9/30/2019

2019 Swahili Gospel Worship song | "Toa Akili na Mwili ili Kutimiza Agizo la Mungu" (Lyrics Video)



2019 Swahili Gospel Worship song | "Toa Akili na Mwili ili Kutimiza Agizo la Mungu" (Lyrics Video)


I

Kama washiriki wa jamii ya wanadamu,
kama wafuasi wa Kristo wa dhati,
ni wajibu wetu, ni jukumu letu
kutoa akili zetu na miili yetu
kwa kutimiza agizo la Mungu.
Kwa maana asili yetu yote ilitoka kwa Mungu,
na twaishi, kwa ajili ya ukuu Wake.
Kwa maana asili yetu, ilitoka kwa Mungu,
na twaishi, kwa ajili ya ukuu Wake.

9/29/2019

Neno la Mungu | Sura ya 108

Neno la Mungu | Sura ya 108

Ndani Yangu, wote wanaweza kupata raha na wote wanaweza kuwa huru. Wale walio nje Yangu hawawezi kupata uhuru na furaha kwa sababu Roho Wangu hayuko pamoja na watu hawa. Watu hawa wanaitwa wafu wasio na roho. Nami Nawaita wale walio ndani Yangu watu walio hai wenye roho. Wao ni Wangu, na watarudi kwenye kiti Changu cha enzi. Wale ambao hutoa huduma na wale ambao ni wa ibilisi ni wafu wasio na roho, nao wanapaswa kuangamizwa hadi wawe katika hali ya kutokuwepo.

9/28/2019

3. Ni lazima mtu atambue tofauti kati ya njia ya toba katika Enzi ya Neema na njia ya uzima wa milele katika siku za mwisho

VII. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Kwamba ni Kile tu Ambacho Kristo wa Siku za Mwisho Analeta Kilicho Njia ya Uzima wa Milele


3. Ni lazima mtu atambue tofauti kati ya njia ya toba katika Enzi ya Neema na njia ya uzima wa milele katika siku za mwisho


Aya za Biblia za Kurejelea:

“Na iwapo mtu yeyote atayasikia maneno yangu, na asiyaamini, Mimi sitamhukumu: kwa kuwa mimi sikuja ili niihukumu dunia, bali kuiokoa dunia. Yeye ambaye ananikataa mimi, na hayakubali maneno yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho” (Yohana 12:47-48).

9/27/2019

“Kumbukumbu Chungu” – Ni Vigezo Vipi vya Kuingia Kwenye Ufalme wa Mbinguni? | Filamu za Kikristo (Movie Clip 2/5)



“Kumbukumbu Chungu” – Ni Vigezo Vipi vya Kuingia Kwenye Ufalme wa Mbinguni? | Filamu za Kikristo (Movie Clip 2/5)


Kuhusiana na ni mtu aina gani anayeweza kuingia kwenye ufalme wa mbinguni, Bwana Yesu alisema, "ila yule atendaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni" (Mathayo 7:21). Kwa hivyo ni mtu aina gani hasa anayefanya mapenzi ya Baba wa mbinguni? Watu wengi husadiki kwamba wale wanaofuata mfano wa Paulo na kufanya kazi kwa uangalifu na bidii nyingi kwa ajili ya Bwana ndio wanaofanya mapenzi ya Baba wa mbinguni. Kisha kunao wale wanaosadiki kwamba wale ambao wanampenda Mungu pekee kwa moyo wao wote, akili na nafsi, ambao hawatendi dhambi tena na wamefikia utakaso, ndio wanaofanya mapenzi ya Baba wa mbinguni. Hivyo ni nani aliye sahihi na nani asiye sahihi kutokana na mitazamo hii miwili? Tafadhali tazama pande zote mbili zikishiriki katika majadiliano makali!

9/26/2019

“Wimbo wa Ushindi” – Jinsi ya Kugundua Mafarisayo wa Kisasa | Swahili Gospel Movie Clip 2/7



Wakati Bwana Yesu alikuja kufanya kazi Yake, mkuu wa ulimwengu wa dini alimshutumu na kumhukumu, na hatimaye wakaungana na serikali ya Kirumi kumsulubisha. Siku hizi mwenendo wa dhambi wa wale walio katika ulimwengu wa kidini ambao humpinga Mwenyezi Mungu ni sawa na maneno na matendo ya kutisha ya Wayahudi waliompinga Bwana Yesu wakati huo. Kwa nini hili liko hivi? Unajua sababu ya msingi ya kwa nini wanampinga Mungu? Je, unataka kuelewa kiini chao? Basi tazama video hii!

Sehemu Vita vya kiroho ni mkusanyiko wa ushuhuda wa Wakristo ambao walishindwa Shetani katika vita vya kiroho chini ya uongozi wa maneno ya Mungu baada ya kukubali wokovu wa Mungu wa siku za mwisho.

9/25/2019

“Wimbo wa Ushindi” – Je, Bwana Atatokeaje na Kufanya Kazi Yake Wakati Atakaporudi? | Swahili Gospel Movie Clip 1/7



“Wimbo wa Ushindi” – Je, Bwana Atatokeaje na Kufanya Kazi Yake Wakati Atakaporudi? | Swahili Gospel Movie Clip 1/7


Ishara ya maafa makubwa wakati wa siku za mwisho- miezi minne ya damu imetokea na nyota za angani zimechukua kuonekana kwa ajabu; maafa makubwa yanakaribia, na wengi wa wale walio na imani katika Bwana wamepata hisia ya kurudi Kwake kwa pili au kwamba tayari Amewasili. Wakati wote wanasubiri kuja kwa mara ya pili kwa Bwana kwa hamu kubwa, labda tumefikiria juu ya maswali yafuatayo: Je, Bwana ataonekanaje kwa mwanadamu Atakaporudi katika siku za mwisho? Je, ni kazi gani ambayo Bwana atafanya wakati Atakapokuja tena? Je, unabii wa hukumu ya kiti kikuu cheupe cha enzi kutoka Kitabu cha Ufunuo utatimizwaje hasa? Video hii fupi itafunua majibu kwako!

9/24/2019

Neno la Mungu | Sura ya 12

Ikiwa una tabia ambayo si thabiti, nyepesi kuhamaki kama upepo au mvua, kama huwezi kuendelea kusonga mbele, basi fimbo Yangu haitakuwa mbali na wewe. Unaposhughulikiwa, kadiri hali ilivyo mbaya zaidi, na kadiri unavyoteswa zaidi, ndivyo upendo wako kwa Mungu unavyoongezeka, na unaacha kushikilia dunia. Bila njia nyingine, unakuja Kwangu, na unapata tena nguvu na imani yako. Ilhali, katika hali rahisi, ungeboronga. Ni lazima uingie ndani kwa mtazamo chanya, uwe mwenye vitendo na si baridi.

9/23/2019

Wale Ambao Mungu Atawaokoa ni wa Kwanza Kabisa Moyoni Mwake

Wale Ambao Mungu Atawaokoa ni wa Kwanza Kabisa Moyoni Mwake

I
Kazi ya Mungu ya kuokoa ni muhimu vipi,
muhimu zaidi kuliko vitu vingine vyote Kwake.
Kwa mipango na mapenzi yaliyokusudiwa, sio mawazo na maneno tu,
Anafanya kila kitu kwa wanadamu wote.
Oh ni muhimu kiasi gani, kazi ya Mungu ya kuokoa, kwa ajili ya mwanadamu na Yeye Mwenyewe.
Jinsi gani Mungu anajishughulisha, ni juhudi gani Anayofanya.
Anasimamia kazi Yake, anatawala vyote, watu wote.
Hajawahi kuonekana kabla, kwa gharama kubwa sana.

9/22/2019

2. Kuna tofauti ipi kati ya jinsi ambavyo Bwana Yesu alifanya kazi katika Enzi ya Neema na jinsi Mwenyezi Mungu anavyofanya katika Enzi ya Ufalme?

V. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Tofauti Kati ya Kazi ya Mungu ya Hukumu Katika Siku za Mwisho na Kazi Yake ya Ukombozi Katika Enzi ya Neema

2. Kuna tofauti ipi kati ya jinsi ambavyo Bwana Yesu alifanya kazi katika Enzi ya Neema na jinsi Mwenyezi Mungu anavyofanya katika Enzi ya Ufalme?

Maneno Husika ya Mungu:
Wakati wa kupata mwili Kwake mara ya kwanza, ilikuwa muhimu kwa Mungu kuponya wagonjwa na kufukuza mapepo kwa sababu kazi Yake ilikuwa ni kukomboa. Ili kulikomboa kabila lote la mwanadamu, Alipaswa kuwa mwenye upendo na mwenye kusamehe. Kazi Aliyoifanya kabla ya kusulubiwa ilikuwa kuponya watu na kufukuza mapepo, ambayo iliashiria wokovu Wake wa mwanadamu kutoka katika dhambi na uchafu.

9/21/2019

“Kumbukumbu Chungu” – Uhusiano Kati ya Hukumu katika Siku za Mwisho na Kuingia kwenye Ufalme wa Mbinguni? | Filamu za Kikristo (Movie Clip 5/5)



“Kumbukumbu Chungu” – Uhusiano Kati ya Hukumu katika Siku za Mwisho na Kuingia kwenye Ufalme wa Mbinguni? | Filamu za Kikristo (Movie Clip 5/5)


Katika ulimwengu wa kidini, kunao wengi wanaosadiki kwamba mradi tu wanahifadhi jina la Bwana, kusadiki kabisa katika ahadi ya Bwana na kufanya kazi kwa uangalifu na bidii nyingi kwa ajili ya Bwana, wakati Atarudi wanaweza kunyakuliwa na kuingia kwenye ufalme wa mbinguni. Je, yeyote anaweza kuingia kwenye ufalme wa mbinguni kwa kumsadiki Bwana kwa njia hii? Ni nini kitatufanyikia kama tusipoikubali kazi ya hukumu ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho?

9/20/2019

"Mazungumzo" – Upingaji wa Ajabu wa Mkristo wa Mawazo ya Mchungaji wa Utatu | Swahili Christian Video Clip 5/6


"Mazungumzo" – Upingaji wa Ajabu wa Mkristo wa Mawazo ya Mchungaji wa Utatu | Swahili Christian Video Clip 5/6


CCP kinamkaribisha mchungaji na Kanisa la Utatu kujaribu kumtia kasumba na kumbadilisha Mkristo mmoja. Huyu Mkristo na mchungaji wanafungua mjadala mzuri katika kukabiliana na dhana zilizotolewa na mchungaji wa Utatu. Je, Mkristo huyu atampingaje huyu mchungaji? Kwa nini jaribio hili la CCP katika kutia kasumba na ubadilishaji utaishia kushindwa?

Zaidi: 1. Ni jinsi gani mtu anafaa kuitambua sauti ya Mungu? Je, mtu anawezaje kuthibitisha kwamba Mwenyezi Mungu kweli ni Bwana Yesu aliyerudi?

9/19/2019

"Mazungumzo" – Kuitii Serikali Inayotawala Sio Sawa na Kumtii Mungu | Swahili Christian Video Clip 4/6




"Mazungumzo" – Kuitii Serikali Inayotawala Sio Sawa na Kumtii Mungu | Swahili Christian Video Clip 4/6


Ili kumdanganya na kumjaribu Mkristo mmoja kumtelekeza Mungu, CCP kilimwita mchungaji mmoja wa Kanisa la Utatu kumtia kasumba, na Mkristo huyu na mchungaji wakazua mjadala mzuri juu ya maneno ya Paulo: "Acha kila nafsi itii mamlaka ya juu zaidi. Kwani hakuna mamlaka isipokuwa ya Mungu: mamlaka yaliyoko yameamriwa na Mungu" (Warumi 13:1). Fasiri zao tofauti ni zipi za maneno haya? Mchungaji wa Utatu yuko chini ya CCP na huchukua njia ya Kanisa la Utatu—kwa kweli ni kusudi gani la siri liko hapo? Mkristo atakanaje hoja hii ya mchungaji "kuwa chini ya mamlaka ya juu"?


Iliyotazamwa Mara Nyingi: Filamu za Kikristo | "Mazungumzo" | Christian Testimony of Overcoming Satan

9/18/2019

2. Ni lazima mtu aelewe kwamba ukweli wote ulioonyeshwa na Mungu katika siku za mwisho ndio njia ya uzima wa milele

VII. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Kwamba ni Kile tu Ambacho Kristo wa Siku za Mwisho Analeta Kilicho Njia ya Uzima wa Milele

2. Ni lazima mtu aelewe kwamba ukweli wote ulioonyeshwa na Mungu katika siku za mwisho ndio njia ya uzima wa milele

Aya za Biblia za Kurejelea:
Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana hatazungumza juu yake mwenyewe; bali chochote atakachosikia, atakinena: na atawaonyesha mambo yajayo” (Yohana 16:12-13).

9/17/2019

"Mazungumzo" – Upingaji wa Wakristo wa Kushangaza kwa Uvumi na Kashfa za CCP | Swahili Christian Video Clip 3/6



"Mazungumzo" – Upingaji wa Wakristo wa Kushangaza kwa Uvumi na Kashfa za CCP | Swahili Christian Video Clip 3/6


Ili kuwadanganya Wakristo kumsaliti Mungu na kuiacha imani yao, CCP kimemsaliti Kristo wa siku za mwisho na Bwana Yesu hadharani, kikisema kuwa wote wawili ni watu wa kawaida na sio Mungu mwenye mwili. CCP kimewakashifu Wakristo kama wanaomwamini mtu tu na sio Mungu. Pia kimeeneza uvumi kwamba Kanisa la Mwenyezi Mungu liliundwa na mtu kwa kuwa tu mtu ambaye hutumiwa na Mungu ndiye anayeyaendesha mambo yote ya utawala ya kanisa. Kupata mwili kwa kweli ni nini? Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzwaje, na ni nani aliyelianzisha? Wakristo wanautumiaje ukweli na mambo ya hakika kukanusha uvumi na kashfa za umma ambazo CCP kinaeneza kuhusu Kristo na Kanisa la Mwenyezi Mungu?

Unaweza Pia Kupenda: 1. Ni jinsi gani mtu anafaa kuitambua sauti ya Mungu? Je, mtu anawezaje kuthibitisha kwamba Mwenyezi Mungu kweli ni Bwana Yesu aliyerudi?

9/16/2019

"Mazungumzo" – Jinsi Wakristo Wanavyoukabili Utiaji Kasumba wa Ukanaji Mungu wa CCP | Swahili Christian Video Clip 2/6



"Mazungumzo" – Jinsi Wakristo Wanavyoukabili Utiaji Kasumba wa Ukanaji Mungu wa CCP | Swahili Christian Video Clip 2/6


Ili kuwalazimisha Wakristo kumtelekeza Mungu na kuiacha imani yao, CCP haijawaashawishi Wakristo kwa umaarufu na hadhi tu, lakini imewatia kasumba ya ukanaji Mungu, uyakinifu, kuamini mageuko, na maarifa ya kisayansi. Kwa hiyo Wakristo wamepokeaje utiaji kasumba na ubadilishaji wa CCP? Kwa nini wanaendelea kufuatilia kwa ukaidi njia ya kumwamini Mungu na kumfuata Mungu? Video hii fupi ya ajabu umetayarishiwiwa ili kuyajibu maswali haya.

Tazama Video: Filamu za Kikristo | "Mazungumzo" | Christian Testimony of Overcoming Satan

9/15/2019

"Mazungumzo" – Kwa nini CCP Huwafuatia na Kuwakandamiza Wakristo Sana? | Swahili Christian Video Clip 1/6



"Mazungumzo" – Kwa nini CCP Huwafuatia na Kuwakandamiza Wakristo Sana? | Swahili Christian Video Clip 1/6


Katiba ya China hutamka kwa dhahiri uhuru wa dini, lakini kisirisiri, serikali hutumia rasilimali nyingi mno za binadamu na za kifedha kwa kuikandamiza imani ya dini na kuwatesa Wakristo kikatili. Hata hawajaacha kununua vifaa vya hali ya juu zaidi kuwafuatia, kuwafuma, na kuwakamata Wakristo. Serikali ya China imewanyang'anya raia wake haki ya uhuru wa imani na imewanyima kwa utundu haki ya kuishi. Kwa hiyo kwa kweli ni nini sababu na lengo la CCP kufanya yote haya?

9/14/2019

Ulimwengu wote ni Mpya Kabisa katika Utukufu wa Mungu

Katika ufalme Wake, maneno ya Mungu hutoka.
Naye hutembea kila mahali duniani.
Naye amefanikiwa juu ya maeneo yote ya duniani,
juu ya nchi yote iliyo najisi na yenye uchafu.
Sio mbingu tu bali dunia inabadilika.
Na hivi karibuni dunia itafanywa upya.
Ulimwengu wote ni Mpya Kabisa katika Utukufu wa Mungu.
Ni ajabu iliyoje kwa kila mtu kuona.
Inaonekana kama mmwanadamu anaishi mbinguni ambako mwanadamu anafikiria,
huru kutoka kwa mfumbato wa Shetani na mashambulizi ya maadui.

9/13/2019

“Kupita Katika Mtego” – Je, Kuamini katika Biblia Kunaweza Kuwakilisha Kumwamini Mungu? | Filamu za Injili (Movie Clip 3/7)



“Kupita Katika Mtego” – Je, Kuamini katika Biblia Kunaweza Kuwakilisha Kumwamini Mungu? | Filamu za Injili (Movie Clip 3/7)


Wachungaji na wazee wa ulimwengu wa dini hushikilia maneno ya Paulo katika Biblia yanayosema "Maandiko yote yametolewa kwa msukumo wa Mungu," wakiamini kwamba Biblia ni maneno ya Mungu kabisa na kufanya yote wanayoweza kuiinua Biblia na kuishuhudia, na kuifanya Biblia na Mungu kuwa visawe. Wanaamini kwamba Biblia inamwakilisha Bwana na kwamba imani katika Bwana ni imani katika Biblia. Je, Biblia nzima kweli imetolewa kwa msukumo wa Mungu? Je, Bwana, Mungu, yuko ndani ya Biblia? Je, ni kazi ya Mungu ambayo imetoa Biblia, au Biblia ambayo imetoa kazi ya Mungu? Je, Biblia inaweza kweli kumwakilisha Bwana? Video hii fupi itakuonyesha njia sahihi.

Zaidi: Maneno ya Roho Mtakatifu | "Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?"

9/12/2019

2. Ni nini tofauti muhimu kati ya kuokolewa na wokovu?

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

VI. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Kipengele cha Ukweli Kuhusu Tofauti Kati ya Kuokolewa Katika Enzi ya Neema na Wokovu katika Enzi ya Ufalme

2. Ni nini tofauti muhimu kati ya kuokolewa na wokovu?

Aya za Biblia za Kurejelea:
Hakika nawaambieni, Yeyote ambaye hutenda dhambi ni mtumishi wa dhambi. Na mtumishi haishi katika nyumba milele: lakini Mwana huishi milele” (Yohana 8:34-35).
Siye kila mmoja ambaye aliniambia, Bwana, Bwana, ataingia ufalme wa mbinguni, ila yeye atendaye mapenzi ya Baba yangu ambaye yuko mbinguni” (Mathayo 7:21).

9/11/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 28

Unaona kwamba muda ni mfupi sana na kazi ya Roho Mtakatifu inavurumisha mbele, ikikusababisha kupata baraka kubwa hivi, kumpokea Mfalme wa ulimwengu, Mwenyezi Mungu, ambaye ni Jua ling’aalo, Mfalme wa ufalme—hii yote ni neema na huruma Yangu. Kuna nini kinachoweza kuwepo kinachoweza kukutoa kwa upendo Wangu? Tafakari kwa makini, usijaribu kuepa, subiri kwa ustahamilivu mbele Yangu kila wakati na usiwe ukizurura nje daima. 

9/10/2019

Swahili Christian Skit "Mipaka ya Meya wa Kijiji" | Why Is There No Religious Freedom in China?



Swahili Christian Skit "Mipaka ya Meya wa Kijiji" | Why Is There No Religious Freedom in China?


Mchezo mfupi Mipaka ya Meya wa Kijiji inaeleza hadithi ya kweli ya mume na mke Wakristo ambao wanalazimishwa kutoroka kwa sababu ya mateso ya serilaki ya CCP.

Mkristo Liu Ming'en anahukumiwa na CCP miaka saba gerezani kwa kuamini katika Mungu. Hata baada ya kuachiliwa kutoka gerezani, anabakia kuwa wakulengwa na uchunguzi mkali wa CCP. Meya wa kijiji anatumia mfumo wa wajibu wa kaya-tano , kamera za usalama, ziara za nyumba, na njia nyingine kumzuia Liu Ming'en na mkewe kuamini katika Mungu, lakini hakuna inayoleta na matokeo yanayotakiwa.

9/09/2019

Filamu za Injili | "Kupita Katika Mtego" | See Through Rumors and Welcome the Lord



Filamu za Injili | "Kupita Katika Mtego" | See Through Rumors and Welcome the Lord


Miaka 2,000 iliyopita, Bwana Yesu alipofanya kazi ya ukombozi, Alipitia kashfa mbaya na shutuma kutoka kwa jamii ya kidini ya Kiyahudi. Viongozi wa Kiyahudi walijiunga na serikali ya Kirumi na kumsulubisha msalabani. Katika siku za mwisho, Mwenyezi Mungu—Bwana Yesu aliyerudi katika mwili—Amefika nchini China kufanya kazi ya hukumu. Tena, Anakabiliwa na hukumu ya kichaa, kukandamiza, na kukamatwa wakati huu na serikali ya Kikomunisti ya China na ulimwengu wa kidini. Uvumi ulioenea na mawazo yasiyofaa ambayo huhukumu na kuliharibia jina Kanisa la Mwenyezi Mungu ni kama mtego usioonekana, unaofunga na kuwadhibiti waumini wasiohesaka. Tanzia ya historia inajirudia yenyewe ...

Yaliyopendekezwa: Pakua Programu Bila Malipo

9/08/2019

1. Kuokolewa ni nini? Wokovu ni nini?

VI. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Kipengele cha Ukweli Kuhusu Tofauti Kati ya Kuokolewa Katika Enzi ya Neema na Wokovu katika Enzi ya Ufalme

1. Kuokolewa ni nini? Wokovu ni nini?

Aya za Biblia za Kurejelea:
Yule ambaye anaamini na kubatizwa ataokolewa; lakini yule ambaye haamini atahukumiwa” (Marko 16:16).
Kwa kuwa hii ni damu yangu ya agano jipya, ambayo inamwagwa kwa ajiki ya msamaha wa dhambi” (Mathayo 26:28).
Siye kila mmoja ambaye aliniambia, Bwana, Bwana, ataingia ufalme wa mbinguni, ila yeye atendaye mapenzi ya Baba yangu ambaye yuko mbinguni” (Mathayo 7:21).

9/07/2019

Mungu Anamthamini Yule Anayeweza Kusikiliza Neno Lake na Kumtii


Mungu Anamthamini Yule Anayeweza Kusikiliza Neno Lake na Kumtii



I

Mungu hajali kama mtu ni wa chini ama mkubwa.
Mradi tu anamsikiliza Mungu,
anatii kile ambacho Mungu anaamuru na kumwaminia,
anaweza kushirikiana na kazi Yake, na mpango Wake na mapenzi Yake,
ili mapenzi Yake na mpango uweze kuendelea bila kizuizi,
kitendo kama hiki kinastahili, kinastahili kukumbukwa na Mungu,
na kinastahili kupokea, kupokea baraka Yake.
Mungu anathamini watu kama hao, na Anapenda sana matendo yao,
na moyo wao na upendo Kwake.
Huu ni mtazamo wa Mungu.

9/06/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 33

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 33

Ufalme Wangu unawahitaji wale ambao ni waaminifu, wasio wanafiki, na wasio wadanganyifu. Je, si watu wenye moyo safi na waaminifu duniani hawapendwi na watu? Mimi ni kinyume kabisa cha jinsi ilivyo. Inakubalika kwa watu waaminifu kuja Kwangu; Nafurahia mtu wa aina hii, pia Ninamhitaji mtu wa aina hii. Hii ni haki Yangu hasa. Watu wengine ni wajinga; hawawezi kuhisi kazi ya Roho Mtakatifu na hawawezi kuyaelewa mapenzi Yangu. Hawawezi kuona familia yao na hali zinazowazingira kwa uwazi, wanafanya vitu bila kufikiri na kupoteza fursa nyingi za neema.

9/05/2019

Jinsi Upendo wa Mungu kwa Mwanadamu Ulivyo Muhimu




Jinsi Upendo wa Mungu kwa Mwanadamu Ulivyo Muhimu


I

Mandhari iliyochorwa katika Biblia "Amri ya Mungu kwa Adamu" ni ya kugusa na yenye kutia moyo. Ingawa hiyo picha ina Mungu na mtu tu, uhusiano kati ya hao wawili ni wa ndani sana tunaanza kuhisi mshangao, mshangao na uvutiwaji.

II

Upendo wa Mungu unaofurika umepewa mwanadamu bure, upendo wa Mungu umemzunguka. Mwanadamu, maasumu na safi, bila ya wajibu wa kumnyima uhuru, huishi kwa furaha kamili machoni mwa Mungu. Mungu humtunza mtu, na mtu huishi chini ya mabawa Yake. Yote ambayo mtu hufanya, maneno yake yote na matendo, yamefungwa pamoja na Mungu, hayawezi kujitenga.

9/04/2019

Mungu Mwenye Mwili Awaongoza Binadamu Kuingia Katika Enzi Mpya

Mungu Mwenye Mwili Awaongoza Binadamu Kuingia Katika Enzi Mpya

I

Mungu mwenye mwili, Anaitamatisha enzi
wakati tu mgongo wa Yehova ulionekana.
Pia Anahitimisha enzi ya imani
ambapo kutokuwa yakini kwa Mungu kulifikiriwa.
Kazi ya Mungu wa mwisho mwenye mwili
humleta mwanadamu katika enzi ya utendaji zaidi.
Kazi Anayofanya huwaleta binadamu wote
kwa wakati wa kupendeza na wa kweli zaidi.
Anatamatisha enzi ya udhahania,
Anatamatisha enzi ambapo mwanadamu
alitamani kuutafuta uso wa Mungu lakini hakuweza wakati huo.
Anatamatisha huduma ya mwanadamu kwa Shetani, mwanadamu anaongozwa hadi katika enzi mpya.
Yote haya yanafanikishwa na kazi ya Mungu katika mwili,
badala ya Roho wa Mungu pekee.

9/03/2019

Neno la Mungu "Je, Kazi ya Mungu ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania?" (Official Video)



Maneno ya Mungu "Je, Kazi ya Mungu ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania?"(Official Video)


Mwenyezi Mungu anasema, "Unapaswa kuona kuwa mapenzi Yake na kazi Yake si rahisi kama ilivyokuwa katika kuumba mbingu na nchi na vyote vilivyomo. Kwa sababu kazi ya leo ni kubadilisha wale waliopotoshwa, wale waliokufa ganzi, na kutakasa walioumbwa kisha kushughulikiwa na Shetani, si kuumba Adamu na Hawa, ama hata kuumba mwanga, ama aina yote ya mimea na wanyama. Kazi Yake sasa ni kutakasa wote waliopotoshwa na Shetani ili kwamba wamrejelee, wawe miliki Yake na wawe utukufu wake. Kazi kama ile si rahisi jinsi mwanadamu anavyofikiria kuhusu kuumbwa kwa mbingu na nchi na vilivyomo, wala si sawa na kumkemea Shetani aende katika shimo lisilo na mwisho, kama anayvodhania mwanadamu. Bali, ni kumbadilisha mtu, kubadili kilicho hasi kuwa chanya na kufanya kuwa miliki Yake ambacho si chake."

Iliyotazamwa Mara Nyingi: Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Maneno

9/02/2019

Latest Swahili Gospel Movie "Siri ya Utauwa: Mfuatano" | God is the Way, the Truth, and the Life




Lin Bo'en ni mhubiri mzee ambaye amemwani Bwana kwa miongo mingi. Tangu alipomkubali Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho, alihukumiwa, akatengwa, na akafukuzwa kutoka kwa jumuiya ya kidini na wachungaji na wazee wa kanisa, nguvu zinazompinga Kristo. Lakini ingawa Lin Bo’en alishambuliwa, akahukumiwa na kusingiziwa, hakusita kwa woga. Badala yake, imani yake ikawa thabiti zaidi kuliko ilivyowahi kuwa, na hili lilimwongoza kufahamu hatimaye kwamba wachungaji na wazee wa kanisa wa ulimwengu wa dini walikuwa wakiigiza kwa udanganyifu sura adilifu. 

9/01/2019

Best Christian Worship Songs Swahili | Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho



Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho


Mungu ndiye Mwanzo, Mungu ndiye Mwanzo, Mungu ndiye Mwanzo, na tena Mwisho, na tena Mwisho, na tena Mwisho. Mungu ndiye Mpanzi, Mungu ndiye Mpanzi, Mungu ndiye Mpanzi, na Mvunaji (Mvunaji). Mungu ndiye Mwanzo na Mwisho; Mungu ndiye Mpanzi na Mvunaji. Mungu ndiye Mwanzo na Mwisho; Mungu ndiye Mpanzi na Mvunaji. Mungu ndiye Mwanzo na Mwisho; Mungu ndiye Mpanzi na Mvunaji. Mungu Anakuwa mwili hasa kwa ajili ya kuikaribisha enzi mpya, na, kwa hakika, Anapoikaribisha enzi mpya, Atakuwa Ameikamilisha enzi ya kale wakati uo huo. 

Sauti ya Mungu | Sura ya 110

Kila kitu kitakapofichuliwa utakuwa wakati ambapo Nitapumzika, na hata zaidi, utakuwa wakati ambapo kila kitu kitakuwa sawa. Mimi hufanya kazi Yangu binafsi; Mimi hupanga kila kitu na kusafidi kila kitu Mwenyewe. Nitakapotoka Sayuni na Nitakaporejea, wazaliwa Wangu wa kwanza watakapokuwa wamekamilishwa na Mimi, Nitakuwa Nimemaliza kazi Yangu kubwa. Katika mawazo ya watu kitu ambacho kinafanywa ni sharti kiweze kuonekana na kuguswa, lakini jinsi Ninavyoona, kila kitu ni kikamilifu wakati ambapo Ninafanya mpango Wangu.