Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo ushuhuda-wa-injili. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo ushuhuda-wa-injili. Onyesha machapisho yote

8/27/2019

Mama wa "Vijijini" Akutana na Binti Mkwe wa "Mjini"

Liu Jie, Hunan
Mama wa "Vijijini" Akutana na Binti Mkwe wa "Mjini"
Maoni Tofauti, Migongano Ya Siku Zote
Mimi ni mke wa kawaida, mke mzuri na mama mwenye upendo, mimi huwatunza vizuri mume wangu na watoto wangu, mimi hufanya kazi kwa bidii na mwekevu katika kuendesha nyumba yangu, na sijawahi kamwe kutumia fedha zangu bila hadhari. Lakini kitu kisichofikirika kilinifika. Mwanangu alimuoa msichana wa kisasa ambaye kwa kweli alipenda kujifurahisha na kuvaa na kufuata mitindo ya ulimwengu. Alifuatilia na kununua chochote kilichopendwa ulimwenguni, alipoteza pesa nyingi mno, na kiasi cha pesa alichopata kila mwezi ndicho kiasi alichotumia.

8/23/2019

Maisha ya Kikristo: Huenda Nisiwe Tajiri, lakini Nina Bahati Sana

Maisha ya Kikristo: Huenda Nisiwe Tajiri, lakini Nina Bahati Sana

Na Bong, Philippines
Nataka Kuwa Tajiri
“Mwalimu mkuu, tafadhali mpe mwanangu fursa na kumruhusu afanye mtihani!” Macho ya mama yangu yalimsihi mwalimu mkuu alipokuwa akizungumza kwa sauti ya kutetemeka kidogo.
Bila kuonyesha hisia, mwalimu mkuu akasema, “Hapana, shule ina kanuni. Mtoto anaweza kufanya mtihani tu wakati ada ya mtihani imelipwa!”

7/31/2019

Ni Nini Maana ya Krismasi, na Je, Unamwabudu Bwana Yesu Kweli?

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Ushuhuda

Na Siyuan
Vyanzo vya Krismasi
     Kila mwaka, Krismasi inapokaribia, maduka kwenye mitaa hutayarisha maonyesho yang’aayo ya zawadi za Krismasi, pamoja na Baba Krismasi na miti ya Krismasi, na kadhalika. Kuna taa nyingi za rangi nyingi zilizoning’inizwa katika miti na kwenye majengo, na miji mizima hupambwa kwa fanusi na mapazia ya rangi nyingi, na kila mahali kuna furaha na msisimko. Kwa Ukristo, Krismasi ni likizo ya pekee sana, na miezi kadhaa kabla ya Krismasi, makanisa mengi yataanza kujishughulisha na kuandaa kila kitu kilicho muhimu kwa likizo ya Krismasi.

7/30/2019

Baada ya Usaliti wa Mumewe Mungu Alimuokoa Kutoka kwenye Fadhaa ya Uchungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Maombi

     Baada ya miongo miwili ya mema na mabaya ambayo yeye na mumewe walipitia pamoja, hakuwahi kamwe kufikiria kwamba mumewe angekuwa na uhusiano wa nje ya ndoa. Alishindwa kabisa kuvumilia wakati alipogundua hilo. Licha ya kujaribu kila kitu ili kumfanya mumewe ampende tena, yote ilikuwa kazi bure. Katikati ya maumivu yake na kutokuwa na tumaini, ni maneno ya Mungu yaliyomwokoa, yakimsaidia kupata kiini cha maumivu yake, kuelewa maana ya maisha, na hatua kwa hatua kutoka kwenye fadhaa ya mateso yake.

2/26/2019

Ushuhuda wa Mkristo: Jinsi Alivyoshinda Majaribu ya Kuwa na Mpenzi wa Siri (Sehemu ya 2)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Wakristo
 
Na Xiyue, Mkoa wa Henan
Katika siku chache zilizofuata, ingawa Jingru hakuwa ameanguka katika majaribu ya Shetani na alijua kwamba hangeweza kuwa mwenzi wa Wang Wei kamwe, mkutano wake na Wang Wei jioni hiyo na ungamo lake la kweli vilirudiwa akilini mwake tena na tena kama onyesho katika filamu …
Wang Wei alipompigia simu tena, moyo wa Jingru ulishtuka kidogo, naye akajiambia: “Sote wawili hatuwezi kuwa kitu kimoja, lakini bado tunaweza kuwa marafiki wa kawaida.

2/24/2019

Ushuhuda wa Mkristo: Jinsi Alivyoshinda Majaribu ya Kuwa na Mpenzi wa Siri (Sehemu ya 1)

 
Na Xiyue, Mkoa wa Henan
Jioni moja, Jingru alikuwa akinadhifisha kwake.
“Krr, krr.” Simu ilianza kulia. Aliijibu na sauti ngeni lakini bado inayojulikana ililia sikioni mwake: “Halo! Ni Wang Wei. Uko nyumbani!”
“Wang Wei?” Jingru kwa namna fulani alistaajabu: Kwa nini alikuwa akimpigia simu sasa baada ya miaka mingi sana?
“Ndiyo … niko nyumbani. Kuna nini?” aliuliza Jingru kwa mshangao.

2/16/2019

Swahili Christian Video "Macho Kila Mahali" | The Means the CCP Uses to Capture Christians🎬👍

Filamu za Injili "Macho Kila Mahali" (Mazungumzo Chekeshi) | The Means the CCP Uses to Capture Christians


           Mchezo wa kuchekesha Macho Kila Mahali unaeleza jinsi Chama cha Kikomunisti cha China kinavyojaribu kuondoa dini kwa kutumia uchunguzi mkubwa kote nchini, pamoja na kuwageuza watu katika kila tabaka na kazi ya maisha kuwa macho ili kuchunguza, kusimamia, na kupeleleza Wakristo.

1/17/2019

Maneno ya Mungu Huniongoza Kujifunza Jinsi ya Kuwafundisha Wanangu (I)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Ushuhuda
Nina wana wawili wa kiume na wameachana na mwaka mmoja. Ili kuwalea kuwa watu waliostaarabika, wenye tabia nzuri, watu wema ambao wataweza watajijengea jina katika jamii na kufanikiwa, walipokuwa na umri wa miaka miwili, nilijadiliana na mume wangu juu ya kuwatafutia shule nzuri ya chekechea. Baada ya ziara kadhaa, maulizo na kulinganisha, tulichagua shule ya chekechea ya Kiingereza kwa sababu waliweka umuhimu juu ya ubora wa tabia au akili na uwezo wa watoto, ambao ulifanana na mtazamo wangu juu ya kufundisha watoto.

12/16/2018

Maneno ya Mungu Huniongoza Kujifunza Jinsi ya Kufundisha Watoto Wangu (II)


Maneno ya Mungu Huniongoza Kujifunza Jinsi ya Kufundisha Watoto Wangu (II)

Xiaoxue, Malesia
Siku moja baada ya mlo mkuu wa siku, nilimfundisha mwanangu mvulana mkubwa jinsi ya kusoma Kichina—maneno rahisi tu, “Mbinguni, dunia, watu, na, dunia, baba, mama….” Nilimfundisha mara chache hasa, lakini bado hakuweza kuandika. Angeandika neno la kwanza na kisha kusahau lililofuata. Hasira ndani yangu ilipanda, na kunyakua rula iliyokuwa juu ya meza na kumgonga mara kadhaa. Nilimpigia kelele kwa sauti kubwa: “Wewe ni mpumbavu jinsi gani! Huwezi hata kujifunza maneno haya machache!”

12/01/2018

Ushuhuda wa Injili | Kwaheri kwa Zile Siku za Kushindana na Majaliwa

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Ushuhuda
Kijiji cha kishamba kilichojikokota kimaendeleo, wazazi wangu waliochoka kwa sababu ya kazi zao, maisha ya shida za kifedha … kumbukumbu hizi za huzuni zilitia alama kwa mawazo yangu machanga, zilikuwa ni hisia yangu ya kwanza ya “majaliwa.” Baada ya kuanza kwenda shule, mara ya kwanza nilipomsikia mwalimu wangu akisema kwamba “Unadhibiti majaliwa yako katika mikono yako mwenyewe,” niliweka maneno haya imara mawazoni mwangu. Niliamini kuwa ingawa sikuweza kubadili ukweli kwamba nilizaliwa katika umaskini, ningeweza bado kubadili majaliwa yangu kwa kufanya kazi kwa bidii.