Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Maisha-ya-Petro. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Maisha-ya-Petro. Onyesha machapisho yote

2/20/2019

Wimbo Injili | Kutafuta Wandani

I
Umefanya kazi katika bustani kwa muda mrefu na Umepanda upendo Wako ndani sana.
Umelipa kila gharama, Ukitamani kuwapata watu ambao wana moyo mmoja na Wewe.
Umetafuta kwa muda mrefu—ni nani anayeweza kuelewa dhiki Yako?
Umewekeza upendo mwingi sana wa kweli, lakini ni vigumu Kwako kupata faraja katika maumivu Yako.

4/22/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kuhusu Maisha ya Petro

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kuhusu Maisha ya Petro

    Mwenyezi Mungu alisema, Petro ni mfano ambao Mungu aliutambulisha kwa wanadamu, na yeye ni mtu mashuhuri anayejulikana vizuri. Kwa nini mtu mnyonge kama huyo aliwekwa mahala kama mfano na Mungu na amesifiwa na vizazi vya baadaye? Bila shaka, ni wazi kwamba hili halitenganishwi na maonyesho yake na azimio lake la upendo kwa Mungu. Kuhusu wapi ambapo moyo wa Petro wa upendo kwa Mungu ulionyeshwa na kile ambacho uzoefu wake wa maishani ulivyokuwa kwa kweli, lazima turudi kwa Enzi ya Neema kutazama tena desturi za wakati huo, ili kumwona Petro wa enzi hiyo.
Petro alizaliwa katika nyumba ya kawaida ya wakulima wa Kiyahudi. Wazazi wake waliikimu familia yote kwa kufanya ukulima, naye alikuwa mzaliwa wa kwanza kati ya watoto wote; alikuwa na ndugu wanne.