VI. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Kipengele cha Ukweli Kuhusu Tofauti Kati ya Kuokolewa Katika Enzi ya Neema na Wokovu katika Enzi ya Ufalme
2. Ni nini tofauti muhimu kati ya kuokolewa na wokovu?
Aya za Biblia za Kurejelea:
“Hakika nawaambieni, Yeyote ambaye hutenda dhambi ni mtumishi wa dhambi. Na mtumishi haishi katika nyumba milele: lakini Mwana huishi milele” (Yohana 8:34-35).
“Siye kila mmoja ambaye aliniambia, Bwana, Bwana, ataingia ufalme wa mbinguni, ila yeye atendaye mapenzi ya Baba yangu ambaye yuko mbinguni” (Mathayo 7:21).
“Kwa hivyo mtakuwa watakatifu, kwa sababu mimi ni mtakatifu” (Walawi 11:45).
“Na waliimba kwani ilikuwa wimbo mpya mbele ya kiti cha enzi, na mbele yao wao wanyama wanne, na wao wazee: na hakuna mwanadamu angeweza kujifunza wimbo huo ila wao elfu mia arobaini na nne, ambao walikuwa wamekombolewa kutoka duniani. Hao ndio wale hawakunajisiwa na wanawake; kwani wao ni bikira. Hao ndio wale wanaomfuata Mwanakondoo popote aendapo. Hawa walikombolewa kutoka miongoni mwa wanadamu, wakiwa matunda ya kwanza kwa Mungu na Mwanakondoo. Na vinywani mwao hakukuwa na hila: kwani hawana hatia mbele ya Kiti cha Mungu cha enzi” (Ufunuo 14:3-5).
Maneno Husika ya Mungu:
Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima.
kutoka katika Dibaji ya Neno Laonekana katika Mwili
Kupata mwili mara ya kwanza kulikuwa kumkomboa mwanadamu kutoka katika dhambi kupitia mwili wa Yesu, hivyo, Aliokoa mwanadamu kutoka kwa msalaba, lakini tabia potovu ya kishetani ilibaki ndani ya mwanadamu. Kupata mwili mara ya pili si kwa ajili ya kuhudumu tena kama sadaka ya dhambi ila ni kuwaokoa kamilifu wale waliokombolewa kutoka kwa dhambi. Hii inafanyika ili wale waliosamehewa wakombolewe kutoka kwa dhambi zao, na kufanywa safi kabisa, na kupata mabadiliko ya tabia, hivyo kujikwamua kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza na kurudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu. Hivyo tu ndivyo mwanadamu ataweza kutakaswa kikamilifu.
kutoka katika “Fumbo la Kupata Mwili (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Baadhi ya watu siku zote hufikiria: “Je, kumwamini Mungu ni kuhudhuria tu mikutano, kuimba nyimbo, kulisikiliza neno la Mungu, kuomba, kufanya baadhi ya wajibu? Je, hali haiko hivyo?” Haijalishi ni kwa muda gani mmekuwa waumini wa Mungu bado hamjaelewa kabisa umuhimu wa imani kwa Mungu. Kwa hakika, umuhimu wa imani kwa Mungu ni wa kina sana, na watu hawajaifikiria kabisa kuihusu. Mwishowe, mambo yaliyo ndani ya watu ambayo ni ya Shetani, na mambo ya asili yao lazima yabadilike, na lazima yalingane na mahitaji ya ukweli; kufanya hivi tu ndiko kuutimiza kwa kweli wokovu. Iwapo, kama ulivyofanya wakati ulikuwa ndani ya dini, unatoa tu baadhi ya maneno ya mafundisho au kupiga kelele ukitaja kaulimbiu fulani, na kisha utende vitendo fulani vizuri, uwe na tabia fulani nzuri na usitende dhambi za waziwazi, hii bado haimaanishi kwamba umeingia katika njia sahihi ya kumsadiki Mungu. Kwa sababu tu unaweza kuzitii sheria, hiyo inamaanisha kwamba unaitembelea njia sahihi? Je, inamaanisha kuwa umechagua kwa usahihi? Kama mambo ndani ya asili yako hayajabadilika na mwishowe ungali unampinga Mungu na kumkosea Mungu, basi haya ndiyo matatizo makubwa zaidi. Kama unamwamini Mungu lakini hulitatui tatizo hili, basi unaweza kuchukuliwa kuwa umeokolewa? Mimi kuyasema haya, kunamaanisha nini? Ni kuwafanya nyote kufahamu ndani ya mioyo yenu kwamba imani kwa Mungu haiwezi kutenganishwa na maneno ya Mungu, na Mungu au na ukweli. Lazima uichague njia yako vyema, utie jitihada katika ukweli na kutia jitihada ndani ya maneno ya Mungu. Usipate tu maarifa kiasi ya kijinga, au ufahamu kadiri, na kisha kujiona kuwa umemaliza. Ukiyafanya mambo kwa njia ya haraka, utajidhuru tu mwenyewe.
kutoka katika “Wale Waliopoteza Kazi ya Roho Mtakatifu Ndio Walio katika Hatari Kubwa Zaidi” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Ili kuokolewa, kuzungumza kwa lugha ya wenyeji, kunamaanisha unaweza kuendelea kuishi, na kwamba unafufuliwa na Mungu. Kwa hiyo kabla ya hayo, unaweza kuzungumza, unaweza kupumua, je, umekufa? (Roho imekufa.) Kwa nini inasemekana kwamba watu wamekufa ikiwa roho yao imekufa? Msingi wa msemo huu ni upi? Kabla ya kuokolewa, watu wanaishi chini ya ushawishi mwovu wa Shetani, na wanaishi kwa kufuata asili yao potovu ya shetani. Kwa hiyo, kutoka kwa mtazamo wa Mungu, nafsi nzima ya watu imekufa, ikiwa ni pamoja na miili yao na vipengele vingine vyote kama vile roho na mawazo yao. Kwa juu juu, unaonekana kuwa unapumua, ukipepesa macho yako, na kufikiria, lakini kila kitu unachokifikiria daima ni kiovu; unafikiria kuhusu vitu ambavyo vinamwasi Mungu na vya ukaidi dhidi ya Mungu, vitu ambavyo Mungu huchukia, hukirihi, na kushutumu. Machoni pa Mungu, mambo haya yote si ya mwili tu, bali pia ni ya Shetani na ya pepo kikamilifu. Kwa hiyo watu ni nini machoni pa Mungu? Je, wao ni wanadamu? Mungu huwaona kama pepo, kama wanyama, na kama Shetani waishio! Watu wanaishi kulingana na asili ya Shetani, na machoni pa Mungu, wao ni Shetani waishio waliovalia miili ya binadamu. Mungu huwafafanua watu kama hao kama maiti zinazotembea; kama wafu. Mungu anafanya kazi Yake ya sasa ya wokovu kuwachukua watu kama hawa—maiti hizi zinazotembea zinazoishi kwa kufuata tabia zao za kishetani na kwa kufuata viini vyao vipotovu vya kishetani—Anawachukua hawa wanaodaiwa kuwa wafu na kuwageuza kuwa walio hai. Hii ndiyo maana ya kuokolewa.
Sababu ya kumwamini Mungu ni kupata wokovu. Kuokolewa kunamaanisha kuwa unageuka kutoka kuwa mtu aliyekufa hadi kuwa mtu aliye hai. Yaani, pumzi yako inafufuliwa, na wewe unakuwa hai; unafungua macho yako na kumwona Mungu, unaweza kumtambua, na unaweza kusujudu ili umwabudu Yeye. Moyoni mwako huna upinzani zaidi dhidi ya Mungu; humkatai tena, humshambulii tena, au kumuasi tena. Watu kama hawa tu ndio walio hai kwa kweli machoni pa Mungu. Mtu akisema tu kwamba anamkubali Mungu na anaamini moyoni mwake kwamba kuna Mungu, kwamba Mungu anatawala juu ya vitu vyote na Anatawala majaliwa ya wanadamu, ikiwa anaamini kwamba watu wanaongozwa na Mungu katika maisha yao yote, kwamba Anaweza kubadilisha majaliwa ya watu na Anaweza kuwaongoza katika njia iliyo mbele, akiwa na imani ya aina hii basi ni mmoja wa walio hai au la? (La, sio.) Kwa hiyo watu waishio ni wa aina gani? Je, waishio wana uhalisi wa aina gani? Ni kwamba kila kitu unachofichua, kila kitu unachofikiria, na kila kitu unachofanya ni cha kumcha Mungu na kuepuka uovu. Ili kuliweka kwa usahihi zaidi, kila tendo na kila wazo lako hakihukumiwi na Mungu au kuchukiwa na kukataliwa na Mungu; badala yake, yanaidhinishwa na kusifiwa na Mungu. Hiki ndicho watu waishio hufanya, na pia ndicho ambacho watu waishio wanapaswa kufanya.
kutoka katika “Kuwa Mtiifu Kwa Kweli Pekee Ndiyo Imani ya Kweli” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Wale wanaoishi chini ya ushawishi wa giza, ni wale ambao wanaishi katikati ya kifo, ni wale ambao wametawaliwa na Shetani. Bila kuokolewa na Mungu, na kuhukumiwa na kuadibiwa na Mungu, watu wanakuwa hawana uwezo kukwepa athari ya kifo, hawawezi kuwa hai. Wafu hawa hawawezi kuwa ushuhuda kwa Mungu, wala hawawezi kutumiwa na Mungu, wala kuingia katika ufalme. Mungu anataka ushuhuda wa walio hai, na sio wafu, na Anaomba kwamba walio hai wafanye kazi kwa ajili Yake, na sio wafu. "Wafu" ni wale ambao wanampinga na kumwasi Mungu, ni wale ambao ni mbumbumbu katika roho na hawaelewi maneno ya Mungu, ni wale ambao hawaweki ukweli katika matendo na hawana utii hata kidogo kwa Mungu, na ni wale ambao wamemilikiwa na Shetani na kunyanyaswa na Shetani. Wafu wanajionyesha wenyewe kwa kuupinga ukweli, kwa kumwasi Mungu, na kwa kuwa duni, wa kudharaulika, kuwa waovu, katili, wadanganyifu, na kudhuru kwa siri. Ingawa watu wa namna hiyo wanakula na kunywa maneno ya Mungu, hawana uwezo wa kuishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu; wanaishi, lakini ni wafu wanaotembea, ni maiti zinazopumua. Wafu hawawezi kabisa kumridhisha Mungu, wala kumtii kikamilifu. Wanaweza tu kumdanganya, kusema maneno ya makufuru juu Yake, na kumsaliti, na yote wanayoyaishi kwa kudhihirisha hufichua asili ya Shetani. Ikiwa watu wanatamani kuwa viumbe hai, na kuwa na ushuhuda wa Mungu, na kuthibitishwa na Mungu, wanapaswa kukubali wokovu wa Mungu, wanapaswa kuwa watiifu katika hukumu na kuadibu Kwake, na wanapaswa kukubali kwa furaha kushughulikiwa na kupogolewa na Mungu. Ni hapo tu ndipo wataweza kuweka katika matendo ukweli wote unaohitajika na Mungu, na baada ya hapo ndipo wataweza kupata wokovu wa Mungu, na kuwa viumbe hai kabisa. Walio hai wanaokolewa na Mungu, wamehukumiwa na kuadibiwa na Mungu, wapo tayari kujitoa wenyewe na wana furaha kutoa maisha yao kwa Mungu, na wapo tayari kujitoa maisha yao yote kwa Mungu. Pale ambapo walio hai watachukua ushuhuda wa Mungu ndipo Shetani ataweza kuaibishwa, ni walio hai tu ndio wanaweza kueneza kazi ya injili ya Mungu, ni walio hai tu ndio wanaoupendeza moyo wa Mungu, ni walio hai tu ndio watu halisi. Mwanadamu wa asili aliyeumbwa na Mungu alikuwa hai, lakini kwa sababu ya uharibifu wa Shetani mwanadamu anaishi katikati ya kifo, na anaishi chini ya ushawishi wa Shetani, na hivyo watu hawa wamekuwa wafu ambao hawana roho, wamekuwa ni maadui ambao wanampinga Mungu, wamekuwa nyenzo ya Shetani, na wamekuwa mateka wa Shetani. Watu wote walio hai ambao wameumbwa na Mungu wamekuwa wafu, na hivyo Mungu amepoteza ushuhuda wake, na Amempoteza mwanadamu, ambaye Alimuumba na ndiye kiumbe pekee aliye na pumzi Yake. Ikiwa Mungu ataamua kurejesha ushuhuda Wake, na kuwarejesha wale ambao waliumbwa kwa mkono wake lakini ambao wamechukuliwa mateka na Shetani, basi ni lazima awafufue ili waweze kuwa viumbe hai, na ni lazima awaongoe ili kwamba waweze kuishi katika nuru Yake. Wafu ni wale ambao hawana roho, wale ambao ni mbumbumbu kupita kiasi, na wale ambao wanampinga Mungu. Aidha, ni wale ambao hawamjui Mungu. Watu hawa hawana nia hata ndogo ya kumtii Mungu, kazi yao ni kumpinga na kuasi dhidi Yake, na hawana hata chembe ya utii. Walio hai ni wale ambao roho zao zimezaliwa upya, wale wanaojua kumtii Mungu, na ambao ni watii kwa Mungu. Wanao ukweli, na ushuhuda, na ni watu wa aina hii tu ndio wanaompendeza Mungu katika nyumba Yake.
kutoka katika “Je, Umekuwa Hai Tena?” katika Neno Laonekana katika Mwili
Licha ya kile ambacho Mungu anafanya au mbinu ambazo Anatumia kufanya, licha ya gharama, au lengo Lake, kusudio la hatua Zake halibadiliki. Kusudio Lake ni kuweza kumshughulikia binadamu ili maneno ya Mungu yaingie ndani yake, mahitaji ya Mungu, na mapenzi ya Mungu kwa binadamu; kwa maneno mengine, ni kufanyia kazi huyu binadamu ili vyote ambavyo Mungu Anasadiki kuwa vizuri kulingana na hatua Zake, kumwezesha binadamu kuuelewa moyo wa Mungu na kufahamu kiini cha Mungu, na kumruhusu yeye kutii ukuu na mipangilio ya Mungu, na hivyo basi kumruhusu binadamu kuweza kufikia kiwango cha kumcha Mungu na kujiepusha na maovu—yote ambayo ni kipengele kimoja ya kusudio la Mungu katika kila kitu Anachofanya. Kipengele kingine ni kwamba, kwa sababu Shetani ndiye foili[a] na chombo cha huduma katika kazi ya Mungu, mara nyingi binadamu hukabidhiwa Shetani; hizi ndizo mbinu ambazo Mungu hutumia ili kuwaruhusu watu kuweza kuona maovu, ubaya, kudharaulika kwa Shetani katikati ya majaribio na mashambulizi ya Shetani na hivyo basi kuwasababisha watu kumchukia Shetani na kuweza kutambua kile ambacho ni kibaya. Mchakato huu unawaruhusu kwa utaratibu kuanza kuwa huru dhidi ya udhibiti wa Shetani, na dhidi ya mashtaka, uingiliaji kati, na mashambulizi ya Shetani—mpaka, kwa sababu ya maneno ya Mungu, maarifa yao na utiifu wao kwa Mungu, na imani yao kwa Mungu na kuweza kwao kumcha Mungu, wanashinda dhidi ya mashambulizi ya Shetani na kushinda dhidi ya mashtaka ya Shetani; hapo tu ndipo watakapokuwa wamekombolewa kabisa dhidi ya utawala wa Shetani. Ukombozi wa watu unamaanisha kwamba Shetani ameshindwa, unamaanisha kwamba wao si tena chakula kwenye kinywa cha Shetani—kwamba badala ya kuwameza wao, Shetani amewaachilia. Hii ni kwa sababu watu kama hao ni wanyofu, kwa sababu wanayo imani, utiifu na wanamcha Mungu, na kwa sababu wako huru kabisa dhidi ya Shetani. Wamemletea Shetani aibu, wamemfanya kuonekana mjinga, na wamemshinda kabisa Shetani. Imani yao katika kumfuata Mungu, na utiifu na kumcha Mungu kunamshinda Shetani, na kumfanya Shetani kukata tamaa kabisa na wao. Watu kama hawa ndio ambao Mungu amewapata kwa kweli, na hili ndilo lengo kuu la Mungu katika kumwokoa binadamu. Kama wangependa kuokolewa, na wangependa Mungu awapate kabisa, basi wote wanaomfuata Mungu lazima wakabiliane na majaribio na mashambulizi yakiwa makubwa na hata madogo kutoka kwa Shetani. Wale wanaoibuka katika majaribio na mashambulizi haya na wanaweza kumshinda Shetani ni wale waliookolewa na Mungu. Hivi ni kusema kwamba wale waliookolewa na Mungu ni wale ambao wamepitia majaribio ya Mungu, na ambao wamejaribiwa na kushambuliwa na Shetani mara nyingi. Wale waliookolewa na Mungu wanayaelewa mapenzi na mahitaji ya Mungu, na wanaweza kuukubali ukuu na mipangilio ya Mungu na hawaachi njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu katikati ya majaribio ya Shetani. Wale waliookolewa na Mungu wanamiliki uaminifu, wao ni wakarimu, na wanaweza kutofautisha upendo na chuki, wanayo hisia ya haki na urazini, na wanaweza kumtunza Mungu na kuthamini sana kila kitu ambacho ni cha Mungu. Watu kama hao hawatekwi bakunja, kufanyiwa upelelezi, kushtakiwa au kudhulumiwa na Shetani, wako huru kabisa, wamekombolewa na kuachiliwa kabisa.
kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” katika Neno Laonekana katika Mwili
Watu ambao wamezaliwa siku za mwisho ni watu wa aina gani? Ni wale ambao wamepitia miaka mingi ya upotovu wa Shetani, ambao wamepotoshwa kwa kina sana kiasi kwamba hawana mfanano wa binadamu tena. Lakini hatimaye, baada ya kupitia hukumu, kuadibu na kufunuliwa kwa neno la Mungu, baada ya kushindwa, wanapata ukweli kutoka ndani ya maneno ya Mungu na wanashawishiwa kwa dhati na Mungu; wanafikia uelewa wa Mungu na wanaweza kutii Mungu kikamilifu na kuyakidhi mapenzi Yake. Mwishowe, kundi la watu wanaopatwa kupitia mpango wa Mungu wa usimamizi watakuwa watu kama hawa. Watu watakaopatwa katika mpango mzima wa usimamizi ni kundi linaloweza kuelewa mapenzi ya Mungu, wanaoupata ukweli kutoka kwa Mungu, na wanaomiliki aina ya maisha na mfanano wa binadamu ambao Mungu anahitaji. … Kundi la watu ambao watapatwa mwishowe ni wale ambao watabaki mwishowe, na pia ni wale ambao Mungu anawahitaji, ambao Amefurahishwa nao na ambao wanamridhisha.
kutoka katika “Ni Kwa Kuujua Uweza wa Mungu Pekee Ndipo Unaweza Kuwa na Imani ya Kweli” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Tanbihi:
a. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni