Mwenyezi Mungu anasema, “Katika kipindi kile alichomfuata Yesu, Petro alitazama na kutia moyoni kila kitu kuhusu maisha Yake: Matendo Yake, maneno Yake, mwendo Wake na maonyesho Yake. Alipata ufahamu wa kina kwamba Yesu hakuwa kama binadamu wa kawaida. Ingawa mwonekano Wake wa binadamu ulikuwa wa kawaida kabisa, Alijaa upendo, huruma, na ustahimilivu kwa binadamu. Kila kitu alichokifanya au kusema kilikuwa chenye msaada mkubwa kwa wengine, na akiwa kando Yake, Petro aliona na kujifunza mambo ambayo hakuwahi kuyaona wala kuyasikia awali. ... Haijalishi ni vipi Yesu alivyotenda, Petro alizidi kuwa na upendo na heshima isiyokuwa na mipaka Kwake. Kicheko cha Yesu kilimjaza kwa furaha, huzuni Yake ikamtia simanzi, hasira Yake ikamtetemesha, huku huruma Zake, msamaha na ukali vyote vikamfanya kuja kumpenda Yesu kwa kweli, na akaweza kumcha na kumtamani kwa kweli. Bila shaka, Petro alikuja kutambua haya yote kwa utaratibu baada ya kuishi kando yake Yesu kwa miaka michache.”
Kuhusu Sisi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni