Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Video-za-Uzoefu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Video-za-Uzoefu. Onyesha machapisho yote

7/23/2019

Video ya Kiswahili ya Ushuhuda wa Kikristo "Mungu Ndiye Nguvu ya Maisha Yangu"


Video ya Kiswahili ya Ushuhuda wa Kikristo "Mungu Ndiye Nguvu ya Maisha Yangu" | Jinsi Wakristo Humtegemea Mungu Kushinda 


Fang Jin ni Mkristo. Alikamatwa na serikali ya CCP kwenye mkusanyiko. Ili kumlazimisha kuwataja ndugu zake wa kike na kiume na kumsaliti Mungu, polisi walimnyima chakula, maji na usingizi kwa siku saba mchana na siku sita usiku, na kusababisha kila aina ya mateso ya kinyama juu yake: mapigo makali, kuning’inizwa, kuchuchumaa, kudhihakiwa na kufedheheshwa. Alikuwa amejaa majeraha na alipooza miguu. Katika maumivu, alimwomba Mungu. Neno la Mungu lilimpatia nuru na kumwongoza kubaini tena na tena hila za Shetani na lilimwongezea imani na nguvu. Hivyo aliweza kunusurika na uharibifu wa Shetani na kuwa shahidi kwa Mungu!

4/28/2019

Swahili Christian Movie Trailer | Nyendo za Mateso ya Kidini | "Saa ya Giza Kabla ya Mapambazuko"


Utambulisho


Tangu kilipokuja mamlakani katika China Bara mnamo mwaka wa 1949, Chama Cha Kikomunisti cha China kimekuwa hakikomi katika mateso yake kwa imani ya kidini. Kwa wayowayo kimewashika na kuwaua Wakristo, kuwafukuza na kuwadhulumu wamishonari wanaofanya kazi nchini China, wakachukua ngawira na kuchoma nakala nyingi za Biblia, wakafunga kabisa na kubomoa majengo ya kanisa, na bila mafanikio wakajaribu kukomesha makanisa yote ya nyumbani.

4/25/2019

Swahili Christian Video 2018 | "Ni Vizuri Sana Kutupa Mbali Pingu za Hadhi" | Wokovu wa Mungu


Baada ya Liang Zhi kumwamini Mungu, bila kukoma alitafuta kwa shauku, na kujitosa katika kutimiza wajibu wake. Baada ya miaka kadhaa, alichaguliwa kama kiongozi wa kanisa. Wakati alipokuwa akitekeleza wajibu wake kama kiongozi wa kanisa, aligundua kwamba baadhi ya ndugu walikuwa na uwezo zaidi kumliko, ambayo ilimfanya asiwe na furaha kwa kiasi kwamba alikuwa na wivu kwao. Ili kuokoa uso na kulinda hali yake, alishindana nao kwa siri ili kuona ni nani aliyekuwa bora, na alikimbilia umaarufu na hadhi. Umaarufu na hadhi vilionekana kama pingu zisizoonekana zilizomfunga sana, kumnyima uhuru, kumsababisha afanye mambo kinyume na ukweli na kupinga Mungu.

4/03/2019

Video ya Injili 2018 | "Kutoka Kinywani mwa Mauti" | Mungu Amenipa Fursa ya Pili Katika Maisha



Video ya Injili 2018 | "Kutoka Kinywani mwa Mauti" | Mungu Amenipa Fursa ya Pili Katika Maisha

Liu Zhen, mwenye umri wa miaka 78, ni mke wa nyumbani wa kawaida wa mashambani. Baada ya kumwamini Mungu, alihisi furaha isiyo na kisawe na kusoma maneno Yake na kuimba nyimbo za kumsifu siku zote, na mara nyingi kukusanyika pamoja na ndugu zake kushirikiana juu ya ukweli. ... Hata hivyo, mambo mazuri hayadumu. Anakamatwa na kuteswa na serikali ya Kikomunisti ya China, ikimtia katika shida mbaya sana. Polisi wanampeleka kwenye kituo cha polisi kwa ajili ya kuhojiwa mara tatu, na kumwonya asimwamini Mungu tena.

3/13/2019

Filamu za Kikristo "Chama Hakijamaliza Kuzungumza"


Li Ming’ai ni Mkristo nchini China Bara. Yeye ni mwanamke mwadilifu ambaye anawaheshimu wakweze, humsaidia mumewe na kumuelimisha mtoto wake, na ana familia ya furaha na patanifu. Katika China, ambako ukanaji Mungu unatawala, hata hivyo, serikali ya Kikomunisti ya China daima huwakamata na kuwatesa ovyo ovyo watu wanaomwamini Mungu. Katika mwaka wa 2006, Li Ming'ai alikamatwa na kutozwa faini kwa sababu ya imani yake kwa Mungu. Baada ya Li Ming'ai kurudi nyumbani, polisi wa Kikomunisti wa China daima walimtisha na kumwogofya yeye na familia yake, na walijaribu kumzuia Li Ming'ai kuendeleza imani yake kwa Mungu.

11/24/2018

Swahili Christian Movie | Nyendo za Mateso ya Kidini | "Kukaribia Hatari na Kurudi"


Tangu kilipokuja mamlakani katika China Bara mnamo mwaka wa 1949, Chama Cha Kikomunisti cha China kimekuwa hakikomi katika mateso yake kwa imani ya kidini. Kwa wayowayo kimewashika na kuwaua Wakristo, kuwafukuza na kuwadhulumu wamishonari wanaofanya kazi nchini China, wakachukua ngawira na kuchoma nakala nyingi za Biblia, wakafunga kabisa na kubomoa majengo ya kanisa, na bila mafanikio wakajaribu kukomesha makanisa yote ya nyumbani. 

5/10/2018

Christian Testimony Video Swahili "Moyo Uliopotea Waja Nyumbani" Wokovu wa Ajabu wa Mungu


Tangu alipokuwa mdogo, Novo alimwamini Bwana Yesu, kama mama yake tu. Hata kama alisoma Biblia, kuomba, na kuhudhuria mahubiri mara kwa mara, mara nyingi hangeweza kujizuia bali kufuata mielekeo mibaya ya dunia, kutamani raha za mwili, na kudanganya na kusema uwongo…. Alikusudia mara nyingi kuyaacha maisha ya aina hiyo ya kuzunguka katika kutenda dhambi na kukiri, kukiri na kutenda dhambi. Hata hivyo, kila wakati hakufaulu. Baadaye Novo alipokuwa akifanya kazi nchini Taiwan alisikia injili ya ufalme, na kwa kuyasoma maneno Yake Mwenyezi Mungu alifikia hitimisho kuwa Mwenyezi Mungu ni kurudi kwa Bwana Yesu, na kuwa kazi Yake ya hukumu na utakaso katika siku za mwisho ina uwezo wa kusuluhisha kikamilifu tatizo la asili ya mwanadamu ya dhambi.