Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kutofautisha-Vipi. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kutofautisha-Vipi. Onyesha machapisho yote

8/13/2018

Unafaa Utofautishe Vipi Kati ya Kazi ya Roho Mtakatifu na Kazi ya Pepo Wabaya?

Sura ya 6 Aina Mbalimbali za Utofautishaji Ambazo Unafaa Kumiliki katika Kusadiki Kwako kwa Mungu

2. Utofautishaji Kati ya Kazi ya Roho Mtakatifu na Ile ya Pepo Wabaya

Maneno Husika ya Mungu:
Mungu harudii kazi Yake, Hafanyi kazi ambayo si halisi, Hamtaki mwanadamu afanye mambo zaidi ya uwezo wake, na Hafanyi kazi ambayo inazidi akili ya mwanadamu. Kazi yote Anayofanya ipo ndani ya mawanda ya akili ya kawaida ya mwanadamu, na haizidi ufahamu wa ubinadamu wa kawaida, na kazi Yake ni kulingana na mahitaji ya kawaida ya mwanadamu. Ikiwa ni kazi ya Roho Mtakatifu, mwanadamu anakuwa wa kawaida zaidi, na ubinadamu wake unakuwa wa kawaida kabisa.

8/11/2018

Unafaa Kutofautisha Vipi Kati ya Kazi ya Mungu na ya Mwanadamu?

Sura ya 6 Aina Mbalimbali za Utofautishaji Ambazo Unafaa Kumiliki katika Kusadiki Kwako kwa Mungu

1. Utofautishaji Kati ya Kazi ya Mungu na Ile ya Mwanadamu

Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya Mungu Mwenyewe inahusisha kazi ya wanadamu wote, na pia inawakilisha kazi ya enzi nzima. Hii ni kusema kwamba, kazi ya Mungu mwenyewe inawakilisha harakati na mwelekeo wa kazi yote ya Roho Mtakatifu, ilhali kazi ya mitume inafuata kazi ya Mungu na wala haiongozi enzi, na wala haiwakilishi mwelekeo wa kufanya kazi wa Roho Mtakatifu katika enzi nzima. Huwa wanafanya tu kazi ambayo mwanadamu anapaswa kufanya, ambayo haihusishi kabisa kazi ya usimamizi. Kazi ya Mungu ni mradi ndani ya kazi ya usimamizi. Kazi ya mwanadamu ni wajibu tu wa wanadamu kuweza kutumika na wala haina uhusiano na kazi ya usimamizi.