Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mwendelezo-wa-Neno-Laonekana-katika-Mwili. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mwendelezo-wa-Neno-Laonekana-katika-Mwili. Onyesha machapisho yote

8/10/2018

Mahitaji ya Mungu kwa Wanadamu | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

Utambulisho na Hadhi ya Mungu Mwenyewe
Tumefikia mwisho wa mada ya "Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote," vilevile na ile ya "Mungu ni wa kipekee Mungu Mwenyewe." Baada ya kufanya hivyo, tunahitaji kufanya muhtasari. Muhtasari wa aina gani? Unaomhusu Mungu Mwenyewe. Kwa kuwa ni kumhusu Mungu Mwenyewe, basi lazima ugusie kila kipengele cha Mungu, vilevile aina ya imani ya watu kwa Mungu. Na kwa hiyo, kwanza lazima Niwaulize: Baada ya kusikia mahubiri, Mungu ni nani katika jicho la mawazo yako? (Muumbaji).

5/03/2018

C. Jinsi Ambavyo Shetani Anatumia Desturi ya Kitamaduni Kumpotosha Mwanadamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, uaminifu
Mwenyezi Mungu alisema, Je, kuna mambo mengi yanayochukuliwa kuwa sehemu ya desturi ya kitamaduni? (Ndiyo.) Hii desturi ya kitamaduni inamaanisha nini? (Inapitishwa kutoka kwa mababu.) Inapitishwa kutoka kwa mababu, hiki ni kipengele kimoja. Familia, vikundi vya makabila, na hata jamii ya binadamu imepitisha njia yao ya maisha kutoka mwanzo, ama imepitisha mila, misemo, na kanuni, ambazo zimeingizwa kwa fikira za watu. Watu wanafikiria nini kuhusu mambo haya? Watu wanayachukulia kuwa yasiyoweza kutengwa na maisha yao. Wanayachukua mambo haya na kuyachukulia kuwa kanuni na uhai wa kutii, na daima hawako tayari kuyabadilisha ama kuyaacha mambo haya kwa sababu yalipitishwa kutoka kwa mababu.

Majaribu ya Shetani | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V

 Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Yesu
Mwenyezi Mungu alisema, Sasa, hebu tuchambue kirai hiki alichotumia Shetani: “amuru kwamba mawe haya yawe mikate” Kubadili mawe yawe mikate—hili linamaanisha chochote? Halina maana. Iwapo kuna chakula, mbona usile? Mbona ni muhimu kubadili mawe yawe mikate? Kuna maana hapa? (La.) Ingawa alikuwa amefunga wakati huo, kwa hakika Bwana Yesu alikuwa na chakula cha kula? Je, Alikuwa na chakula? (Alikuwa nacho.) Kwa hivyo, hapa, tunaona upuuzi wa matumizi ya Shetani ya kirai hiki. Kwa usaliti na uovu wake wote, tunaona upuuzi na ujinga wake, siyo? Shetani anafanya idadi fulani ya mambo. Unaona asili yake ovu na unaona akiharibu kazi ya Mungu.

5/02/2018

Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Watu Wanaomfuata Mungu | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

Neno la Mwenyezi Mungu | 3) Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Watu Wanaomfuata Mungu

    Baada ya hayo, hebu tuzungumzie mzunguko wa uhai na mauti wa wale wanaomfuata Mungu. Hili linawahusu, hivyo kuweni makini. Kwanza, fikiria kuhusu ni makundi gani ambamo watu wanaomwamini Mungu wanaweza kugawika. Kuna mawili: wateule wa Mungu na watendaji-huduma. Kwanza tutazungumza kuhusu wateule wa Mungu, ambao ni wachache. “Wateule wa Mungu” inarejelea nini? Baada ya Mungu kuumba vitu vyote na baada ya kuwepo wanadamu, Mungu alichagua kundi la watu ambao walimfuata, na Akawaita “wateule wa Mungu.” Kuna mipaka maalum na umuhimu katika uchaguzi wa Mungu wa watu hawa. Mipaka ni kwamba kila wakati Mungu anafanya kazi muhimu ni lazima waje—ambacho ni kitu cha kwanza kati ya vinavyowafanya maalum.

Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Wasioamini | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

     Mwenyezi Mungu alisema, Hebu tuanze na mzunguko wa uhai na mauti wa wasioamini. Baada ya watu kufa, wanachukuliwa na msimamizi kutoka ulimwengu wa kiroho. Na ni kitu gani chao kinachukuliwa? Sio miili yao, bali ni roho zao. Roho zao zikichukuliwa, wanawasili katika sehemu ambayo ni ofisi ya ulimwengu wa kiroho, sehemu ambayo hasa hupokea roho za watu ambao wamekufa. (Kumbuka: sehemu ya kwanza wanapokwenda baada ya mtu yeyote kufa ni pageni kwa roho.) Wanapofikishwa mahali hapa, afisa anafanya ukaguzi wa kwanza, anathibitisha majina yao, anwani, umri, na walichokifanya maishani mwao.

4/25/2018

Hadithi ya 2. Mlima Mkubwa, Kijito Kidogo, Upepo Mkali, na Wimbi Kubwa | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII

Kijito Kidogo,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Hadithi ya 2. Mlima Mkubwa, Kijito Kidogo, Upepo Mkali, na Wimbi Kubwa

Mwenyezi Mungu alisema, Kulikuwa na kijito kidogo kilichotiririka kwa kuzungukazunguka, hatimaye kikawasili chini ya mlima mkubwa. Mlima ulikuwa unazuia njia ya kijito hiki, hivyo kijito kikauomba mlima kwa sauti yake dhaifu na ndogo, "Tafadhali noamba kupita, umesimama kwenye njia yangu na umenizibia njia yangu kuendelea mbele." Basi mlima ukauliza, "Unakwenda wapi?" Swali ambalo kijito kililijibu, "Ninatafuta makazi yangu." Mlima ukasema, "Sawa, endelea na tiririkia juu yangu!" Lakini kwa sababu kijito kilikuwa dhaifu sana na kichanga sana, hakukuwa na namna kwake kutiririka juu ya mlima mkubwa hivyo, hivyo hakikuwa na uchaguzi bali kuendelea kutiririka chini ya mlima...
Upepo mkali ukavuma, ukiwa umekusanya mchanga na vumbi kuelekea ambapo milma ulikuwa umesimama. Upepo ukauungurumia mlima, "Hebu nipite!" Mlima ukauliza, "Unakwenda wapi?" Upepo ukavuma kwa kujibu, "Ninataka kwenda upande ule wa mlima." Mlima ukasema, "Sawa, kama unaweza kupenya katikati yangu, basi unaweza kwenda!"

4/21/2018

Amri ya Mungu kwa Shetani | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Neno la Mwenyezi Mungu  | 4. Amri ya Mungu kwa Shetani

Ayubu 2:6 Naye Yehova akasema kwa Shetani, Tazama, yeye yuko katika mkono wako; lakini uuhifadhi uhai wake.

Shetani Hajawahi Kuthubutu Kukiuka Mamlaka ya Muumba, na Kwa Sababu Hiyo, Vitu Vyote Vinaishi kwa Mpangilio

Hili ni dondoo kutoka katika Kitabu cha Ayubu, na “yeye” katika maneno haya inaashiria Ayubu. Ingawaje imeandikwa kwa muhtasari, sentensi hii inaelezea masuala mengi. Inafafanua mabadilishano fulani kati ya Mungu na Shetani kwenye ulimwengu wa kiroho, na inatwambia kuwa kiini cha maneno ya Mungu kilikuwa Shetani. Pia inarekodi kile kilichozungumziwa mahususi na Mungu.

4/18/2018

Ukadiriaji wa Ayubu na Mungu na kwenye Biblia | Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Ayubu

Neno la Mwenyezi Mungu  | 1. Ukadiriaji wa Ayubu na Mungu na kwenye Biblia

(Ayubu 1:1) Palikuwa na mtu katika nchi ya Uzi, jina lake aliitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mnyoofu, na mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu .
(Ayubu 1:5) Na ilikuwa hivyo, hizo siku za karamu zao zilipokuwa zimetimia, Ayubu aliwatuma na kuwatakasa, kisha akaamka asubuhi na mapema, na kutoa sadaka za kuteketezwa kulingana na hesabu yao wote ilivyokuwa; kwani Ayubu alisema, Inaweza kuwa kwamba wanangu wamefanya dhambi, na kumkufuru Mungu mioyoni mwao. Hivyo ndivyo Ayubu alivyofanya siku zote.
(Ayubu 1:8) Kisha BWANA akamwuliza Shetani, Je, umemwangalia mtumishi wangu Ayubu, kwa kuwa hakuna hata mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mnyofu, mwenye kumcha Mungu, na kuuepuka uovu?

4/12/2018

Maneno ya Yesu kwa Wanafunzi Wake Baada ya Kufufuka Kwake | Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III

    12. Maneno ya Yesu kwa Wanafunzi Wake Baada ya Kufufuka Kwake
(Yohana 20:26-29) Na baada ya siku nane wanafunzi wake walikuwa ndani tena, na Tomaso pamoja nao: Kisha akaja Yesu, na milango imefungwa, na akasimama katikati, kisha akasema, Amani iwe kwenu. Kisha akamwambia Tomaso, Weka hapa kidole chako, na utazame mikono yangu; na ulete mkono wako uuweke ubavuni mwangu, na usiwe asiyeamini, bali uwe aaminiye. Naye Tomaso akajibu akamwambia, Bwana wangu na Mungu wangu! Yesu akamwambia, Tomaso, kwa kuwa umeniona, umeamini; heri wanayo wale ambao hawajaona, ilhali wameamini.
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,Yesu

   
(Yohana 21:16-17) Akamwambia tena mara ya pili, Simoni wa Yona, je, wanipenda? Akamwambia, Ndiyo, Bwana; wewe unajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Lisha kondoo wangu. Akamwambia mara ya tatu, Simoni, mwana wa Yona, je, unanipenda? Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, je, unanipenda? Na akamwambia, Bwana, wewe unajua mambo yote; wewe unajua ya kwamba nakupenda. Yesu akamwambia, Lisha kondoo wangu.

4/11/2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,mwenyezi mungu

Neno la Mwenyezi Mungu  | Utakatifu wa Mungu (III)

    Mnahisi vipi baada ya kusema sala zenu? (Tunafurahia na kuguswa sana.) Wacha tuanze ushirika wetu. Tulishiriki mada ipi wakati uliopita? (Utakatifu wa Mungu.) Na ni kipengele kipi cha Mungu Mwenyewe kinahusisha utakatifu wa Mungu? Je, kinahusisha kiini cha Mungu? (Ndiyo.) Kwa hivyo ni nini hasa mada inayohusiana na kiini cha Mungu? Je, ni utakatifu wa Mungu? (Ndiyo.) Utakatifu wa Mungu: hiki ni kiini cha kipekee cha Mungu. Ni nini ilikuwa dhamira kuu tuliyoshiriki wakati uliopita? (Kutambua uovu wa Shetani.) Na ni yapi tuliyoyashiriki wakati uliopita kuhusu uovu wa Shetani? Mnaweza kukumbuka? (Jinsi Shetani anampotosha mwanadamu. Anatumia maarifa, sayansi, desturi ya kitamaduni, ushirikina, na mienendo ya kijamii kutupotosha.) Sahihi, hii ndiyo ilikuwa mada kuu tuliyojadili wakati uliopita.

4/10/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | (III) Aina Tano za Watu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | (III) Aina Tano za Watu

    Kwa sasa, Nitaacha ushirika wetu kuhusu tabia ya haki ya Mungu umalizikie hapo. Kinachofuata Nitaainisha wafuasi wa Mungu katika kategoria mbalimbali, kulingana na ufahamu wao wa Mungu na ufahamu wao na kile wamepitia kuhusiana na tabia ya haki Yake, ili muweze kujua awamu ambayo kwa sasa mnapatikana ndani pamoja na kimo chenu cha sasa. Kuhusiana na maarifa yao ya Mungu na ufahamu wao wa tabia Yake ya haki, awamu na kimo tofauti ambavyo watu huwa navyo vinaweza kugawanywa katika aina tano. Mada hii imeelezewa kwa msingi wa kumjua Mungu wa kipekee na tabia Yake ya haki; kwa hivyo, unaposoma maudhui yafuatayo, unafaa kujaribu kwa makini kuchambua ni kiwango kipi haswa cha ufahamu na maarifa ulichonacho kuhusiana na upekee wa Mungu na tabia Yake ya haki, na kisha utumie hayo kujua ni awamu gani ambayo kwa kweli unapatikana ndani, kimo chako ni kikubwa vipi kwa kweli, na wewe ni aina gani ya mtu kwa kweli.

4/08/2018

Kifo: Awamu ya Sita | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Maisha

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kifo: Awamu ya Sita

    Baada ya mahangaiko mengi na masikitiko mengi, na kuvunjwa moyo kwingi, baada ya furaha nyingi na huzuni nyingi na baada ya misukosuko ya maisha, baada ya miaka mingi sana isiyosahaulika, baada ya kutazama misimu ikipita na kujirudia, mtu hupita kwenye kiungo muhimu sana cha maisha bila ya arifa, na kwa ghafla tu mtu anajipata kwenye miaka yake ya kufifia. Alama za muda zimejichora kotekote kwenye mwili wa mtu: Mtu hawezi tena kusimama wima, kichwa cha nywele nyeusi kinageuka na kuwa cha nywele nyeupe, macho maangavu na mazuri yanabadilika na kuanza kufifiliza na kuwa na wingu mbele yao, nayo ngozi laini, yenye unyumbufu inageuka na kuwa na makunyanzi na madoadoa.

Uhuru: Awamu ya Tatu | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III


Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Watoto

Neno la Mwenyezi Mungu | Uhuru: Awamu ya Tatu

    Baada ya mtu kupita utoto na wakati wake wa kubaleghe na kwa utaratibu bila kuzuilika kufikia ukomavu, hatua inayofuata ni kwake yeye kuuaga kabisa ule ujana wake, kuwaaga wazazi wake, na kukabiliana na barabara iliyo mbele yake akiwa mtu mzima huru. Wakati huo[c] lazima wakabiliane na watu, matukio na mambo yote ambayo mtu mzima lazima apitie, na kukabiliana na viungo mbalimbali katika msururu wa hatima yake. Hii ndiyo awamu ya tatu ambayo lazima mtu apitie.

1. Baada ya Kuwa Huru, Mtu Huanza Kupitia Ukuu wa Muumba

    Kama kuzaliwa kwa mtu na kulelewa kwake ni “kipindi cha matayarisho” katika safari ya mtu maishani, kuweka lile jiwe la msingi katika hatima ya mtu, basi uhuru wa mtu ndio mazungumzo nafsi ya kufungua hatima ya maisha ya mtu.

4/07/2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III


Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Neno la Mwenyezi Mungu  | Mamlaka ya Mungu (II)

    Leo tutaendelea na ushirika wetu kuhusu mada ya “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee.” Tayari tumekuwa na ushirika mara mbili katika mada hii, wa kwanza kuhusiana na mamlaka ya Mungu na wa pili kuhusiana na tabia ya haki ya Mungu. Baada ya kusikiliza ushirika huu mara mbili, je, umepata ufahamu mpya wa utambulisho wa Mungu, hadhi, na hali halisi? Je, maono haya yamekusaidia kufikia maarifa mazito zaidi na uhakika wa ukweli kuuhusu uwepo wa Mungu? Leo Ninapanga kufafanua mada hii ya “Mamlaka ya Mungu.”

Kuelewa Mamlaka ya Mungu Kutoka kwa Mitazamo Mikubwa na Midogo

    Mamlaka ya Mungu ni ya kipekee. Ndiyo maonyesho ya sifa ya, na hali halisi maalum ya, utambulisho wa Mungu Mwenyewe. Hakuna kiumbe ambacho kiliumbwa wala kile ambacho hakikuumbwa kinachomiliki maonyesho ya sifa kama hizi na hali halisi maalum;

4/04/2018

Umeme wa Mashariki | Dibaji🔔⭐

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kanisa

Umeme wa Mashariki | Dibaji

~~~~~~~~~~       🎀🎀            ~~~~~~~~~~~         🎀🎀           ~~~~~~~~~~~
 🌺🌺🌺**************     🌺🌺🌺     **************     🌺🌺🌺          
    Kila mmoja anapaswa kuchunguza maisha yake upya ya kumwamini Mungu ili kuona iwapo, katika kumtafuta Mungu, ameelewa kwa dhati, amefahamukwa dhati, na kuja kumjua Mungukwa dhati, iwapo anajua kweli ni mawazo gani Mungu Anayo kwa aina tofauti za binadamu, na iwapo kweli anaelewa kile ambacho Mungu Anafanya juu yake na jinsi Mungu Anaeleza kila tendo lake. Huyu Mungu, Ambaye yuko kando yako, Akiongoza mwelekeo wa kuendelea kwako, Akiamuru hatima yako, na kukupa mahitaji yako—ni kiasi gani ambacho, katika uchambuzi wako, unaelewa nani kiasi gani ambacho kweli unajua kumhusu Yeye?

4/03/2018

B. Mungu Lazima Aangamize Sodoma.


 Neno la Mwenyezi Mungu  | B. Mungu Lazima Aangamize Sodoma.

    (Mwa 18:26) Kisha BWANA akasema, Nikipata katika Sodoma wenye haki hamsini mjini, basi Nitapaacha mahali pote kwa ajili yao.
    (Mwa 18:29) Na akazungumza tena naye, akasema, Huenda wakapatikana humo arobaini. Akasema, Sitafanya hivyo.
    (Mwa 18:30) Akamwambia, labda watapatikana huko thelathini. Naye akasema, Sitafanya hivyo.
    (Mwa 18:31) Kisha akasema, huenda wakaonekana huko ishirini. Naye akasema, Sitauharibu.
    (Mwa 18:32) Naye akasema, huenda wakaonekana huko kumi. Naye akasema, Sitauharibu.
    Hizi ni dondoo chache Nilizochagua kutoka kwenye Biblia. Dondoo hizi si kamilifu, za matoleo ya awali. Kama mngependa kuziona hizo, mnaweza kuzitafuta kwenye Biblia nyinyi wenyewe; ili kuokoa muda, Nimeiacha sehemu ya maudhui asilia. Hapa Nimechagua tu vifungu na sentensi mbalimbali kuu, huku nikiziacha sentensi mbalimbali ambazo hazina umuhimu katika ushirika wetu wa leo.

3/31/2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I📖🎉


Katika Mamlaka ya Muumba, Viumbe Vyote ni Timilifu

🎉~~~~~~~~*~~~~~~~~🤲***************👂~~~~~~~~~*~~~~~~~~🔔    

^^^^^      ~~~~~~      ^^^^^       ~~~~~~       ^^^^^^      ~~~~~~    ^^^^^

    Mwenyezi Mungu alisema, Viumbe vyote vilivyoumbwa na Mungu, vikiwemo vile vilivyoweza kusonga na vile visingeweza kusonga, kama vile ndege na samaki, kama vile miti na maua, na hata ikiwemo mifugo, wadudu na wanyama wa mwituni, wote walioumbwa kwenye siku ya sita—wote walikuwa wazuri mbele ya Mungu, na, vilevile, machoni mwa Mungu, viumbe hivi, kulingana na mpango Wake, vilikuwa vimetimiza kilele cha utimilifu, navyo vilikuwa vimefikia viwango ambavyo Mungu alitaka kutimiza.

3/26/2018

Sura ya 38. Yeye Ambaye Hukosa Ukweli Hawezi Kuwaongoza Wengine📖🤲

📖📖📖***********👍👍👍***********📚📚📚*********🙂🙂🙂🙂
    Mwenyezi Mungu alisema, Je, kweli mnaelewa kuhusu mabadiliko katika tabia ya mtu? Mabadiliko katika tabia yanamaanisha nini? Je, mnaweza kutambua mabadiliko katika tabia? Ni hali zipi zinaweza kufikiriwa kuwa mabadiliko katika tabia ya maisha ya mtu, na ni hali zipi ambazo ni mabadiliko tu katika tabia ya nje? Tofauti ni ipi kati ya mabadiliko katika tabia ya mtu ya nje na mabadiliko katika maisha ya mtu ya ndani? Je, mnaweza kueleza tofauti? Mnamwona mtu mwenye hamu ya kukimbia pote kwa ajili ya kanisa, na mnasema: "Yeye amebadilika!" Mnamwona mtu akiitelekeza familia yake au kazi, na mnasema: "Yeye amebadilika!" Ikiwa amejitoa mhanga kwa namna hiyo, mnafikiri kwa hakika lazima amebadilika.

3/25/2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X📖💖

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Neno la Mwenyezi Mungu | Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)

**************🌼🌼🌼🌼*************🙂🙂🙂*************🌻🌻🌻*************
~~~~~~~~~~~                   ~~~~~~~~~~~~                  ~~~~~~~~~~
Leo, tunafanya ushirika juu ya mada maalum. Kwa kila mmoja wenu, kuna vitu viwili vikuu tu ambavyo mnapaswa kujua, kuvipitia na kuvielewa—na vitu hivi viwili ni vipi? Cha kwanza ni kuingia binafsi kwa watu katika maisha, na cha pili kinahusu kumjua Mungu. Leo Nawapa uchaguzi: Chagua kimoja. Mngependa kusikia kuhusu mada inayouhusu uzoefu wa maisha ya kibinafsi ya watu, au mngependa kusikia inayohusu kumjua Mungu Mwenyewe? Na kwa nini Ninawapa uchaguzi huu? Kwa sababu leo Ninafikiria kufanya ushirika nanyi juu ya mambo mapya kuhusu kumjua Mungu. Lakini, hata hivyo, kwanza nitawaacha mchague kimoja kati ya vitu viwili ambavyo Nimezungumzia hivi punde.

3. Mungu Atumia upinde wa mvua kuasisi agano na mwanadamu😊📖

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Injili
    (Mwa 9:11-13) Na Nitalithibitisha agano langu nanyi, wala kila chenye mwili hakitafutwa tena kwa maji ya gharika; wala hakutakuwa tena gharika kuiharibu nchi. Na Mungu akasema, Hii ndiyo ishara ya agano Ninalofanya kati yangu na nyinyi na kila kiumbe hai kilicho pamoja nanyi, kwa vizazi vyote mpaka milele: Mimi Nauweka upinde wangu mawinguni, na utakuwa ni ishara ya agano kati yangu na nchi.
    Kisha, hebu tuangalie sehemu hii ya maandiko kuhusu namna Mungu alivyounda upinde wa mvua kama ishara ya Agano lake na binadamu.
    Watu wengi zaidi wanajua upinde wa mvua ni nini na wamesikia baadhi ya hadithi zinazohusiana na pinde za mvua. Kuhusiana na hadithi ile ya upinde wa mvua kwenye biblia, baadhi wa watu wanaisadiki, baadhi wanaichukulia tu kama hadithi ya kale, huku wengine hawaisadiki kamwe.