Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Imani-Katika-Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Imani-Katika-Mungu. Onyesha machapisho yote

6/17/2019

Mchezo Mfupi wa Kuchekesha | "Njama za Polisi" (Swahili Subtitles)


Ili kuondoa imani za dini, serikali ya CCP ambayo inakana Mungu mara kwa mara inatumia mikakati ya kuchunguza Wakristo kama vile kuendesha uchunguzi wa siri na kufuatilia ili kuwafutilia mbali wote. Kichekesho cha Njama za Polisi kinahusu ushirikiano wa maafisa waovu wa CCP katika sura fiche na ofisa msaidizi, punda anayevaa ngozi ya simba, anayeendesha ufuatiliaji wa siri wa kuwatia mbaroni Wakristo wanaokusanyika kwenye nyumba ya Zhao Yuzhi. Je, Zhao Yuzhi na familia yake watashughulikiaje njama ovu za polisi wa Kichina? Je, ni shida gani zitakazowakumba wao?

7/21/2018

Latest Swahili Christian Movie "Imani katika Mungu" | Hufunua Fumbo la Imani Katika Mungu



Yu Congguang huhubiri injili kwa niaba ya Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wakati wa kuhubiri injili, aliandamwa na serikali ya Kikomunisti ya China. Alikimbia milimani, ambapo alipokea msaada kutoka kwa Zheng Xun, mfanyakazi mwenza wa kanisa la nyumba la mahali pale. Walipokutana mara ya kwanza, walihisi kama tayari walikuwa wamejuana kwa muda mrefu. Zheng Xun alimpeleka Yu Congguang kwenye kibanda cha makuti ambapo yeye na wafanyakazi wenzake walikusanyika.

6/11/2018

Matamshi ya Mungu | Kile Ambacho Mchungaji wa Kutosha Anapaswa Kujiandaa Nacho

Mwenyezi Mungu alisema, Lazima uwe na ufahamu wa hali nyingi ambazo watu watakuwa ndani wakati Roho Mtakatifu anafanya kazi juu yao. Hasa, wale wanaofanya kazi kwa namna sawa kumtumikia Mungu lazima wawe na ufahamu bora zaidi wa hali nyingi zinazoletwa na kazi ambayo Roho Mtakatifu hutekeleza kwa wanadamu. Ikiwa unasema tu kuhusu uzoefu mwingi na njia nyingi za kuingia ndani, inaonyesha kwamba uzoefu wa watu unaegemea upande mmoja sana. Bila kufahamu hali nyingi kwa kweli, huwezi kufikia mbadiliko katika tabia yako.

5/26/2018

64. Huku Ni Kuweka Ukweli Katika Vitendo

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Wakristo
Fan Xing    Mji wa Zhumadian, Mkoa wa Henan
Katika siku za nyuma, nilikuwa nimeunganishwa na dada mmoja kufanya kazi kwa wajibu fulani. Kwa sababu nilikuwa na majisifu na mwenye kiburi na sikutafuta ukwelinilikuwa na mawazo kiasi ya kabla kuhusu dada huyu ambayo niliweka moyoni mwangu daima na sikuzungumza waziwazi naye. Tulipotengana, sikuwa nimeingia katika ukweli wa uhusiano wa kufanya kazi wenye kuridhisha.

4/17/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Utendaji (3)

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Utendaji (3)

Lazima muwe na uwezo wa kuishi kwa kujitegemea, kuweza kula na kunywa maneno ya Mungu ninyi wenyewe, kupitia maneno ya Mungu ninyi wenyewe, na kuishi maisha ya kiroho ya kawaida bila uongozi wa wengine; lazima muweze kuyategemea maneno ya Mungu ya leo ili kuishi, kuingia katika uzoefu wa kweli, na kuona kwa hakika. Ni wakati huo tu ndipo mtaweza kusimama imara. Leo, watu wengi hawaelewi kikamilifu majonzi na majaribio ya siku za usoni. Katika siku za usoni, watu wengine watapitia majonzi, na wengine watapitia adhabu. Adhabu hii itakuwa kali zaidi; itakuwa ni kuwasili kwa ukweli. Leo, yote unayopitia, kufanya, na kuonyesha yanaweka msingi wa majaribio ya siku za usoni, na kwa kiwango cha chini mno, lazima uweze kuishi kwa kujitegemea.

3/30/2018

Sura ya 48. Ni kwa Kuzielewa Hali Zako tu Ndipo Utakapoweza Kutembea Katika Njia Sawa

Matamshi ya Mungu | Sura ya 48. Ni kwa Kuzielewa Hali Zako tu Ndipo Utakapoweza Kutembea Katika Njia Sawa 

🤲🤲~~~~~~~~~~~👏👏👏~~~~~~~~~~👏👏~~~~~~~~~~😊😊😊

Mwenyezi Mungu alisema, Ndani ya mwanadamu mara nyingi zipo baadhi ya hali mbaya. Miongoni mwao ni baadhi ya hali ambazo zinaweza kuwaathiri watu au kuwadhibiti. Kunazo baadhi ya hali ambazo zinaweza hata kumfanya mtu kuiacha njia ya kweli na kuelekea katika njia mbovu. Kile mwanadamu anachokitafuta, kile wanachozingatia na njia wanayochagua kuifuata—haya yote yanahusiana na hali zao za ndani. Hata zaidi ni udhaifu wa mwanadamu au nguvu inayohuhusiana moja kwa moja na hali zao za ndani. Kwa mfano, watu wengi sasa hutilia mkazo hasa kwa siku ya Mungu; wote wana hamu nayo, wakiionea shauku siku ya Mungu ifike haraka ili waweze kujinasua kutoka kwenye mateso haya, magonjwa haya, mateso haya na zaidi.

3/12/2018

🤗📖Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Njia… (5)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Njia… (5)

Ilikuwa kwamba hakuna aliyejua Roho Mtakatifu, na hasa hawakujua njia ya Roho Mtakatifu ilikuwa gani. Ndio maana watu kila mara walifanya upumbavu mbele ya Mungu. Inaweza kusemwa kwamba karibu watu wote wanaoamini katika Mungu hawamjui Roho, lakini tu wana aina ya imani iliyochanganyikiwa. Ni wazi kutokana na hili kwamba watu hawamfahamu Mungu, na hata ingawa wanasema wanaamini katika Yeye, kuhusu kiini chake, kulingana na matendo yao wanaamini katika wao wenyewe, sio Mungu. Kutokana na uzoefu Wangu binafsi wa kweli, Naweza kuona kwamba Mungu humshuhudia Mungu katika mwili, na kutoka nje, watu wote hulazimishwa kukubali ushahidi Wake, na inaweza tu kusemwa kwa shida kuwa wanaamini kwamba Roho wa Mungu hana kosa kabisa.

2/12/2018

21 Ukimbizaji Ukweli Tu Ndiyo Imani ya Kweli katika Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kanisa

 21 Ukimbizaji Ukweli Tu Ndiyo Imani ya Kweli katika Mungu

     Mwenyezi Mungu alisema, Kama huna uzoefu wa kitu, basi wewe hakika hutajua jinsi ya kukisimamia na utakisimamia vibaya. Hata kama unakisimamia, na ufikiri: “Mimi nimeeleza kiasi haya yote na nikasema mengi kulihusu. Wao pia wamelisikiza mara nyingi. Nimeongea sana kulihusu. Nafikiri yote ambayo nimeshiriki kuhusu tatizo hili kimsingi ni kweli, sivyo?” lakini kwa kweli, yote tu ni mafundisho, na wewe unatumia mafundisho kutatua tatizo. Mbona unasema ni mafundisho? Kila neno unalosema ni sahihi, lakini kile unachosema hakijaelekezwa kwa tatizo na hakifikii kiini cha tatizo hili–ambapo tatizo hili lipo, shida yake ni nini, kwa nini hawa watu wanaweza kufanya mambo kama hayo au ni hali gani imejitokeza ndani yao.

1/10/2018

Sura ya 10. Wale Wanaopenda Ukweli Wana Njia ya Kufuata

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,kanisa

1. Kama hali ya Watu Ni Ya Kawaida Inategemea na Kama Wanapenda Ukweli au La

Mwenyezi Mungu alisema, Watu wengi wameibua suala lifuatalo: Baada ya ushirika wa juu, wanahisi wazi kabisa, wanakuwa na nguvu zaidi, na hawana hisia hasi—lakini hali kama hiyo inabaki tu kwa karibu siku kumi, ambapo baadaye hawawezi kudumisha hali ya kawaida. Suala ni nini? Je mmewahi kujiuliza kinachosababisha hili? Mbona hali zenu ni nzuri sana katika siku hizo takriban kumi za kwanza? Wengine wanasema kuwa hili ni tokeo la kutolenga ukweli. Lakini hivyo ungeweza vipi kufikia kiwango hiki cha kawaida baada ya kusikia ushirika? Mbona ulikuwa na furaha sana baada ya kuusikia ukweli? Wengine wanasema ni kwa sababu ya kazi ya Roho Mtakatifu.

1/09/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu, Maoni Wanayopaswa Kushikilia Waumini

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Biblia
neno la mungu,biblia

Matamshi ya Mwenyezi Mungu, Maoni Wanayopaswa Kushikilia Waumini 

Ni kitu gani ambacho mwanadamu amepokea tangu alipomwamini Mungu mara ya kwanza? Umejua kitu gani kumhusu Mungu? Umebadilika kiasi gani kwa sababu ya imani yako kwa Mungu? Sasa mnajua nyote ya kwamba imani ya mwanadamu katika Mungu si kwa ajili ya wokovu wa roho na ustawi wa mwili tu, wala si kuimarisha maisha yake kwa njia ya upendo wa Mungu, na kadhalika. Kama ilivyo sasa, kama unampenda Mungu kwa ajili ya ustawi wa mwili au furaha ya muda, basi hata kama, mwishoni, upendo wako kwa Mungu utafikia kilele chake na wewe hutaulizia kitu chochote, upendo huu unaoutafuta ni upendo mchafu na haumpendezi Mungu.

11/23/2017

Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu
Umeme wa Mashariki | Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu
Mwenyezi Mungu alisema, Kila mmoja anapaswa kuchunguza maisha yake upya ya kumwamini Mungu ili kuona iwapo, katika kumtafuta Mungu, ameelewa kwa dhati, amefahamukwa dhati, na kuja kumjua Mungukwa dhati, iwapo anajua kweli ni mawazo gani Mungu Anayo kwa aina tofauti za binadamu, na iwapo kweli anaelewa kile ambacho Mungu Anafanya juu yake na jinsi Mungu Anaeleza kila tendo lake. Huyu Mungu, Ambaye yuko kando yako, Akiongoza mwelekeo wa kuendelea kwako, Akiamuru hatima yako, na kukupa mahitaji yako—ni kiasi gani ambacho, katika uchambuzi wako, unaelewa nani kiasi gani ambacho kweli unajua kumhusu Yeye?