Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kondoo-wa-Mungu-Huisikia-Sauti-ya-Mungu-Mambo-Muhimu-ya-Muumini-Mpya. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kondoo-wa-Mungu-Huisikia-Sauti-ya-Mungu-Mambo-Muhimu-ya-Muumini-Mpya. Onyesha machapisho yote

9/18/2018

Waumini katika Mungu Wanapasa Kujiandaa kwa Ajili ya Hatima Yao kwa Matendo Mema ya Kutosha

Sura ya 7 Vipengele Vingine vya Ukweli Ambavyo Unafaa Kueleweka Katika Imani Yako kwa Mungu

7. Waumini katika Mungu Wanapasa Kujiandaa kwa Ajili ya Hatima Yao kwa Matendo Mema ya Kutosha

Maneno Husika ya Mungu:
Huruma Zangu zinaonyeshwa kwa wale wanaonipenda Mimi na kujinyima wenyewe. Na adhabu inayoletwa kwa waovu ni thibitisho hasa la tabia Yangu ya haki na, zaidi sana, ushuhuda wa hasira Yangu. Msiba utakapokuja, njaa na baa litawakumba wale wote wanaopinga Mimi na watalia kwa uchungu. Wale wote ambao wametenda aina zote za uovu, lakini ambao wamenifuata kwa miaka mingi, hawataepuka kulipia dhambi zao; wao pia, wakijipata katika maafa, ambayo yameonekana kwa nadra katika mamilioni ya miaka, wataishi katika hali ya kila siku ya taharuki na woga.

9/12/2018

Maana ya Mateso na ni Mateso ya Aina Gani Ambayo Waumini wa Mungu Lazima Wastahimili

Sura ya 7 Vipengele Vingine vya Ukweli Ambavyo Unafaa Kueleweka Katika Imani Yako kwa Mungu

6. Maana ya Mateso na ni Mateso ya Aina Gani Ambayo Waumini wa Mungu Lazima Wastahimili

Maneno Husika ya Mungu:
Leo, watu wengi sana hawana ufahamu huo. Wao huamini kwamba mateso hayana thamani, wao hukanwa na ulimwengu, maisha yao ya nyumbani yamesumbuliwa, wao si wapendwa wa Mungu, na matazamio yao ni matupu. Kuteseka kwa watu wengine hufikia kiwango fulani, na fikira zao hugeukia kifo. Huu si upendo wa kweli kwa Mungu; watu kama hao ni waoga, hawana ustahamilivu, wao ni wadhaifu na wasio na nguvu!

9/10/2018

Imani Katika Mungu Haipasi Kuwa kwa ajili ya Kutafuta Amani na Baraka Pekee

Sura ya 7 Vipengele Vingine vya Ukweli Ambavyo Unafaa Kueleweka Katika Imani Yako kwa Mungu

5. Imani Katika Mungu Haipasi Kuwa kwa ajili ya Kutafuta Amani na Baraka Pekee

Maneno Husika ya Mungu:
Ni kitu gani ambacho mwanadamu amepokea tangu alipomwamini Mungu mara ya kwanza? Umejua kitu gani kumhusu Mungu? Umebadilika kiasi gani kwa sababu ya imani yako kwa Mungu? Sasa mnajua nyote ya kwamba imani ya mwanadamu katika Mungu si kwa ajili ya wokovu wa roho na ustawi wa mwili tu, wala si kuimarisha maisha yake kwa njia ya upendo wa Mungu, na kadhalika. Kama ilivyo sasa, kama unampenda Mungu kwa ajili ya ustawi wa mwili au furaha ya muda, basi hata kama, mwishoni, upendo wako kwa Mungu utafikia kilele chake na wewe hutaulizia kitu chochote, upendo huu unaoutafuta ni upendo mchafu na haumpendezi Mungu. 

9/08/2018

Adabu Takatifu Ambayo Waumini wa Mungu Wanapasa Kuwa Nayo

Sura ya 7 Vipengele Vingine vya Ukweli Ambavyo Unafaa Kueleweka Katika Imani Yako kwa Mungu

4. Adabu Takatifu Ambayo Waumini wa Mungu Wanapasa Kuwa Nayo

Maneno Husika ya Mungu:
Ni nini kinashirikishwa ndani ya ubinadamu wa kawaida? Utambuzi, hisia, dhamiri na tabia. Iwapo unaweza kufanikisha ukawaida katika kila mojawapo ya vipengele hivi, ubinadamu wako uko katika kiwango kinachostahili. Unapaswa kuwa na mfanano wa binadamu wa kawaida na utende kama anayemwamini Mungu. Sio lazima ufikie viwango vya juu zaidi au kujishughulisha na diplomasia. Unapaswa tu kuwa mwanadamu wa kawaida, na hisia za kawaida za mtu, uweze kung’amua vitu, na kwa kiwango cha chini uonekane kama mwanadamu wa kawaida.

9/05/2018

Katika Kutafuta Njia ya Kweli, Lazima Uwe na Mantiki

Sura ya 7 Vipengele Vingine vya Ukweli Ambavyo Unafaa Kueleweka Katika Imani Yako kwa Mungu

2. Katika Kutafuta Njia ya Kweli, Lazima Uwe na Mantiki

Maneno Husika ya Mungu:
Mungu na mwanadamu hawawezi kuzungumziwa kama wa kulingana. Dutu ya Mungu na kazi Yake ni vitu visivyoeleweka na kufahamika kwa mwanadamu. Ikiwa Mungu hawezi kufanya kazi Yake binafsi na kuzungumza maneno Yake katika ulimwengu wa mwanadamu, basi mwanadamu hangeweza kuelewa mapenzi ya Mungu, na kwa hivyo, hata wale waliotoa maisha yao yote kwa ajili ya Mungu hawataweza kupata idhini ya Mungu. Bila kazi ya Mungu, haijalishi jinsi gani mwanadamu anatenda mema, haitahesabika kama chochote, kwa maana fikira za Mungu daima zitakuwa juu ya fikira za mwanadamu, na hekima ya Mungu haieleweki kwa mwanadamu.

9/04/2018

Katika Kumwamini Mungu, Unapaswa Kuweka Uhusiano wa Kawaida na Mungu

Sura ya 7 Vipengele Vingine vya Ukweli Ambavyo Unafaa Kueleweka Katika Imani Yako kwa Mungu

3. Katika Kumwamini Mungu, Unapaswa Kuweka Uhusiano wa Kawaida na Mungu

Maneno Husika ya Mungu:
Katika kuwa na imani kwa Mungu, ni lazima angalau utatue swala la kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu. Bila uhusiano wa kawaida na Mungu, basi umuhimu wa kumwamini Mungu unapotea. Kuunda uhusiano wa kawaida na Mungu kunapatikana kikamilifu kupitia kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu. Uhusiano wa kawaida na Mungu unamaanisha kuweza kutoshuku au kukataa kazi yoyote ya Mungu na kutii, na zaidi ya hayo unamaanisha kuwa na nia sahihi mbele ya Mungu, sio kufikiria kujihusu, daima kuwa na maslahi ya familia ya Mungu kama jambo muhimu zaidi haijalishi kile unachofanya, kukubali kutazamiwa na Mungu, na kukubali mipangilio ya Mungu.

9/02/2018

Kujua Chanzo cha Upinzani wa Watu kwa Kazi Mpya ya Mungu katika Imani Yao kwa Mungu

Sura ya 7 Vipengele Vingine vya Ukweli Ambavyo Unafaa Kueleweka Katika Imani Yako kwa Mungu

1. Kujua Chanzo cha Upinzani wa Watu kwa Kazi Mpya ya Mungu katika Imani Yao kwa Mungu

Maneno Husika ya Mungu:

Sababu kwamba mwanadamu humpinga Mungu inatoka, kwa upande mmoja, katika tabia potovu ya mwanadamu, na kwa upande mwingine, kutokana na kutomfahamu Mungu na kutoelewa kanuni za kazi ya Mungu na mapenzi Yake kwa mwanadamu. Vipengele hivi viwili vinaunganishwa katika historia ya upinzani wa mwanadamu kwa Mungu. Wanafunzi katika imani wanampinga Mungu kwa sababu upinzani kama huu uko ndani ya asili yao, ilhali upinzani dhidi ya Mungu wa wale walio na miaka mingi katika imani unatokana na kutomfahamu Mungu, kuongeza kwa tabia yao potovu.

8/29/2018

Tofauti Kati Ya Matendo Mazuri ya Nje na Mabadiliko Katika Tabia

Sura ya 6 Aina Mbalimbali za Utofautishaji Ambazo Unafaa Kumiliki katika Kusadiki Kwako kwa Mungu

7. Tofauti Kati Ya Matendo Mazuri ya Nje na Mabadiliko Katika Tabia

Maneno Husika ya Mungu:
Mabadiliko katika tabia hasa huhusu mabadiliko katika asili ya watu. Mambo ya asili ya mtu hayawezi kuonekana kutoka kwa mienendo ya nje; yanahusisha moja kwa moja thamani na umuhimu wa kuwepo kwake. Yaani, yanahusisha moja kwa moja mitazamo ya mtu kuhusu maisha na maadili yake, mambo yaliyo ndani kabisa ya nafsi yake, na kiini chake. Mtu ambaye hawezi kukubali ukweli hatakuwa na mabadiliko katika hali hizi. Ni kwa kupitia kazi ya Mungu pekee, kuingia kikamilifu katika ukweli, kubadili maadili na mitazamo yake kuhusu kuwepo na maisha, kulinganisha msoni yake na ya Mungu, na kuwa na uwezo wa kutii na kujitoa kabisa kwa Mungu ndio tabia zake zinaweza kusemekana zimebadilika. 

8/28/2018

Utofautishaji Kati ya Viongozi wa Kweli na wa Uongo, na Kati ya Wachungaji wa Kweli na wa Uongo

Sura ya 6 Aina Mbalimbali za Utofautishaji Ambazo Unafaa Kumiliki katika Kusadiki Kwako kwa Mungu

6. Utofautishaji Kati ya Viongozi wa Kweli na wa Uongo, na Kati ya Wachungaji wa Kweli na wa Uongo

Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya mtenda kazi mwenye sifa inaweza kuwaleta watu katika njia sahihi na kuwaruhusu kuzama kwa kina katika ukweli. Kazi anayofanya inaweza kuwaleta watu mbele ya Mungu. Aidha, kazi anayofanya inaweza kutofautiana kutoka kwa mtu hadi mtu mwingine na wala haifungwi na kanuni, inawapa watu uhuru. Aidha, wanaweza kukua katika uzima kwa taratibu, wakiendelea kukua na kuzama ndani kabisa katika ukweli. Kazi ya mtenda kazi asiyehitimu haifikii kiwango hiki; kazi yake ni ya kipumbavu. Anaweza kuwaleta watu katika kanuni tu; kile anachowataka watu kufanya hakitofautiani kati ya mtu na mtu mwingine; hafanyi kazi kulingana na mahitaji halisi ya watu.

8/24/2018

Tofauti Kati Ya Kumfuata Mungu na Kuwafuata Watu

Sura ya 6 Aina Mbalimbali za Utofautishaji Ambazo Unafaa Kumiliki katika Kusadiki Kwako kwa Mungu

5. Tofauti Kati Ya Kumfuata Mungu na Kuwafuata Watu

Maneno Husika ya Mungu:
Kilicho na umuhimu mkuu katika kumfuata Mungu ni kwamba kila kitu kinapaswa kuwa kwa kadri ya maneno ya Mungu leo: Kama unafuatilia kuingia katika uzima au kutimiza mapenzi ya Mungu, kila kitu kinapaswa kulenga maneno ya Mungu leo. Kama kile ambacho unawasiliana kwa karibu na kufuatilia hakilengi maneno ya Mungu leo, basi wewe ni mgeni kwa maneno ya Mungu, na umeondolewa kabisa katika kazi ya Roho Mtakatifu. Kile ambacho Mungu hutaka ni watu ambao huzifuata nyayo Zake. 

8/18/2018

Unawezaje Kutambua Tofauti Kati ya Njia za Kweli na za Uongo, na Makanisa ya Kweli na ya Uongo?

Sura ya 6 Aina Mbalimbali za Utofautishaji Ambazo Unafaa Kumiliki katika Kusadiki Kwako kwa Mungu

4. Utofautishaji Kati ya Njia za Kweli na za Uongo, na Kati ya Makanisa ya Kweli na ya Uongo

Maneno Husika ya Mungu:
Kanuni ya msingi kabisa katika kuutafuta ukweli ni nini? Unapaswa kuangalia kama kuna kazi ya Roho Mtakatifu au la kwa njia hii, iwapo maneno haya ni maonyesho ya ukweli, yanamshuhudia nani, na ni kitu gani yanaweza kukupatia. Kutofautisha kati ya njia ya kweli na hizi njia za uongo kunahitaji njia kadhaa za maarifa ya msingi, ya msingi kabisa kati ya zote ni kusema iwapo kuna Kazi ya Roho Mtakatifu au la. Maana kiini cha imani ya mwanadamu katika Mungu ni imani katika Roho Mtakatifu. Hata imani yake katika Mungu mwenye mwili ni kwa sababu mwili huu ni mfano halisi wa Roho wa Mungu, ikiwa na maana kwamba imani hiyo bado ni imani katika Roho.

8/16/2018

Unawezaje Kutambua Tofauti Kati ya Kristo wa Kweli na Makristo wa Uongo?

Sura ya 6 Aina Mbalimbali za Utofautishaji Ambazo Unafaa Kumiliki katika Kusadiki Kwako kwa Mungu

3. Utofautishaji Kati ya Kristo wa Kweli na Makristo wa Uongo

Maneno Husika ya Mungu:
Mungu aliyepata mwili Anaitwa Kristo, na hivyo Kristo ambaye Anaweza kuwapa binadamu ukweli anaitwa Mungu. Hakuna kitu kikuu kuliko hiki, kwa kuwa Anayo hali ya Mungu, na ana tabia za Mungu, na hekima katika kazi Yake, ambayo haiwezi kupatikana kwa binadamu. Wale wanaojiita Kristo, walakini hawawezi kufanya kazi ya Mungu, ni matapeli. Kristo wa kweli sio tu udhihirisho wa Mungu duniani, bali pia, mwili hasa ulioigwa na Mungu kufanya na kutimiza kazi Yake kati ya wanadamu. Mwili huu si ule unaoweza kubadilishwa na mtu yeyote tu, lakini ambao unaweza kutosha kufanya kazi ya Mungu duniani, na kueleza tabia ya Mungu, na pia kumwakilisha Mungu, na kumpa binadamu maisha.

8/13/2018

Unafaa Utofautishe Vipi Kati ya Kazi ya Roho Mtakatifu na Kazi ya Pepo Wabaya?

Sura ya 6 Aina Mbalimbali za Utofautishaji Ambazo Unafaa Kumiliki katika Kusadiki Kwako kwa Mungu

2. Utofautishaji Kati ya Kazi ya Roho Mtakatifu na Ile ya Pepo Wabaya

Maneno Husika ya Mungu:
Mungu harudii kazi Yake, Hafanyi kazi ambayo si halisi, Hamtaki mwanadamu afanye mambo zaidi ya uwezo wake, na Hafanyi kazi ambayo inazidi akili ya mwanadamu. Kazi yote Anayofanya ipo ndani ya mawanda ya akili ya kawaida ya mwanadamu, na haizidi ufahamu wa ubinadamu wa kawaida, na kazi Yake ni kulingana na mahitaji ya kawaida ya mwanadamu. Ikiwa ni kazi ya Roho Mtakatifu, mwanadamu anakuwa wa kawaida zaidi, na ubinadamu wake unakuwa wa kawaida kabisa.

8/12/2018

Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili

Sura ya 5 Ukweli Kuhusu Mungu Kupata Mwili

5. Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili

Maneno Husika ya Mungu:
Kupata mwili mara ya kwanza kulikuwa kumkomboa mwanadamu kutoka katika dhambi kupitia mwili wa Yesu, hivyo, Aliokoa mwanadamu kutoka kwa msalaba, lakini tabia potovu ya kishetani ilibaki ndani ya mwanadamu. Kupata mwili mara ya pili si kwa ajili ya kuhudumu tena kama sadaka ya dhambi ila ni kuwaokoa kamilifu wale waliokombolewa kutoka kwa dhambi. Hii inafanyika ili wale waliosamehewa wakombolewe kutoka kwa dhambi zao, na kufanywa safi kabisa, na kupata mabadiliko ya tabia, hivyo kujikwamua kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza na kurudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu. Hivyo tu ndivyo mwanadamu ataweza kutakaswa kikamilifu. Mungu Alianza kazi ya wokovu katika Enzi ya Neema baada ya Enzi ya Sheria kufika mwisho.

8/11/2018

Unafaa Kutofautisha Vipi Kati ya Kazi ya Mungu na ya Mwanadamu?

Sura ya 6 Aina Mbalimbali za Utofautishaji Ambazo Unafaa Kumiliki katika Kusadiki Kwako kwa Mungu

1. Utofautishaji Kati ya Kazi ya Mungu na Ile ya Mwanadamu

Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya Mungu Mwenyewe inahusisha kazi ya wanadamu wote, na pia inawakilisha kazi ya enzi nzima. Hii ni kusema kwamba, kazi ya Mungu mwenyewe inawakilisha harakati na mwelekeo wa kazi yote ya Roho Mtakatifu, ilhali kazi ya mitume inafuata kazi ya Mungu na wala haiongozi enzi, na wala haiwakilishi mwelekeo wa kufanya kazi wa Roho Mtakatifu katika enzi nzima. Huwa wanafanya tu kazi ambayo mwanadamu anapaswa kufanya, ambayo haihusishi kabisa kazi ya usimamizi. Kazi ya Mungu ni mradi ndani ya kazi ya usimamizi. Kazi ya mwanadamu ni wajibu tu wa wanadamu kuweza kutumika na wala haina uhusiano na kazi ya usimamizi.

8/07/2018

Sura ya 5 Ukweli Kuhusu Mungu Kupata Mwili

Sura ya 5 Ukweli Kuhusu Mungu Kupata Mwili

4. Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

Maneno Husika ya Mungu:
Wokovu wa Mungu kwa mwanadamu haufanywi moja kwa moja kupitia njia ya Roho ama kama Roho, kwani Roho Wake hawezi kuguzwa ama kuonekana na mwanadamu, na hawezi kukaribiwa na mwanadamu. Kama Angejaribu kumwokoa mwanadamu moja kwa moja kwa njia ya Roho, mwanadamu hangeweza kupokea wokovu Wake. Na kama sio Mungu kuvalia umbo la nje la mwanadamu aliyeumbwa, mwanadamu hawangeweza kupokea wokovu huu. Kwani mwanadamu hawezi kumkaribia kwa njia yoyote ile, zaidi kama jinsi hakuna anayeweza kukaribia wingu la Yehova.

8/05/2018

Tofauti Kati ya Kazi ya Mungu Mwenye Mwili na Kazi ya Roho

Sura ya 5 Ukweli Kuhusu Mungu Kupata Mwili

3. Tofauti Kati ya Kazi ya Mungu Mwenye Mwili na Kazi ya Roho

Maneno Husika ya Mungu:
Wokovu wa Mungu kwa mwanadamu haufanywi moja kwa moja kupitia njia ya Roho ama kama Roho, kwani Roho Wake hawezi kuguzwa ama kuonekana na mwanadamu, na hawezi kukaribiwa na mwanadamu. Kama Angejaribu kumwokoa mwanadamu moja kwa moja kwa njia ya Roho, mwanadamu hangeweza kupokea wokovu Wake. Na kama sio Mungu kuvalia umbo la nje la mwanadamu aliyeumbwa, mwanadamu hawangeweza kupokea wokovu huu. Kwani mwanadamu hawezi kumkaribia kwa njia yoyote ile, zaidi kama jinsi hakuna anayeweza kukaribia wingu la Yehova.

8/03/2018

Umuhimu wa Mungu Kupata Mwili

Sura ya 5 Ukweli Kuhusu Mungu Kupata Mwili

2. Umuhimu wa Mungu Kupata Mwili

Maneno Husika ya Mungu:
Mwili huu ni muhimu sana kwa mwanadamu kwa sababu ni mwanadamu hata zaidi ni Mungu, kwa sababu Anaweza kufanya kazi ambayo hakuna mwanadamu wa kawaida anayeweza kufanya, na kwa sababu Anaweza kumwokoa mwanadamu aliyepotoka, ambaye anaishi pamoja na Yeye duniani. Ingawa Anafanana na mwanadamu, Mungu mwenye mwili ni wa muhimu sana kwa mwanadamu kuliko mtu yeyote wa thamani, kwa maana Anaweza kufanya kazi ambayo haiwezi kufanywa na Roho wa Mungu, ni mwenye uwezo zaidi kuliko Roho wa Mungu kuwa na ushuhuda kwa Mungu Mwenyewe, na ni mwenye uwezo zaidi kuliko Roho wa Mungu kuweza kumpata mwanadamu kabisa. 

7/31/2018

Unahitaji Kusadiki Vipi Mungu Ili Kuweza Kuokolewa na Kufanywa Kuwa Mtimilifu?

Sura ya 4 Ukweli wa Kazi ya Mungu ya Siku za Mwisho

5. Unahitaji Kusadiki Vipi Mungu Ili Kuweza Kuokolewa na Kufanywa Kuwa Mtimilifu?

Maneno Husika ya Mungu:
Kufanya muhtasari wa kuishika njia ya Petro katika kumwamini Mungu, ni kuishika njia ya kufuatilia ukweli, ambayo pia ni njia ya kujijua na kubadilisha tabia ya mtu. Ni kwa kuishika tu njia ya Petro ndio mtu atakuwa anashika njia ya kukamilishwa na Mungu. Mtu lazima aelewe hasa jinsi ya kuishika njia ya Petro na jinsi ya kuiweka katika vitendo. Kwanza, mtu lazima aweke kando madhumuni yake mwenyewe, shughuli zisizofaa, na hata familia yake na vitu vyote vya mwili wake. Lazima ajitolee kwa moyo wote, yaani, ajitolee kabisa kwa neno la Mungu, azingatie kula na kunywa neno la Mungu, azingatie kutafuta ukweli, utafutaji wa nia ya Mungu katika maneno Yake, na ajaribu kufahamu mapenzi ya Mungu katika kila kitu.

7/28/2018

Mungu Kupata Mwili Ni Nini? Kiini cha Mungu Kupata Mwili Ni Nini?

Sura ya 5 Ukweli Kuhusu Mungu Kupata Mwili

1. Mungu Kupata Mwili Ni Nini? Kiini cha Mungu Kupata Mwili Ni Nini?

Maneno Husika ya Mungu:
Maana ya kupata mwili ni kwamba Mungu Anajionyesha katika mwili, na Anakuja kufanya kazi miongoni mwa wanadamu wa uumbaji Wake katika umbo la mwili. Hivyo, ili Mungu kuwa mwili, ni lazima kwanza Apate umbo la mwili, mwili wenye ubinadamu wa kawaida; hili ndilo hitaji la kimsingi zaidi. Kwa kweli, maana ya kupata mwili kwa Mungu ni kwamba Mungu Anaishi na kufanya kazi katika mwili, Mungu katika kiini Chake Anakuwa mwili, Anakuwa mwanadamu. Maisha Yake ya kimwili na kazi vinaweza kugawanywa katika hatua mbili. Kwanza ni maisha Anayoishi kabla ya kuanza kutekeleza huduma Yake.