Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Petro. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Petro. Onyesha machapisho yote

10/26/2018

Maonyesho ya Mungu | "Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu" | Only Those Who Know God Can Be Perfected



      Mwenyezi Mungu anasema, “Katika kipindi kile alichomfuata Yesu, Petro alitazama na kutia moyoni kila kitu kuhusu maisha Yake: Matendo Yake, maneno Yake, mwendo Wake na maonyesho Yake. Alipata ufahamu wa kina kwamba Yesu hakuwa kama binadamu wa kawaida. Ingawa mwonekano Wake wa binadamu ulikuwa wa kawaida kabisa, Alijaa upendo, huruma, na ustahimilivu kwa binadamu. Kila kitu alichokifanya au kusema kilikuwa chenye msaada mkubwa kwa wengine, na akiwa kando Yake, Petro aliona na kujifunza mambo ambayo hakuwahi kuyaona wala kuyasikia awali. ... 

9/12/2018

Maana ya Mateso na ni Mateso ya Aina Gani Ambayo Waumini wa Mungu Lazima Wastahimili

Sura ya 7 Vipengele Vingine vya Ukweli Ambavyo Unafaa Kueleweka Katika Imani Yako kwa Mungu

6. Maana ya Mateso na ni Mateso ya Aina Gani Ambayo Waumini wa Mungu Lazima Wastahimili

Maneno Husika ya Mungu:
Leo, watu wengi sana hawana ufahamu huo. Wao huamini kwamba mateso hayana thamani, wao hukanwa na ulimwengu, maisha yao ya nyumbani yamesumbuliwa, wao si wapendwa wa Mungu, na matazamio yao ni matupu. Kuteseka kwa watu wengine hufikia kiwango fulani, na fikira zao hugeukia kifo. Huu si upendo wa kweli kwa Mungu; watu kama hao ni waoga, hawana ustahamilivu, wao ni wadhaifu na wasio na nguvu!

6/09/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kujijua Mwenyewe Hasa Ni Kujua Asili ya Binadamu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kujijua Mwenyewe Hasa Ni Kujua Asili ya Binadamu 

La muhimu katika kufikia badiliko la tabia ni kujua asili ya mtu mwenyewe, na hili ni lazima litoke kwa ufunuo na Mungu. Ni katika neno la Mungu tu ambapo mtu anaweza kujua asili yake ya kutia kinyaa, afahamu katika asili yake mwenyewe sumu mbalimbali za Shetani, atambue kuwa yeye ni mjinga na mpumbavu, na atambue dalili dhaifu na hasi katika asili yake mwenyewe. Mara haya yanapojulikana kikamilifu, na unaweza kwa hakika kunyima mwili, daima kutekeleza neno la Mungu, na kuwa na mapenzi ya kujiwasilisha kikamilifu kwa Roho Mtakatifu na kwa neno la Mungu, basi umeianza njia ya Petro.

5/18/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Utendaji (5)

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Utendaji (5)

Wakati wa Enzi ya Neema, Yesu alizungumza maneno kiasi na Akatekeleza hatua moja ya kazi. Kulikuwa na muktadha kwayo, na yalikuwa ya kufaa kwa hali za watu kwa wakati huo; Yesu alinena na kufanya kazi kama ilivyostahili muktadha wa wakati huo. Pia Alinena unabii kiasi. Alitabiri kwamba Roho wa ukweli angekuja wakati wa siku za mwisho, wakati ambapo Roho wa ukweli angetekeleza hatua ya kazi. Ambalo ni kusema, nje ya kazi ambayo Yeye Mwenyewe alikuwa Afanye wakati wa enzi hiyo, Hakuwa dhahiri kuhusu lingine lolote; yaani, kulikuwa na mipaka kwa kazi iliyoletwa na Mungu mwenye mwili. Hivyo, Alifanya tu kazi ya enzi hiyo, na hakufanya kazi nyingine ambayo haikuwa na uhusiano na Yeye.

4/24/2018

Umeme wa Mashariki | Ufafanuzi wa Tamko la Thelathini na Mbili

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Umeme wa Mashariki | Ufafanuzi wa Tamko la Thelathini na Mbili

Maneno ya Mungu huwaacha watu wakikuna vichwa vyao; ni kana kwamba, Anapozungumza, Mungu anaepukana na mwanadamu na kuzungumza na hewa, kana kwamba Hafikirii hata kidogo kuzingatia zaidi matendo ya mwanadamu, na Hatilii maanani kabisa kimo cha mwanadamu, kana kwamba maneno Anayozungumza hayaelekezwi kwa dhana za watu, lakini kuepukana na mwanadamu, kama lilivyokuwa kusudi la Mungu la asili. Kwa sababu nyingi sana, maneno ya Mungu hayaeleweki na mwanadamu hawezi kuyapenya. Hili halishangazi. Lengo la asili la maneno yote ya Mungu si kwa watu kupata ujuzi au ustadi kwayo; badala yake, ni njia moja kati ya zile Mungu ametumia kufanya kazi kutoka mwanzo hadi leo.

4/17/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Utendaji (3)

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Utendaji (3)

Lazima muwe na uwezo wa kuishi kwa kujitegemea, kuweza kula na kunywa maneno ya Mungu ninyi wenyewe, kupitia maneno ya Mungu ninyi wenyewe, na kuishi maisha ya kiroho ya kawaida bila uongozi wa wengine; lazima muweze kuyategemea maneno ya Mungu ya leo ili kuishi, kuingia katika uzoefu wa kweli, na kuona kwa hakika. Ni wakati huo tu ndipo mtaweza kusimama imara. Leo, watu wengi hawaelewi kikamilifu majonzi na majaribio ya siku za usoni. Katika siku za usoni, watu wengine watapitia majonzi, na wengine watapitia adhabu. Adhabu hii itakuwa kali zaidi; itakuwa ni kuwasili kwa ukweli. Leo, yote unayopitia, kufanya, na kuonyesha yanaweka msingi wa majaribio ya siku za usoni, na kwa kiwango cha chini mno, lazima uweze kuishi kwa kujitegemea.

4/12/2018

Maneno ya Yesu kwa Wanafunzi Wake Baada ya Kufufuka Kwake | Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III

    12. Maneno ya Yesu kwa Wanafunzi Wake Baada ya Kufufuka Kwake
(Yohana 20:26-29) Na baada ya siku nane wanafunzi wake walikuwa ndani tena, na Tomaso pamoja nao: Kisha akaja Yesu, na milango imefungwa, na akasimama katikati, kisha akasema, Amani iwe kwenu. Kisha akamwambia Tomaso, Weka hapa kidole chako, na utazame mikono yangu; na ulete mkono wako uuweke ubavuni mwangu, na usiwe asiyeamini, bali uwe aaminiye. Naye Tomaso akajibu akamwambia, Bwana wangu na Mungu wangu! Yesu akamwambia, Tomaso, kwa kuwa umeniona, umeamini; heri wanayo wale ambao hawajaona, ilhali wameamini.
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,Yesu

   
(Yohana 21:16-17) Akamwambia tena mara ya pili, Simoni wa Yona, je, wanipenda? Akamwambia, Ndiyo, Bwana; wewe unajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Lisha kondoo wangu. Akamwambia mara ya tatu, Simoni, mwana wa Yona, je, unanipenda? Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, je, unanipenda? Na akamwambia, Bwana, wewe unajua mambo yote; wewe unajua ya kwamba nakupenda. Yesu akamwambia, Lisha kondoo wangu.

3/28/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Thelathini na Nne📖📖

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu,

    Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Thelathini na Nne

    Wakati mmoja Nilimwalika mwanadamu kama mgeni nyumbani Kwangu, lakini alikimbia huku na huko kwa sababu ya miito Yangu–kama kwamba, badala ya kumwalika kama mgeni, Nilikuwa nimemleta kwenye eneo la kuuawa. Kwa hiyo, nyumba yangu inaachwa tupu, kwa maana mwanadamu ameepukana Nami daima, na daima amejilinda dhidi Yangu. Hili limeniacha bila njia yoyote ya kutekeleza sehemu ya kazi Yangu, ambalo ni kusema, ni kama kwamba Nimeirudisha karamu Niliyomtayarishia, kwa maana mwanadamu hayuko radhi kuifurahia karamu hii, na kwa hiyo Sitamlazimisha kufanya hivyo.

3/26/2018

Sura ya 38. Yeye Ambaye Hukosa Ukweli Hawezi Kuwaongoza Wengine📖🤲

📖📖📖***********👍👍👍***********📚📚📚*********🙂🙂🙂🙂
    Mwenyezi Mungu alisema, Je, kweli mnaelewa kuhusu mabadiliko katika tabia ya mtu? Mabadiliko katika tabia yanamaanisha nini? Je, mnaweza kutambua mabadiliko katika tabia? Ni hali zipi zinaweza kufikiriwa kuwa mabadiliko katika tabia ya maisha ya mtu, na ni hali zipi ambazo ni mabadiliko tu katika tabia ya nje? Tofauti ni ipi kati ya mabadiliko katika tabia ya mtu ya nje na mabadiliko katika maisha ya mtu ya ndani? Je, mnaweza kueleza tofauti? Mnamwona mtu mwenye hamu ya kukimbia pote kwa ajili ya kanisa, na mnasema: "Yeye amebadilika!" Mnamwona mtu akiitelekeza familia yake au kazi, na mnasema: "Yeye amebadilika!" Ikiwa amejitoa mhanga kwa namna hiyo, mnafikiri kwa hakika lazima amebadilika.

3/17/2018

🌿🙂😇9. Ninaona njia ya kumjua Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Wakristo
Xiaocao Mji wa Changzhi, Mkoa wa Shanxi
Siku moja, niliona kifungu hiki kifuatacho cha neno la Mungu kwa maandishi “Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu”: “Kwenye kipindi kile alichomfuata Yesu, Petro alitazama na kutia moyoni kila kitu kuhusu maisha Yake: Matendo Yake, maneno Yake, mwendo Wake na maonyesho Yake. … Tangu wakati huo akiwa na Yesu, Petro alitambua pia kwamba hulka Yake ilikuwa tofauti na ile ya binadamu wa kawaida. Siku zote alikuwa na mwenendo dhabiti na hakuwahi kuwa na haraka, hakupigia chuku wala kupuuza chochote, na aliyaishi maisha Yake kwa njia iliyokuwa ya kawaida na ya kuvutia. Katika mazungumzo, Yesu alikuwa mwenye madaha na uzuri, mwenye uwazi na mchangamfu ilhali pia mtulivu, na Hakuwahi kupoteza heshima Yake katika utekelezaji wa kazi Yake.

3/09/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Utendaji (2)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Utendaji (2)

Katika nyakati zilizopita, watu walijifundisha wenyewe kuwa na Mungu na kuishi katikati ya roho kila wakati, ambao, ukilinganishwa na utendaji wa leo, ni mafundisho rahisi ya kiroho tu. Utendaji kama huu huja kabla ya kuingia kwa watu katika njia sahihi ya maisha, na ni mbinu ya juujuu zaidi na rahisi zaidi kati ya mbinu zote za utendaji. Ni utendaji wa hatua za mwanzoni kabisa za imani ya watu kwa Mungu. Ikiwa watu wataishi kila mara kwa utendaji huu, watakuwa na hisia nyingi sana, na hawataweza kuingia katika uzoefu ambao ni wa kina na wa kweli. Wataweza tu kuzifundisha roho zao, kuifanya mioyo yao iweze kusonga kwa kawaida karibu na Mungu, na kupata kila mara furaha nyingi mno katika kuwa na Mungu.

2/08/2018

Umeme wa Mashariki | 8. Kutambua Kuwa Nimekuwa Nikiitembea Njia ya Mafarisayo

Umeme wa Mashariki | 8. Kutambua Kuwa Nimekuwa Nikiitembea Njia ya Mafarisayo

Wuxin Mji wa Taiyuan, Mkoa wa Shanxi
Kitu ambacho tumezungumzia mara kwa mara katika ushirikiano wa awali ni njia ambazo zilitembewa na Petro na Paulo. Inasemekana kwamba Petro alizingatia kujijua mwenyewe na kumjua Mungu, na alikuwa mtu ambaye Mungu alimpenda, ilhali Paulo alizingatia tu kazi yake, sifa na hadhi yake, na alikuwa mtu ambaye Mungu alimdharau. Daima nimekuwa na hofu ya kuitembea njia ya Paulo, ambayo ndiyo sababu mimi kwa kawaida mara nyingi husoma maneno ya Mungu kuhusu uzoefu wa Petro ili kuona jinsi alivyopata kumjua Mungu. Baada ya kuishi hivi kwa muda, nilihisi kwamba nilikwishakuwa mtiifu zaidi kuliko hapo awali, hamu yangu ya sifa na hadhi ilikuwa imedidimia, na kwamba nilikuwa nimepata kujijua kidogo.

1/31/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 6

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu, Sura ya 6

    Binadamu wanapigwa bumbuazi kwa sababu ya matamshi ya Mungu wanapotambua kwamba Mungu amefanya kitendo kikubwa katika ulimwengu wa kiroho, kitu ambacho mwanadamu hawezi na ambacho Mungu Mwenyewe pekee ndiye Anaweza kufanikisha. Kwa sababu hii, Mungu mara tena anawasilisha maneno ya huruma kwa wanadamu. Mioyo ya watu inapojaa ukinzani, ikishangaa: “Mungu ni Mungu asiye na huruma au upendo, lakini badala yake Mungu aliyejitolea kuwaangusha binadamu; kwa hiyo mbona Atuonyeshe huruma? Yawezekana kwamba Mungu kwa mara nyingine amehamia kwa utaratibu?”

11/18/2017

Tofauti Muhimu Kati ya Mungu Aliyepata Mwili na Wanadamu Wanaotumiwa na Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki


Kwa miaka mingi Roho wa Mungu Amekuwa Akifanya kazi kwa kutafuta duniani. Kwa enzi nyingi Mungu Ametumia wanadamu wengi kufanya kazi Yake. Hata hivyo Roho wa Mungu bado hana mahali pazuri pa kupumzika. Kwa hivyo Mungu hupitia wanadamu mbalimbali kufanya kazi Yake na kwa kiasi kikubwa hutumia wanadamu kufanya hivyo. Yaani, katika miaka hii yote mingi, kazi ya Mungu haijawahi kusimama. Inaendelezwa mbele kupitia mwanadamu, bila kikomo mpaka siku ya leo. Ingawa Mungu Amesema na Ametenda mengi, mwanadamu bado hamjui Mungu, hii ni kwa sababu Mungu hajawahi kuonekana na mwanadamu na Yeye Hana umbo.

11/17/2017

Umeme wa Mashariki | Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,ukweli
Matamshi ya Mwenyezi Mungu - "Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea"

Matamshi ya Mwenyezi Mungu - "Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea"

Watu wengi wanamwamini Mungu kwa ajili ya hatima yao ya baadaye au kwa ajili ya starehe ya muda mfupi. Kwa wale ambao hawajapitia ushughulikiaji wowote, imani kwa Mungu ni kwa ajili ya kuingia mbinguni, ili kupata tuzo. Sio ili kufanywa wawe na ukamilifu, au kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu. Ambayo ni kusema kwamba watu wengi hawamwamini Mungu ili watimize majukumu yao, au kukamilisha wajibu wao. Mara chache watu humwamini Mungu ili waishi maisha ya maana, wala hamna wale ambao wanaamini kwamba kwa kuwa mwanadamu yu hai, anapaswa ampende Mungu kwa kuwa ni sheria ya Mbinguni na kanuni ya dunia kufanya hivyo, na ni wito wa asili wa mwanadamu.

11/05/2017

Unapaswaje Kuitembea Hatua ya Mwisho ya Njia?

Umeme wa Mashariki | Unapaswaje Kuitembea Hatua ya Mwisho ya Njia?
Sasa mko kwenye hatua ya mwisho ya njia, na hii ni sehemu muhimu. Labda umevumilia mateso mengi kabisa, umefanya kazi nyingi, umetembea barabara nyingi, na umesikiliza mahubiri mengi, na haijakuwa rahisi kufika hadi sasa. Ikiwa huwezi kuvumilia mateso yaliyo mbele yako na kama unaendelea kama ulivyofanya zamani, basi huwezi kufanywa mkamilifu. Hii si ili kukutisha—huu ni ukweli. Baada ya Petro kupitia kazi ya Mungu kiasi fulani, alipata umaizi na ufahamu mwingi. Pia alielewa kiasi fulani cha kanuni ya huduma, na baadaye aliweza kujitolea kikamilifu kwa kile ambacho Yesu alimwaminia. Usafishaji mkubwa alioupokea mara nyingi ulikuwa kwa sababu katika mambo aliyoyafanya, alihisi kwamba alikuwa na deni kubwa kwa Mungu na kwamba hangeweza kamwe kumfidia, na aligundua kuwa wanadamu wamepotoka sana, kwa hivyo alikuwa na dhamiri yenye hatia. Yesu alikuwa amemwambia mambo mengi na wakati huo alikuwa na ufahamu mdogo tu.

10/29/2017

Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu

    Ni sheria ya Mbinguni na kanuni za duniani kumwamini Mungu na kumjua Mungu, na leo—wakati wa enzi ambapo Mungu mwenye mwili Anafanya kazi Yake mwenyewe—ndio wakati mwafaka hasa wa kumjua Mungu. Kumridhisha Mungu kunaafikiwa kwa msingi wa kufahamu mapenzi ya Mungu, na kuyafahamu mapenzi ya Mungu, ni muhimu kumjua Mungu. Ufahamu huu wa Mungu ni maono ambayo muumini anapaswa kuwa nayo; huu ndio msingi wa imani ya mwanadamu katika Mungu. Iwapo mwanadamu hana ufahamu huu, basi imani yake katika Mungu si dhahiri, na imejengwa juu ya nadharia tupu.

10/11/2017

Hudumu kama Waisraeli Walivyofanya

Umeme wa Mashariki | Hudumu kama Waisraeli Walivyofanya
Siku hizi watu wengi hawatilii maanani mafunzo yapi yanayopaswa kusomwa wakati wa upatano na wengine. Nimegundua kuwa wengi wenu hawawezi kujifunza mafunzo hata kidogo wakati wa ushirikiano na wengine. Wengi wenu mnashikilia maoni yenu mwenyewe, na wakati mnafanya kazi kanisani, unatoa maoni yako na yeye anatoa yake, moja uhusiano na mingine, bila kushirikiana kabisa. Mnajihusisha tu katika kutoa umaizi wenu wenyewe wa ndani, unaingia tu katika kuachilia huru "mizigo" ndani yenu, si kutafuta uzima hata kidogo. Inaonekana kwamba unafanya tu kazi hiyo kwa kutimiza wajibu, daima ukiamini kwamba unapaswa kufuata njia yako mwenyewe bila kujali jinsi watu wengine walivyo, na kwamba unapaswa kushiriki jinsi Roho Mtakatifu anavyokuongoza, bila kujali jinsi watu wengine walivyo. Hamna uwezo wa kugundua uwezo wa wengine, na hamuwezi kujichunguza. Njia yenu ya kupokea vitu ni yenye makosa sana.