sifu Mungu,Kurudi kwa Yesu mara ya pili |
Je, Wajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu
Mwenyezi Mungu alisema, Enzi ya zama ishaenda, na enzi mpya imefika. Mwaka baada ya mwaka na siku baada ya siku, Mungu amefanya kazi nyingi. Alikuja duniani, kisha Akaondoka. Mzunguko kama huu umeendelea kwa vizazi vingi. Siku ya leo, Mungu anaendelea kama mbeleni kufanya kazi Anayopaswa kufanya, kazi ambayo bado Hajaikamilisha, kwani hadi leo, bado Hajaingia mapumzikoni. Kutoka wakati wa uumbaji hadi leo, Mungu amefanya kazi nyingi, lakini ulijua kwamba kazi anayoifanya Mungu leo ni nyingi kuliko awali na kipimo ni kikubwa zaidi? Hii ndiyo maana Nasema Mungu amefanya jambo kubwa miongoni mwa wanadamu. Kazi zote za Mungu ni muhimu sana, iwe kwa mwanadamu ama Mungu, kwani kila kitu cha kazi Yake kina uhusiano na mwanadamu.
Sababu kazi ya Mungu haiwezi kuonekana wala kuguswa, sembuse kuonwa na ulimwengu, basi jinsi gani ikawa kitu kikubwa? Ni jambo la aina gani linachukuliwa kuwa kubwa? Hakika hakuna anayeweza kukataa kuwa kazi zote za Mungu zinaweza kuchukuliwa kuwa kubwa, lakini mbona Nasema kazi anayofanya Mungu leo iko hivi? Ninaposema kwamba Mungu amefanya kitu kikubwa, hii bila shaka inahusisha siri nyingi ambazo mwanadamu bado hajazielewa. Wacha tuzizungumzie sasa.
Sababu kazi ya Mungu haiwezi kuonekana wala kuguswa, sembuse kuonwa na ulimwengu, basi jinsi gani ikawa kitu kikubwa? Ni jambo la aina gani linachukuliwa kuwa kubwa? Hakika hakuna anayeweza kukataa kuwa kazi zote za Mungu zinaweza kuchukuliwa kuwa kubwa, lakini mbona Nasema kazi anayofanya Mungu leo iko hivi? Ninaposema kwamba Mungu amefanya kitu kikubwa, hii bila shaka inahusisha siri nyingi ambazo mwanadamu bado hajazielewa. Wacha tuzizungumzie sasa.
Yesu alizaliwa horini wakati ambao hungevumilia kuwepo Kwake, lakini dunia bado haingemzuia, na Aliishi miongoni mwa wanadamu kwa miaka thelathini na tatu chini ya ulinzi wa Mungu. Kwa miaka hiyo yote ya maisha, Alikuwa na uzoefu wa uchungu wa dunia na Akaonja maisha ya taabu duniani. Alilichukua jukumu zito la kusulubiwa ili kuwakomboa wanadamu wote. Aliwakomboa wote wenye dhambi walioishi chini ya miliki ya Shetani, na mwishowe, mwili Wake uliofufuka ukarudi mahali Pake pa mapumziko. Sasa kazi mpya ya Mungu imeanza, na pia ni mwanzo wa enzi mpya. Mungu analeta nyumbani Kwake wale waliokombolewa kuanza kazi Yake ya wokovu. Wakati huu, kazi ya wokovu ni ya kina kuliko nyakati za nyuma. Haitafanywa na Roho Mtakatifu akifanya kazi ndani ya mwanadamu ili kumruhusu kubadilika mwenyewe, wala haitafanywa kupitia mwili wa Yesu akijitokeza miongoni mwa wanadamu, na sembuse haitafanywa kwa namna ingine. Badala yake, kazi itafanywa na kuongozwa na Mungu mwenye mwili Mwenyewe. Hii inafanywa ili kumwongoza binadamu katika kazi mpya. Hili si jambo zuri? Mungu hafanyi kazi hii kupitia sehemu ya wanadamu ama kupitia unabii, lakini kwa Mungu Mwenyewe. Wengine wanaweza kusema kuwa hili si jambo kubwa na kwamba haliwezi kumletea mwanadamu furaha mno. Hata hivyo, Nitakuambia kwamba kazi ya Mungu siyo tu hii, ila kitu kikubwa zaidi na kingi zaidi.
Wakati huu, Mungu haji kufanya kazi kwa mwili wa kiroho ila kwa ule wa kawaida sana. Sio tu mwili wa kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili, lakini pia mwili ambao Mungu anarudia. Ni mwili wa kawaida sana. Ndani Yake, huwezi kuona chochote kilicho tofauti na cha wengine, lakini unaweza kupokea kutoka Kwake ukweli ambao hujawahi kusikia mbeleni. Mwili huu usio na umuhimu ni mfano halisi wa maneno yote ya kweli kutoka kwa Mungu, ambao hufanya kazi ya Mungu siku za mwisho, na maonyesho ya tabia nzima ya Mungu kwa mwanadamu kuja kujua. Je, hukutamani sana kumwona Mungu aliye mbinguni? Je, hukutamani sana kumwelewa Mungu aliye mbinguni? Je, hukutamani sana kuona hatima ya mwanadamu? Atakueleza hizi siri zote ambazo hakuna mwanadamu ameweza kukuambia, na hata Atakuelezea kuhusu ukweli usioelewa. Yeye ndiye lango la kuingia katika ufalme, na mwongozo wako katika enzi mpya. Mwili wa kawaida kama huu una siri nyingi zisizoeleweka. Matendo Yake labda hayaeleweki kwako, lakini lengo la kazi yote Anayoifanya limekutosha kuona kuwa Yeye si mwili wa kawaida anavyoamini mwanadamu. Kwani Anawakilisha mapenzi ya Mungu na pia utunzaji anaoonyesha Mungu kwa mwanadamu siku za mwisho. Ingawa huwezi kuyasikia maneno Anayozungumza yanayoonekana kutingisha mbingu na dunia wala kuona macho Yake kama moto mkali, na ingawa huwezi kuhisi nidhamu ya fimbo Yake ya chuma, unaweza kusikia kupitia maneno Yake ghadhabu ya Mungu na kujua kwamba Mungu Anaonyesha huruma kwa mwanadamu; unaweza kuona tabia ya haki ya Mungu na hekima Yake, na zaidi ya hayo, kutambua wasiwasi na utunzaji anao Mungu kwa wanadamu wote, Kazi ya Mungu ya siku za mwisho ni kuruhusu mwanadamu kumwona Mungu aliye mbinguni Akiishi miongoni mwa wanadamu duniani, na kumwezesha mwanadamu kuja kumjua, kumtii, kumheshimu, na kumpenda Mungu. Hii ndiyo maana Amerudi kwa mwili kwa mara ya pili. Ingawa kile anachokiona mwanadamu siku hii ni Mungu aliye sawa na mwanadamu, Mungu aliye na pua na macho mawili, na Mungu asiye wa ajabu, mwishowe, Mungu atawaonyesha kwamba bila kuwepo kwa huyu mwanadamu, mbingu na dunia zitapitia mabadiliko makuu; bila kuwepo kwa huyu mwanadamu, mbingu itapungukiwa na mwangaza, dunia itakuwa vurugu, na wanadamu wote wataishi katika njaa na mabaa. Atawaonyesha kuwa bila wokovu wa Mungu mwenye mwili katika siku za mwisho, basi Mungu Angekuwa Ashawaangamiza wanadamu wote kuzimu kitambo sana; bila kuwepo kwa mwili huu, basi daima mngekuwa viongozi wa wenye dhambi na maiti milele. Mnapaswa kujua kwamba bila kuwepo kwa mwili huu, wanadamu wote wangetazamia msiba usioepukika na kupata kuwa ngumu kuponyoka adhabu kali zaidi ya Mungu katika siku za mwisho. Bila kuzaliwa kwa mwili huu wa kawaida, nyinyi nyote mngekuwa katika hali ambayo uhai wala kifo havitakuja bila kujali jinsi mtakavyovitafuta; bila kuwepo kwa mwili huu, basi siku hii hamngeweza kupokea ukweli na kuja mbele ya kiti cha Mungu cha enzi. Badala yake, mngeadhibiwa na Mungu kwa sababu ya dhambi zenu zinazohuzunisha. Je, mnajua? Kama sio kwa kurudi kwa Mungu kwa mwili, hakuna ambaye angepata nafasi ya wokovu; na isipokuwa kwa kuja kwa mwili huu, Mungu angekuwa ameimaliza kitambo enzi ya zamani. Hivyo basi, mnaweza bado kuukataa kupata mwili kwa mara ya pili kwa Mungu? Sababu mnaweza kufaidika sana kutoka kwa huyu mwanadamu wa kawaida, basi mbona hammkubali kwa urahisi?
Kazi ya Mungu ni ile usiyoweza kuelewa. Kama huwezi kufahamu kama uamuzi wako ni sahihi wala kujua kama kazi ya Mungu inaweza kufaulu, basi mbona usijaribu bahati yako na kuona iwapo huyu mwanadamu wa kawaida ni wa msaada mkubwa kwako, na iwapo Mungu amefanya kazi kubwa. Hata hivyo, lazima Nikuelezee kuwa wakati wa Nuhu, wanadamu walikuwa wamekula na kunywa, wakifunga ndoa na kupeana katika ndoa hadi kiwango ambacho Mungu asingevumilia kushuhudia, hivyo, Alituma chini mafuriko makubwa kuangamiza wanadamu na kuacha tu nyuma familia ya Nuhu ya watu wanane na aina yote ya ndege na wanyama. Katika siku za mwisho, hata hivyo, wale waliohifadhiwa na Mungu ni wale wote ambao wamekuwa waaminifu Kwake hadi mwisho. Ingawa nyakati zote mbili zilikuwa za upotovu mkubwa Asizoweza kuvumilia kushuhudia Mungu, na mwanadamu katika enzi zote mbili alikuwa mpotovu kiasi cha kumkana Mungu kama Bwana, watu wote katika wakati wa Nuhu waliangamizwa na Mungu. Mwanadamu katika enzi zote mbili amemhuzunisha Mungu sana, lakini Mungu bado Amebakia mvumilivu na wanadamu katika siku za mwisho hadi sasa. Mbona hivi? Hamjawahi kufikiria haya? Kama kweli hamjui, basi wacha Niwaelezee. Sababu Mungu anaweza kushughulika na wanadamu kwa neema siku za mwisho si kwamba ni wapotovu kidogo zaidi kuliko wanadamu katika wakati wa Nuhu ama kwamba wamemwonyesha Mungu toba, sembuse si kwamba Mungu hawezi kuvumilia kuwaangamiza wanadamu katika siku za mwisho ambapo teknolojia imeendelea. Badala yake, ni kwamba Mungu ana kazi ya kufanya kwa kundi la wanadamu katika siku za mwisho na hii itafanywa na Mungu mwenye mwili Mwenyewe. Zaidi ya hayo, Mungu atachagua sehemu ya kundi hili kama vyombo Vyake vya wokovu, tunda la mpango Wake wa usimamizi, na kuleta wanadamu kama hawa naye katika enzi ifuatayo. Kwa hivyo, bila kujali, hii gharama iliyolipwa na Mungu yote imekuwa katika maandalizi ya kazi ya kupata mwili Kwake katika siku za mwisho. Yote mliyonayo siku hii ni kwa sababu ya huu mwili. Ni kwa sababu Mungu huishi ndani ya mwili ndiyo mna nafasi ya kuishi. Hii bahati yote nzuri imepatwa kwa sababu ya huyu mwanadamu wa kawaida. Siyo haya tu, lakini mwishowe kila taifa litamwabudu huyu mwanadamu wa kawaida, na pia kumpa shukrani na kumtii huyu mwanadamu asiye muhimu. Kwa sababu ni Yeye aliyeleta ukweli, uhai, na njia ya kuwaokoa wanadamu wote, kutuliza migogoro kati ya Mungu na mwanadamu, kuleta Mungu na mwanadamu pamoja karibu zaidi na kuwasilisha mawazo kati ya Mungu na mwanadamu. Pia ni Yeye ambaye Ameleta hata utukufu zaidi kwa Mungu. Mwanadamu wa kawaida kama huyu hastahili uaminifu na ibada yako? Mwili wa kawaida kama huu haufai kuitwa Kristo? Mwanadamu wa kawaida kama huyu hawezi kuwa maonyesho ya Mungu miongoni mwa wanadamu? Mwanadamu kama huyu anayesaidia wanadamu kuepuka maafa hastahili mapenzi yenu na nyinyi kumshikilia? Mkiukataa ukweli unaotamkwa kutoka mdomo Wake na pia kuchukia kuwepo Kwake miongoni mwenu, basi nini itakuwa majaliwa yenu?
Kazi yote ya Mungu katika siku za mwisho inafanywa kupitia huyu mwanadamu wa kawaida. Atakupa kila kitu, na juu ya hayo, Anaweza kuamua kila kitu kukuhusu. Mtu kama huyu anaweza kuwa mnavyoamini: mtu wa kawaida sana kiasi cha kutostahili kutajwa? Ukweli Wake hujatosha kuwashawishi kabisa? Ushuhuda wa vitendo Vyake hujatosha kuwashawishi kabisa? Ama ni kuwa njia Anayowaongozea haistahili nyinyi kuifuata? Ni nini kinachowasababisha kumchukia na kumtupilia mbali na kumwepuka? Ni Yeye anayeonyesha ukweli, ni Yeye anayetoa ukweli, na ni Yeye anayewawezesha kuwa na njia ya kusafiri. Inaweza kuwa kwamba bado hamwezi pata chembe cha kazi ya Mungu ndani ya ukweli huu? Bila kazi ya Yesu, mwanadamu hangeweza kushuka chini kutoka msalabani, lakini bila kupata mwili siku hii, wale wanaoshuka chini kutoka msalabani hawangewahi kusifiwa na Mungu ama kuingia katika enzi mpya. Bila kuja kwa huyu mwanadamu wa kawaida, basi hamngeweza kuwa na hii fursa ama kustahiki kuona uso wa ukweli wa Mungu, kwani nyinyi nyote ni wale ambao wangepaswa kuangamizwa kitambo sana. Kwa sababu ya kuja kwa Mungu mwenye mwili kwa mara ya pili, Mungu amewasamehe na kuwaonyesha huruma. Bila kujali, maneno ambayo lazima Niwaachie mwishowe ni haya: Huyu mwanadamu wa kawaida, ambaye ni Mungu mwenye mwili, ni wa umuhimu sana kwenu. Hili ndilo jambo kubwa ambalo Mungu tayari Amefanya miongoni mwa wanadamu.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Kujua zaidi: Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni