V. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Tofauti Kati ya Kazi ya Mungu ya Hukumu Katika Siku za Mwisho na Kazi Yake ya Ukombozi Katika Enzi ya Neema
1. Kuna tofauti ipi kati ya maneno yaliyoonyeshwa na Bwana Yesu katika Enzi ya Neema na maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu katika Enzi ya Ufalme?
Aya za Biblia za Kurejelea:
“Tubuni: kwa kuwa ufalme wa mbinguni u karibu” (Mathayo 4:17).
“Na kwamba toba na msamaha wa dhambi vinapaswa kuhubiriwa katika jina lake miongoni mwa mataifa yote, kuanzia Yerusalemu” (Luka 24:47).
“Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana hatazungumza juu yake mwenyewe; bali chochote atakachosikia, atakinena: na atawaonyesha mambo yajayo” (Yohana 16:12-13).
“Na iwapo mtu yeyote atayasikia maneno yangu, na asiyaamini, Mimi sitamhukumu: kwa kuwa mimi sikuja ili niihukumu dunia, bali kuiokoa dunia. Yeye ambaye ananikataa mimi, na hayakubali maneno yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho” (Yohana 12:47-48).
Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya Yesu ilikuwa kwa ajili ya ukombozi wa mwanadamu na kusulubiwa tu. Kwa hivyo, hakukuwa na haja Kwake kusema maneno zaidi ili kumshinda mtu yeyote.