10/09/2017

Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu

Umeme wa Mashariki | Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu
Umeme wa Mashariki | Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu
Kazi ya Mungu miongoni mwa mwanadamu haitengani na mwanadamu, kwa kuwa mwanadamu ni chombo cha kazi hii na kiumbe wa pekee aliyeumbwa na Mungu anayeweza kutoa ushuhuda kwa Mungu. Maisha ya mwanadamu na shughuli zake zote havitengani na Mungu, na vyote vinaongozwa na mkono wa Mungu, na inaweza kusemwa kuwa hakuna mtu anayeweza kuishi bila Mungu. Hakuna anayeweza kupinga hili, kwani ndio ukweli. Kila Akifanyacho Mungu ni kwa faida ya mwanadamu, na kinalenga hila za Shetani. Kila anachokihitaji mwanadamu kinatoka kwa Mungu, na Mungu ndiye chanzo cha maisha ya mwanadamu. Hivyo basi, mwanadamu hana uwezo wa kujitenga na Mungu. Vilevile, Mungu Hajawahi kuwa na nia ya kujitenga na mwanadamu. Kazi Aifanyayo Mungu ni kwa ajili ya wanadamu wote na mawazo Yake daima ni mema. Kwa mwanadamu, kwa hivyo, kazi ya Mungu na mawazo ya Mungu kwa mwanadamu (yaani mapenzi ya Mungu) ni “maono” ambayo yanafaa kutambuliwa na mwanadamu. Maono kama hayo pia ni usimamizi wa Mungu, na kazi ambayo haiwezi kufanywa na mwanadamu. Mahitaji ambayo Mungu anatarajia kutoka kwa mwanadamu wakati wa kazi Yake, wakati uo huo, yanaitwa “vitendo” vya mwanadamu. Maono ni kazi ya Mungu Mwenyewe au ni mapenzi Yake kwa mwanadamu au madhumuni na umuhimu wa kazi Yake. Maono pia yanaweza kusemekana kuwa sehemu ya usimamizi, kwani usimamizi huu ni kazi ya Mungu, iliyokusudiwa kwa mwanadamu, kwa maana kwamba ni kazi ambayo Mungu anaifanya miongoni mwa wanadamu. Kazi hii ni ushahidi na njia ambayo kwayo mwanadamu anamfahamu Mungu na ni ya umuhimu wa hali ya juu kwa mwanadamu. Iwapo wanadamu hawatatilia maanani kuijua kazi ya Mungu na badala yake kutilia maanani mafundisho ya dini kuhusu imani kwa Mungu au kutilia maanani vitu vidogo visivyo na maana, hawatamjua Mungu, na, aidha, hawatakuwa wanautafuta moyo wa Mungu. Kazi ya Mungu inamsaidia sana mwanadamu kumfahamu Mungu na inaitwa maono. Maono haya ni kazi ya Mungu, mapenzi, madhumuni na umuhimu wa kazi ya Mungu na yote ni kwa manufaa ya mwanadamu. Vitendo vinamaanisha yale ambayo yanafaa kufanywa na mwanadamu, yale ambayo yanafaa yafanywe na viumbe wanaomfuata Mungu. Ni wajibu wa mwanadamu pia. Kinachotakiwa kufanywa na mwanadamu si kile alichokielewa tangu awali bali ni yale matakwa ya Mungu wakati wa kuifanya kazi Yake. Matakwa haya taratibu yanakuwa ya kina na kuinuliwa kadri Mungu anavyofanya kazi. Kwa mfano, katika Enzi ya Sheria, mwanadamu alilazimika kuifuata sheria na katika Enzi ya Neema mwanadamu alitakiwa kuubeba msalaba. Enzi ya Ufalme ni tofauti: Matakwa kwa mwanadamu ni mazito kuliko yale ya Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema. Kadiri maono yanavyoinuliwa zaidi ndivyo matakwa haya yanavyokuwa mazito, ya wazi zaidi na halisi. Vivyo hivyo, maono yanaendelea kuwa halisi. Maono haya mengi na halisi si fursa tu ya utiifu wa mwanadamu kwa Mungu, bali pia, zaidi ya hayo, yanamsaidia yeye kumfahamu Mungu.
Ikilinganishwa na enzi za awali, kazi ya Mungu katika Enzi ya Ufalme ni ya vitendo zaidi, imekusudiwa zaidi dutu ya mwanadamu na mabadiliko katika tabia yake na uwezo zaidi wa kuwa na ushuhuda wa Mungu Mwenyewe kwa wale wote wamfuatao Mungu. Kwa maneno mengine, katika Enzi ya Ufalme, Mungu anapofanya kazi hujionyesha zaidi kwa mwanadamu, kuliko kipindi kingine chochote kile cha awali, ikiwa inamaanisha kuwa maono ambayo yanafaa kujulikana na mwanadamu ni ya juu kuliko yale ya enzi yoyote ile ya awali. Kwa kuwa kazi ya Mungu miongoni mwa mwanadamu imeingia maeneo ambayo haikuwa imefika, maono yanayojulikana na mwanadamu katika Enzi ya Ufalme ni ya juu zaidi katika kazi nzima ya usimamizi. Kazi ya Mungu imeingia katika maeneo ambayo haikuwa imewahi kufika, na kwa hivyo maono yanayojulikana na mwanadamu yamekuwa ya juu zaidi katika maono yote, na matokeo ya vitendo vya mwanadamu ni ya juu zaidi kuliko enzi za awali kwani utendaji wa mwanadamu hubadilika kulingana na mabadiliko ya maono na ukamilifu wa maono vilevile huonyesha ukamilifu wa vitendo vya mwanadamu. Punde tu usimamizi wa Mungu usitapo, vitendo vya mwanadamu navyo husimama, na bila kazi ya Mungu mwanadamu hatakuwa na jingine ila tu kujikita katika mafundisho ya zamani, vinginevyo hatakuwa na pa kukimbilia. Bila maono mapya, hapatakuwa na utendaji mpya kutoka kwa mwanadamu; bila kuwepo na maono kamili hapatakuwa na utendaji kamili wa mwanadamu; na bila maono ya juu hapatakuwa na utendaji wa juu wa mwanadamu. Utendaji wa mwanadamu huandamana na nyayo za Mungu na vivyo hivyo ufahamu na tajriba ya mwanadamu hubadilika sawa na kazi ya Mungu. Bila kujali mwanadamu ana uwezo kiasi gani, hawezi kujitenga na Mungu, na iwapo Mungu angaliacha kufanya kazi hata kwa muda kidogo, mwanadamu angalikufa ghafla kutokana na ghadhabu ya Mungu. Mwanadamu hana lolote la kujivunia, kwani haijalishi ufahamu wa mwanadamu ulivyo wa juu leo, haijalishi jinsi uzoefu wake ulivyo wa kina, hawezi kujitenga na kazi ya Mungu—kwani vitendo vya mwanadamu na yale yote anayoyaandama katika imani yake kwa Mungu, hayatengani na maono haya. Katika kila aina ya kazi ya Mungu kuna maono yanayofahamika na mwanadamu; maono yanayofuatwa na matarajio mwafaka ya Mungu kwa mwanadamu. Bila haya maono kama msingi, mwanadamu hawezi kuwa na uwezo wa utendaji na pia hangeweza kumfuata Mungu bila kuyumbayumba. Ikiwa mwanadamu hamjui Mungu au hayaelewi mapenzi ya Mungu, basi yote ayafanyayo ni bure na yasiyoweza kukubalika na Mungu. Hata mwanadamu awe na vipawa vingi kiasi gani, bado hawezi kujitenga na kazi ya Mungu na uongozi wa Mungu. Bila kujali uzuri na wingi wa matendo ya mwanadamu, bado hayawezi kuchukua nafasi ya kazi ya Mungu. Kwa hivyo basi, utendaji wa mwanadamu hauwezi kutenganishwa na maono katika hali yoyote ile. Wale ambao hawakubali maono mapya hawana vitendo vipya. Vitendo vyao havina uhusiano na ukweli kwani wanajifunga katika mafundisho ya dini na kufuata sheria zilizokufa; hawana maono mapya kabisa na kwa sababu hiyo hawatendi kulingana na enzi mpya. Wamepoteza maono na kwa kufanya hivyo wamepoteza kazi ya Roho Mtakatifu, hivyo basi kupoteza ukweli pia. Wasio na ukweli ni wazawa wa upuuzi, ni mifano ya Shetani. Bila kujali mtu ni wa aina gani, hawezi kuwepo bila maono ya kazi ya Mungu, hawezi kuishi pasipo na uwepo wa Roho Mtakatifu; punde tu mtu apotezapo maono, anaingia Kuzimu na kuishi gizani. Watu wasio na maono ni wale wamfuatao Mungu kipumbavu, ni wale wasio na kazi ya Roho Mtakatifu, na wanaishi kuzimu. Watu kama hawa huwa hawafuatilii ukweli, na hulitundika jina la Mungu kama bango. Wale ambao hawafahamu kazi ya Roho Mtakatifu, ambao hawamjui Mungu katika mwili, ambao hawajui hatua tatu za kazi katika uzima wa usimamizi wa Mungu—hawajui maono na hivyo wanaishi bila ukweli. Je, si wale wote wasiokuwa na ukweli ni watenda maovu? Wale wanaotaka kuweka ukweli katika vitendo, ambao wako tayari kuutafuta ufahamu wa Mungu, na ambao kwa kweli wanashirikiana na Mungu ni watu ambao maono yanakuwa msingi wao. Wanakubaliwa na Mungu kwa sababu wanashirikiana na Mungu na ushirika huu ndio ambao unafaa kuwekwa katika vitendo na mwanadamu.
Katika maono kuna njia nyingi zinazoelekea kwa vitendo. Matakwa ya utendaji yaliyopo kwa mwanadamu yamo pia ndani ya maono sawa tu na kazi ya Mungu inayopaswa kufahamika na mwanadamu. Katika mikutano maalum ya zamani au mikutano mikuu iliyokuwa katika sehemu mbalimbali, ni kipengele kimoja tu cha vitendo kilichozungumziwa. Vitendo kama hivyo ni vile vilivyotiwa katika vitendo katika Enzi ya Neema na hapakuwa na mfanano wowote na ufahamu wa Mungu kwani maono ya Enzi ya Neema yalikuwa tu maono ya kusulubiwa kwa Yesu, na hapakuwa na maono ya juu zaidi. Mwanadamu hakuhitajika kujua zaidi ya kazi Yake ya ukombozi wa mwanadamu kupitia kusulubiwa, na kwa hivyo katika Enzi ya Neema hapakuwa na maono mengine ya kufahamiwa na mwanadamu. Kwa njia hii, mwanadamu alikuwa na ufahamu mdogo sana wa Mungu na mbali na upendo na huruma za Yesu, kulikuwa na vitu vichache tu vya mwanadamu kuweka katika vitendo, vitu ambavyo vilikuwa tofauti na hali ya leo. Zamani, haikujalisha ni aina gani ya mkutano, mwanadamu hakuwa na uwezo wa kuzungumzia ufahamu wa vitendo wa kazi ya Mungu, aidha hapakuwa na yeyote aliyeweza kusema kwa dhahiri njia iliyokuwa sawa ya utendaji kwa mwanadamu kuiingilia. Aliongeza tu mambo kidogo katika msingi wa stahamala na uvumilivu; hapakuwa na mabadiliko yoyote katika kiini cha vitendo vyake kwani katika enzi hiyo Mungu hakufanya kazi yoyote mpya na matakwa ya pekee Aliyomwekea mwanadamu yalikuwa stahamala na uvumilivu, au kuubeba msalaba. Mbali na vitendo kama hivyo, hapakuwa na maono ya juu zaidi kuliko yale ya kusulubishwa kwa Yesu. Zamani hapakutajwa maono mengine kwa sababu Mungu hakufanya kazi kubwa na kwa sababu Alimwekea mwanadamu matakwa machache. Kwa njia hii, haikujalisha mwanadamu alifanya nini, hakuweza kuivuka mipaka ya viwango hivi, viwango ambavyo vilikuwa rahisi na vya juu juu vya mwanadamu kuweka katika vitendo. Leo Nazungumzia maono mengine kwa kuwa leo kazi nyingi zaidi imefanywa, kazi ambayo ni mara kadha zaidi ya ile ya Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema. Yanayohitajika kwa mwanadamu, aidha, ni mara kadhaa juu zaidi kuliko enzi zilizopita. Iwapo mwanadamu hana uwezo wa kuijua kikamilifu kazi kama hiyo, basi haitakuwa na umuhimu mkubwa; inaweza kuchukuliwa kuwa mwanadamu atakuwa na ugumu kuifahamu kazi yenyewe kikamilifu ikiwa hawezi kuitengea maisha yake yote. Katika kazi ya ushindi, kuzungumzia tu njia ya vitendo kutaufanya ushindi wa mwanadamu kuwa jambo lisilowezekana. Mazungumzo ya maono tu bila matakwa yoyote kwa mwanadamu vilevile kutaufanya ushindi wa mwanadamu kuwa jambo lisilowezekana. Iwapo hapana kitu kingine kitakachoweza kuzungumziwa ila tu njia ya vitendo, basi ingekuwa vigumu kuuweza udhaifu wa mwanadamu, au kuondoa dhana za mwanadamu, na vilevile itakuwa vigumu kumshinda mwanadamu. Maono ni zana muhimu ya ushindi wa mwanadamu, na bado pasingelikuwepo na njia tofauti na maono basi mwanadamu asingelikuwa na njia ya kufuata wala jinsi ya kuingia. Hii imekuwa kanuni ya kazi ya Mungu toka mwanzo hadi mwisho: Katika maono kuna kile ambacho chaweza kuwekwa katika vitendo, na vivyo hivyo kuna maono ambayo hayana vitendo hivyo. Kiwango cha mabadiliko katika maisha na tabia za mwanadamu huambatana na mabadiliko katika maono. Kama mwanadamu angetegemea tu juhudi zake, basi ingekuwa vigumu kwake kufikia kiwango cha juu cha mabadiliko. Maono huzungumzia kazi ya Mungu Mwenyewe na usimamizi wa Mungu. Utendaji hurejelea njia ya vitendo vya mwanadamu na kwa namna ya maisha ya mwanadamu; katika usimamizi wote wa Mungu, uhusiano baina ya maono na vitendo ni uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu. Maono yangetolewa au yangezungumziwa bila kuhusishwa na vitendo, ama kungekuwa tu na maono na vitendo vya mwanaadamu viondolewe, basi vitu kama hivyo visingechukuliwa kama usimamizi wa Mungu, wala isingesemwa kwamba kazi ya Mungu ni kwa ajili ya wanadamu; kwa namna hii, si tu kwamba wajibu wa mwanadamu ungeondolewa, bali pia kazi ya Mungu ingekosa kusudi. Iwapo tangu mwanzo hadi mwisho, mwanadamu angetarajiwa tu kutenda, bila kujihusisha na kazi ya Mungu, na, zaidi ya hayo, kama mwanadamu asingetarajiwa kuifahamu kazi ya Mungu, basi kazi hiyo isingeitwa usimamizi wa Mungu. Kama mwanadamu hangemjua Mungu, na hangejua mapenzi ya Mungu, na huendelea kufanya vitendo kidhahania bila kuwa na uwazi, basi asingekuwa kiumbe kilichohitimu. Hivyo basi, hivi vitu viwili ni vya lazima. Kama kungekuwepo kazi ya Mungu tu, ambayo ni kusema, kungekuwepo maono pekee na hakungekuwepo na ushirikiano au vitendo kutoka kwa mwanadamu, basi hivyo vitu visingeitwa usimamizi wa Mungu. Iwapo kungekuwa tu na vitendo na kuingia kwa mwanadamu, basi bila kujali kuingia kwa mtu kungekuwa kwa juu kiasi gani, haya, pia, hayangekubalika. Kuingia kwa mwanadamu kunafaa kubadilika taratibu kulingana na kazi na maono; hakuwezi kubadilika ghafla. Kanuni za vitendo vya mwanadamu haziko huru na bila vizuizi, lakini ziko ndani ya mipaka fulani. Kanuni hizo hubadilika kwa hatua sawa na maono ya kazi. Hivyo basi usimamizi wa Mungu hatimaye huishia katika kazi ya Mungu na vitendo vya mwanadamu.
Kazi ya usimamizi ilikuja tu kwa ajili ya wanadamu, yaani ilitolewa kwa ajili ya uwepo wa wanadamu. Usimamizi haukuwepo kabla ya uwepo wa wanadamu au mwanzo wakati mbingu na nchi na vilivyomo vilipoumbwa. Iwapo, katika kazi nzima ya Mungu, hakungekuwa na vitendo vinavyomfaidi mwanadamu, yaani kama Mungu asingeweka matakwa maalum kwa mwanadamu aliyepotoka (ikiwa kazi ifanywayo na Mungu haikuwa na njia nzuri ya vitendo vya mwanaadamu), basi kazi hii isingeitwa usimamizi wa Mungu. Iwapo kazi nzima ya Mungu ingehusisha tu kuwaambia wanadamu waliopotoka jinsi ya kuendeleza vitendo vyao, na Mungu hakuendeleza kazi yoyote ya mipango Yake, na Hakuonyesha uwepo wake wa daima au busara, basi bila kujali ni jinsi gani matakwa ya Mungu kwa mwanadamu yangewekwa juu, bila kujali Mungu aliishi muda mrefu kiasi gani miongoni mwa wanadamu, mwanadamu asingejua chochote juu ya tabia ya Mungu; kama ingekuwa hivyo, basi kazi hii isingeweza kukaribia kuitwa usimamizi wa Mungu. Kwa ufupi, kazi ya usimamizi wa Mungu ni kazi iliyofanywa na Mungu na kazi zote zilizofanywa chini ya uongozi wa Mungu na wale ambao wamepatikana na Mungu. Kazi kama hiyo inaweza kuchukuliwa kwa ufupisho kama usimamizi, na inaelezea kazi ya Mungu miongoni mwa wanadamu na vilevile ni ushirikiano Wake na wale wanaomfuata; kwa ujumla, hayo yote yanaweza kuitwa usimamizi. Hapa kazi ya Mungu inaitwa maono na ushirikianao wa mwanadamu unaitwa vitendo. Kadiri kazi ya Mungu ilivyo juu (yaani kadiri maono yalivyo juu), ndivyo tabia za Mungu zinakuwa wazi kwa mwanadamu, na kutoafikiana na mawazo ya mwanadamu, na ndivyo vitendo na ushirikiano wa mwanadamu huwa vya juu. Kadiri matakwa kwa mwanadamu yanavyokuwa ya juu, ndivyo kazi ya Mungu inavyotofautiana mawazo ya mwanadamu, matokeo yake yakiwa majaribu ya mwanadamu, na viwango anavyotarajiwa kuwa navyo, vilevile vinakuwa vya juu. Katika hatima ya kazi hii, maono yote yatakuwa yametimizwa, na yale yote mwanadamu anapaswa kuweka katika vitendo yatakuwa yamefikia kilele cha ukamilifu. Huu ndio wakati pia ambapo kila kitu kitawekwa katika kundi lake kwani kile kinachopaswa kufahamika na mwanadamu kitakuwa kimebainishwa kwake. Kwa hivyo maono yatakapofikia upeo wa juu, vivyo hivyo kazi nayo itakaribia hatima yake na vitendo vya mwanadamu vitakuwa vimefikia ufanisi wake. Vitendo vya mwanadamu vimekitwa katika kazi ya Mungu, na usimamizi wa Mungu unadhihirika tu kupitia vitendo na ushirikiano wa mwanadamu. Mwanadamu ni mfano wa kazi ya Mungu, na mlengwa wa kazi ya usimamizi mzima wa Mungu, na pia mazao ya kazi ya usimamizi wote wa Mungu. Iwapo Mungu angefanya kazi peke yake bila ushirika wa mwanadamu, basi pasingekuwepo na kitu cha kudhihirisha kazi Yake nzima na kwa hali hiyo kusingekuwa na umuhimu hata kidogo wa usimamizi wa Mungu. Ni kwa kuchagua tu chombo kifaacho kilicho nje ya kazi ya Mungu, na kinachoweza kudhihirisha kazi hii, na kuthibitisha kudura na busara zake, je, inawezekana kufikia dhumuni la usimamizi wa Mungu na kufikia dhumuni la kutumia kazi hii yote ili kumshinda kabisa Shetani. Na kwa hivyo mwanadamu ni sehemu muhimu katika kazi ya usimamizi ya Mungu, na mwanadamu ndiye pekee anayeweza kuifanya kazi ya usimamizi ya Mungu izae matunda na kufikia lengo Lake kuu; mbali na mwanadamu, hakuna kiumbe kingine chenye uhai kinachoweza kuchukua nafasi hiyo. Ikiwa mwanadamu atakuwa dhihirisho kamili la kazi ya usimamizi, basi uasi wa wanadamu wenye maovu lazima utokomezwe. Hii inahitaji kuwa mwanadamu apewe utendaji ufaao kwa kila muktadha, na kwamba Mungu afanye kazi inayotangamana miongoni mwa wanadamu. Ni kwa njia hii tu ndipo kutakuwa na kundi la watu waliokubaliwa ambao ni dhihirisho la kazi ya usimamizi. Kazi ya Mungu miongoni mwa wanadamu haiwezi kuwa ushuhuda kwa Mungu Mwenyewe kupitia kazi ya Mungu peke yake; ushuhuda huo vilevile unahitaji wanadamu ambao wanafaa ili kazi yake iafikiwe. Mwanzo Mungu atawatayarisha watu hawa ambao kupitia kwao kazi Yake itadhihirika na ushuhuda Wake utachukuliwa miongoni mwa viumbe. Kwa hili, Mungu atakuwa ameafiki lengo la kazi Yake. Mungu hafanyi kazi peke Yake kumshinda Shetani kwa sababu Mungu hawezi kujishuhudia Mwenyewe moja kwa moja miongoni mwa viumbe wote. Angefanya hivyo, ingekuwa vigumu kumshawishi mwanadamu, kwa hivyo Mungu lazima Afanye kazi kwa mwanadamu ili kumshinda na ndipo Atakapoweza kupata ushuhuda miongoni mwa viumbe vyote. Mungu angefanya kazi peke Yake bila kushirikiana na mwanadamu, au kama mwanadamu asingetakiwa kushirikiana, basi mwanadamu asingeitambua tabia ya Mungu na daima asingefahamu nia ya Mungu; na kwa hali hii haiwezi kuitwa usimamizi wa Mungu. Mwanadamu mwenyewe angejizatiti, na kutafuta, na kufanya bidii, bila kuifahamu kazi ya Mungu, basi mwanadamu angekuwa anafanya mizaha. Bila kazi ya Roho Mtakatifu, akifanyacho mwanadamu ni cha Shetani, ni muasi na mtenda maovu; Shetani anadhihirika katika yote yafanywayo na mwanadamu mwenye maovu na hamna kinachoafikiana na Mungu, na yote ni dalili ya Shetani. Hakuna kati ya vilivyozungumziwa kisichokuwa na maono na vitendo. Katika msingi wa maono, mwanadamu hupata vitendo, anapata njia ya utiifu, ili kwamba aweze kuweka kando mawazo yake ili apate vile ambavyo hajawahi kuwa navyo hapo awali. Mungu huhitaji mwanadamu ashirikiane naye, kwamba mwanadamu asikilize matakwa Yake, na mwanadamu ashikilie kazi ifanywayo na Mungu Mwenyewe na kuupitia uwezo mkubwa wa Mungu na kuifahamu tabia ya Mungu. Kwa kifupi, haya ndiyo usimamizi wa Mungu. Ushirika wa Mungu na mwanadamu ndio usimamizi, na ni usimamizi mkuu zaidi.
Kile kinachohusisha maono kimsingi hurejelea kazi ya Mungu Mwenyewe, na kile kinachohusisha vitendo ni sharti kifanywe na mwanadamu, na hakina uhusiano na Mungu. Kazi ya Mungu hukamilishwa na Mungu Mwenyewe, na vitendo vya mwanadamu hufikiwa na mwanadamu mwenyewe. Kile ambacho ni sharti kifanywe na Mungu Mwenyewe hakihitajiki kufanywa na mwanadamu, na kile kitendwacho na mwanadamu hakihusiani na Mungu. Kazi ya Mungu ni huduma Yake Mwenyewe na haina uhusiano na mwanadamu. Hii kazi haihitaji kufanywa na mwanadamu, na hata zaidi, mwanadamu hatakuwa na uwezo wa kufanya kazi ambayo ni ya kufanywa na Mungu. Kile ambacho kinafaa kutendwa na mwanadamu ni sharti kitimizwe na mwanadamu, iwe ni kujitoa kafara au kuwasilishwa kwake kwa Shetani ili kushuhudia—haya ni lazima yatimizwe na mwanadamu. Mungu Mwenyewe anatimiza kazi Yake yote, na kile ambacho ni wajibu wa mwanadamu, mwanadamu hufunuliwa na kazi iliyobaki huachiwa mwanadamu. Mungu hafanyi kazi ya ziada. Anafanya ile kazi iliyo katika huduma Yake na kumuonyesha mwanadamu na kumfunulia njia tu bali hampambanulii njia; hili lazima lieleweke kwa mwanadamu. Kuweka ukweli katika vitendo kunamaanisha kuweka neno la Mungu katika vitendo, na haya yote ni wajibu wa mwanadamu, ni kile kinachofaa kufanywa na mwanadamu, na wala halihusiani na Mungu. Iwapo mwanadamu atataka Mungu apitie masaibu na utakaso katika ukweli sawa na mwanadamu, basi mwanadamu atakuwa hatii. Kazi ya Mungu ni kuendeleza huduma Yake, na wajibu wa mwanadamu ni kutii uongozi wote wa Mungu, bila pingamizi yoyote. Kinachotakiwa kufikiwa na mwanadamu anawajibika kutimiza, bila kujali ni namna gani Mungu hufanya kazi au kuishi. Ni Mungu Mwenyewe tu ndiye anayeweza kumwekea mwanadamu matakwa, ambayo ni kusema, ni Mungu Mwenyewe tu ndiye anayestahili kumwekea mwanadamu matakwa. Mwanadamu hastahili kuwa na jingine, hastahili kufanya chochote ila tu kutii kikamilifu na kutenda; hii ndiyo busara ambayo mwanadamu anapaswa kuwa nayo. Punde kazi ifaayo kufanywa na Mungu Mwenyewe itakapokamilika, mwanadamu anatakiwa kuipitia, hatua kwa hatua. Iwapo mwishowe, baada ya usimamizi wote wa Mungu kukamilika, mwanadamu atakuwa hajafanya anachotakiwa na Mungu kufanya, basi mwanadamu anafaa aadhibiwe. Ikiwa mwanadamu hatimizi matakwa ya Mungu, basi hili ni kwa sababu ya uasi wa mwanadamu; haimaanishi kuwa Mungu hajakuwa makini vya kutosha katika kazi Yake. Wale wote wasioweka neno la Mungu katika vitendo, ambao hawatimizi matakwa ya Mungu na wale wote wasiokuwa na uaminifu na kutimiza wajibu wao—wataadhibiwa wote. Leo hii mnachohitajika kufikia si madai ya ziada, ila ni wajibu wa mwanadamu, na kile kinachofaa kufanywa na kila mtu. Kama hamuwezi hata kufanya wajibu wenu, au kuufanya vizuri, hamuoni mnajiletea masaibu nyinyi wenyewe? Hamwuoni mnajitakia kifo? Mtatarajiaje maisha ya baadaye na matarajio? Kazi ya Mungu ni kwa ajili ya wanadamu, na ushirika wa mwanadamu ni kwa minajili ya usimamizi wa Mungu. Baada ya Mungu kufanya yale yote Anayopaswa kufanya, mwanadamu anapaswa kufanya vitendo bila kukoma, na kushirikiana na Mungu. Mwanadamu hapaswi kulegeza kamba katika kazi ya Mungu, lazima aonyeshe uaminifu na asijitie katika mawazo mengi au kukaa akisubiri kifo bila kufanya kitu. Mungu Mwenyewe anaweza kujitolea kwa mwanadamu, basi ni kwa nini mwanadamu asiweze kuwa mwaminifu kwa Mungu? Mawazo na moyo wa Mungu vipo kwa mwanadamu, basi ni kwa nini mwanadamu asijitolee katika ushirika? Mungu huwafanyia wanadamu kazi, basi ni kwa nini mwanadamu asifanye wajibu wake kwa minajili ya usimamizi wa Mungu? Kazi ya Mungu imefika umbali huu, bado mnaona ila hutendi, mnasikia ila hamsogei. Je, si watu kama hawa wanafaa kuangamizwa kabisa? Tayari Mungu amejitolea kikamilifu kwa ajili ya mwanadamu, basi ni kwa nini siku hizi mwanadamu hafanyi wajibu wake kwa dhati? Kwa Mungu, kazi Yake ni ya kipaumbele Kwake, na kazi ya usimamizi Wake ni ya umuhimu wa hali ya juu. Kwa mwanadamu, kuweka maneno ya Mungu katika vitendo  na kutimiza mahitaji ya Mungu ndiyo kipaumbele kwake. Ni lazima nyote myafahamu haya. Maneno mliyoambiwa yamefika kiini halisi cha nafsi yenu, na kazi ya Mungu imefika katika maeneo ambayo hayakuwa yamefikiwa awali. Watu wengi bado hawafahamu ukweli na uongo wa njia hii; bado wanasubiri na kutazama na hawafanyi wajibu wao. Badala yake huchunguza kila neno na tendo la Mungu, wanalenga juu ya Anachokula na Anachokivaa na mawazo yao huwa hata ya kuhuzunisha zaidi. Si watu wa aina hii wanafanya msukosuko bure? Hawa wanawezaje kuwa watu wamtafutao Mungu? Wanawezaje kuwa watu wa kumnyenyekea Mungu kwa kudhamiria? Wanasahau uaminifu na wajibu wao na badala yake kujishughulisha na mahali alipo Mungu. Wanaghadhabisha! Ikiwa mwanadamu amefahamu yale yote anayopaswa kufahamu na kuweka katika vitendo yale yote anayopaswa, basi Mungu atampa mwanadamu baraka Zake, kwa sababu kile ambacho Yeye huhitaji kutoka kwa mwanadamu ni wajibu wa mwanadamu, na kile ambacho mwanadamu anastahili kufanya. Ikiwa mwanadamu hawezi kufahamu yale yote anayopaswa kufahamu na hawezi kutia katika vitendo yale anayopasa kuweka katika vitendo, basi mwanadamu ataadhibiwa. Wasioshirikiana na Mungu wana uhasama Naye, wasioikubali kazi mpya wanaipinga, hata kama watu kama hao hawafanyi chochote ambacho ni cha pingamizi dhahiri. Wale wote wasioweka ukweli unaohitajika na Mungu katika vitendo ni watu wanaopinga kwa makusudi na ni waasi wa maneno ya Mungu hata kama watu kama hawa hutilia maanani maalum kwa kazi ya Roho Mtakatifu. Watu wasiotii maneno ya Mungu na kumnyenyekea Mungu ni waasi, na wapinzani wa Mungu. Watu wasiofanya wajibu wao ni wale wasioshirikiana na Mungu, na watu wasioshirikiana na Mungu ni wale wasioikubali kazi ya Roho Mtakatifu.
Wakati kazi ya Mungu inafikia hatua fulani, na usimamizi Wake kufikia hatua fulani, wale wanaoutafuta moyo Wake wote huwa na uwezo wa kutimiza matakwa yake. Mungu humwekea mwanadamu matakwa kulingana na viwango Vyake mwenyewe, na kulingana na kile ambacho mwanadamu anaweza kufanikisha. Akiwa anazungumzia usimamizi Wake, Yeye humwonyesha njia mwanadamu , na kumpa mwanadamu namna ya kudumu. Usimamizi wa Mungu na vitendo vya mwanadamu vipo katika hatua sawia kikazi, na yote yanafanyika kwa wakati mmoja. Mazungumzo kuhusu usimamizi wa Mungu yanagusia mabadiliko katika tabia ya mwanadamu, na yanazungumzia kuhusu yale yafaayo kufanywa na mwanadamu, na mabadiliko katika tabia ya mwanadamu, hugusia kazi ya Mungu; hakuna wakati ambao haya mawili yanaweza kutenganishwa. Vitendo vya mwanadamu vinabadilika, hatua kwa hatua. Hii ni kwa sababu matakwa ya Mungu kwa mwanadamu yanabadilika na vilevile kwa sababu kazi ya Mungu hubadilika na kusonga mbele kila wakati. Iwapo vitendo vya mwanadamu vitasalia ndani ya mafundisho, hii inathibitisha kwamba amepungukiwa na kazi na mwongozo wa Mungu; ikiwa vitendo vya mwanadamu havitabadilika kamwe au kuwa na kina zaidi, basi hili ni thibitisho kwamba vitendo vya mwanadamu hutendeka kulingana na mapenzi ya mwanadamu, na si vitendo vya ukweli; ikiwa mwanadamu hana njia ya kufuata, basi tayari ameanguka mikononi mwa Shetani, na sasa amedhibitiwa na Shetani, ambayo inamaanisha kwamba amedhibitiwa na roho mchafu. Ikiwa vitendo vya mwanadamu haviendi ndani zaidi, basi kazi ya Mungu haitakua, na kama hakuna mabadiliko katika kazi ya Mungu, basi kuingia kwa mwanadamu kutakwama; hili haliepukiki. Katika kazi nzima ya Mungu, mwanadamu angejifunga katika sheria za Yehova basi kazi ya Mungu isingeendelea na zaidi ingekuwa vigumu kutamatisha enzi nzima. Iwapo mwanadamu angeshikilia msalaba daima na kuishi katika uvumilivu na unyenyekevu, basi kazi ya Mungu isingeendelea. Miaka elfu sita ya usimamizi haiwezi kusitishwa miongoni mwa watu wanaoshikilia tu sheria au kushikilia msalaba na kuishi katika uvumilivu na unyenyekevu tu. Badala yake, kazi nzima ya usimamizi wa Mungu inahitimishwa miongoni mwa watu wa siku za mwisho wanaomfahamu Mungu na ambao wamekombolewa kutoka kwa Shetani na wamejinasua kabisa kutoka katika vishawishi vya Shetani. Huu ni mwelekeo wa kazi ya Mungu usioepukika. Kwa nini inasemekana kwamba vitendo vya walio katika makanisa ya kidini vimepitwa na wakati? Ni kwa kuwa wanayoyaweka katika vitendo ni tofauti na kazi ya leo. Katika Enzi ya Neema, walichotenda kilikuwa sahihi, ila kwa kuwa enzi yenyewe imepita na kazi ya Mungu kubadilika, vitendo vyao hatua kwa hatua vimepitwa na wakati. Vimeachwa nyuma na kazi mpya na mwangaza mpya. Ikiwa imesimama juu ya msingi wake asili, kazi ya Roho Mtakatifu imepiga hatua kadhaa kwa kina. Na bado watu hao wamebaki katika hatua ya asili ya kazi ya Mungu na bado wanapenyeza katikati ya vitendo na mwangaza wa zamani. Kazi ya Mungu yaweza kubadilika pakubwa kwa miaka mitatu au mitano, hivyo si mabadiliko hata makubwa zaidi yaweza kuja kwa kipindi cha miaka zaidi ya 2000? Ikiwa mwanadamu hana vitendo vipya ama mwangaza mpya, inamaanisha hajaenda sawia na kazi ya Roho Mtakatifu. Hili ni anguko la mwanadamu; uwepo wa kazi mpya ya Mungu hauwezi kukanwa kwa sababu, leo hii, wale walio na kazi asili ya Roho Mtakatifu bado wanashikilia vitendo vilivyopitwa na wakati. Kazi ya Roho Mtakatifu daima inasonga mbele, na wote walio katika mkondo wa Roho Mtakatifu wanafaa waendelee mbele na kubadilika, hatua kwa hatua. Hawapaswi kukwama katika hatua moja. Ni wale tu wasioifahamu kazi ya Roho Mtakatifu ndio wanaweza kubaki katika hatua ya kazi ya Mungu ya awali na wasikubali kazi mpya ya Roho Mtakatifu. Ni wale tu walio waasi ndio watakosa uwezo wa kuipokea kazi ya Roho Mtakatifu. Ikiwa vitendo vya mwanadamu haviendani na mwendo wa kazi mpya ya Roho Mtakatifu, basi vitendo vya mwanadamu hakika vimetengana na kazi ya leo na kwa hakika havilingani na kazi ya leo. Watu waliopitwa na wakati kama hawa hawawezi kutimiza mapenzi ya Mungu, na zaidi hawawezi kuwa wale watu wa mwisho ambao watamshuhudia Mungu. Aidha, kazi nzima ya usimamizi haiwezi kutimilika miongoni mwa kundi la watu kama hao. Kwa wale walioshikilia sheria za Yehova kipindi fulani, na wale walioumia wakati fulani chini ya msalaba, ikiwa hawawezi kukubali hatua ya kazi ya siku za mwisho, basi yale yote waliyofanya ni bure na yasiyofaa. Dhihirisho la wazi zaidi wa kazi ya Roho Mtakatifu ni kwa kuyakumbatia ya sasa, sio kushikilia ya zamani. Wale ambao hawajiendelezi na kazi ya leo, na wale ambao wametengwa na utendaji wa leo, ni wale wanaopinga na hawaikubali kazi ya Roho Mtakatifu. Watu kama hao wanaipinga kazi ya Mungu ya sasa. Ijapokuwa wanashikilia nuru ya zamani, hili halimaanishi kwamba inaweza kukanwa kwamba hawajui kazi ya Roho Mtakatifu. Kwa nini kumekuwepo na mjadala huu wote kuhusu mabadiliko katika vitendo vya mwanadamu, kuhusu tofauti za utendaji kati ya zamani na sasa, kuhusu jinsi utendaji ulivyokuwa katika enzi za awali na jinsi ulivyo sasa? Migawanyiko kama hiyo katika vitendo vya mwanadamu hujadiliwa kwa sababu kazi ya Roho Mtakatifu daima inasonga mbele na kwa hivyo vitendo vya mwanadamu vinapaswa kubadilika daima. Ikiwa mwanadamu atasalia amekwama katika hatua moja tu, basi hili linaonyesha kuwa haendi sawia na kazi ya Mungu na mwangaza mpya; haimaanishi kuwa mpango wa usimamizi wa Mungu haujabadilika. Walio nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu daima hudhani wako sahihi, lakini kwa hakika, kazi ya Mungu ndani yao ilisita zamani na kazi ya Roho Mtakatifu haimo ndani yao. Kazi ya Mungu imeshahamishiwa kwa kundi jingine la watu, kundi ambalo kwalo Anapania kukamilishia kazi Yake mpya. Kwani walio kwenye dini hawawezi kuikubali kazi mpya ya Mungu, na kushikilia tu kazi kongwe za zamani, hivyo Mungu amewaacha watu hawa na anafanya kazi Yake mpya kwa watu wanaoikubali kazi hii mpya. Hawa ni watu wanaoshiriki katika kazi Yake mpya, na usimamizi Wake utatimilika kwa njia hii tu. Usimamizi wa Mungu daima unasonga mbele na vitendo vya mwanadamu daima vinapanda juu. Mungu daima anafanya kazi na mwanadamu mara zote ni mhitaji ili kwamba wote wanafikia upeo wao, Mungu na mwanadamu wamo katika muungano kikamilifu. Haya ni maonyesho ya kutimilika kwa kazi ya Mungu, na ndiyo matokeo ya mwisho ya kazi nzima ya usimamizi.
Katika kila hatua ya kazi ya Mungu yapo matakwa sawia kwa mwanadamu. Wale wote walio kwenye mkondo wa Roho Mtakatifu wanamilikishwa na uwepo na nidhamu ya Roho Mtakatifu na wasiokuwemo kwenye mkondo wa Roho Mtakatifu wako chini ya utawala wa Shetani na hawana kazi yoyote ya Roho Mtakatifu. Walio kwenye mkondo wa Roho Mtakatifu ni wale walioikubali kazi mpya ya Mungu, wanaoshiriki katika kazi mpya ya Mungu. Iwapo walio ndani ya mkondo huu hawana uwezo wa kushirikiana, na hawawezi kuweka ukweli unaotakiwa na Mungu katika vitendo wakati huu, basi watafundishwa nidhamu, na vibaya zaidi kuachwa na Roho Mtakatifu. Wale ambao wanakubali kazi mpya ya Roho Mtakatifu, wataishi kwenye mkondo wa Roho Mtakatifu, wapokee huduma na ulinzi wa Roho Mtakatifu. Wale ambao wako tayari kuweka ukweli katika vitendo wanapewa nuru na Roho Mtakatifu na wale wasiotaka kuweka ukweli katika vitendo wanafundishwa nidhamu na Roho Mtakatifu na huenda wakaadhibiwa. Bila kujali ni aina gani ya watu, ilimradi tu wamo kwenye mkondo wa Roho Mtakatifu, Mungu atawawajibikia wote wanaoikubali kazi Yake mpya kwa minajili ya jina Lake. Wale wanaolitukuza jina Lake na wako radhi kuweka maneno Yake katika vitendo watapokea baraka Zake; wale wasiomtii na kuyaweka maneno Yake katika vitendo watapokea adhabu Yake. Watu walio kwenye mkondo wa Roho Mtakatifu ni wale wanaoikubali kazi mpya, na kwa sababu wameikubali kazi mpya, wanafaa kuwa na ushirika na Mungu na hawafai kuwa kama waasi wasiofanya wajibu wao. Hili ndilo sharti pekee la Mungu kwa mwanadamu. Sio hivyo na watu wasioikubali kazi mpya: Wako nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu, na adhabu na lawama ya Roho Mtakatifu haitumiki kwao. Kila siku hawa watu wanaishi katika mwili, wanaishi katika mitazamo yao, na yote wayafanyayo ni kulingana na mafundisho ya kidini yaliyozalishwa na uchanganuzi pamoja na utafiti wa bongo zao. Si matakwa ya kazi mpya ya Roho Mtakatifu wala sio ushirika na Mungu. Wale wasioikubali kazi mpya ya Mungu wanajinyima uwepo wa Mungu na, zaidi, wanakosa baraka na ulinzi wa Mungu. Mengi ya maneno na matendo yao yanashikilia matakwa ya zamani ya kazi ya Roho Mtakatifu; ni mafundisho ya kidini tu na wala si ukweli. Mafundisho na taratibu kama hizo ni thibitisho la kutosha kuwa kitu cha pekee kinachowaleta pamoja ni dini; si watu walioteuliwa au vyombo vya kazi ya Mungu. Mikutano ya wote walio miongoni mwao haiwezi kuitwa kanisa bali mkutano mkubwa wa watu wa dini. Huu ni ukweli usioweza kubadilishwa. Hawana kazi mpya ya Roho Mtakatifu; wakifanyacho kinanuka dini, wanachodhihirisha katika maisha yao kimejaa dini; hawana uwepo na kazi ya Roho Mtakatifu, na zaidi hawajahitimu kupokea adhabu au kupata nuru ya Roho Mtakatifu. Watu hawa wote ni miili isiyokuwa na uhai, na funza wasiokuwa na mambo ya kiroho. Hawana ufahamu wa uasi na pingamizi wa mwanadamu, hawana ufahamu wa uovu wote wa mwanadamu na hata zaidi, hawaifahamu kazi ya Mungu na mapenzi ya sasa ya Mungu. Wote ni wapumbavu, waovu, ni watu duni wasiostahili kuitwa waumini! Hakuna wafanyacho kinachoambatana na usimamizi wa Mungu, wala hakiwezi kuidhoofisha mipango ya Mungu. Maneno na matendo yao yanaudhi sana, yanasikitisha mno, na hayafai kutajika. Chochote wakifanyacho walio nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu hakihusiani na kazi mpya ya Roho Mtakatifu. Kwa sababu hii, haijalishi wanafanya nini, hawana adhabu ya Roho Mtakatifu na zaidi, hawana nuru ya Roho Mtakatifu. Kwani wao ni watu wasiopenda ukweli, na wametokwa na kukataliwa na Roho Mtakatifu. Wanaitwa watenda maovu kwani wanatembea katika mwili, na kufanya chochote kiwafurahishacho kwa kisingizio cha bango la Mungu. Mungu anapofanya kazi, wao wanakuwa maadui kwake kwa makusudi, na kumkimbia Mungu. Kutoshirikiana kwa mwanadamu na Mungu ni uasi wa hali ya juu, bila kutaja kutoroka makusudi kwa watu hawa kutoka kwa Mungu. Basi, je, hawatapokea malipo wanayostahili? Uovu wa hawa watu ukitajwa, baadhi ya watu huwalaani huku Mungu akiwapuuza. Kwa mwanadamu, inaonekana kana kwamba matendo ya watu hawa yanajihusisha na jina la Mungu, ila kwa hakika, kwa Mungu, matendo haya hayana uhusiano wowote na jina Lake au ushuhuda Wake. Bila kujali wanachokifanya hawa watu, hakihusiani na Mungu: hakihusiani na kazi Yake na jina Lake leo. Hawa watu hujiaibisha wenyewe na kumdhihirisha Shetani; ni watenda maovu wanaosubiri siku ya ghadhabu. Sasa, bila kujali matendo yao ni yapi, mradi tu hawazuii usimamizi wa Mungu na hawafanyi chochote kuhusiana na kazi mpya ya Mungu, watu kama hao hawatapata adhabu inayolingana na matendo yao sasa kwa kuwa siku ya ghadhabu bado haijatimia. Yapo mengi ambayo watu wanaamini kuwa Mungu angekuwa ameyashughulikia tayari na kufikiri kuwa wale watenda maovu wanastahili kuadhibiwa haraka iwezekanavyo. Lakini kwa sababu kazi ya usimamizi wa Mungu bado haijafikia kikomo, na siku ya ghadhabu haijatimia, waovu bado wanaendelea kutenda matendo yao maovu. Watu wengine husema kuwa walio ndani ya dini hawana uwepo au Kazi ya Roho Mtakatifu, na kwamba wanaliletea aibu jina la Mungu; basi ni kwa nini Mungu asiwaangamize, badala ya kuendelea kustahimili ufidhuli wao? Watu hawa ambao ni dhihirisho la Shetani na ambao ni wa mwili, ni wapumbavu, wa hali duni, ni watu wasio na busara. Hawataiona ghadhabu ya Mungu kabla ya kuelewa jinsi Mungu anavyofanya kazi Yake miongoni mwa wanadamu, na wakishashindwa kabisa, hao watenda maovu wote watalipwa stahili yao na hamna hata mmoja kati yao atakayeweza kuiepuka siku ya ghadhabu. Sasa si wakati wa adhabu ya mwanadamu, ila ni wakati wa kuendeleza kazi ya ushindi, isipokuwa wawepo wanaoizuia kazi ya usimamizi wa Mungu, ambapo wataadhibiwa kulingana na uzito wa matendo yao. Katika kipindi cha usimamizi wa Mungu kwa wanadamu, wote walio ndani ya mkondo wa Roho Mtakatifu huwa na uhusiano na Mungu. Wale wanaochukiwa na kukataliwa na Roho Mtakatifu huishi katika ushawishi wa Shetani na kile wawekacho katika vitendo hakina uhusiano na Mungu. Wanaoikubali kazi mpya ya Mungu, na wanaoshirikiana na Mungu ndio tu wana uhusiano Naye, kwani kazi ya Mungu inakusudiwa tu kwa watu wanaoikubali wala si watu wote, haijalishi kama wanaikubali au la. Kazi inayofanywa na Mungu daima ina kusudi, na haifanywi bure. Walio na uhusiano na Shetani hawafai kuwa na ushuhuda kwa Mungu, na hata zaidi hawafai kushirikiana na Mungu.
Kila hatua ya kazi ya Roho Mtakatifu inahitaji ushuhuda sawia kutoka kwa mwanadamu. Kila hatua ya kazi ni vita kati ya Mungu na Shetani, na mlengwa katika vita hivi ni Shetani, huku atakayekamilishwa na kazi hii ni mwanadamu. Kazi ya Mungu kuzaa au kutozaa matunda inategemea na jinsi ushuhuda wa mwanadamu ulivyo. Huu ushuhuda ndio Mungu anaohitaji kutoka kwa wale wanaomfuata; ni ushuhuda unaofanywa mbele ya Shetani, na unaothibitisha athari za kazi Yake. Usimamizi mzima wa Mungu umegawika kwa hatua tatu, na katika kila hatua, mahitaji yanayopatana yanatokana na mwanadamu. Aidha, kadri enzi zinavyopita na kuendelea, mahitaji ya Mungu kwa wanadamu huongezeka hata zaidi. Kwa hiyo, hatua kwa hatua, kazi hii ya usimamizi wa Mungu hufikia kilele chake, hadi mwanadamu aamini ukweli wa “kuonekana kwa Neno katika mwili,” na hivyo mahitaji ya mwanadamu huongezeka hata zaidi, na mahitaji ya mwanadamu kutoa ushuhuda huongezeka hata zaidi. Kadiri mwanadamu alivyo na uwezo wa kushirikiana na Mungu kikamilifu, ndivyo anavyozidi kumtukuza Mungu. Ushirikiano wa mwanadamu ndio ushuhuda anaohitajika kuwa nao, na huo ushuhuda ndio matendo ya mwanadamu. Kwa hivyo, kazi ya Mungu iwe au isiwe na athari inayohitajika, au pawepo ama pasiwepo ushuhuda wa kweli, ni mambo ambayo yameunganishwa na ushuhuda wa mwanadamu. Wakati kazi itakapokwisha, yaani, wakati usimamizi wa kazi ya Mungu utakapofikia kikomo, Mwanadamu atahitajika kuwa na ushuhuda wa hali ya juu, na wakati kazi ya Mungu itakapofika mwisho wake, matendo na kuingia kwa mwanadamu vitafikia kilele chake. Wakati wa kale, mwanadamu alihitajika kuzingatia sheria na amri, na alihitajika kuwa mpole na mnyenyekevu. Leo, mwanadamu anahitajika kutii mipango yote ya Mungu na awe na upendo mkuu wa Mungu, na zaidi bado anahitajika kumpenda Mungu katika mateso. Hatua hizi tatu ndizo Mungu anazozitazamia toka kwa mwanadamu, hatua kwa hatua, katika usimamizi Wake wote. Kila hatua ya kazi ya Mungu huzidisha kina kuliko iliyopita, na katika kila hatua, mahitaji ya mwanadamu ni makubwa kuliko yaliyopita, na kwa hali hii, umbo la usimamizi mzima wa Mungu huonekana. Ni hasa kwa sababu mahitaji ya mwanadamu kila mara huwa juu kuliko tabia yake inavyoweza kufikia viwango anavyovihitaji Mungu, na ni hapo ambapo wanadamu wataanza kujiondoa polepole kutoka kwa ushawishi wa Shetani, ndipo kazi ya Mungu itafikia kikomo, wanadamu wote watakuwa wameokolewa kutoka kwa ushawishi wa Shetani. Wakati huo utakapowadia, kazi ya Mungu itakuwa imefika mwisho, na ushirikiano wa mwanadamu na Mungu ili abadilishe tabia zake hautakuwepo, na wanadamu wote wataishi kwenye nuru ya Mungu, na kuanzia hapo kuendelea, hapatakuwa na uasi au upinzani wowote kwa Mungu. Aidha Mungu hatamwekea matakwa mwanadamu, na patakuwepo na ushirikiano mwema zaidi kati ya mwanadamu na Mungu, mojawapo ikiwa maisha ya mwanadamu na Mungu pamoja, maisha ambayo yatafuatia baada ya usimamizi wa Mungu kukamilishwa, na baada ya mwanadamu kuokolewa toka katika mafumbato ya Shetani. Wale ambao hawatafuata kwa ukaribu nyayo za Mungu hawatakuwa na uwezo wa kufikia maisha hayo. Watakuwa wamejishusha ndani ya giza, ambapo watalia na kusaga meno; hao ndio watu wanaoamini katika Mungu lakini hawamfuati Yeye, wanaoamini katika Mungu lakini hawatii kazi Yake yote. Kwa kuwa mwanadamu anamwamini Mungu, ni sharti afuate kwa ukaribu nyayo Zake, hatua kwa hatua; anapaswa “kumfuata Mwanakondoo popote Aendapo.” Hawa tu ndio watu wanaotafuta njia ya kweli, na wao ndio wanafahamu kazi ya Roho Mtakatifu. Watu wanaofuata tu nyaraka na mafundisho ya dini kiutumwa ni wale ambao wameondolewa na kazi ya Roho Mtakatifu. Katika kila kipindi cha wakati, Mungu ataanza kazi mpya, na katika kila kipindi, patakuwepo na mwanzo mpya kwa mwanadamu. Laiti mwanadamu angeshikilia ukweli kwamba “Yehova ni Mungu” na “Yesu ni Kristo,” ukweli ambao unazingatiwa kwa kipindi kimoja, basi mwanadamu hataweza kwenda sambamba na kazi ya Roho Mtakatifu, na daima hataweza kupokea kazi ya Roho Mtakatifu. Bila kujali jinsi Mungu anavyofanya, mwanadamu anafaa kufuata bila shaka lolote, na afuate kwa ukaribu. Kwa jinsi hii basi itakuwaje mwanadamu aondolewe na Roho Mtakatifu? Bila kujali kile anachofanya Mungu, kama mwanadamu ana uhakika ni kazi ya Roho Mtakatifu, na kushirikiana katika kazi ya Roho Mtakatifu bila mashaka yoyote, na kujaribu kufikia mahitaji ya Mungu, basi ataadhibiwaje? Kazi ya Mungu kamwe haijasimama, hatua Zake hazijakwama na kabla kukamilisha kazi Yake ya usimamizi, siku zote Mungu amekuwa mwenye kazi nyingi, na kamwe hajasimama. Lakini mwanadamu ni tofauti: Kutokana na kupata kiwango cha chini cha nguvu za Roho Mtakatifu, yeye huchukulia kwamba hakuna chochote kitakachobadilika; baada ya kupata ufahamu kidogo, hajipi msukumo wa kufuata nyayo za kazi mpya ya Mungu; licha ya kwamba ameona kiasi kazi ya Mungu, yeye anamchukulia Mungu kama kifaa, aina fulani ya umbo la sanamu ya mti, na anaamini kwamba Mungu atasalia kuwa hivyo daima kwani hali imekuwa hii tangu hapo awali na hata katika siku zijazo; akiwa amepata ufahamu wa kijuujuu, mwanadamu ni mwenye kiburi hivi kwamba hujisahau na kuanza kutangaza kwa fujo tabia ya Mungu na hali ya Mungu ambayo haipo; na akiwa amejifunga katika hatua moja ya Roho Mtakatifu, pasi kujali ni mtu wa aina gani ambaye anatangaza kazi mpya ya Mungu, mwanadamu huwa haikubali. Hawa ni watu ambao hawawezi kuikubali kazi mpya ya Roho Mtakatifu; ni watu wenye kushikilia ukale sana, na hawawezi kukubali mambo mapya. Watu kama hawa ni watu wanaomwamini Mungu lakini wakati uo huo wanamkataa Mungu. Mwanadamu anaamini kwamba wana wa Israeli walikosea “tu kumuamini Yehova na kukosa kumuamini Yesu,” huku watu wengi wakiiga jukumu ambapo “humwamini Yehova tu na kumkataa Yesu” na “kusubiri kwa hamu kurejea kwa Masihi lakini wanamkataa Masihi ambaye ni Yesu”. Ndiyo maana, basi, watu wengi bado wanaishi chini ya mamlaka ya Shetani baada ya kukubali hatua moja tu ya Roho Mtakatifu na bado hawapokei baraka za Mungu. Je, si hii ni kutokana na uasi wa mwanadamu? Wakristo ulimwenguni kote ambao hawajazingatia kazi mpya ya sasa wote wameshikilia imani kwamba wao ni wenye bahati na kwamba Mungu atawatimizia kila mojawapo ya malengo yao. Lakini hawawezi kueleza mbona Mungu atawapeleka katika mbingu ya tatu na wala hawafahamu jinsi Yesu atakavyokuja juu ya wingu jeupe na kuwachukua, wala kusema kwa uhakika kamili kama kweli Yesu atawasili akiwa juu ya wingu jeupe siku ambayo wanaiwaza. Wote wana wasiwasi, na kukanganywa; wao wenyewe hata hawafahamu kama Mungu atachukua kila mmoja wao, watu wachache sana, wanaotoka katika madhehebu yote. Kazi ambayo Mungu anafanya kwa sasa, enzi ya sasa,, mapenzi ya Mungu—ni vitu ambavyo watu hawavifahamu, na hawana cha kufanya bali kusubiri na kuhesabu siku katika vidole vyao. Ni wale tu wanaofuata nyayo za Mwanakondoo hadi mwisho kabisa ndio wanaoweza kufaidi baraka za mwisho, huku wale watu werevu, ambao hawawezi kumfuata hadi mwisho ilhali wanaamini wamepata yote, ndio wasiokuwa na uwezo wa kushuhudia kuonekana kwa Mungu. Wote huamini wao ndio werevu zaidi duniani, na wanasitisha maendeleo ya kazi ya Mungu bila sababu yoyote kabisa, na huonekana kuamini pasi na shaka kwamba Mungu atawachukua mbinguni, wao “wenye uaminifu wa juu zaidi kwa Mungu, humfuata Mungu, na hutii neno la Mungu”. Hata ingawa wana “uaminifu wa hali ya juu” kwa maneno yaliyozungumzwa na Mungu; maneno yao na matendo yao bado hukera kwa sababu wao huipinga kazi ya Roho Mtakatifu, na kufanya uongo na uovu. Wale wasiofuata hadi mwisho kabisa, ambao hawazingatii kazi ya Roho Mtakatifu, na ambao wanashikilia kazi ya zamani hawajakosa tu kupata uaminifu kwa Mungu, bali kwa kinyume, wamekuwa wale wanaompinga Mungu, wamekuwa wale ambao wamekanwa na enzi mpya, na watakaoadhibiwa. Kuna wa kuhurumiwa zaidi kuliko wao? Wengi hata wanaamini kuwa wale wanaokana sheria ya zamani na kukubali kazi mpya hawana dhamiri. Watu hawa, ambao huongea tu kuhusu “dhamiri,” na hawajui kazi ya Roho Mtakatifu, hatimaye watapata kuwa matarajio yao yamekatizwa na dhamiri yao yenyewe. Kazi ya Mungu haizingatii mafundisho, na ingawa ni kazi Yake Mwenyewe, bado Mungu haishikilii. Kile kinachopaswa kukataliwa kinakataliwa, kile kinachopaswa kuondolewa kinaondolewa. Lakini mwanadamu anajiweka kwenye uadui wa Mungu kwa kushikilia sehemu moja ndogo ya kazi ya usimamizi wa Mungu. Si huu ndio upuuzi wa mwanadamu? Si huu ndio ujinga wa mwanadamu? Kadri watu wanakuwa waoga na wenye tahadhari sana kwa sababu wanachelea kutopata baraka za Mungu, ndivyo wanavyopungukiwa zaidi na uwezo wa kupata baraka zaidi, na wa kupata ile baraka ya mwisho. Watu wale wanaoshikilia kiutumwa sheria huwa wanadhihirisha uaminifu wa hali ya juu kwa sheria, na kadri wanavyodhihirisha uaminifu jinsi hiyo kwa sheria, ndivyo wanavyokuwa waasi wanaompinga Mungu. Kwa kuwa sasa ni Enzi ya Ufalme na wala si Enzi ya Sheria, na kazi ya leo haiwezi kulinganishwa na kazi ya zamani wala kazi ya zamani haiwezi kulinganishwa na kazi ya sasa. Kazi ya Mungu imebadilika, na vitendo vya mwanadamu pia vimebadilika; si kushikilia sheria au kuubeba msalaba. Basi, uaminifu wa watu kwa sheria na msalaba hautapata kibali cha Mungu.
Mwanadamu atakamilishwa kabisa katika Enzi ya Ufalme. Baada ya kazi ya ushindi, mwanadamu atapitishwa kwenye mambo magumu ya kusafishwa na taabu. Wale ambao wanaweza kushinda na kushuhudia katika taabu hii ndio hatimaye watakaofanywa wakamilifu; wao ndio washindi. Katika taabu hii, mwanadamu anahitajika kukubali kusafishwa huku, na kusafishwa huku ndio tukio la mwisho la kazi ya Mungu. Itakuwa mara ya mwisho ambapo mwanadamu atasafishwa kabla ya hitimisho la kazi zote za usimamizi wa Mungu, na wale wote wanaomfuata Mungu lazima wakubali jaribio hili la mwisho, lazima wakubali kusafishwa huku kwa mwisho. Wale ambao wamekabiliwa na taabu ni wale wasiokuwa na kazi ya Roho Mtakatifu na uelekezi wa Mungu, lakini wale ambao wameshindwa kwa kweli na wanatafuta mapenzi ya Mungu kwa kweli hatimaye watasimama imara; ndio wale ambao wana ubinadamu, na wanaompenda Mungu kwa kweli. Bila kujali Mungu hufanya nini, hawa washindi hawatapungukiwa na maono, na bado watauweka ukweli katika matendo bila kufeli katika ushuhuda wao. Wao ndio watakaosimama mwishowe kutoka kwenye taabu kubwa. Hata ingawa wale wanaovua samaki katika maji yenye mawimbi mengi bado wanaweza kusaidiwa leo, hakuna yeyote atakayeepuka taabu, na hakuna atakayeepuka jaribio la mwisho. Kwa wale wanaoshinda, taabu ya aina hii ni usafisho mkubwa; lakini wale wanaovua katika maji yenye mawimbi, ni kazi ya kuondolewa kamili. Bila kujali jinsi wanavyojaribiwa, utii wa wale wenye Mungu ndani ya mioyo yao hubaki vile vile; lakini kwa wale wasiokuwa na Mungu ndani ya mioyo yao, wakati kazi ya Mungu hainufaishi miili yao, wanabadilisha mtazamo wao kwa Mungu, na hata kumkimbia Mungu. Hawa ndio wale hawatasimama imara mwishoni, wanaotafuta baraka za Mungu na hawana tamaa ya kujitolea wenyewe kwa Mungu na kujikabidhi wenyewe Kwake. Aina hii ya watu wa msingi watafukuzwa wakati kazi ya Mungu itakapofikia kikomo, na hawafai kuonewa huruma yoyote. Wale wasiokuwa na ubinadamu, hawawezi kumpenda Mungu kwa kweli. Wakati mazingira ni mema na salama, au kama watapata faida, wao ni watiifu kabisa kwa Mungu, lakini wakati walilokuwa wanataka limepatikana au hatimaye kukataliwa, wanageuka mara moja. Hata kama ni kwa muda wa usiku mmoja tu, wao watatoka katika hali ya tabasamu, watu wenye “mioyo mikunjufu” hadi wenye sura mbovu na wauaji wakatili, ghafla wakiwatendea wafadhili wao wa jana kana kwamba ni adui wa milele, bila chanzo wala sababu. Ikiwa mapepo haya hayatarushwa nje, mapepo ambayo yanaweza kuua kwa kufumba na kufumbua jicho, je, hayatakuwa chanzo cha mateso zaidi? Kazi ya kumwokoa mwanadamu haitimizwi kufuatia kazi ya kukamilisha ushindi. Ingawa kazi ya ushindi imefika kikomo, kazi ya kumtakasa mwanadamu haijafika kikomo; kazi hiyo itamalizika tu wakati mwanadamu amesafishwa kikamilifu, wakati wale ambao wamejikabidhi kwa Mungu kikweli wamekamilishwa, na wakati wale wadanganyifu wasiokuwa na Mungu ndani ya mioyo yao wamesafishwa. Wale ambao hawamridhishi Mungu katika hatua ya mwisho ya kazi Yake wataondolewa kabisa, na wale watakaoondolewa kabisa ni wa yule mwovu. Kwa kuwa hawawezi kumtosheleza Mungu, wao ni waasi dhidi ya Mungu, na hata kama watu hawa wanamfuata Mungu leo, hili si thibitisho kwamba wao ndio watakaosalia mwisho. Kwa maneno mengine “wale ambao humfuata Mungu hadi mwisho watapokea wokovu,” maana ya “kufuata” ni kusimama imara katikati ya taabu. Leo, wengi wanaamini kwamba kumfuata Mungu ni rahisi, lakini wakati kazi ya Mungu inakaribia kuisha, utajua maana halisi ya “kufuata.” Kwa sababu tu kwamba unaweza kumfuata Mungu leo baada ya kushindwa, si thibitisho kwamba umo miongoni mwa wale watakaokamilishwa. Wale wasioweza kustahimili majaribu, wale wasioweza kuwa washindi wakiwa kwenye taabu, hatimaye, watashindwa kusimama imara, na basi kushindwa kumfuata Mungu hadi mwisho kabisa. Wale wanaomfuata Mungu kiukweli wana uwezo wa kuhimili majaribu ya kazi yao, ilhali wale wasiomfuata hawawezi kuhimili majaribu yoyote ya Mungu. Karibuni au baadaye watatimuliwa, huku washindi wakisalia kwenye ufalme. Mwanadamu amtafute au asimtafute Mungu kwa ukweli itapimwa kulingana na kazi yake, yaani, kupitia kwa majaribu ya Mungu na hayahusiani na uamuzi wa mwanadamu mwenyewe. Mungu hamkatai mtu yeyote kwa wazo la ghafla; yote ambayo Yeye hufanya ni ili mwanadamu aweze kushawishika mwenyewe. Hafanyi lolote ambalo halionekani kwa mwanadamu ama kazi yoyote ambayo haiwezi kumthibitishia mwanadamu. Iwapo imani ya mwanadamu ni ya ukweli au sio huthibitishwa na ushahidi, na haiwezi kuamuliwa na mwanadamu. Kwamba “ngano haiwezi kufanywa magugu, na magugu hayawezi kufanywa ngano” ni jambo lililo wazi. Wale wote wanaompenda Mungu kwa dhati hatimaye watasalia katika ufalme, na Mungu hatamtesa yeyote ambaye Yeye anampenda kwa kweli. Kwa misingi ya kazi zao na shuhuda zao tofauti, washindi katika ufalme watatumika kama makuhani au wafuasi, na wale wote watakaoshinda taabu watakuwa mwili wa makuhani katika ufalme. Baraza la makuhani litaundwa wakati kazi ya injili ulimwenguni kote itafikia kikomo. Wakati huo ukitimia, yale yanayopaswa kufanywa na mwanadamu yatakuwa jukumu lake ndani ya ufalme wa Mungu, na kuishi kwake pamoja na Mungu katika ufalme. Katika baraza la makuhani, patakuwepo makuhani wakuu na makuhani, na watakaosalia watakuwa wana na watu wa Mungu. Haya yote huamuliwa na ushuhuda wao kwa Mungu wakati wa majaribu; sio nyadhifa zinazopeanwa kwa wazo la ghafla. Wakati hadhi ya mwanadamu itakuwa imeianzishwa, kazi ya Mungu itamalizika, kwa kuwa kila mojawapo imewekwa kulingana na aina yake na kurejeshwa katika hali yake halisia, na hii ndiyo alama ya ukamilisho wa kazi ya Mungu, na haya ndiyo matokeo ya mwisho ya kazi ya Mungu na matendo ya mwanadamu, na ndiko kubainika kwa yale maono ya kazi ya Mungu na ushirikiano wa mwanadamu. Mwishowe, mwanadamu atapata pumziko katika ufalme wa Mungu, na, Mungu pia, atarejea kwenye makazi Yake kupumzika. Haya ndiyo yatakayokuwa matokeo ya miaka 6,000 ya ushirikiano wa mwisho kati ya Mungu na mwanadamu.
Sikiliza zaidi :Umeme wa Mashariki

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni