Mwenyezi Mungu alisema, Sasa, hebu tuchambue kirai hiki alichotumia Shetani: “amuru kwamba mawe haya yawe mikate” Kubadili mawe yawe mikate—hili linamaanisha chochote? Halina maana. Iwapo kuna chakula, mbona usile? Mbona ni muhimu kubadili mawe yawe mikate? Kuna maana hapa? (La.) Ingawa alikuwa amefunga wakati huo, kwa hakika Bwana Yesu alikuwa na chakula cha kula? Je, Alikuwa na chakula? (Alikuwa nacho.) Kwa hivyo, hapa, tunaona upuuzi wa matumizi ya Shetani ya kirai hiki. Kwa usaliti na uovu wake wote, tunaona upuuzi na ujinga wake, siyo? Shetani anafanya idadi fulani ya mambo. Unaona asili yake ovu na unaona akiharibu kazi ya Mungu.
Ni wa kuchukiza na kuudhi. Lakini kwa upande mwingine, unapata asili ya kitoto na ujinga nyuma ya maneno na vitendo vyake? (Ndiyo.) Huu ni ufunuo kuhusu asili ya Shetani; ana asili ya aina hii na atafanya kitu kama hiki. Kwa wanadamu, kirai hiki ni cha upuuzi na cha kuchekesha. Lakini maneno kama hayo kwa hakika yanaweza kutamkwa na Shetani. Tunaweza kusema kwamba ni asiyejua? Mjinga? Uovu wa Shetani uko kila mahali na daima unafichuliwa. Na Bwana Yesu anamjibu aje? (“Mtu hataishi kwa mkate peke yake, ila kwa kila neno linalotoka katika kinywa cha Mungu ”) Maneno haya yana nguvu yoyote? (Yanayo.) Mbona tunasema kwamba yana nguvu? (Ni ya ukweli.) Sahihi. Maneno haya ni ukweli. Sasa, mtu anaishi kwa mkate tu? Bwana Yesu alifunga kwa siku na usiku 40. Alikufa kwa njaa? (La.) Hakufa kwa njaa, kwa hivyo Shetani alimkaribia, akimwambia abadili mawe yawe chakula kwa kusema kitu kama hiki: Ukiyabadili mawe yawe chakula, Hutakuwa basi na vitu vya kula? Si basi Hutalazimika kufunga, Hutalazimika kuwa na njaa? Lakini Bwana Yesu alisema, Mtu hataishi kwa mkate peke yake inayomaanisha kwamba, ingawa mwanadamu anaishi katika mwili, kile kinachompa uhai, kile kinachouruhusu mwili wake kuishi na kupumua, si chakula, ila maneno yote yaliyotamkwa na kinywa cha Mungu. Katika upande mmoja, mwanadamu anachukulia maneno haya kuwa ukweli. Maneno haya yanampa imani, yanamfanya ahisi kwamba anaweza kumtegemea Mungu, kwamba Mungu ni ukweli. Kwa upande mwingine, kuna kipengele cha vitendo katika maneno haya? (Kunacho.) Mbona? Kwa sababu Bwana Yesu amefunga kwa siku na usiku 40 na bado Anasimama hapo, bado ako hai. Huu ni mfano? Cha maana hapa ni kwamba Hajakula chochote, chakula chochote kwa siku na usiku 40. Bado ako hai. Huu ni ushahidi wa nguvu nyuma ya kirai Chake. Kirai hiki ni rahisi, lakini, kuhusiana na Bwana Yesu, Alifunzwa kirai hiki na mtu mwengine, ama Alikifikiria tu kwa sababu ya kile Shetani alimwambia? Fikiria jambo hili. Mungu ni ukweli. Mungu ni uhai. Je, ukweli na uhai wa Mungu uliongezwa kwa kuchelewa? Ulitokana na uzoefu? (La.) Ni ya asili ndani ya Mungu, kumaanisha kwamba ukweli na uhai vipo ndani ya kiini cha Mungu. Licha ya kile kinachomfanyikia, Anachofichua ni ukweli. Ukweli huu, kirai hiki—iwapo maudhui yake ni ndefu ama fupi—kinaweza kumwacha mwanadamu aishi, kimpe uhai; kinaweza kumwezesha mwanadamu kupata, ndani yake, ukweli, uwazi kuhusu safari ya maisha, na kumwezesha kuwa na imani kwa Mungu. Hiki ndicho chanzo cha matumizi ya Mungu ya kirai hiki. Chanzo ni chema, kwa hivyo kitu hiki chema ni takatifu? (Ndiyo.) Kirai cha Shetani kinatoka kwa asili ya Shetani. Shetani anafichua asili yake ovu, asili yake yenye kijicho, kila mahali, daima. Sasa, ufunuo huu, anaufanya kiasili? (Ndiyo.) Kuna yeyote anayemchochea? Kuna yeyote anayemsaidia? Kuna yeyote anayemshurutisha? (La.) Anautoa kwa hiari yake mwenyewe. Hii ni asili ovu ya Shetani. Licha ya kile Mungu anafanya na jinsi Anavyokifanya, Shetani ako nyuma Yake. Kiini na sura ya ukweli ya vitu hivi ambavyo Shetani anasema na kufanya ni kiini cha Shetani—kiini ovu, kiini cha kuonea kijicho. Sasa, kuendelea kusoma, ni nini tena Shetani anasema? Tuendelee kusoma hapa chini.
(Mat 4:5-6) Kisha Ibilisi akamchukua hadi mji mtakatifu, na kumweka juu ya kinara cha hekalu, Na akamwambia, Ukiwa wewe ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini: kwa maana imeandikwa,
Atawaagiza malaika wake wakuchunge: Na mikononi mwao watakubeba, usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe wakati wowote.
Hebu kwanza tuzungumze kuhusu kirai hiki cha Shetani. Alisema “Ukiwa wewe ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini ,” na kisha akadondoa kutoka kwa maandiko, “Atawaagiza malaika wake wakuchunge: Na mikononi mwao watakubeba, usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe wakati wowote .” Unahisi vipi unaposikia maneno ya Shetani? Si ni ya kitoto sana? Ni ya kitoto, upuuzi na kuchukiza. Mbona Nasema hivi? Daima Shetani hufanya kitu kijinga, anaamini kwamba ni mwerevu sana; na mara nyingi hutaja maandiko—hata neno la Mungu—anajaribu kuyabadili maneno haya dhidi ya Mungu kumshambulia na kumjaribu. Lengo lake la kufanya hivi ni kuharibu mpango wa kazi ya Mungu. Hata hivyo, unaona chochote kwa kile Shetani amesema? (Kuna nia mbaya hapo.) Shetani daima amekuwa mjaribu; haongei kwa njia inayoeleweka rahisi, huongea kwa njia isiyo wazi akitumia majaribu, ulaghai na ushawishi. Shetani anamjaribu Mungu na pia mwanadamu: Anafikiri kwamba Mungu na mwanadamu wote hawajui, ni wajinga, na hawawezi kutofautisha kwa wazi vitu vilivyo. Shetani anafikiri kwamba Mungu na pia mwanadamu hawataona hadi kwa kiini chake na kwamba Mungu na mwanadamu wote hawataona ujanja wake na nia zake mbaya. Si hapa ndipo Shetani anapata ujinga wake? (Ndiyo.) Zaidi, Shetani anataja maandiko wazi; anafikiria kwamba kufanya hivyo kunamfanya kuaminika, na kwamba hutaweza kuona dosari zozote kwa haya ama kuepuka kudanganywa na haya. Si hapa ndipo Shetani anakuwa mjinga na kama mtoto? (Ndiyo.) Hii ni kama wakati watu wengine wanaeneza injili na kuwa na ushuhuda kwa Mungu, si wasioamini watasema kitu kama alichosema Shetani? Umesikia watu wakisema kitu kama hiki? (Ndiyo.) Unahisi kuchukizwa unaposikia vitu kama hivyo? (Ndiyo,) Unapohisi kuchukizwa, pia unahisi kutiwa kinyaa na kukirihishwa? (Ndiyo.) Unapokuwa na hisia hizi unaweza kutambua kwamba Shetani na tabia potovu ambayo Shetani anamfanyia mwanadamu ni ovu? Katika mioyo yenu mmewahi kuwa na utambuzi kama, “Mungu kamwe haongei namna hiyo. Maneno ya Shetani yanaleta mashambulizi na majaribu, maneno yake ni ya ujinga, ya kuchekesha, ya kitoto, na ya kuchukiza. Hata hivyo, katika matamshi ya Mungu na vitendo vya Mungu, Hangetumia mbinu kama hizi kuzungumza ama kufanya kazi Yake, na Hajawahi kufanya hivyo”? Bila shaka, katika hali hii watu wana tu kiasi kidogo cha kuhisi kuendelea na hawana utambuzi wa utakatifu wa Mungu; wanaweza tu kukubali kwamba neno la Mungu ni ukweli, lakini hawajui kwamba ukweli ni utakatifu wenyewe. Na kimo chenu cha sasa, mnahisi tu hivi: “Kila kitu Mungu anasema ni ukweli, ni cha manufaa kwetu, na lazima tukikubali”; bila kujali iwapo unaweza kukubali hili au la, bila ubaguzi unasema kwamba maneno ya Mungu ni ukweli na kwamba Mungu ni ukweli, lakini hujui kwamba ukweli ni utakatifu wenyewe na kwamba Mungu ni mtakatifu. Hivyo, jibu la Yesu kwa maneno ya Shetani lilikuwa lipi?
(Mat 4:7) Yesu akamwambia, Imeandikwa tena, Usimjaribu Bwana Mungu wako.
Kuna ukweli katika kirai hiki ambacho Yesu alisema? (Ndiyo.) Kuna ukweli kwa kirai hicho. Juujuu inaonekana kama amri ya watu kufuata, ni kirai rahisi sana, lakini ni kimoja ambacho mwanadamu na Shetani wamekiuka mara nyingi. Hivyo, Bwana alimwambia, “Usimjaribu Bwana Mungu wako.” kwa sababu hiki ndicho kile Shetani alifanya mara nyingi na alifanya kila juhudi kufanya hivyo, unaweza hata kusema kwamba Shetani alifanya hivyo bila haya. Ni asili ya msingi ya Shetani kutomcha Mungu na kutomheshimu Mungu kwa moyo wake. Hivyo, hata wakati Shetani alikuwa kando ya Mungu na angeweza kumwona, Shetani hakuweza kuacha kumjaribu Mungu. Kwa hivyo, Bwana Yesu alimwambia Shetani, “Usimjaribu Bwana Mungu wako.” Hiki ni kirai ambacho Mungu amemwambia Shetani mara nyingi. Si kutumia kirai hiki kunafaa hata leo? (Ndiyo.) Mbona? (Kwa sababu pia sisi humjaribu Mungu mara nyingi.) Watu mara nyingi humjaribu Mungu, lakini mbona watu hufanya hivyo mara nyingi? Je, ni kwa sababu watu wamejawa na tabia potovu ya kishetani? (Ndiyo.) Kwa hivyo kile Shetani alisema hapa juu ni kitu ambacho watu husema mara nyingi? (Ndiyo.) Katika hali gani? Mtu anaweza kusema kwamba watu wamekuwa wakisema mambo kama haya na kuyafichua kiasili licha ya wakati na mahali. Hii inadhihirisha kwamba tabia ya watu ni sawa kabisa na tabia potovu ya Shetani. Bwana Yesu alisema kirai rahisi, ambacho kinawakilisha ukweli na ambacho watu wanahitaji. Hata hivyo, katika hali hii Bwana Yesu alikuwa akigombana na Shetani? Kulikuwa na chochote cha kukabiliana kwa kile Alisema kwa Shetani? (La.) Bwana Yesu aliyachukulia vipi majaribu ya Shetani kwa moyo Wake? Je, Alihisi kuchukizwa na kutiwa kinyaa? (Ndiyo.) Bwana Yesu alihisi kutiwa kinyaa na kuchukizwa lakini Hakugombana na Shetani, wala hata chini zaidi Hakuzungumza kuhusu kanuni zozote kubwa, sivyo? (Ndiyo.) Mbona hivyo? (Bwana Yesu hakutaka kumkiri Shetani.) Kwa nini Hakutaka kumkiri Shetani? (Kwa sababu Shetani daima ako hivyo, hawezi kubadilika.) Tunaweza kusema kwamba Shetani hana akili? (Ndiyo, tunaweza.) Je, Shetani anaweza kutambua kwamba Mungu ni ukweli? Shetani hatawahi kutambua kwamba Mungu ni ukweli na hatawahi kukubali kwamba Mungu ni ukweli; hii ni asili yake. Zaidi, kuna kitu kingine kuhusu asili ya Shetani kinachotia watu kinyaa, ni nini? Katika majaribio yake ya kumjaribu Bwana Yesu, aliamini nini katika moyo wake? Hata kama alimjaribu Mungu na hangefaulu, ila Shetani alijaribu tu. Hata kama angeadhibiwa, aliifanya tu. Hata kama hangepata chochote chema kutoka kwa kufanya hivyo, aliifanya tu, na kuendelea na kusimama dhidi ya Mungu hadi mwisho kabisa. Hii ni asili ya aina gani? Si huo ni uovu? (Ndiyo.) Yule anayekasirika sana wakati Mungu anatajwa, amemwona Mungu? Yule anayekuwa na hasira wakati Mungu anatajwa, anamjua Mungu? Hajui Mungu ni nani, hamwamini, na Mungu hajamwongelesha. Mungu hajawahi kumsumbua, kwa hivyo mbona akuwe na hasira? Tunaweza kusema kwamba mtu huyu ni mwovu? (Ndiyo.) Huyu anaweza kuwa mtu mwenye asili ovu? Haijalishi ni mienendo gani inafanyika duniani, iwe ya kufurahisha, chakula, watu maarufu, watu wenye sura nzuri, hakuna yoyote haya yanayomsumbua, lakini kutajwa mara moja kwa neno “Mungu” na anakasirika; huu si mfano wa asili ovu? Huu unatumika kama ushahidi wa kuridhisha wa asili ovu ya mwanadamu. Sasa, mkijizungumzia, kuna wakati ambapo ukweli unatajwa, ama wakati majaribio ya Mungu kwa mwanadamu yanatajwa ama wakati maneno ya Mungu ya hukumu dhidi ya mwanadamu yanatajwa, na mnahisi kusumbuliwa, kutiwa kinyaa, na hamtaki kusikia kuyahusu? Mioyo yenu inaweza kufikiri: Huu ni ukweli vipi? Si watu wote walisema kwamba Mungu ni ukweli? Huu si ukweli, haya bila shaka ni maneno ya Mungu ya maonyo kwa mwanadamu! Watu wengine hata wanaweza kuhisi kuchukizwa kwa mioyo yao: Haya yanatajwa kila siku, majaribio Yake kwetu yanatajwa kila siku kama hukumu Yake; haya yote yataisha lini? Tutapokea lini hatima njema? Haijulikani hasira hii isiyo na busara inatoka wapi. Hii ni asili ya aina gani? (Asili ovu.) Inasababishwa na asili ovu ya Shetani. Na kwa Mungu kuhusu asili ovu ya Shetani na tabia potovu ya mwanadamu, Hagombani kamwe wala kubishana na watu, na kamwe Halalamiki wakati watu wanatenda kutokana na ujinga. Hamtamwona Mungu akiwa na mitazamo sawa kuhusu vitu ambavyo watu wanavyo, na zaidi hamtamwona Akitumia maoni ya wanadamu, maarifa yao, sayansi yao ama filosofia yao ama fikira za mwanadamu kushughulikia vitu, Badala yake, kila kitu anachofanya Mungu na kila kitu Anachofichua kinahusiana na ukweli. Yaani, kila neno ambalo amesema na kila kitendo amefanya kinahusiana na ukweli. Ukweli huu sio tu ndoto isiyo na msingi; ukweli huu na maneno haya yanaelezwa na Mungu kwa sababu ya kiini cha Mungu na uhai Wake. Kwa sababu maneno haya na kiini cha kila kitu Mungu amefanya ni ukweli, hivyo tunaweza kusema kwamba kiini cha Mungu ni kitakatifu. Kwa maneno mengine, kila kitu ambacho Mungu anasema na kufanya kinaleta uzima na mwangaza kwa watu, kinawaruhusu watu kuona vitu vyema na uhalisi wa vitu hivi vyema na kuashiria ubinadamu kwa njia ya mwangaza ili waweza kutembea njia njema. Vitu hivi vinaamuliwa kwa sababu ya kiini cha Mungu na vinaamuliwa kwa sababu ya kiini cha utakatifu Wake. Mmekiona, siyo? Tutaendelea kuyasoma maandiko. .
(Mat 4:8-11) Tena, Ibilisi akamchukua hadi kwenye mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na utukufu wao; Na akamwambia, Hivi vyote nitakupa, ukianguka chini na kuniabudu. Kisha Yesu akamwambia, Ondoka uende zako, Shetani; kwa kuwa imeandikwa, Muabudu Bwana Mungu wako, na ni yeye peke yake utakayemtumikia. Basi Ibilisi akamwacha, na, tazama, malaika wakaja na wakamhudumia. Shetani, ibilisi, baada ya kushindwa katika hila zake mbili za awali, alijaribu nyingine tena: Alionyesha falme zote duniani na utukufu wa falme hizi kwa Bwana Yesu na kumwambia amwabudu ibilisi. Unaona nini kuhusu sura za ukweli za ibilisi kutoka kwa hali hii? Si Shetani ibilisi hana haya kabisa? (Ndiyo.) Anaweza kukosa haya namna gani? Kila kitu kiliumbwa na Mungu, lakini Shetani anakigeuza na kumwonyesha Mungu akisema, “Hivi vyote nitakupa, ukianguka chini na kuniabudu.” Je, si hili ni mabadiliko ya jukumu? Si Shetani hana haya? Mungu aliumba kila kitu, lakini kilikuwa cha raha Zake? Mungu alimpa mwanadamu kila kitu, lakini Shetani alitaka kunyakua vyote na baadaye akasema, “Niabudu! Niabudu na ntakupa Wewe haya yote.” Huu ni uso usiopendeza wa Shetani; hana haya kabisa, siyo? Shetani hata hajui maana ya neno “haya,” na huu ni mfano mwingine tu wa uovu wake. Hata hajui “haya” ni nini. Shetani anajua vyema kwamba Mungu aliumba kila kitu na kwamba Anavisimamia na Anavitawala. Kila kitu ni cha Mungu, si cha mwanadamu, sembuse Shetani, lakini Shetani ibilisi bila haya alisema kwamba angempa Mungu kila kitu. Si tena Shetani anafanya kitu cha ujinga na kisicho na aibu? Mungu anamchukia Shetani hata zaidi sasa, siyo? Lakini licha ya kile Shetani alijaribu kufanya, Bwana Yesu alikiamini? (La.) Bwana Yesu alisema nini? (“Muabudu Bwana Mungu wako,.”) Je, kirai hiki kina maana ya utendaji? (Ndiyo.) Maana gani ya utendaji? Tunaona uovu na kutokuwa na aibu kwa Shetani katika matamshi yake. Kwa hivyo iwapo mwanadamu angemwabudu Shetani, hitimisho lingekuwa nini? Angepokea utajiri na utukufu wa falme zote? (La.) Angepokea nini? Je, wanadamu wangekuwa wasio na haya na wa kuchekwa kama tu Shetani? (Ndiyo.) Hawangekuwa tofauti na Shetani basi. Kwa hivyo, Bwana Yesu alisema kirai hiki ambacho ni muhimu kwa kila mtu: “Muabudu Bwana Mungu wako, na ni yeye peke yake utakayemtumikia,” kinachosema kwamba isipokuwa Bwana, isipokuwa Mungu Mwenyewe, ukimhudumia mwengine, ukimwabudu Shetani ibilisi, basi utagaagaa katika uchafu sawa na Shetani. Kisha utashiriki kutokuwa na haya na uovu wa Shetani, na kama tu Shetani ungemjaribu Mungu na kumshambulia Mungu. Na basi mwisho wako ungekuwa upi? Ungechukiwa na Mungu, kufilishwa na Mungu na kuangamizwa na Mungu, sivyo? Baada ya Shetani kumjaribu Bwana Mungu mara kadhaa bila mafanikio, alijaribu tena? Shetani hakujaribu tena na kisha akaondoka. Hii inathibitisha nini? Inathibitisha kwamba asili ovu ya Shetani, kuonea kijicho kwake, na ujinga na upuuzi wake yote hayastahili kutajwa mbele ya Mungu kwa sababu Bwana Yesu alimshinda Shetani kwa sentensi tatu tu, na baadaye akatoroka na mkia wake katikati ya miguu yake, kuaibika sana asiweze kuonyesha uso wake tena, na hakumjaribu Yeye tena. Kwa sababu Bwana Yesu alikuwa amelishinda jaribio hili la Shetani, Angeweza kuendelea kwa urahisi kazi ambayo Alipaswa kufanya na kuanza kazi zilizokuwa mbele Yake. Je, yote aliyoyasema Bwana Yesu na kufanya katika hali hii yanabeba maana kiasi ya vitendo kwa kila mtu yakitumika sasa? (Ndiyo.) Maana ya utendaji ya aina gani? Je, kumshinda Shetani ni kitu rahisi kufanya? (La.) Ingekuwa nini basi? Ni lazima watu wawe na uelewa wazi wa asili ovu ya Shetani? Ni lazima watu wawe na uelewa sahihi wa majaribu ya Shetani? (Ndiyo.) Ukiwahi kupitia majaribu ya Shetani katika maisha yako, na iwapo unaweza kuona hadi kwa asili ovu ya Shetani, utaweza kumshinda? Iwapo unajua kuhusu ujinga na upuuzi wa Shetani, bado unaweza kusimama kando ya Shetani na kumshambulia Mungu? (La, hatungeweza.) Ikiwa unaelewa jinsi kuwa na kijicho na kutokuwa na aibu kwa Shetani vinafichuliwa kupitia kwako—iwapo unatambua wazi na kujua mambo haya—bado ungemshambulia na kumjaribu Mungu kwa njia hii? (La, hatungeweza.) Utafanya nini? (Tutaasi dhidi ya Shetani na kumwacha.) Hili ni jambo rahisi kufanya? (La.) Hili si rahisi, kufanya hivi, watu wanalazimika kuomba mara nyingi, ni lazima wajiweke mbele ya Mungu, na lazima wajichunguze. Lazima watii nidhamu ya Mungu na hukumu Yake na kuadibu Kwake na kwa njia hii tu ndipo watu wataweza kujitoa polepole kutoka kwa utawala na udhibiti wa Shetani.
Tunaweza kuweka pamoja mambo yanayojumuisha kiini cha Shetani kutoka kwa mambo haya ambayo amesema. Kwanza, kiini cha Shetani kwa jumla kinaweza kusemwa kuwa ovu, ambacho ni kinyume na utakatifu wa Mungu. Kwa nini Nasema kiini cha Shetani ni ovu? Mtu anapaswa kuangalia matokeo ya kile Shetani anafanyia watu ili kuona haya. Shetani anapotosha na kudhibiti mwanadamu, na mwanadamu anatenda chini ya tabia potovu ya Shetani, na anaishi katika dunia iliyopotoshwa na Shetani na kuishi miongoni mwa watu potovu. Wengi wanamilikiwa na kusimilishwa na Shetani bila kusudi na mwanadamu hivyo ana asili ovu ya Shetani. Kutoka kwa yote Shetani amesema na kufanya, tunaweza kuona kiburi chake na kuona ujanja na kijicho chake. Kiburi cha Shetani kimsingi kinaonekana vipi? Je, Shetani daima anataka kuchukua nafasi ya Mungu? Shetani daima anataka kuharibu kazi ya Mungu na nafasi ya Mungu na kuyachukua kuwa yake ili watu waunge mkono na kuabudu Shetani; hii ni asili ya kiburi ya Shetani. Lakini wakati Shetani anapotosha watu, anafanya hivyo kwa njia ya ujanja na ya usaliti: Wakati Shetani anafanya kazi yake kwa watu, hawaambii watu moja kwa moja jinsi ya kumkataa na kumpinga Mungu. Wakati Shetani anamjaribu Mungu, hatoki na kusema, “Nakujaribu, nitakushambulia,” hivyo Shetani anatumia mbinu gani? (Ushawishi.) Anashawishi, anajaribu, anashambulia, na anaweka mitego yake, na hata kwa kutaja maandiko, Shetani anazungumza na kutenda kwa njia mbalimbali ili kutimiza nia zake mbaya. Baada ya Shetani kufanya hivi, ni nini kinachoweza kuonekana kutoka kile kilichojitokeza kwa mwanadamu? Je, si watu wana kiburi? Mwanadamu ameteseka kutoka kwa upotovu wa Shetani kwa maelfu ya miaka na hivyo mwanadamu amekuwa mwenye kiburi na mwenye majivuno mengi sana, na amekuwa mjanja, mwenye kijicho, na asiyefikiri, siyo? Haya mambo yote yametokana kwa sababu ya asili ya Shetani. Kwa sababu asili ya Shetani ni ovu, amempa mwanadamu asili hii ovu na kumletea mwanadamu tabia hii potovu. Kwa hivyo, mwanadamu anaishi chini ya tabia potovu ya kishetani na, kama Shetani, mwanadamu anaenda kinyume na Mungu, anamshambulia Mungu, na kumjaribu Yeye hadi kwa kiwango ambacho mwanadamu hamwabudu Mungu na hamheshimu katika moyo wake, siyo?
Kuhusu utakatifu wa Mungu, hata kama inaweza kuwa mada inayojulikana, katika majadiliano inaweza kuwa dhahania kiasi kwa watu wengine, na maudhui yake yanaweza kuwa ya kina sana. Zamani, watu hawakushughulika sana na mada ya utakatifu wa Mungu, kwa hivyo hawaielewi. Lakini msijali, Nitawasaidia kuelewa maana ya utakatifu wa Mungu. Naona kwamba ni vigumu kidogo kwenu kupokea, wacha tuseme hili kwanza: Iwapo unataka kujua mtu, angalia tu kile anachofanya na matokeo ya vitendo vyake, na utaweza kuona kiini cha mtu huyo. Kwa hivyo hebu tushiriki kuhusu utakatifu wa Mungu kutoka kwa mtazamo huu kwanza. Tulisema kwamba kiini cha Shetani ni ovu na chenye kijicho, na kwa hivyo vitendo vya Shetani kwa mwanadamu vimekuwa kumpotosha bila kikomo. Shetani ni mwovu, kwa hivyo watu ambao amepotosha hakika ni waovu, siyo? Kuna yeyote anayeweza kusema, “Shetani ni mwovu, pengine mtu aliyepotosha ni mtakatifu”? Ni mzaha, siyo? Je, hata inawezekana? (La.) Kwa hivyo usimfikirie hivyo, wacha tumzungumzie kutoka kwa kipengele hiki: Shetani ni mwovu, hiki ni kiini chake na ni halisi, haya si mazungumzo matupu tu. Hatujaribu kusema uwongo juu ya Shetani; tunashiriki tu kuhusu ukweli na uhalisi na pia kuhusu ukweli unaomzunguka. Hii inaweza kuumiza watu wengine ama sehemu fulani ya watu, lakini hakuna nia mbaya hapa; pengine mtasikia haya leo na kuhisi kutostareheka kiasi, lakini siku fulani hivi punde, wakati mnaweza kumtambua, mtajichukia, na mtahisi kwamba kile tulichozungumzia leo ni cha manufaa kwenu na chenye thamani.
Kiini cha Shetani ni ovu, kwa hivyo matokeo ya vitendo vya Shetani bila shaka ni ovu, ama kwa kiwango cha chini kabisa, yanahusiana na uovu wake, tunaweza kusema hayo? (Ndiyo.) Kwa hivyo, je Shetani anampotosha mwanadamu vipi? Kwanza lazima tuangalie hasa—uovu uliofanywa na Shetani duniani na miongoni mwa ubinadamu ambao unaonekana, tunaoweza kuhisi; mmewahi kuyafikiria haya awali? Pengine hamkuyafikiria sana, kwa hivyo wacha Nitaje pointi kadhaa muhimu ili muweze kuona jinsi Shetani anampotosha mwanadamu. Kuna nadharia inayoitwa mageuko; kila mtu anajua kuihusu, siyo? Mageuko na uyakinifu huu, si sehemu ya maarifa yanayosomwa na mwanadamu? (Ndiyo.) Hivyo, Shetani kwanza anatumia maarifa kumpotosha mwanadamu, na kisha anatumia sayansi kuamsha mvuto wa wanadamu kwa maarifa, sayansi, na vitu vya ajabu, ama kwa vitu ambavyo watu wanataka kuchunguza; hii ni kusema, Shetani anatumia maarifa ya kisayansi kumpotosha mwanadamu. Vitu vifuatavyo vinavyotumiwa na Shetani kumpotosha mwanadamu ni desturi ya kitamaduni na ushirikina, na baada ya vitu hivyo, anatumia mienendo ya kijamii. Hivi vyote ni vitu ambavyo watu wanapatana navyo katika maisha yao ya kila siku na hivi vyote vinahusiana na vitu vilivyo karibu na watu, vitu wanavyoona, wanavyosikia, wanavyogusa na wanavyopitia. Mtu anaweza kusema kwamba vinazunguka kila mtu, haviwezi kutorokwa na kuepukika. Wanadamu hawana njia ya kuepuka kuathiriwa, kuambukizwa, kudhibitiwa, na kufungwa na vitu hivi; hawana nguvu za kuvisukuma mbali.
Kwanza tutazungumza kuhusu maarifa. Si kila mtu angechukulia maarifa kuwa kitu chema? Ama kwa kiwango cha chini kabisa, watu wanafikiri kwamba kidokezo cha neno “maarifa” ni chema badala ya hasi. Kwa hivyo mbona tunataja hapa kwamba Shetani anatumia maarifa kwanza kumpotosha mwanadamu? Si nadharia ya mageuko ni kipengele cha maarifa? Si sheria za kisayansi za Newton ni sehemu ya maarifa? Si mvuto wa dunia ni sehemu ya maarifa, siyo? (Ndiyo.) Hivyo mbona maarifa yametajwa miongoni mwa maudhui anayoyatumia Shetani kumpotosha mwanadamu? Maoni yenu hapa ni yapi? Je, maarifa yana hata chembe cha ukweli ndani yake? (La.) Kwa hivyo ni nini kiini cha maarifa? (Yanaenda kinyume na ukweli.) Maarifa ambayo mwanadamu anatafiti yanafunzwa kwa msingi upi? Yanalingana na nadharia ya mageuko? Si maarifa ambayo mwanadamu amechunguza, ujumla wake, unatokana na ukanaji Mungu? (Ndiyo.) Hivyo, kuna sehemu yoyote ya maarifa haya ambayo ina uhusiano na Mungu? Je, yanahusiana na kumwabudu Mungu? Yanahusiana na ukweli? (La.) Shetani anatumiaje maarifa kumpotosha mwanadamu? Nimetoka tu kusema kwamba hakuna sehemu yoyote ya maarifa haya inahusiana na kumwabudu Mungu ama na ukweli. Watu wengine wanayafikiria hivi: “Yanaweza kutokuwa na chochote kuhusiana na ukweli, lakini hayawapotoshi watu.” Mnafikiri nini kuhusu haya? Ulifundishwa na maarifa kwamba furaha ya watu ilitegemea kile walichokiumba na mikono yao? Je, maarifa yaliwahi kukufunza kwamba hatima ya mwanadamu ilikuwa mikononi mwake? (Ndiyo.) Haya ni mazungumzo ya aina gani? (Ni upuuzi.) Sahihi! Ni upuuzi! Maarifa yanatatiza kujadili. Unaweza kuiweka kwa urahisi kwamba eneo la maarifa ni maarifa tu. Hili ni eneo la maarifa linalofunzwa kwa msingi wa ukanaji Mungu na kutokuwa na uelewa kwamba Mungu aliumba mambo yote. Watu wanaposoma aina hii ya maarifa, hawaoni Mungu anatawala mambo yote, hawaoni Mungu anaongoza ama anasimamia mambo yote. Badala yake, wanayofanya tu ni kutafiti, kuchunguza, na kutafuta majibu ya kisayansi bila kikomo kwa sehemu hiyo ya maarifa. Hata hivyo, iwapo watu hawamwamini Mungu na badala yake wanatafiti tu, kamwe hawatapata majibu ya kweli, siyo? Maarifa yanakupa tu riziki, yanakupa tu kazi, yanakupa tu mapato ili usiwe na njaa, lakini kamwe hayawezi kukusaidia kumjua Mungu, hayatakusaidia kumwamini Yeye, kumtii Yeye, na maarifa kamwe hayatakuweka mbali na maovu. Kadiri unavyosoma maarifa, ndivyo utatamani zaidi kuasi dhidi ya Mungu, kumtafiti Mungu, kumjaribu Mungu, na kwenda kinyume na Mungu. Hivyo sasa, tunaona yapi ambayo maarifa yanawafunza watu? Yote ni filosofia ya Shetani. Je, filosofia za Shetani na kanuni za kuishi zinazopatikana kwa wanadamu potovu zina uhusiano wowote na ukweli? (La.) Hazina uhusiano wowote na ukweli na, kwa kweli, ni kinyume cha ukweli. Watu mara nyingi husema, “Maisha ni mwendo”; haya ni mazungumzo ya aina gani? (Upuuzi.) Watu pia wanasema, “Mwanadamu ni chuma, mchele ni chuma, mwanadamu huhisi anataabika kwa njaa asipokula mlo”; hii ni nini? (Upuuzi, maneno ya Shetani.) Hata ni uwongo mbaya zaidi na inachukiza kuisikia. Hivyo, maarifa ni kitu ambacho pengine kila mtu anakijua. Kwa yanayoitwa maarifa ya mwanadamu, Shetani amejaza kidogo filosofia yake ya maisha na kufikiria kwake. Na wakati Shetani anafanya haya, Shetani anamruhusu mwanadamu kuomba kufikiria kwake, filosofia, na mtazamo wake ili mwanadamu aweze kukana uwepo wa Mungu, kukana utawala wa Mungu juu ya mambo yote na utawala juu ya hatima ya mwanadamu. Kwa hivyo, masomo ya mwanadamu yanapoendelea, anahisi uwepo wa Mungu kuwa usio yakini anapopata maarifa zaidi, na mwanadamu anaweza hata kuhisi kwamba Mungu hayupo kwa sababu ya mitazamo, dhana, na fikira ambazo Shetani ameongeza kwa akili ya mwanadamu. Shetani anapoweka fikira hizi ndani ya akili ya mwanadamu, si watu wanapotoshwa na mambo haya? (Ndiyo.) Ni nini msingi wa maisha ya mwanadamu sasa? Kweli anategemea maarifa haya? La; msingi wa maisha ya mwanadamu ni fikira, mitazamo na filosofia za Shetani ambazo zimefichwa kwa maarifa haya. Hapa ndipo kiini cha upotovu wa Shetani wa mwanadamu unafanyika, hili ndilo lengo la Shetani na mbinu yake ya kumpotosha mwanadamu.
A. Jinsi Ambavyo Shetani Anatumia Maarifa Kumpotosha Mwanadamu
Kwanza tutazungumzia kipengele cha juujuu zaidi cha mada hii. Mlipokuwa mnafunzwa Kiswahili shuleni, je, lugha na maandishi yaliweza kuwapotosha watu? Hayangeweza. Maneno yanaweza kupotosha watu? (La.) Maneno hayapotoshi watu; ni chombo kinachowaruhusu watu kuongea na chombo ambacho watu wanatumia kuwasiliana na Mungu. Zaidi, lugha na maneno ni jinsi ambavyo Mungu anawasiliana na watu sasa, ni vyombo, ni vya umuhimu. Moja ongeza moja ni mbili, haya ni maarifa, siyo? Mbili zidisha kwa mbili ni nne, haya ni maarifa, siyo? Lakini yanaweza kukupotosha? Hii ni akili ya wote na kanuni kwa hivyo haiwezi kupotosha watu. Kwa hivyo ni maarifa gani yanayopotosha watu? Ni maarifa ambayo yamechanganywa mitazamo na fikira za Shetani, Shetani anataka kujaza mitazamo na fikira hizi ndani ya ubinadamu kupitia maarifa. Kwa mfano, katika insha, kuna chochote kibaya na maneno yaliyoandikwa? (La.) Hivyo, shida inaweza kuwa wapi? Mitazamo na nia ya mwandishi alipoandika insha hiyo na pia maudhui ya fikira zake—haya ni mambo ya kiroho—yanaweza kuwapotosha watu. Kwa mfano, iwapo ungekuwa ukitazama kipindi kwa runinga, ni mambo yapi ndani yake yangeweza kubadili mtazamo wako? Je, yale yaliyosemwa na wasanii, maneno yenyewe, yangeweza kuwapotosha watu? (La.) Ni mambo yapi ambayo yangeweza kuwapotosha watu? Ingekuwa fikira na maudhui ya kiini ya kipindi, ambayo yangewakilisha mitazamo ya mwelekezi, na taarifa iliyo kwa mitazamo hii ingeshawishi mioyo na akili za watu. Siyo? (Ndiyo.) Je, mnajua Narejelea nini katika mjadala Wangu wa Shetani kutumia maarifa kuwapotosha watu? (Ndiyo, tunajua.) Hutafahamu vibaya, siyo? Hivyo unaposoma riwaya ama insha tena, unaweza kutathmini iwapo fikira zilizoelezwa katika insha hiyo zinapotosha ama hazipotoshi mwanadamu ama kuchangia kwa ubinadamu? (Tunaweza kufanya hivyo kidogo.) Hiki ni kitu ambacho lazima kisomwe na kupitiwa polepole, si kitu kinachoeleweka kwa urahisi mara moja. Kwa mfano, unapotafiti ama kusoma sehemu ya maarifa, baadhi ya vipengele vyema vya maarifa hayo vinaweza kukusaidia kuelewa baadhi ya akili ya wote kuhusu eneo hilo, na kile ambacho watu wanapaswa kuepukana nacho. Chukua mfano wa “umeme,” hili ni eneo la maarifa, siyo? Ungekuwa mjinga kama hungejua kwamba umeme unaweza kuwatetemesha watu, siyo? Lakini utakapoelewa sehemu hii ya maarifa, hutakuwa na uzembe kuhusu kugusa kitu cha umeme na utajua jinsi ya kutumia umeme. Haya yote ni mambo mema. Unaelewa kile tunachojadili kuhusu jinsi maarifa yanawapotosha watu? (Ndiyo, tunaelewa.) Iwapo unaelewa hatutaendelea kukizungumzia zaidi kwa sababu kuna aina nyingi za maarifa ambazo zinasomwa duniani na lazima mchukue wakati wenu kuzitofautisha wenyewe.
B. Jinsi ambavyo Shetani Anatumia Sayansi Kupotosha Mwanadamu
Sayansi ni nini? Si sayansi imewekwa kwa hadhi ya juu na kuchukuliwa kuwa muhimu katika akili za karibu kila mtu? (Ndiyo, imewekwa kwa hadhi ya juu.) Sayansi inapotajwa, si watu wanahisi, “Hiki ni kitu ambacho watu wa kawaida hawawezi kuelewa, hii ni mada ambayo tu watafiti wa kisayansi ama wataalam wanaweza kugusia. Haina uhusiano wowote na sisi watu wa kawaida”? Je, ina uhusiano lakini? (Ndiyo.) Shetani anatumiaje sayansi kuwapotosha watu? Hatutazungumza kuhusu mambo mengine isipokuwa mambo ambayo watu mara nyingi wanapatana nayo katika maisha yao binafsi. Umesikia kuhusu “jeni,” siyo? (Ndiyo.) Nyote mnalijua neno hili, siyo? Je, jeni ziligunduliwa kupitia sayansi? Jeni zinamaanisha nini hasa kwa watu? Hazifanyi watu kuhisi kwamba mwili ni kitu cha ajabu? Wakati watu wanajulishwa kwa mada hii, si kutakuwa na watu—hasa wenye kutaka kujua—ambao watataka kujua zaidi ama kutaka maelezo zaidi? Hawa watu wanaotaka kujua wataweka nguvu zao zote kwa mada hii na wakati hawana shughuli watatafuta maelezo kwa vitabu na intaneti kujifunza maelezo zaidi kuihusu. Sayansi ni nini? Kuongea waziwazi, sayansi ni fikira na nadharia ya vitu ambavyo mwanadamu anataka kujua, vitu visivyojulikana, na ambavyo hawajaambiwa na Mungu; sayansi ni fikira na nadharia za siri ambazo mwanadamu anataka kuchunguza. Unafikiria wigo wa sayansi ni upi? Unaweza kusema kwamba unajumuisha mambo yote, lakini mwanadamu anafanya vipi kazi ya sayansi? Je, ni kupitia utafiti? Inahusiana na kutafiti maelezo na sheria za vitu hivi na kuweka mbele nadharia zisizoaminika ambazo watu wote wanafikiria, “Wanasayansi hawa ni wakubwa mno! Wanajua mengi na wana maarifa mengi kuelewa mambo haya!” Wanapendezwa sana na watu hao, siyo? Watu wanaotafiti sayansi, wana mitazamo ya aina gani? Hawataki kutafiti ulimwengu, kutafiti mambo ya ajabu ya maeneo ya maslahi yao? Matokeo ya mwisho ya haya ni nini? Baadhi ya sayansi ina watu wanaofikia mahitimisho yao kwa kubahatisha, nyingine ina watu wanaotegemea uzoefu wa binadamu kwa mahitimisho yao na hata eneo lingine la sayansi litakuwa na watu wanaofikia mahitimisho yao kutokana na uzoefu ama uchunguzi wa kihistoria na usuli. Sivyo? (Ndiyo.) Hivyo, sayansi inawafanyia nini watu? Kile sayansi inafanya ni kwamba inawaruhusu tu watu kuona vyombo katika ulimwengu wa maumbile na tu kuridhisha kutaka kujua kwa mwanadamu; haimruhusu mwanadamu kuona sheria ambazo Mungu anatumia kutawala mambo yote. Mwanadamu anaonekana kupata majibu kutoka kwa sayansi, lakini majibu hayo yanachanganya na yanaleta tu uradhi wa muda mfupi, uradhi ambao unawekea moyo wa mwanadamu mipaka kwa ulimwengu wa maumbile. Mwanadamu anahisi kwamba tayari amepata majibu kutoka kwa sayansi kwa hivyo licha ya suala litakaloibuka, anaamini kwa dhati mitazamo yao ya kisayansi kulithibitisha ama kulikubali. Moyo wa mwanadamu unamilikiwa na sayansi na kushawishiwa nayo hadi pahali ambapo mwanadamu tena hana akili ya kumjua Mungu, kumwabudu Mungu, na kuamini kwamba mambo yote yanatoka kwa Mungu na mwanadamu anapaswa kumwangalia kupata majibu. Hii si ukweli? Unaweza kuona kwamba kadiri ambavyo mtu anaamini sayansi, anakuwa mjinga zaidi, akiamini kwamba kila kitu kina suluhisho la sayansi, kwamba utafiti unaweza kutatua chochote. Hamtafuti Mungu na haamini kwamba Yupo; hata watu wengine ambao wamemfuata Mungu kwa miaka mingi wataenda na kutafiti vimelea kwa msukumo ama kutafuta baadhi ya maelezo ili kupata majibu. Mtu kama huyo haangalii masuala kwa mtazamo wa ukweli na wakati mwingi anataka kutegemea mitazamo na maarifa ya kisayansi ama majibu ya kisayansi kutatua shida; lakini hamtegemei Mungu na hamtafuti Mungu. Je, watu kama hao wana Mungu katika mioyo yao? (La.) Hata kuna watu wengine wanaotaka kutafiti Mungu kwa njia sawa na vile wanasoma sayansi. Kwa mfano, kuna wataalam wengi wa kidini walioenda mahali safina ilisimama baada ya mafuriko makubwa. Wameiona safina, lakini katika kuonekana kwa safina hawaoni uwepo wa Mungu. Wanaamini tu hadithi na historia na haya ni matokeo ya utafiti wao wa kisayansi na utafiti wa dunia ya maumbile. Ukitafiti vitu yakinifu, viwe mikrobiolojia, falaki, ama jiografia, hutawahi kupata matokeo yanayosema kwamba Mungu yupo ama kwamba anatawala mambo yote, Sivyo? (Ndiyo.) Kwa hivyo sayansi inamfanyia nini mwanadamu? Si inamweka mbali na Mungu? Si hii inawaruhusu watu kumtafiti Mungu? Si hii inawafanya watu kuwa na shaka zaidi kuhusu uwepo wa Mungu? (Ndiyo.) Kwa hivyo Shetani anataka kutumia vipi sayansi kumpotosha mwanadamu? Si Shetani anataka kutumia mahitimisho ya kisayansi kuwadanganya na kuwanyima watu hisia? Shetani anatumia majibu yenye maana nyingi kushikilia mioyo ya watu ili wasitafute ama kuamini uwepo wa Mungu, na hivyo watakuwa wenye tuhuma kwa Mungu, kumkanusha Mungu na kuwa mbali na Yeye. Hivyo, hii ndiyo sababu tunasema ni njia moja Shetani anawapotosha watu.
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili
Soma Zaidi: Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu, Chanzo cha Mafanikio ya Umeme wa Mashariki
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni