Na Xiyue, Mkoa wa Henan
Katika siku chache zilizofuata, ingawa Jingru hakuwa ameanguka katika majaribu ya Shetani na alijua kwamba hangeweza kuwa mwenzi wa Wang Wei kamwe, mkutano wake na Wang Wei jioni hiyo na ungamo lake la kweli vilirudiwa akilini mwake tena na tena kama onyesho katika filamu …
Wang Wei alipompigia simu tena, moyo wa Jingru ulishtuka kidogo, naye akajiambia: “Sote wawili hatuwezi kuwa kitu kimoja, lakini bado tunaweza kuwa marafiki wa kawaida.
Mradi nijizuie ili nisifanye chochote kinachoenda mbali mno, basi itakuwa sawa.” Kisha akajibu simu kutoka kwa Wang Wei na kuzungumza naye. Siku zilipopita, Jingru aliwaza daima kuhusu kama Wang Wei angepiga simu au la, kiasi kwamba moyo wa Jingru ulianza kutarajia tukio hilo. Kila wakati alipopiga simu, Jingru angejifariji kabla ya kujibu simu kikawaida sana.… Mambo yalipoendelea, miito ya simu kati ya Wang Wei na Jingru ikawa ya mara nyingi zaidi. Lakini baada ya kila wito, Jingru angehisi wasiwasi na kuumia, na alitambua kwamba vitendo vyake havikufuata mapenzi ya Mungu, na kwamba hisia zake za maumivu na wasiwasi zilikuwa hasa Mungu akimkumbusha na kumkaripia. Kisha akaenda mara moja mbele ya Mungu na kuomba: “Ewe Mungu! Najua sipaswi kuwasiliana na Wang Wei, lakini siwezi kudhibiti moyo wangu mwenyewe. Siwezi kujizuia kujiacha na kuteleza kuelekea dhambini. Ee Mungu! Sitaki matendo yangu katika jambo hili yakukasirishe. Ee Mungu! Tafadhali niokoe!”
Baadaye, Jingru aliona vifungu kadhaa vya maneno, na alipata njia ya kujiweka huru kutoka kwenye maumivu. Maneno ya Mungu yanasema: “Nyinyi nyote mnaishi mahala pa dhambi na ufisadi; nyinyi nyote ni watu wapotovu na wenye dhambi. Leo hii hamwezi tu kumwona Mungu, ila la muhimu zaidi, mmepokea kuadibu na hukumu, mmepokea wokovu wa kina, yaani, mmepokea upendo mkubwa zaidi wa Mungu. … Kwa kuwa hamjui jinsi ya kuishi, na mnaishi katika mahala pa ufisadi na dhambi na ni mapepo wenye ufisadi na uchafu, Hana moyo wa kuwaacha mpotoshwe zaidi; wala Hana moyo wa kutaka kuwaona mkiishi mahala pachafu kama hapa, mkikandamizwa na Shetani apendavyo, Hana moyo wa kuwaacha mtumbukie Kuzimu. Anataka tu kulipata hili kundi lenu na kuwakomboa vilivyo” (“Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (4)”). Inasema katika Mahubiri na Ushirika: “Kwa sasa, unaelewa jinsi watu wote ambao wamenaswa na tamaa hatimaye huishia, sawa? Ni nini matokeo ya mwisho kwa watu wengi kati ya hawa? Wao hukabiliwa na laana? Kuna matokeo mazuri? Huwa hawapati amani maisha yao yote! Haya ndiyo machafuko na shida ambazo husababishwa na tamaa; ni mateso yasiyovumilika! Kwa watu wote ambao hutafuta mwenzi wa ndoa kwa kutojali au kwa njia isiyo ya kawaida, kuna wowote ambao wana matokeo ya furaha? Hakuna matokeo mazuri ya mwisho, na wao hatimaye hukumbana na laana. Hicho si kitu cha kuchezewa” (“Ni Mtu wa Aina Gani Atakamilishwa na Mungu” katika Mahubiri na Ushirika Juu ya Kuingia Katika Maisha (VII)). “Fikiria wakati unapomwona mtu wa jinsia tofauti nawe na una mawazo ya uzinifu, wewe hushughulikiaje tatizo hili? Angalau sana ni lazima kwanza uheshimu ndoa. Kama mtu ana mume (au mke), basi unahitaji kuiheshimu ndoa ya mtu huyu. Huwezi kuichezea ndoa ya mtu fulani; kuwaheshimu wengine ni kujiheshimu, kama huwaheshimu wengine basi hujiheshimu. Kama unawaheshimu wengine, basi wengine watakuheshimu. Kama moyoni mwako huiheshimu ndoa basi huna ubinadamu. Kama unaweza kuiheshimu ndoa, kama unaweza kuwapenda wengine na kuwaheshimu wengine, basi hutafanya mambo ambayo huwadhuru wengine. Kama unaweza kumkataa mtu hata anapojitupa mikononi mwako, basi unashughulikia mambo vizuri. Ni lazima ujiandaeje ili uweze kuyakataa majaribu haya na ushawishi? Ni lazima ujiandae na ukweli, halafu utaweza kuona mambo haya kwa dhahiri. Baada ya kuweza kuona kwa dhahiri kiini cha suala hili, basi utajua ni aina gani ya madhara ambayo vitendo vya upande wako vitawaletea wengine, utajua ni aina gani ya majeraha wengine hupitia ndani ya mioyo yao, utajua ni kwa kiwango gani umevunja nafsi ya mtu, na mara unapoyaelewa mambo haya hutatenda tena kwa njia zinazoyasababisha; wakati wowote aina hizi za mawazo na fikira zinapokuja akilini mwako utaweza kuzikataa, hutakuwa na haja nazo, hutazizingatia, kwa sababu hazitaugeuza moyo wako” (“Kulenga Kutatua Matatizo Matatu Ambayo Kwa Sasa Yameenea Kanisani” katika Mahubiri na Ushirika Juu ya Kuingia Katika Maisha (VI)).
Alipoyazingatia kwa makini maneno ya Mungu na maneno ya ushirika, Jingru alijua kwamba alikuwa ameangukia ndani ya mzunguko wa hisia usioweza kuepukika kwa sababu hakuwa ameubaini mpango wa hila wa Shetani au kiini, uharibifu, na matokeo ya kuichezea tamaa. Ni alipokuwa akitafakari juu ya hili tu alipojua kwamba ni Shetani ambaye alikuwa akimfundisha mawazo ya “Upendo ni mkuu,” “Wapenzi hatimaye huoana,” “Usiulize milele, furahishwa na sasa,” na “Upendo sio dhambi” yakimfanya awaze juu ya mapenzi mazuri na hivyo kutozuiliwa na maadili au dhamiri yake, yakimfanya daima awaze juu ya Wang Wei, daima akiwasiliana naye, kuwa amesongamana naye, na kuishi katika dhambi na kutamani raha ya dhambi huku akikosa kuamini kuwa hilo ni kosa. Jingru aliwafikiria watu wengi walio karibu naye ambao walijihusisha na uhusiano nje ya ndoa, na juu ya wanaume wengi ambao walikuwa na mahawara. Ingawa waliridhisha tamaa zao za muda mfupi, waliishia kusababisha ugomvi wa familia na kuvunjika kwa ndoa, na hata kulikuwa na watu wengine ambao waliuawa kwa sababu ya kuzongwa katika mapenzi ya wawili kwa mmoja. Sasa, tapo la mtandaoni la “hata mimi” lilikuwa limelipuka kwenye maeneo ya vyuo vikuu na katika maeneo ya ustawi wa umma na habari za umma, na kwenye vyombo vya habari, na kulikuwa na watu wengi maarufu na wasomi ambao walikuwa wamepatikana wakiwa na ushirikiano wa ngono wa usiku mmoja, ambao walikuwa wameaibishwa kabisa na ambao majina yao yalikuwa yamekuwa mithali ya uzinzi. Hasa wafanyakazi wa serikali ya China wana wake na mahawara, na wengi wao wamekuwa wakitumiwa kwa njia isiyo sawa na kuliwa njama na maadui wao wa kisiasa kwa kujihusisha na uhusiano nje ya ndoa, na kusababisha wao kufungwa gerezani kama wakosaji. Jingru aliona wazi kwamba watu walijihusisha na uhusiano nje ya ndoa ili kuziridhisha tamaa zao, na kwamba lilikuwa ni jambo hasi, ovu ambalo lingewakwamisha tu watu matopeni katika bwawa la dhambi. Kama vile tu ambavyo wachezaji kamari hutaka kucheza tena wanapopoteza, na ambao mwishowe huziangamiza familia zao kifedha na kufanya wanafamilia wao watawanyike kotekote, wale ambao hucheza na tamaa hucheza mara moja na kisha wao hutaka kucheza tena, wanalifanya mara moja na kisha wanataka kulifanya tena, na kadiri wanavyocheza ndivyo wanavyokuwa watupu zaidi, hadi hatimaye wanaingia katika uasherati na dhambi na hawawezi kutoka tena. Hatimaye, wanaharibu miili yao wenyewe na kujisababishia matatizo yasiyo na mwisho katika siku zijazo, na hata kuna baadhi ya watu wanaopoteza utashi wa kuishi, na kuchagua kuyakatiza maisha yao wenyewe. Hivyo ilionekana kwa Jingru kwamba kucheza na tamaa halikuwa jambo jema kufanya; lilikuwa ni jambo lenye dhambi ambalo lingeleta tu adhabu na ghadhabu ya mbinguni kwa wale waliojihusisha nalo, na hilo lingeweza tu kuwaongoza watu kwenye njia ya maangamizo. Jingru kisha akaelewa kwamba falsafa na mantiki ya Shetani na mantiki vyote vilikuwa uongo mdanganyifu, uongo ambao uliwadanganya watu, na zana ambazo Shetani aliwapotoshea watu, na kwamba hapakuwa na upendo wa kweli kati ya watu waliohusika na uhusiano wa nje ya ndoa. Ikiwa mtu angekuwa na upendo wa kweli, basi angekuwa na ubinadamu, angemheshimu yule mtu mwingine na kuiheshimu taasisi ya ndoa, na hangefanya chochote ambacho kingemdhuru mtu mwingine. Watu ambao walihusika na uhusiano nje ya ndoa kwa kweli walikuwa wakicheza na tamaa za wao kwa wao na kutumiana. Alipofikia utambuzi huu, Jingru basi alikwenda mbele ya Mungu na kuomba: “Ee Mungu! Sasa ninatambua matokeo mabaya ya kuishi kwa sumu ya Shetani. Sitaki kuishi katika tamaa ya kimwili nikizitegemea hizi sumu za Shetani tena. Kuendelea kuwasiliana na Wang Wei ni kuishi maisha yasiyo na uadilifu au heshima, sembuse napenda kufanya chochote ambacho kinaweza kuleta aibu kwa jina Lako au kunifanya nipoteze ushuhuda wa Mkristo. Ninaomba kuwa Unipe moyo wa kumwogopa Mungu, nifanye niweze kustahimili na kanuni za ukweli na kuunyima mwili wangu, kuwa mtu mwenye hekima anayeepuka hatari akiiona, na kuwa mtu anayeishi kwa kudhihirisha mfano wa binadamu wa kweli kwa utukufu wa Mungu.”
Siku moja, alipokuwa akielekea kanisani, Jingru alikutana na Wang Wei. Alikuwa akiendesha gari barabarani na akamwita, na Jingru alitaka sana kuitikia, lakini mara moja alifikiria maneno ya Mungu na sala aliyokuwa ameinena mbele ya Mungu. Alijua kuwa hangeweza kwendelea kwa njia hiyo, hivyo akamtazama tu Wang Wei akiwa ameketi katika gari lake, na kutosema kitu. Aliendelea na safari yake, akiendesha skuta yake ya umeme, na Wang Wei akaanza kumfuata nyuma, akipiga honi yake. Katika moyo wake, Jingru alisali kwa Mungu kimya kimya na kumwomba Amuweke ili aweze kuubaini mpango wa hila wa Shetani na kuwa shahidi kama Mkristo. Baada ya kuomba, moyo wa Jingru ulitulizwa, na hakumpa Wang Wei jibu. Aliendelea kujaribu kufikiria jinsi ambavyo angeweza kumuepuka. Ilitokea tu kwamba baadaye walifika kwenye njiapanda, na alipoona gari la Wang Wei likipiga kona, mara moja akageukia mwelekeo kinyume na akatoka kwa kasi …
Jingru alimwona Wang Wei barabarani mara nyingi baadaye, na daima alimtendea kwa njia hii kila wakati, na Mungu alimfungulia suluhisho: Ama Wang Wei angekutana na watu wengi aliowajua, au ingekuwa ni msongamano wa magari, na hivyo hakupata kamwe fursa ya kuwa karibu na Jingru. Ili asiweze kuwa na mawasiliano mengine na Wang Wei, Jingru alibadilisha nambari ya simu yake ya mkononi, na siku zlipoendelea, wawili hao hawakutangamana tena.
Akikumbuka uzoefu huu, Jingru kwa kweli alikuja kufurahia jambo hili: Sasa, katika ulimwengu huu uliojaa majaribu mengi, tutakutana na kila aina za majaribu na ushawishi kutoka kwa Shetani kila siku, na kwa sababu hatuna ukweli na hatuwezi kutofautisha mambo haya, na kwa sababu sisi huishi kwa sumu ya Shetani, hatutaweza kujizuia kufuata mienendo miovu, tutakwamishwa katika dhambi ambazo tunashindwa kuziepa, na tutadanganywa na kudhuriwa na Shetani. Kama tunataka kuyabaini majaribu mbalimbali na mipango ya hila ya Shetani, basi kuna njia moja pekee, ambayo ni kuja mbele ya Mungu, kujihami zaidi na maneno ya Mungu, kuuelewa ukweli zaidi, kujifunza jinsi ya kuelezea tofauti kati ya mambo chanya na mambo hasi, kuzielewa kabisa hila zote za ujanja za Shetani, kuyategemeza matarajio yetu kwenye maneno ya Mungu tunapokutana na watu wote, mambo na vitu, kutenda kulingana na maneno ya Mungu, na kutenda kwa kanuni, na ni hapo tu tutakapoepuka kuingia katika majaribu ya Shetani. Kama tu maneno ya Mungu yanavyosema: “Ukweli ambao mtu anahitaji kumiliki unapatikana katika neno la Mungu, ukweli ambao ni faida zaidi na manufaa kwa mtu. Ni lishe na riziki ambayo miili yenu inahitaji, kitu ambacho huwasaidia kurejesha ubinadamu wenu wa kawaida, ukweli ambao mnapaswa kujiandaa nao. Zaidi mnavyotenda neno la Mungu, kwa haraka ndivyo zaidi maisha yenu yatachanua; zaidi mnavyotenda neno la Mungu, ndio wazi ukweli unakuwa. Mnavyokua katika kimo, mtaona mambo ya ulimwengu wa kiroho wazi zaidi, na mtakuwa na nguvu zaidi ya ushindi juu ya Shetani” (“Tendeni Ukweli Mara Mnapouelewa”).
Jingru akashusha pumzi kwa hisia, na kuwaza: “Isingekuwa kwa ajili ya Mungu kuniokoa na kunilinda kupitia maneno Yake, ningekuwa nimeharibika zamani sana na kuwa mtu bila mfano wa binadamu, na ningekuwa nimefanya mambo bila uadilifu au heshima, kama wale watu ambao wana uhusiano nje ya ndoa, ambao huwa wapenzi wa watu waliooa, na ambao huwa yule mwanamke mwingine. Pia ningetwishwa mzigo na jina baya la mvunja familia, na ningeishi maisha yaliyoshushwa hadhi, nikipitia shutuma ya dhamiri yangu mwenyewe.” Kwa dhati, Jingru alitoa shukrani na sifa kwa Mungu! Leo, maisha yake yamepata tena utulivu wake wa awali, kwa furaha yeye hutekeleza wajibu wake kanisani, hukubali hukumu na utakaso wa maneno ya Mungu, na anapiga hatua kwelekea kwenye maisha ya furaha ya kweli. Utukufu wote uwe kwa Mungu!
kutoka katika Ushuhuda wa Injili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni