Kanisa la Mwenyezi Mungu | Una Mtazamo Upi Kuhusu Nyaraka Kumi na Tatu
Mwenyezi Mungu alisema, Agano Jipya la Biblia lina nyaraka kumi na tatu za Paulo. Barua hizi kumi na tatu ziliandikwa na Paulo kwa makanisa yaliyomwamini Yesu Kristo wakati wa kazi yake. Yaani, aliziandika barua baada ya Yesu kupaa mbinguni na alifufuliwa. Barua zake ni ushuhuda wa ufufuo wa Bwana Yesu na kupaa mbinguni baada ya kifo Chake, na zinahubiri njia ya watu kutubu na kuubeba msalaba. Kwa kweli, njia hizi na shuhuda zote zilikuwa za kuwafundisha ndugu na dada katika sehemu mbalimbali za Uyahudi wakati huo, kwa sababu wakati huo Paulo alikuwa mtumishi wa Bwana Yesu, na alikuwa ameinuliwa kutoa ushuhuda kwa Bwana Yesu. Watu tofauti huinuliwa kutekeleza kazi Yake tofauti wakati wa kila kipindi cha kazi ya Roho Mtakatifu, yaani, kufanya kazi ya mitume ili kuendeleza kazi ambayo Mungu anakamilisha Mwenyewe.
Kama Roho Mtakatifu angefanya hivyo moja kwa moja na hakuna watu walioinuliwa, basi ingekuwa vigumu kwa kazi hiyo kutekelezwa. Kwa hiyo, Paulo akawa ambaye aliangushwa chini njiani kuelekea Dameski na kisha akainuliwa kuwa shahidi wa Bwana Yesu. Alikuwa mtume kando na wanafunzi kumi na wawili wa Yesu. Mbali na kueneza injili, pia alianza kazi ya kuyachunga makanisa katika maeneo mbalimbali, ambayo ni kuwatunza ndugu wa makanisa, yaani, kuwaongoza ndugu katika Bwana. Ushuhuda wake ni kujulisha ukweli wa ufufuo wa Bwana Yesu na kupaa mbinguni, na kuwafundisha watu kutubu na kukiri na kutembea katika njia ya msalabaa. Alikuwa mmoja wa mashahidi wa Yesu Kristo wakati huo.
Nyaraka kumi na tatu za Paulo zilichaguliwa kwa ajili ya matumizi katika Biblia. Barua hizi kumi na tatu zote ziliandikwa na Paulo zikilenga hali tofauti za watu katika maeneo mbalimbali. Aliguswa hisi na Roho Mtakatifu kuziandika na aliwafundisha ndugu katika maeneo yote kutoka katika nafasi ya mtume (akisimama kwa mtazamo wa mtumishi wa Bwana Yesu). Kwa hivyo, barua za Paulo hazikutokana na unabii au kutoka kwa maono moja kwa moja, lakini zilitoka kwenye kazi aliyoianza. Barua hizi si za ajabu, wala si vigumu kuelewa kama unabii. Maneno haya ni barua tu na sio unabii au mafumbo. Ni maneno tu ya kawaida ya mafunzo. Hata ingawa ni vigumu kufahamu maneno mengi au hayaeleweki kwa urahisi na watu, siyo zaidi ya kupata nuru kwa Roho Mtakatifu na maono aliyoyaona Paulo. Paulo ni mtume tu, mtumishi aliyetumiwa na Bwana Yesu, si nabii. Alichukua nafasi alipokuwa akitembea kila mahali kuandika barua kwa ndugu wa makanisa, au wakati alipokuwa mgonjwa, aliyaandikia makanisa ambayo yalikuwa hasa katika akili yake lakini hakuweza kuenda. Kwa hivyo, barua zake zilihifadhiwa na watu wakati huo, na baadaye, watu walizikusanya, kuziainisha, kisha wakaziweka baada ya Injili Nne za Biblia. Bila shaka, walichagua na kuweka pamoja barua zote bora alizoziandika. Barua hizi bila shaka ni za manufaa kwa maisha ya ndugu na dada wa makanisa na zilikuwa hasa barua maarufu za wakati huo. Paulo alipoziandika barua hizi wakati huo, kusudi lake halikuwa kuandika kazi ya kiroho ili kuwaruhusu ndugu kupata njia ya mazoea ndani yake, au wasifu wa kiroho kuelezea uzoefu wake mwenyewe. Yeye hakuwa na nia ya kuandika kitabu ili kuwa mwandishi; alikuwa tu akiwaandikia barua ndugu na dada wa kanisa la Bwana Yesu Kristo. Aliwafundisha ndugu katika nafasi yake kama mtumishi, kuwaambia kuhusu mzigo wake, mapenzi ya Bwana Yesu, na kile Alichowaaminia watu siku zijazo. Hiyo ndiyo kazi aliyoitekeleza. Maneno yake yalikuwa hasa ya kujenga kwa uzoefu wa ndugu na dada wa baadaye. Kuna ukweli mwingi katika barua hizi nyingi, na wote ulikuwa kile ambacho watu wa Enzi ya Neema walipaswa kutekeleza, na ndiyo sababu baadaye watu waliweka barua hizi katika Agano Jipya. Bila kujali matokeo ya Paulo baadaye yalivyokuwa, alikuwa mtu ambaye alitumiwa wakati huo, ambaye aliwasaidia ndugu na dada katika makanisa. Matokeo yake yaliamuliwa na asili yake na kuangushwa kwake chini mwanzoni. Aliweza kuyasema maneno hayo wakati huo kwa sababu alikuwa na kazi ya Roho Mtakatifu. Ilikuwa kwa sababu ya kazi ya Roho Mtakatifu kwamba aliubeba mzigo kuelekea makanisa. Kwa njia hiyo, aliweza kuwakimu ndugu na dada. Hata hivyo, kwa sababu ya baadhi ya hali maalum, hakuweza kwenda kibinafsi kwa makanisa kufanya kazi, kwa hiyo aliandikia barua ili kuwaonya ndugu na dada katika Bwana. Hapo awali aliwatesa wanafunzi wa Bwana Yesu, lakini baada ya Yesu kupaa mbinguni, yaani, baada yake kupokea nuru, aliacha kuwatesa wanafunzi wa Bwana Yesu na hakuwatesa tena wale watakatifu ambao walihubiri injili kwa ajili ya njia ya Bwana. Baada ya kumwona Yesu, aliinuliwa na kuwa mtu aliyetumiwa na Roho Mtakatifu.
Kazi ya Paulo wakati huo ilikuwa tu kuwasaidia na kuwakimu ndugu na dada. Yeye hakuwa kama watu wengine ambao walitaka kufanikiwa katika kazi au kuandika kazi fulani za fasihi, kufungua njia nyingine, au kutafuta njia nyingine nje ya Biblia ili kuwaongoza watu katika makanisa ili waweze kupata kuingia kupya. Alikuwa mtu ambaye alitumiwa; alifanya hivi ili tu kutimiza wajibu wake. Kama hangeubeba mzigo kuelekea makanisa, basi ingechukuliwa kama kutotimiza wajibu. Ikiwa kitu kiharibifu kingetokea au kungekuwa na tukio la usaliti katika kanisa likipelekea kuwa na hali isiyo ya kawaida ya watu huko, basi hiyo ingechukuliwa kama yeye kutotekeleza kazi yake vizuri. Mfanyakazi akiubeba mzigo kuelekea kanisa na pia afanye kazi kadri ya uwezo wake, basi hii inathibitisha kwamba yeye ni mfanyakazi ambaye ana sifa, mtu anayestahili kutumiwa. Ikiwa hahisi mzigo kuelekea kanisa, kazi yake pia haitimizi matokeo, na wengi wa watu anaowaongoza ni wadhaifu au hata wanaanguka, basi mfanyakazi kama huyo hajatimiza wajibu wake. Vivyo hivyo, Paulo hakuachwa. Ndiyo sababu alipaswa kuyatunza makanisa au kuandika barua mara nyingi kwa ndugu na dada. Ilikuwa kupitia mbinu hii ndipo alifaulu kuyakimu makanisa na kuwachunguza ndugu na dada—ilikuwa tu njia hii ambayo makanisa yangeweza kupata ruzuku na uchungaji kutoka kwake. Maneno ya barua alizoandika yalikuwa yenye kina sana, lakini barua zake ziliandikwa kwa ndugu na dada chini ya kigezo cha kupata nuru ya Roho Mtakatifu, zikishirikishwa na uzoefu wake binafsi na mzigo. Alikuwa tu mtu aliyetumiwa na Roho Mtakatifu. Uzoefu wake binafsi ulichanganywa katika yaliyokuwamo katika barua zake zote. Kazi aliyoitenda inawakilisha tu kazi ya mtume, sio kazi inayofanywa na Roho Mtakatifu moja kwa moja, na pia ni tofauti na kazi ya Kristo. Alikuwa tu akitimiza wajibu wake, ndiyo sababu alitoa mzigo wake pamoja na uzoefu wake binafsi na umaizi kwa ndugu na dada katika Bwana. Alikuwa tu akifanya kazi ya Agizo la Mungu kwa kutoa umaizi na ufahamu wa binafsi—hakika haikuwa Mungu Mwenyewe aliyefanya kazi moja kwa moja. Kwa hivyo, kazi yake ilichanganywa na uzoefu wa mwanadamu na jinsi mtu anavyotazama na kuelewa kazi ya kanisa. Hata hivyo, maoni haya na maarifa ya mwanadamu hayawezi kusemwa kuwa ni kazi ya roho wabaya au kazi ya mwili na damu. Inaweza tu kusemwa kuwa ni maarifa na uzoefu wa mtu aliyepatiwa nuru na Roho Mtakatifu. Ninachomaanisha kwa hili ni kwamba barua za Paulo sio vitabu kutoka mbinguni. Si takatifu na hazijatamkwa au kuonyeshwa na Roho Mtakatifu—ni maonyesho tu ya mzigo wa Paulo kuelekea kanisa. Madhumuni Yangu kusema haya yote ni kuwafanya muelewe tofauti kati ya kazi ya Mungu na mwanadamu. Kazi ya Mungu inawakilisha Mungu Mwenyewe, wakati kazi ya mwanadamu inawakilisha wajibu na uzoefu wa mwanadamu. Mtu hapaswi kuangalia kazi ya kawaida ya Mungu kama ilivyokusudiwa na mwanadamu na kazi Yake isiyo ya kawaida kama ilivyopangwa na Mungu. Zaidi ya hayo, mtu hapaswi kuzingatia mahubiri ya mtu ya fahari sana kama matamshi ya Mungu au kama vitabu vya mbinguni. Yote haya ni kinyume na maadili. Watu wengi wanaposikia Nikichambua nyaraka kumi na tatu za Paulo, wanafikiri barua za Paulo haziwezi kusomwa na kwamba Paulo ni mtu mwenye dhambi sana. Hata kuna watu wengi ambao wanafikiria maneno Yangu hayana huruma, kwamba makadirio Yangu ya barua za Paulo si sahihi, na kwamba barua zake haziwezi kuonekana kama maonyesho ya uzoefu na mzigo wa mwanadamu. Wanadhani zinapaswa kuzingatiwa kama maneno ya Mungu, ni muhimu kama Kitabu cha Ufunuo cha Yohana, hayawezi kupunguzwa au kuongezwa, na aidha hayawezi kuelezewa kwa kawaida. Je, si hizi taarifa zote za watu si sahihi? Je, si yote ni kwa sababu watu hawana hisia? Barua za Paulo zinawafaidi watu sana, na tayari zina historia ya zaidi ya miaka 2,000. Sasa, bado kuna watu wengi ambao hawawezi kuelewa kile alichoandika wakati huo. Katika hisia za mwanadamu, barua za Paulo ni kazi bora zaidi katika Ukristo wote. Hakuna mtu anayeweza kuzifumbua na hakuna mtu anayeweza kuzielewa kikamilifu. Kwa kweli, barua hizi ni kama wasifu wa mtu wa kiroho na haziwezi kulinganishwa na maneno ya Yesu au maono makuu aliyoyaona Yohana. Kwa upande mwingine, maono aliyoyaona Yohana yalikuwa maono makuu kutoka mbinguni, unabii wa kazi ya Mungu Mwenyewe, ambao haukutimizwa na mwanadamu, wakati barua za Paulo ni maelezo tu ya kile mtu alichoona na kupitia. Ni kile ambacho mtu anaweza na sio unabii wala maono—barua tu zilizotumwa maeneo mbalimbali. Lakini kwa watu wakati huo, Paulo alikuwa mfanyakazi na hivyo maneno yake yalikuwa na thamani, kwa sababu alikuwa mtu ambaye alikubali alichoaminiwa. Hivyo, barua zake zilikuwa za manufaa kwa wale waliomtafuta Kristo. Ingawa maneno hayakuzungumzwa na Yesu mwenyewe, yalikuwa, hata hivyo, muhimu kwa wakati wao. Kwa hiyo, wale waliokuja baada ya Paulo waliziweka barua hizi katika Biblia, na kuziwezesha kupitishwa mpaka sasa. Je, mnaelewa Ninachomaanisha? Ninaelezea tu kwa usahihi barua hizi, kuzichambua, si kukataa faida na thamani yazo kama kumbukumbu kwa watu. Ikiwa baada ya kuyasoma maneno Yangu hamkatai tu barua za Paulo lakini pia mnaamua kuwa ni tetesi au hazina thamani yoyote, basi inaweza tu kusemwa kwamba uwezo wenu wa kupokea kwa wepesi ni duni sana na maarifa yenu na uwezo wa kuona vitu ni duni sana—hakika haiwezi kusemwa kwamba maneno Yangu pia yanaegemea upande mmoja sana. Je, mnaelewa sasa? Jambo muhimu kwenu kuelewa ni hali halisi ya kazi ya Paulo wakati huo na usuli wa barua zake. Ikiwa mna mtazamo sahihi wa mambo haya, vivyo hivyo, mtakuwa na mtazamo sahihi wa barua za Paulo. Wakati huo huo, baada yako kuelewa kiini cha barua za Paulo, makadirio yako ya Biblia yatakuwa sahihi, na utaelewa kwa nini barua za Paulo zimeabudiwa sana na watu wa baadaye kwa miaka mingi, na kwa nini hata kuna wengi wanaomchukulia kama Mungu. Je, si hivyo ndivyo mngefikiri pia kama hamkuelewa?
Mtu ambaye si Mungu Mwenyewe hawezi kumwakilisha Mungu Mwenyewe. Kazi ya Paulo inaweza tu kusemwa kuwa kwa kiasi fulani mtu alivyoona na alivyopatiwa nuru na Roho Mtakatifu kwa kiasi fulani. Aliyaandika maneno haya kupitia kwa yale aliyoyaona pamoja na kupata nuru ya Roho Mtakatifu. Hii haishangazi. Kwa hivyo haiwezi kuepukika kwamba maneno yake yanachanganywa na uzoefu fulani wa kibinadamu, na baadaye alitumia uzoefu wake binafsi kuwakimu na kuwasaidia ndugu na dada wakati huo. Barua alizoandika haziwezi kuainishwa kama utafiti wa maisha, na sio za kikundi cha wasifu au ujumbe, na zaidi ya hayo sio ukweli unaotendwa na kanisa au amri za utawala za kanisa. Kama mtu aliye na mzigo, mtu aliyepewa kazi na Roho Mtakatifu, hiki kilikuwa alichopaswa kufanya. Roho Mtakatifu akimuinua mtu na kuongeza mzigo wake lakini asijishughulishe na kazi ya kanisa, kusimamia masuala ya kanisa vizuri, na kutatua matatizo yote ya kanisa, basi hii inathibitisha kwamba hakutimiza wajibu wake vizuri. Kwa hiyo si jambo la ajabu sana kwa mtume kuweza kuandika barua wakati wa kazi yake. Hii ilikuwa sehemu ya kazi yake, na aliwajibika kuifanya. Kusudi lake la kuandika barua hizi halikuwa kuandika mafunzo ya maisha au wasifu wa kiroho, na zaidi ya hayo haikuwa kuwafungulia watakatifu njia nyingine watakatifu. Ilikuwa kwa ajili ya kutimiza kazi yake mwenyewe na kuwa mtumishi mwaminifu kwa Mungu, ili apate kujielezea kwa Mungu kwa kukamilisha kile Mungu alichomwaminia. Aliwajibika kwake mwenyewe na kwa ndugu zake na dada katika kazi yake, ndiyo sababu alipaswa kufanya kazi yake vizuri na kuweka mambo ya kanisa moyoni. Hii ilikuwa sehemu ya kazi yake.
Ikiwa una ufahamu wa barua za Paulo, utakuwa pia na ufahamu na makadirio sahihi ya barua za Petro na Yohana. Hutawahi tena kutazama barua hizi kama vitabu kutoka mbinguni na takatifu na ya heshima, sembuse hutamwona Paulo kama Mungu. Hata hivyo, kazi ya Mungu ni tofauti na kazi ya mwanadamu, basi maonyesho ya Mungu na maonyesho ya mwanadamu yanawezaje kuwa sawa? Mungu ana tabia mahsusi ya Mungu, wakati mtu ana wajibu ambao mtu anapaswa kutimiza. Tabia ya Mungu inaonyeshwa katika kazi Yake, wakati wajibu wa mwanadamu unajumuishwa katika uzoefu wa mwanadamu na kuonyeshwa katika shughuli za mwanadamu. Kwa hivyo, inawezekana kujua kama ni maonyesho ya Mungu au ya mtu kupitia kazi yao. Haihitaji kuelezewa na Mungu Mwenyewe au kuhitaji mtu kujitahidi kushuhudia, na pia hakuhitaji Mungu Mwenyewe kumkandamiza mtu yeyote. Yote haya ni ufunuo wa asili; hailazimishwi au si kitu ambacho mwanadamu anaweza kuingilia kati. Wajibu wa mwanadamu unaweza kujulikana kupitia uzoefu wake na hauhitaji kufanya kazi yoyote ya ziada inayotokana na uzoefu wa mtu. Kiini chote cha mwanadamu kinaweza kufunuliwa anapotekeleza wajibu wake, wakati Mungu anaweza kuonyesha tabia Yake ya asili anapotekeleza kazi Yake. Ikiwa ni kazi ya mwanadamu basi haiwezi kufunikwa. Ikiwa ni kazi ya Mungu basi tabia ya Mungu haiwezekani hata zaidi kufunikwa na mtu yeyote, na aidha haiwezi kudhibitiwa na mwanadamu. Mtu hawezi kusemekana kuwa ni Mungu, na aidha kazi na maneno yake hayawezi kutazamwa kuwa matakatifu au kuonekana kuwa dhabiti. Mungu anaweza kusemwa kuwa mwanadamu kwa sababu Alijivika mwili, lakini kazi Yake haiwezi kuchukuliwa kama kazi ya mwanadamu au wajibu wa mwanadamu. Zaidi ya hayo, matamshi ya Mungu na barua za Paulo haviwezi kulinganishwa, wala hukumu na kuadibiwa kwa Mungu na maneno ya mafundisho ya mwanadamu kusemekana kuwa ni sawa. Kwa hivyo, kuna kanuni za kutofautisha baina ya kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu. Zinatofautishwa kulingana na asili zao, sio wigo wa kazi au ufanisi wa muda wa kazi. Watu wengi hufanya makosa ya kanuni juu ya mada hii. Hii ni kwa sababu mwanadamu huangalia nje, inayoweza kufanikishwa na mwanadamu, wakati ambapo Mungu huangalia dutu, ambayo haiwezi kuchunguzwa na macho ya kimwili ya wanadamu. Ukizingatia maneno ya Mungu na kufanya kazi kama mtu wa kawaida, na kuona kazi kubwa ya mwanadamu kama kazi ya Mungu iliyojivishwa mwili, kinyume na mtu anayetimiza wajibu wake, basi si wewe umekosea kimsingi? Barua za mwanadamu na wasifu vinaweza kufanywa kwa urahisi, lakini ni juu ya msingi wa kazi ya Roho Mtakatifu. Hata hivyo, matamshi na kazi ya Mungu haviwezi kutimizwa kwa urahisi na mwanadamu au kufikiwa kwa hekima na fikra za kibinadamu. Aidha, haiwezi kuelezewa kabisa kutoka kwa uchunguzi wa mwanadamu. Ikiwa hamna majibu yoyote kwa mambo haya ya kanuni, basi hiyo inathibitisha kuwa imani yenu si ya kweli sana na iliyosafishwa. Inaweza tu kusemwa kuwa imani yenu imejawa na wasiwasi na pia imechanganyikiwa na isio na maadili. Bila hata kuelewa masuala ya msingi ya Mungu na mwanadamu, si imani ya aina hii ni imani bila mtazamo wowote? Je, Paulo angewezaje kuwa mtu pekee aliyetumiwa katika miaka yote ya historia? Je, Paulo angewezaje kuwa mtu pekee aliyefanyia kanisa kazi? Je, angewezaje kuwa mtu pekee aliyeandika kwa makanisa kwa ajili ya kuwasaidia? Bila kujali ukubwa au ushawishi wa kazi ya watu hawa au matokeo ya kazi yao, si kanuni na dutu ya kazi hiyo yote ni sawa? Je, si kuna vitu ambavyo vina tofauti kabisa kuhusu kazi ya watu hawa na kazi ya Mungu? Hata ingawa kuna tofauti zilizo wazi kati ya kila hatua ya kazi ya Mungu na njia nyingi za kazi si sawa kabisa, je si zina dutu moja tu na chanzo kimoja? Kwa hivyo, kama mtu bado hana udhahiri kuhusu mambo haya sasa, basi pia hana mantiki kabisa. Ikiwa, baada ya kusoma maneno haya, mtu bado anasema barua za Paulo ni takatifu na za heshima nazo ni tofauti na wasifu wa mtu yeyote wa ajabu wa kiroho, basi mtu huyu ana mantiki ambayo si wa kawaida kupita kiasi, na mtu huyo bila shaka ni mtaalamu wa mafundisho ya dini ambaye hana akili. Hata ukimwabudu Paulo, huwezi kutumia hisia zako kunjufu kumwelekea ili kubadilisha ukweli wa mambo ya hakika au kukataa kuwepo kwa ukweli. Zaidi ya hayo, kile ambacho Nimesema hakiteketezi kazi zote na barua za Paulo kwa namna yoyote, au kukana kabisa thamani yake kama kumbukumbu. Bila kujali lolote, maana ya kile ambacho Nimesema ni ili kwamba muwe na ufahamu sahihi na makadirio ya maana ya vitu vyote na watu. Hii ni mantiki ya kawaida. Hicho ndicho kile watu wenye haki walio na ukweli wanapaswa kujiandaa nacho.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Kujua zaidi : Umeme wa Mashariki
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni