10/31/2018

Christian Video Swahili "Uaminifu ni wa Thamani Mno" | Wokovu wa Bwana


Christian Video Swahili "Uaminifu ni wa Thamani Mno" | Wokovu wa Bwana

Zhen Cheng alikuwa mmiliki wa duka la urekebishaji wa vifaa vya stima. Alikuwa mkarimu, mwaminifu, na alifanya biashara inavyopasa kufanywa. Hangejaribu kumdanganya mtu, lakini alikuwa anachuma tu pesa za kutosha angalau kuimudu tu famillia yake. Baada ya muda, mmoja wa jamaa yake na mfanya biashara mwenza alimhimiza atende kulingana na sheria zisizoandikwa za biashara, na Zhen Cheng alianza kuamini katika misemo inayowakilisha falsafa ya kama vile: "Mwanaume bila kipato cha pili hawezi kamwe kuwa tajiri kama tu jinsi farasi aliyenyimwa nyasi kavu usiku hawezi kamwe kuongeza uzani,” “Wajasiri hufa kwa ajili ya tamaa; waoga hufa kwa njaa," "Pesa si kila kitu, lakini bila pesa, huwezi kufanya chochote," na "Pesa kwanza."

10/30/2018

New Swahili Christian Video "Kufufuka" | Hukumu ya Mungu katika Siku za Mwisho Iliniokoa


Jina lake ni Zheng Lu, na tangu utotoni, alikuwa hasa ovyo. Kwa sababu ya ushawishi wa kijamii na elimu ya utamaduni wa kidesturi wa Kichina, alisoma bila kuchoka, akitumai kufikia chuo kikuu na kufanikisha ndoto yake ya kuwapiku marika wake na kuwa na mafanikio, lakini ajali isiyotarajiwa ilimharibia ndoto yake. Wakati tu alipohisi vibaya, mnyonge, na asiyeweza kuupata mwelekeo maishani, wokovu wa Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho ulimpata.

10/29/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Mia Moja na Tano

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Mia Moja na Tano 

Kwa sababu ya kanuni za maneno Yangu, kwa sababu ya utaratibu wa kazi Yangu, watu hunikana; hili ndilo kusudi Langu la kuzungumza kwa muda mrefu (imezungumzwa kuhusu wazao wote wa joka kubwa jekundu). Ni njia ya hekima ya kazi Yangu; ni hukumu Yangu ya joka kubwa jekundu; huu ni mkakati Wangu, hakuna mtu hata mmoja anayeweza kuuelewa kikamilifu.

10/28/2018

Swahili Christian Movie "Kutamani Sana" (1) - Hivyo Hivi Ndivyo Bwana Anavyorudi

Waumini wengi ndani ya Bwana wameusoma unabii ufuatao wa kibiblia: "Wao watamwona yule Mwana wa Adamu akifika kwa mawingu ya mbinguni akiwa na nguvu na utukufu mkubwa" (Mathayo 24:30). Wanasadiki kwamba wakati Bwana atakaporudi, ni yakini kwamba Atashuka akiwa juu ya wingu, lakini kuna unabii mwingine katika Biblia unaosema: "Tazama, mimi nakuja kama mwizi" (Ufunuo 16:15). "Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi;

10/27/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Hamsini

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Hamsini

Mwenyezi Mungu alisema, Makanisa yote na watakatifu wote wanapaswa kutafakari kuhusu siku zilizopita na kutumainia siku za usoni: Ni mangapi kati ya matendo yenu ya zamani ndiyo yanayostahili, na ni mangapi kati yao yalishiriki katika ujenzi wa ufalme? Usiwe mtu mwenye kujifanya kujua kila kitu! Unapaswa kuona wazi dosari zako na unafaa kuelewa hali zako mwenyewe.

10/26/2018

Maonyesho ya Mungu | "Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu" | Only Those Who Know God Can Be Perfected



      Mwenyezi Mungu anasema, “Katika kipindi kile alichomfuata Yesu, Petro alitazama na kutia moyoni kila kitu kuhusu maisha Yake: Matendo Yake, maneno Yake, mwendo Wake na maonyesho Yake. Alipata ufahamu wa kina kwamba Yesu hakuwa kama binadamu wa kawaida. Ingawa mwonekano Wake wa binadamu ulikuwa wa kawaida kabisa, Alijaa upendo, huruma, na ustahimilivu kwa binadamu. Kila kitu alichokifanya au kusema kilikuwa chenye msaada mkubwa kwa wengine, na akiwa kando Yake, Petro aliona na kujifunza mambo ambayo hakuwahi kuyaona wala kuyasikia awali. ... 

10/25/2018

Katika Enzi ya Ufalme, Neno Linatimiza Kila Kitu

I
Katika Enzi ya Ufalme, Mungu anaikaribisha enzi mpya na neno.
Anabadilisha mbinu ya kazi Yake, anafanya kazi ya enzi nzima na neno.
Hii ni kanuni ambayo Mungu anafanya kazi nayo katika Enzi ya Neno.
Alikuwa mwili ili kunena kutoka sehemu tofauti,
hivyo mwanadamu kweli anamwona Mungu, Neno likionekana katika mwili,
anaona ajabu Yake, na anaona hekima Yake.

10/24/2018

Swahili Christian Sketch "Onyo Kutoka kwa Historia" (Kichekesho)


Miaka elfu mbili iliyopita, wakati Bwana Yesu alipotokea na kufanya kazi, Mafarisayo walikwamia sheria na kukashifu kazi Yake, wakisema kuwa kazi Yake ilienda zaidi ya Maandiko.Ili kulinda hali zao na maisha yao, walijitahidi kwa nguvu zao zote ili kuwazuia watu kutafuta kazi ya Bwana Yesu, na kujiunga na serikali ya Kirumi kumsulubisha msalabani.

10/23/2018

Kujijua kwa Hakika kwa Kuuelewa Ukweli Tu

Wenwen Mji wa Changchun, Mkoa wa Jilin
Kwa maoni yangu, daima nililidhani kwamba mradi matendo ya nje yalionekana ya kufaa ambapo watu hawangeweza kuona upotovu wowote, basi lilichukuliwa kuwa mabadiliko. Kwa hiyo, nilizingatia kwa namna ya kipekee matendo ya nje katika kila kitu nilichokifanya. Nilijali tu kuhusu kama matendo yangu yalikuwa sahihi au la, na mradi tabia zangu za nje na matendo yalikuwa ya maana, nilikuwa sawa.

10/22/2018

Neno la Mungu | "Kumwamini Mungu Lazima Kulenge Uhalisi, Si Tamaduni za Kidini" | Can Your Faith Gain the Praise of God?


Mwenyezi Mungu alivyosema, "Je, ni desturi ngapi za kidini unazozizingatia? Ni mara ngapi wewe umeasi dhidi ya neno la Mungu na kwenda kwa njia yako mwenyewe? Ni mara ngapi wewe umetia katika vitendo neno la Mungu kwa sababu wewe kwa kweli unajali mizigo Aliyobeba na unatafuta kutimiza mapenzi Yake? Lielewe neno la Mungu na uliweke katika vitendo. Kuwa mwenye maadili katika vitendo na matendo yako;

10/21/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Thelathini na Sita

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Thelathini na Sita

Mwenyezi Mungu wa kweli, Mfalme katika kiti cha enzi, hutawala ulimwengu mzima, Anakabiliana na mataifa yote na watu wote, kila kitu chini ya mbingu hung’aa kwa utukufu wa Mungu. Viumbe vyote hai katika miisho ya ulimwengu vitaona. Milima, mito, maziwa, ardhi, bahari na viumbe vyote viishivyo, katika nuru ya uso wa Mungu wa kweli wamefungua mapazia yao, kuhuishwa, kama kuamka kutoka kwa ndoto, kuchipuka kwa kuvunja uchafu!

10/20/2018

Swahili Christian Movie "Ujinga Angamizi" | Why Can’t Foolish Virgins Enter the Kingdom of Heaven?


Zheng Mu'en ni mfanyakazi mwenza katika kanisa la Kikristo nchini Marekani, amemwamini Bwana kwa miaka mingi, na anafanya kazi kwa bidii na humtumia Bwana. Siku moja, shangazi yake anashuhudia kwake kwamba Bwana Yesu amerudi kuonyesha ukweli na kufanya kazi ya kumhukumu na kumtakasa mtu katika siku za mwisho, habari ambazo zinampendeza sana. Baada ya kusoma neno la Mwenyezi Mungu na kutazama filamu na video za Kanisa la Mwenyezi Mungu, moyo wa Zheng Mu'en unathibitisha kuwa maneno ya Mwenyezi Mungu ni ukweli, na kwamba Mwenyezi Mungu huenda akawa ndiye kurudi kwa Bwana Yesu, hivyo anaanza kuchunguza kazi ya Mungu katika siku za mwisho pamoja na ndugu zake.

10/19/2018

Ufafanuzi wa Matamko ya Ishirini na Nne na Ishirini na Tano

Mwenyezi Mungu alisema, Bila kusoma kwa makini, haiwezekani kugundua kitu chochote katika matamko ya siku hizi mbili; kwa kweli, yangepaswa kunenwa kwa siku moja, lakini Mungu aliyagawanya kwa siku mbili. Hiyo ni kusema, matamko ya siku hizi mbili yanaunda moja kamili, lakini ili iwe rahisi kwa watu kuyakubali, Mungu aliyagawanya kwa siku mbili ili kuwapa watu nafasi ya kupumua.

10/18/2018

Maonyesho ya Mungu | "Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo ni Mungu Mwenyewe"


Maonyesho ya Mungu | "Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo ni Mungu Mwenyewe"

Mwenyezi Mungu alivyosema, "Kuonekana kwa Mungu katika mwili kunamaanisha kuwa kazi yote na maneno ya Roho wa Mungu yanafanywa katika ubinadamu wake wa kawaida, na kupitia mwili Wake uliopatikana. Kwa maneno mengine, Roho wa Mungu huelekeza kazi Yake ya ubinadamu na hutekeleza kazi Yake ya uungu katika mwili, na katika Mungu kupata mwili unaweza kuona kazi ya Mungu katika ubinadamu na kazi kamili ya uungu; huu ndio umuhimu hasa wa kuonekana kwa Mungu wa vitendo katika mwili.

10/17/2018

Nyimbo za Kanisa | Umuhumi wa Maombi

Nyimbo za Kanisa | Umuhumi wa Maombi

I
Maombi ni njia moja ya mwanadamu kishirikiana na Mungu,
kuita Roho Wake na kuguswa na Mungu.
Kadiri unavyoomba zaidi, ndivyo utakavyoguswa zaidi, kutiwa nuru na kuwa na mawazo ya nguvu zaidi.
Watu kama hao wanaweza kufanywa kamili hivi karibuni.
Kadiri unavyoomba zaidi, ndivyo utakavyoguswa zaidi, kutiwa nuru na kuwa na mawazo ya nguvu zaidi.

10/16/2018

Ushahidi | Mapambano ya Kufa na Kupona

Chang Moyang Mjini Zhengzhou, Mkoani Henan
"Unapoutelekeza mwili, bila shaka kutakuwa na mapambano ndani. Shetani anataka ufuate dhana za mwili, kulinda maslahi ya mwili. Hata hivyo, neno la Mungu bado linakupa nuru na kukuangaza ndani, linakupa msukumo kwa ndani na kufanya kazi kutoka ndani. Katika hatua hii, ni juu yako kama unamfuata Mungu, au Shetani.

10/15/2018

Kuwa Mtu Mpya na Uuliwaze Moyo wa Mungu

I
Umeona ndani ya moyo wangu, kiburi kilichoje ndani yangu.
Nafikiri kuwa mimi ni mzuri sana na kila kitu ni duni kwangu.
Mkuu na mwenye majivuno, asili yangu ni ngumu kutupa.
Zaidi ya kudharau, mimi ni mdogo. Binadamu wamepotea. Oo, binadamu wamepotea.
Maneno Yako yanauyeyusha moyo wangu. Mbele Yako nimekuja.

10/14/2018

Filamu za Kikristo 2018 | "Kumbukumbu Chungu" | Welcoming the Return of the Lord in Judgement


🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺❤❤❤❤❤❤❤❤❤

Fan Guoyi alikuwa mzee wa kanisa la nyumba kule Uchina. Wakati wa zaidi ya miaka ishirini ya huduma, siku zote alimwiga Paulo, na kufanya kazi kwa bidii na akamtumikia Bwana kwa shauku kubwa. Aidha, alisadiki kabisa kwamba katika kufuata imani yake kwa njia hii, alikuwa akitenda mapenzi ya Baba wa mbinguni, na kwamba wakati Bwana angerudi, angenyakuliwa kwa hakika na kuenda kwenye ufalme wa mbinguni. Hata hivyo, wakati wokovu wa Mwenyezi Mungu wa siku za mwisho ulipomjia, alishikilia kwa dhana zake.

10/13/2018

Siwezi Kusema Yote Yaliyo Moyoni Mwangu

I
Leo nimekutana na Wewe, matumaini yangu yote yametimia.
Nimefurahia utajiri wote katika kumbatio Lako la upendo na ukunjufu.
Moyo Wako hakika ni mzuri sana, upendo Wako unanivutia.
Kile Ulicho nacho na kile Ulicho, ni vya thamani sana kwangu.
Siwezi kuelezea, hakuna maneno:
Jinsi gani anavyopendeza Mwenyezi Mungu!

10/12/2018

Best Christian Music "Yule Anayeshikilia Ukuu Juu ya Kila Kitu" (Swahili Musical Documentary)

Kote katika ulimwengu mkubwa mno, sayari zote ya mbingu husogea kwa usahihi katika mizunguko yazo zenyewe. Chini ya mbingu, milima, mito, na maziwa vyote vina mipaka yavyo, na viumbe vyote huishi na kuzaana wakati wa misimu yote minne kulingana na sheria za maisha…. Hili lote limepangwa vizuri sana—je, kuna Mwenye Uwezo Mmoja anayepanga na kutawala yote haya? Tangu tuje katika ulimwengu huu tukilia tumeanza kutekeleza majukumu tofauti katika maisha.

10/11/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Utajiri wa Maisha

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Wakristo

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Utajiri wa Maisha

Wang Jun Mkoa wa Shandong
Kwa miaka mingi tangu kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho, mke wangu na mimi tumepitia hili pamoja chini ya ukandamizaji wa joka kubwa jekundu. Katika wakati huu, ingawa nimekuwa na udhaifu, maumivu, na machozi, nahisi kwamba nimenufaika pakubwa kutoka kwa uzoefu wa ukandamizaji huu.

10/10/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ufafanuzi wa Tamko la Kumi na Saba

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Ufafanuzi wa Tamko la Kumi na Saba

Kwa kweli, maneno yote kutoka katika kinywa cha Mungu ni mambo ambayo wanadamu hawayajui; yote ni lugha ambayo watu hawajasikia, kwa hiyo inaweza kusemwa hivi: Maneno ya Mungu yenyewe ni siri. Watu wengi kwa kutojua wanaamini kwamba ni mambo tu ambayo watu hawawezi kutimiza kimawazo, mambo ya mbinguni ambayo Mungu anawawezesha watu kuyajua sasa, au ukweli kuhusu kile Mungu anachofanya katika ulimwengu wa kiroho ni siri.

10/09/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Anga Hapa ni Samawati Sana

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Anga Hapa ni Samawati Sana

Hii hapa anga,
anga iliyo tofauti sana!
I
Harufu ya kupendeza inasambazwa kote kwenye nchi, na hewa ni safi.
Mwenyezi Mungu alikuwa mwili na anaishi miongoni mwetu,
Akionyesha ukweli na kuanza hukumu ya siku za mwisho.
Maneno ya Mungu yanaweka wazi ukweli wa upotovu wetu,
tunatakaswa na kukamilishwa na kila aina ya jaribio na usafishaji.

10/08/2018

Wimbo wa Injili "Ni Muumba Pekee Anayemhurumia Binadamu Huyu" | The Love of God Is the Truest Love (Kiitikio cha sauti ya Kike)


Muumba yuko miongoni mwa binadamu siku zote,
kwamba siku zote Anazungumza na binadamu na uumbaji mzima,
na kwamba Anatekeleza matendo mapya, kila siku. 
Hali Yake halisi na tabia vyote vimeelezewa katika mazungumzo Yake na binadamu;
fikira na mawazo Yake vyote vinafichuliwa kabisa kwenye matendo Yake haya;
Anaandamana na kufuatilia mwanadamu siku zote.

10/07/2018

Kuuonja Upendo wa Mungu Katikati ya Dhiki

Kuuonja Upendo wa Mungu Katikati ya Dhiki

Chen Lu Wilaya ya Tonglu, Mkoa wa Zhejiang
Nilizaliwa miaka ya 1980 katika kijiji—tulikuwa tumekuwa familia ya wakulima kwa vizazi vingi. Nilijiingiza katika masomo yangu ili niweze kuhitimu kuingia katika chuo na kuepuka maisha ya kijijini ya umasikini na hali ya kuwa nyuma. Nilipoanza shule ya upili, nilikutana na Historia ya Sanaa ya Magharibi, na wakati nilipoona picha nyingi za kupendeza kama vile "Mwanzo," "Bustani ya Edeni," na "Mlo wa Mwisho," ni hapo tu nilipojua kwamba kulikuwa na Mungu katika ulimwengu aliyeumba vitu vyote. Sikuweza kujizuia kuwa na moyo uliojaa hamu ya Mungu.

10/06/2018

Matamshi ya Roho Mtakatifu | "Inapofikia Mungu, Ufahamu Wako ni Upi?"


Mwenyezi Mungu alivyosema, "Huyu Aitwaye Mungu si Roho Mtakatifu pekee, huyo Roho, Roho aliyoongezeka mara saba, Roho anayehusisha yote, bali pia mtu, mtu wa kawaida, mtu wa kipekee wa kawaida. Si wa kiume pekee, bali pia kike. Wako sawa kwamba wote wanazaliwa kwa binadamu, na tofauti kwamba mmoja anachukuliwa katika mimba na Roho Mtakatifu na mwingine Anazaliwa kwa mwanadamu lakini Anatoka kwa Roho moja kwa moja.

10/05/2018

Msifuni Mwenyezi Mungu | Umo Moyoni Mwangu

Msifuni Mwenyezi Mungu  | Umo Moyoni Mwangu
I
Ninapotenda wajibu wangu mbali na nyumbani,
nawaza kukuhusu, na ninakuomba.
Kupitia kusoma maneno Yako,
nimekuja kukuamini zaidi na moyo wangu unapozwa, oo.
Kukushuhudia Wewe, ninapitia machungu mengi,
na najua hata vizuri zaidi jinsi Unavyopendeza.

10/04/2018

Swahili Praise and Worship Song "Ushuhuda wa Maisha" | Overcomers' Testimonies


Siku moja huenda nikakamatwa na kuteswa na CCP,
kuteseka huku ni kwa ajili ya haki, ambayo najua moyoni mwangu.
Maisha yangu yakitoweka mara moja ghafla bin vu,
bado nitasema kwa fahari kwamba nimemkubali Kristo wa siku za mwisho.
Ikiwa siwezi kuona tukio kuu la ukuaji wa injili ya ufalme,
bado nitatoa matarajio mazuri zaidi.
Ikiwa siwezi kuiona siku ambayo ufalme unafanikishwa,
lakini naweza kumwaibisha Shetani leo, basi moyo wangu utajawa na furaha na amani.

10/03/2018

Hakuna Anayeweza Kufanya Kazi Badala Yake

Kazi ya Mungu hufanywa na Mungu Mwenyewe.
Ni Yeye ndiye Anayeianzisha kazi Yake, na ni Yeye anayeikamilisha.
Ni Yeye anayeipanga kazi.
Ni yeye ndiye anayeisimamia, na zaidi kuifanikisha kazi hiyo.
Ni kama ilivyosemwa katika Biblia,
“Mungu ndiye Mwanzo na Mwisho;

10/02/2018

Wimbo wa Maneno ya Mungu | "Jinsi ya Kujua Kuonekana na Kazi ya Kristo wa Siku za Mwisho"


🎵🎵🎵🎵🎵👏👏👏👏👏👏🌺🌺🌺🌺🌺🌺❤❤❤❤❤❤
I
Mwili wa Mungu utajumlisha kiini cha Mungu na maonyesho Yake.
Atakapofanywa mwili, Ataleta matunda ya kazi Aliyopewa
ajidhihirishe na Alete Ukweli kwa wote,
awape uhai na awaonyeshe njia.
Mwili wowote usiokuwa na dutu Yake sio Mwili wa Mungu.
II
Thibitisha mwili Wake na njia ya kweli tazamia tabia, maneno na matendo Yake.

10/01/2018

Kupitia kwa Majonzi Makuu, Nimevuna Faida Kubwa

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa
Rongguang   Mji wa Zhengzhou, Mkoa wa Henan
Baada ya kumfuata Mwenyezi Mungu, niliwekwa katika jela kwa sababu mimi niliamini katika Mungu. Wakati huo nilikuwa muumini mpya na Mungu alikuwa amenipa nguvu ili niweze shikilia msimamo katika ushahidi wangu. Hata hivyo, niliamini kimakosa kuwa nilikuwa na kimo; nilidhani kwamba nilikuwa na kiasi kikubwa cha imani, upendo na uaminifu kwa Mungu, kwa hiyo sikuzingatia hasa kula na kunywa maneno ya Mungu ya hukumu na kuadibu. Ingawa nilisoma, nililinganisha neno ambalo kwalo Mungu humfichua mtu na watu wengine na kujitenga mwenyewe kutoka kwa maneno ya kuhukumu ya Mungu.