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

10/15/2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo"


Maneno ya Roho Mtakatifu | "Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo"


Mwenyezi Mungu anasema, "Ninyi mnatafuta tu uwiano na Mungu asiye yakini, na kutafuta tu imani zisizo yakini ilhali ninyi hulingani na Kristo. Si uovu wenu utapata adhabu kama ile wanayostahili waovu? Wakati uo huo, mtagundua kuwa hakuna mtu yeyote asiyelingana na Kristo atakayeepuka siku ya ghadhabu, na mtagundua ni aina gani ya adhabu italetwa juu ya wale walio katika uadui na Kristo. Siku hiyo itakapofika, ndoto yenu ya kubarikiwa kwa imani yenu katika Mungu na kupata kuingia mbinguni, yote itakatizwa. Lakini, hata hivyo, si hivyo kwa wale ambao wanalingana na Kristo. Ingawa wao wamepoteza sana, ingawa wamekabiliwa na mengi ya ugumu wa maisha, watapokea urithi wote ambao Nimeutoa kwa ajili ya mwanadamu. Hatimaye, mtaelewa kwamba Mimi tu ndiye Mungu mwenye haki, na kwamba ni Mimi tu Niliye na uwezo wa kuwachukua binadamu mpaka kwenye hatima yao yenye kupendeza."


Tufuate: Asili na Maendeleo ya Kanisa la Mwenyezi Mungu


10/13/2019

Matamshi ya Roho Mtakatifu | "Mazungumzo Mafupi Kuhusu 'Ufalme wa Milenia Umefika'"



Matamshi ya Roho Mtakatifu | "Mazungumzo Mafupi Kuhusu 'Ufalme wa Milenia Umefika'"


Mwenyezi Mungu anasema, "Wakati wa Enzi ya Ufalme wa Milenia, watu tayari watakuwa wamefanywa wakamilifu, na tabia mbovu ndani yao zitakuwa zimetakaswa. Wakati huo, maneno yasemwayo na Mungu yatawaongoza wanadamu hatua kwa hatua, na kufichua siri za kazi ya Mungu tangu uumbaji hadi leo, na maneno Yake yatawaambia watu kuhusu matendo ya Mungu katika kila enzi na kila siku, jinsi Anavyowaongoza watu ndani, kazi Aifanyayo katika ufalme wa kiroho, na yatawaambia watu kuhusu mienendo ya ufalme wa kiroho. Hapo tu ndipo itakuwa Enzi ya kikweli ya Neno; kwa sasa ni mfano tu."

Kujua zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu.