|
Umeme wa Mashariki | Kujadili Maisha ya Kanisa na Maisha Halisi |
Mwenyezi Mungu alisema, Watu huhisi kuwa wao wanaweza tu kubadilika katika maisha yao ya kanisani, na kuwa iwapo hawaishi ndani ya
kanisa, mbadiliko hauwezekani, kuwa hawawezi kutimiza mbadiliko katika maisha yao halisi. Mwaweza kutambua suala hili ni lipi? Nimeongea juu ya kumleta
Mungu katika maisha halisi, na hii ndiyo njia kwa wale wanaomwamini Mungu kuingia katika uhalisi wa maneno ya Mungu. Kwa kweli, maisha ya kanisa ni njia ndogo tu ya kuwakamilisha watu. Mazingira ya msingi ya kuwakamilisha wanadamu bado ni maisha halisi. Hiki ndicho kitendo halisi na mafunzo halisi Niliyozungumzia, yanayowaruhusu wanadamu kutimiza maisha ya ubinadamu wa kawaida na kuishi kwa kudhihirisha mfano wa mtu wa kweli katika maisha ya kila siku. Kipengele kimoja ni kwamba mtu lazima aelimike ili kuinua kiwango chake mwenyewe cha elimu, aweze kuelewa maneno ya Mungu, na kutimiza uwezo wa kuelewa.