Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Paulo. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Paulo. Onyesha machapisho yote

9/03/2018

"Imani katika Mungu" (1) - Je, Utiifu kwa Wale Walio Madarakani Kweli ni Sawa na Utiifu kwa Mungu?πŸŽ¬πŸ‘‡



Katika Biblia, Paulo alisema, "Acha kila nafsi itii mamlaka ya juu zaidi. Kwani hakuna mamlaka isipokuwa ya Mungu: mamlaka yaliyoko yameamriwa na Mungu. Yeyote yule anayepinga nguvu, anapinga amri ya Mungu: na yule anayepinga atapokea laana” (Warumi 13:1-2). Sisi waumini tunapaswa kuwatendea vipi wale walio madarakani? Je, utiifu kwa wale walio madarakani ni sawa na utiifu kwa Mungu kweli?

Sikiliza zaidi: Neno la Mwenyezi Mungu, Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

7/30/2018

"Wakati wa Mabadiliko" (1) - Wanawali Wenye Hekima Hunyakualiwaje?πŸŽ¬πŸ‘


Kanisa la Mwenyezi Mungu | "Wakati wa Mabadiliko" (1) - Wanawali Wenye Hekima Hunyakualiwaje?

Watu wengine huongozwa na maneno ya Paulo katika suala la kumngoja Bwana ili kuinuliwa kwenda katika ufalme wa mbinguni: "Kwa ghafla, kufumba na kufumbua, wakati wa tarumbeta ya mwisho: kwa maana tarumbeta italia, na wafu watafufuliwa bila uovu, na tutabadilishwa" (1Kor 15:52). Wanaamini kwamba ingawa bado tunatenda dhambi siku zote bila kujinasua kutoka kwa pingu za asili ya dhambi, Bwana atazibadili taswira zetu mara moja na kutuleta katika ufalme wa mbinguni Atakapokuja.

5/18/2018

Umeme wa Mashariki | Utendaji (6)

Umeme wa Mashariki | Utendaji (6)

Mwenyezi Mungu alisema, Leo, watu wengi hawana hata urazini au kujitambua kwa Paulo, ambaye, ingawa aliangushwa na Bwana Yesu, tayari alikuwa na azimio la kufanya kazi na kuteseka kwa ajili Yake. Yesu alimpa ugonjwa, na baadaye, Paulo aliendelea kuvumilia ugonjwa huu mara alipoanza kufanya kazi. Kwa nini alisema alikuwa na mwiba mwilini mwake? Mwiba, kwa kweli, ulikuwa ugonjwa, na kwa Paulo, ulikuwa ugonjwa wa kufisha. Haijalishi alivyofanya kazi vizuri au jinsi azimio lake kuteseka lilivyokuwa kuu, alikuwa na ugonjwa huu kila mara. Paulo alikuwa mwenye uhodari thabiti zaidi kuliko ninyi watu wa leo;

5/02/2018

Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Watu Wanaomfuata Mungu | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

Neno la Mwenyezi Mungu | 3) Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Watu Wanaomfuata Mungu

    Baada ya hayo, hebu tuzungumzie mzunguko wa uhai na mauti wa wale wanaomfuata Mungu. Hili linawahusu, hivyo kuweni makini. Kwanza, fikiria kuhusu ni makundi gani ambamo watu wanaomwamini Mungu wanaweza kugawika. Kuna mawili: wateule wa Mungu na watendaji-huduma. Kwanza tutazungumza kuhusu wateule wa Mungu, ambao ni wachache. “Wateule wa Mungu” inarejelea nini? Baada ya Mungu kuumba vitu vyote na baada ya kuwepo wanadamu, Mungu alichagua kundi la watu ambao walimfuata, na Akawaita “wateule wa Mungu.” Kuna mipaka maalum na umuhimu katika uchaguzi wa Mungu wa watu hawa. Mipaka ni kwamba kila wakati Mungu anafanya kazi muhimu ni lazima waje—ambacho ni kitu cha kwanza kati ya vinavyowafanya maalum.

4/25/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Una Mtazamo Upi Kuhusu Nyaraka Kumi na Tatu

 Kanisa la Mwenyezi Mungu | Una Mtazamo Upi Kuhusu Nyaraka Kumi na Tatu

Mwenyezi Mungu alisema, Agano Jipya la Biblia lina nyaraka kumi na tatu za Paulo. Barua hizi kumi na tatu ziliandikwa na Paulo kwa makanisa yaliyomwamini Yesu Kristo wakati wa kazi yake. Yaani, aliziandika barua baada ya Yesu kupaa mbinguni na alifufuliwa. Barua zake ni ushuhuda wa ufufuo wa Bwana Yesu na kupaa mbinguni baada ya kifo Chake, na zinahubiri njia ya watu kutubu na kuubeba msalaba. Kwa kweli, njia hizi na shuhuda zote zilikuwa za kuwafundisha ndugu na dada katika sehemu mbalimbali za Uyahudi wakati huo, kwa sababu wakati huo Paulo alikuwa mtumishi wa Bwana Yesu, na alikuwa ameinuliwa kutoa ushuhuda kwa Bwana Yesu. Watu tofauti huinuliwa kutekeleza kazi Yake tofauti wakati wa kila kipindi cha kazi ya Roho Mtakatifu, yaani, kufanya kazi ya mitume ili kuendeleza kazi ambayo Mungu anakamilisha Mwenyewe.

3/26/2018

Sura ya 38. Yeye Ambaye Hukosa Ukweli Hawezi Kuwaongoza WengineπŸ“–πŸ€²

πŸ“–πŸ“–πŸ“–***********πŸ‘πŸ‘πŸ‘***********πŸ“šπŸ“šπŸ“š*********πŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚
    Mwenyezi Mungu alisema, Je, kweli mnaelewa kuhusu mabadiliko katika tabia ya mtu? Mabadiliko katika tabia yanamaanisha nini? Je, mnaweza kutambua mabadiliko katika tabia? Ni hali zipi zinaweza kufikiriwa kuwa mabadiliko katika tabia ya maisha ya mtu, na ni hali zipi ambazo ni mabadiliko tu katika tabia ya nje? Tofauti ni ipi kati ya mabadiliko katika tabia ya mtu ya nje na mabadiliko katika maisha ya mtu ya ndani? Je, mnaweza kueleza tofauti? Mnamwona mtu mwenye hamu ya kukimbia pote kwa ajili ya kanisa, na mnasema: "Yeye amebadilika!" Mnamwona mtu akiitelekeza familia yake au kazi, na mnasema: "Yeye amebadilika!" Ikiwa amejitoa mhanga kwa namna hiyo, mnafikiri kwa hakika lazima amebadilika.

11/18/2017

Tofauti Muhimu Kati ya Mungu Aliyepata Mwili na Wanadamu Wanaotumiwa na Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki


Kwa miaka mingi Roho wa Mungu Amekuwa Akifanya kazi kwa kutafuta duniani. Kwa enzi nyingi Mungu Ametumia wanadamu wengi kufanya kazi Yake. Hata hivyo Roho wa Mungu bado hana mahali pazuri pa kupumzika. Kwa hivyo Mungu hupitia wanadamu mbalimbali kufanya kazi Yake na kwa kiasi kikubwa hutumia wanadamu kufanya hivyo. Yaani, katika miaka hii yote mingi, kazi ya Mungu haijawahi kusimama. Inaendelezwa mbele kupitia mwanadamu, bila kikomo mpaka siku ya leo. Ingawa Mungu Amesema na Ametenda mengi, mwanadamu bado hamjui Mungu, hii ni kwa sababu Mungu hajawahi kuonekana na mwanadamu na Yeye Hana umbo.

11/17/2017

Umeme wa Mashariki | Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,ukweli
Matamshi ya Mwenyezi Mungu - "Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea"

Matamshi ya Mwenyezi Mungu - "Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea"

Watu wengi wanamwamini Mungu kwa ajili ya hatima yao ya baadaye au kwa ajili ya starehe ya muda mfupi. Kwa wale ambao hawajapitia ushughulikiaji wowote, imani kwa Mungu ni kwa ajili ya kuingia mbinguni, ili kupata tuzo. Sio ili kufanywa wawe na ukamilifu, au kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu. Ambayo ni kusema kwamba watu wengi hawamwamini Mungu ili watimize majukumu yao, au kukamilisha wajibu wao. Mara chache watu humwamini Mungu ili waishi maisha ya maana, wala hamna wale ambao wanaamini kwamba kwa kuwa mwanadamu yu hai, anapaswa ampende Mungu kwa kuwa ni sheria ya Mbinguni na kanuni ya dunia kufanya hivyo, na ni wito wa asili wa mwanadamu.

11/05/2017

Unapaswaje Kuitembea Hatua ya Mwisho ya Njia?

Umeme wa Mashariki | Unapaswaje Kuitembea Hatua ya Mwisho ya Njia?
Sasa mko kwenye hatua ya mwisho ya njia, na hii ni sehemu muhimu. Labda umevumilia mateso mengi kabisa, umefanya kazi nyingi, umetembea barabara nyingi, na umesikiliza mahubiri mengi, na haijakuwa rahisi kufika hadi sasa. Ikiwa huwezi kuvumilia mateso yaliyo mbele yako na kama unaendelea kama ulivyofanya zamani, basi huwezi kufanywa mkamilifu. Hii si ili kukutisha—huu ni ukweli. Baada ya Petro kupitia kazi ya Mungu kiasi fulani, alipata umaizi na ufahamu mwingi. Pia alielewa kiasi fulani cha kanuni ya huduma, na baadaye aliweza kujitolea kikamilifu kwa kile ambacho Yesu alimwaminia. Usafishaji mkubwa alioupokea mara nyingi ulikuwa kwa sababu katika mambo aliyoyafanya, alihisi kwamba alikuwa na deni kubwa kwa Mungu na kwamba hangeweza kamwe kumfidia, na aligundua kuwa wanadamu wamepotoka sana, kwa hivyo alikuwa na dhamiri yenye hatia. Yesu alikuwa amemwambia mambo mengi na wakati huo alikuwa na ufahamu mdogo tu.