11/18/2017

Tofauti Muhimu Kati ya Mungu Aliyepata Mwili na Wanadamu Wanaotumiwa na Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki


Kwa miaka mingi Roho wa Mungu Amekuwa Akifanya kazi kwa kutafuta duniani. Kwa enzi nyingi Mungu Ametumia wanadamu wengi kufanya kazi Yake. Hata hivyo Roho wa Mungu bado hana mahali pazuri pa kupumzika. Kwa hivyo Mungu hupitia wanadamu mbalimbali kufanya kazi Yake na kwa kiasi kikubwa hutumia wanadamu kufanya hivyo. Yaani, katika miaka hii yote mingi, kazi ya Mungu haijawahi kusimama. Inaendelezwa mbele kupitia mwanadamu, bila kikomo mpaka siku ya leo. Ingawa Mungu Amesema na Ametenda mengi, mwanadamu bado hamjui Mungu, hii ni kwa sababu Mungu hajawahi kuonekana na mwanadamu na Yeye Hana umbo. Hivyo Mungu lazima Akamilishe kazi hii—kuwa wanadamu wote wajue umuhimu wa Mungu wa matendo. Kwa sababu hii, Mungu lazima aonyeshe wanadamu Roho wake katika nafsi na kufanya kazi miongoni mwao. Ni wakati tu ambapo Roho wa Mungu anaingia katika hali ya kimwili, kuchukua nyama na mifupa na kuonekana anatembea kati ya wanadamu, kuandamana nao katika maisha yao, wakati mwingine kuonekana na wakati mwingine kujificha, ndipo wanadamu wataweza kumuelewa kwa undani zaidi. Kama Mungu daima Angebaki katika mwili, Hangeweza kumaliza kwa ukamilifu kazi Yake. Baada ya kufanya kazi katika mwili kwa kipindi cha muda, kufanya huduma ambayo inastahili kufanyika Akiwa katika mwili, Mungu lazima Aondoke kwenye mwili na Afanye kazi katika ulimwengu wa kiroho kwa mfano wa mwili kama vile Yesu Alifanya baada ya kufanya kazi kwa kipindi cha muda katika ubinadamu wa kawaida na kukamilisha kazi yote ambayo Yeye Alihitajika kukamilisha. Mnaweza kukumbuka hili kutoka kwa Njia...(5): "Nakumbuka Baba yangu Akiniambia, "Duniani, tekeleza tu mapenzi yangu na ukamilishe agizo Langu. Hakuna jambo lingine linalokuhusu Wewe.’" Je, unaona nini katika kifungu hiki? Wakati Mungu Anakuja duniani, Yeye Anafanya tu kazi ya Uungu. Hili ni agizo la Roho wa mbinguni kwa Mungu mwenye mwili. Yeye Anakuja tu kwenda kila mahali na kuzungumza, kupaza sauti Yake kwa njia tofauti na kutoka kwa mitazamo tofauti. Yeye kimsingi Anachukulia kumruzuku mwanadamu na kumfundisha mwanadamu kama malengo Yake na kanuni Zake za kazi. Yeye hajihusishi na vitu kama uhusiano kati ya wanadamu au maelezo ya maisha ya wanadamu. Huduma Yake kuu ni kuzungumza kwa niaba ya Roho. Wakati Roho wa Mungu Anaonekana katika mwili kwa hali iliyo wazi, Yeye hukimu kwa ajili ya uzima wa mwanadamu na kuuweka wazi ukweli. Yeye hajihusishi katika masuala ya mwanadamu, yaani, yeye hashiriki katika kazi ya ubinadamu. Binadamu hawezi kufanya kazi ya Mungu, na Mungu hashiriki katika kazi za binadamu. Katika miaka yote ya Mungu kufanya kazi katika dunia hii, Yeye daima Ametumia wanadamu kufanya kazi Yake. Lakini wanadamu hawa hawawezi kuchukuliwa kama Mungu mwenye mwili; wao wanaweza tu kuchukuliwa kama wanadamu wanaotumiwa na Mungu. Lakini Mungu wa leo Anaweza kuzungumza moja kwa moja kutoka katika mtazamo wa Uungu, Apeleke sauti ya Roho, na kufanya kazi kwa niaba ya Roho. Wanadamu wote ambao Mungu Ametumia katika enzi nyingi huonekana kuwa Roho wa Mungu Anafanya kazi kupitia miili yao, hivyo basi kwa nini hawawezi kuitwa Mungu? Mungu wa leo ni Roho wa Mungu Anayefanya kazi moja kwa moja katika mwili, na Yesu pia Alikuwa Roho wa Mungu Aliyefanya kazi katika mwili. Hawa wawili wa mwisho wanaitwa Mungu. Basi tofauti ni nini? Tangu mwanzo, wanadamu ambao Mungu Ametumia wote wana mawazo ya kawaida na fikra. Wao wote wanajua jinsi ya kujiendesha na kushughulikia mambo ya maisha. Wanashikilia itikadi za kawaida za binadamu na kuwa na vitu vyote ambavyo wanadamu wa kawaida wanapaswa kuwa navyo. Wengi wao wana vipaji vya pekee na werevu wa kiasili. Kwa kufanya kazi kupitia wanadamu hawa, Roho wa Mungu Anakusanya na kutumia vipaji vyao, ambavyo ni zawadi yao Aliyowapa Mungu. Ni Roho wa Mungu Ndiye Anayeleta vipaji vyao katika kazi, na kuwasababisha kutumia uwezo wao kumhudumia Mungu. Hata hivyo, kiini cha Mungu hakina itikadi na hakina fikira. Hakiungani na mawazo ya binadamu na hata kinakosa vitu ambavyo binadamu wa kawaida huwa navyo. Yaani, Mungu hata haelewi kanuni za maadili ya binadamu. Hivi ndivyo ilivyo Mungu wa leo Anapokuja duniani. Yeye Anafanya kazi na Anaongea bila kuhusisha mawazo ya binadamu au fikra za binadamu, lakini kwa wazi Anaashiria maana asili ya Roho na moja kwa moja Anafanya kazi kwa niaba ya Mungu. Hii ina maana Roho huja kufanya kazi, ambayo Haweki ndani mawazo ya mwanadamu hata kidogo. Yaani, Mungu katika mwili Anajumuisha Uungu moja kwa moja, Hana mawazo ya binadamu au itikadi, na Haelewi kanuni za maadili ya binadamu. Kama kungekuwa na kazi ya Uungu tu (kumaanisha iwapo ingekuwa Mungu mwenyewe pekee ndiye Anayefanya kazi hiyo), kazi ya Mungu haingeweza kufanyika duniani. Kwa hivyo Mungu Anapokuja duniani, lazima Awe na wanadamu wachache Anaowatumia kufanya kazi katika ubinadamu pamoja na kazi Yake katika Uungu. Kwa maneno mengine, Yeye Anatumia kazi ya mwanadamu ili kusaidia kazi Yake takatifu. La sivyo, mwanadamu hangeweza kuja katika mawasiliano ya moja kwa moja na kazi ya Mungu. Hivi ndivyo ilivyokuwa baina ya Yesu na wanafunzi wake. Wakati wa maisha Yake duniani Yesu alipiga marufuku sheria za zamani na kuanzisha amri mpya. Pia alizungumza mengi. Yote haya yalifanyika katika Uungu. Wengine, kama vile Petro, Paulo, na Yohana, wote waliweka kazi yao ya baadaye juu ya maneno ya Yesu kama msingi wake. Yaani, Mungu Alikuwa Akifanya kazi ya uzinduzi katika enzi hiyo, Akiialika Enzi ya Neema. Alileta enzi mpya, Akaiondoa ile ya zamani, na Alifanya maneno haya "Mungu ni Mwanzo na Mwisho" kutimika. Kwa maneno mengine, mwanadamu lazima afanye kazi ya mwanadamu juu ya msingi wa kazi ya Mungu. Yesu alipomaliza kusema yote Aliyohitajika kusema na kumaliza kazi Yake hapa duniani, alitoka katika mwanadamu. Na wanadamu baada Yake walifanya kazi kwa mujibu wa kanuni katika maneno Yake na kutenda kwa mujibu wa ukweli Alioongea. Hawa wote walikuwa watu waliomfanyia Yesu kazi. Kama ingekuwa ni Yesu pekee Yake anafanya kazi, haijalishi kiasi gani Yeye Angezungumza, bado wanadamu hawangeweza kuwa na uhusiano na neno Lake, kwa sababu Yeye Alifanya kazi katika Uungu na usemi Wake ulikuwa wa Uungu peke yake. Ilikuwa vigumu Kwake kueleza mambo kwa namna ambayo wanadamu wa kawaida wangeweza kuelewa neno Lake. Hivyo basi ilimpasa kuwa na mitume na manabii waliokuja kabla Yake kuongezea kazi Yake. Hii ni kanuni ya jinsi Mungu mwenye mwili Hufanya kazi - kwa kutumia mwili kusema na kutenda ili kukamilisha kazi ya Uungu, na kisha kwa kutumia wanadamu wachache au zaidi wanaopendeza moyo wa Mungu ili kujaliza kazi ya Mungu. Yaani, Mungu Anatumia wanadamu wanaopendeza moyo Wake kuongoza na kunyunyiza ubinadamu ili kila mwanadamu aweze kupokea ukweli.
Kama Mungu Anakuja tu katika mwili na anafanya kazi ya Uungu bila kuwa na wanadamu wachache wa ziada wanaopendeza moyo Wake kushirikiana na Yeye, basi mwanadamu hatakuwa na uwezo wa kuelewa mapenzi ya Mungu na hataweza kuwa katika mawasiliano na Mungu. Mungu Anatumia wanadamu wa kawaida wanaopendeza moyo Wake ili kukamilisha kazi hii, kutunza na kuchunga makanisa, ili kwamba fikra za mwanadamu na ubongo wake uweze kufikiria kazi ya Mungu. Kwa maneno mengine, Mungu anatumia wanadamu wachache wanaopendeza moyo wake "kutafsiri" kazi Yake katika Uungu, kuifichua, yaani, kubadilisha lugha ya Mungu kuwa lugha ya binadamu, hivyo kwamba wanadamu wote waweze kuielewa lugha Yake. Kama Mungu hangefanya hivyo, hakuna mwanadamu angeweza kuelewa lugha ya Mwenyezi Mungu, kwa sababu idadi ya wanadamu walio na moyo unaompendeza Mungu, ni wachache mno, na uwezo wa mwanadamu kufahamu ni dhaifu. Hiyo ndiyo maana Mungu Hutumia njia hii wakati wa kufanya kazi katika mwili. Kama kungekuwa na kazi ya Uungu peke yake, mwanadamu hangeweza kujua au kuwa katika mawasiliano na Mungu kwa sababu mwanadamu haelewi lugha ya Mungu. Mwanadamu anaweza kuelewa lugha hii tu kupitia kwa wanadamu wanaopendeza moyo wa Mungu kufafanua maneno Yake. Hata hivyo, kama kungekuwa na wanadamu kama hao pekee wakifanya kazi katika ubinadamu, ingeweza tu kudumisha maisha ya kawaida ya mwanadamu; isingekuwa na uwezo wa kubadilisha tabia ya mwanadamu. Kazi ya Mungu haingeweza kuwa na mwanzo mpya; kungekuwa tu na nyimbo zile za zamani, na maelezo yale ya zamani. Ni kupitia kwa Mungu Aliye katika mwili Akisema yote aliyohitaji kusema na kufanya yote ambayo yanafaa kufanyika katika hali ya mwili, na wanadamu wanaofanana na Yeye kufanya kazi na kuishi kulingana na maneno Yake, ndipo tabia ya maisha yao inaweza kubadilika na waweze kusonga na nyakati. Yeye ambaye Anafanya kazi katika Uungu Anawakilisha Mungu, ilhali wale wanaofanya kazi katika ubinadamu ni wanadamu wanaotumiwa na Mungu. Yaani, Mungu katika mwili ana utofauti halisi na wanadamu wanaotumiwa na Mungu. Mungu mwenye mwili Anaweza kufanya kazi ya Uungu, lakini wanadamu wanaotumiwa na Mungu hawawezi. Mwanzoni mwa kila enzi, Roho wa Mungu anaongea binafsi kuzindua enzi mpya na kuleta mwanadamu kwenye mwanzo mpya. Wakati Yeye Atamaliza mazungumzo Yake, itaashiria kwamba kazi ya Mungu katika Uungu imekamilika. Baada ya hapo, wanadamu wote hufuata mwongozo wa wale hutumiwa na Mungu kuingia katika uzoefu wa maisha. Vile vile, katika hatua hii Mungu huleta mwanadamu katika enzi mpya na Anampa kila mwanadamu mwanzo mpya. Na hivyo, kazi ya Mungu katika mwili inahitimishwa.
Mungu haji duniani kufanya ubinadamu Wake wa kawaida uwe mkamilifu. Yeye haji kufanya kazi ya ubinadamu wa kawaida, ila kufanya kazi ya Uungu ndani ya ubinadamu wa kawaida. Kile ambacho Mungu anaona kama ubinadamu wa kawaida si kile ambacho mwanadamu anafikiria. Mwanadamu hufafanua "ubinadamu wa kawaida" kama kuwa na mke, au mume, na watoto. Kwa mwanadamu, [a] mambo haya yanamaanisha yeye ni mwanadamu wa kawaida. Lakini Mungu haoni hivi. Anaona ubinadamu wa kawaida kama kuwa na mawazo ya kawaida ya binadamu na maisha na kuzaliwa na wanadamu wa kawaida. Lakini ukawaida Wake hauhusishi kuwa na mke, au mume na watoto vile ambavyo mwanadamu anaelewa hali ya kawaida. Yaani, kwa mwanadamu, ubinadamu wa kawaida ambao Mungu Anazungumzia ni kile mwanadamu angeona kama kukosekana kwa ubinadamu, karibu ukose kuwa na hisia na kuonekana hauna mahitaji ya kimwili, kama vile Yesu, Ambaye Alikuwa tu nje ya mwanadamu wa kawaida na alichukua umbo la juu la mwanadamu wa kawaida, lakini katika kiini hakuwa kabisa na vitu alivyo navyo mwanadamu wa kawaida. Kutokana na hili inaweza kuonekana kwamba dutu ya Mungu mwenye mwili haihusishi kwa ukamilifu hali ya ubinadamu wa kawaida, lakini sehemu tu ya mambo ambayo wanadamu wanapaswa kuwa nayo, ili kuendeleza kanuni za maisha ya kawaida ya binadamu na akili ya kawaida ya binadamu. Lakini hivi vitu havihusiani na kile ambacho mwanadamu anaona kama ukawaida wa binadamu. Hivi ni vile Mungu mwenye mwili Anapaswa kuwa navyo. Hata hivyo baadhi ya wanadamu wanasema kwamba Mungu mwenye mwili Anaweza tu kuwa na ubinadamu wa kawaida iwapo Yeye ana mke, watoto na familia. Bila mambo haya, wanasema, Yeye si mwanadamu wa kawaida. Nakuuliza hivi basi, je, Mungu Ana mke? Je, inawezekana kwa Mungu kuwa na mume? Je, Mungu Anaweza kuwa na watoto? Je, hizi sio dhana zenye kosa tu? Hata hivyo, Mungu katika mwili Hawezi kuchomoka kutoka katika nyufa kwenye miamba au kuanguka chini kutoka mbinguni. Anaweza tu kuzaliwa kwa familia ya kawaida ya binadamu. Hiyo ndio maana Anao wazazi na dada. Haya ni mambo ambayo binadamu wa kawaida ndani ya Mungu katika mwili lazima Awe nayo. Hivi ndivyo Yesu alivyokuwa. Yesu Alikuwa na baba na mama, na ndugu. Haya yote yalikuwa ya kawaida. Lakini kama Angekuwa na mke na watoto, basi Wake haungekuwa ubinadamu wa kawaida ambao Mungu alitaka katika Mungu mwenye mwili. Kama ni hivyo, Yeye Hangekuwa na uwezo wa kuwakilisha Uungu katika kazi Yake. Ilikuwa ni kwa sababu Hakuwa na mke au watoto lakini Alizaliwa na wanadamu wa kawaida katika familia ya kawaida ndipo yeye alikuwa na uwezo wa kufanya kazi ya Uungu. Kwa kufafanua, kile ambacho Mungu anaona kama mwanadamu wa kawaida ni mwanadamu aliyezaliwa katika familia ya kawaida. Mwanadamu kama huyo tu ndiye anayeweza kufanya kazi ya Mungu. Kama, kwa upande mwingine, mtu huyo angekuwa na mke, watoto, au mume, mwanadamu huyo basi hangekuwa na uwezo wa kufanya kazi ya Mungu kwa sababu angekuwa tu na ubinadamu wa kawaida ambao binadamu anahitaji lakini si ubinadamu wa kawaida ambao Mungu Anahitaji. Mawazo ya Mungu na ufahamu wa wanadamu mara nyingi huwa na tofauti kubwa na zenye viwango tofauti. Mengi katika hatua hii ya kazi ya Mungu huwa na mapambano dhidi ya, na hutofautiana na fikra za wanadamu. Unaweza kusema kwamba hatua hii ya kazi ya Mungu yote hufanyika kwa mikono ya Uungu moja kwa moja, na ubinadamu ukiwa na jukumu la kusaidia. Kwa sababu Mungu anakuja duniani kufanya kazi Yake mwenyewe badala ya kumwacha mwanadamu aifanye, Yeye Hujiweka Mwenyewe katika mwili (mwili wa mwanadamu wa kawaida asiye mkamilifu) ili kufanya kazi Yake. Anatumia mwili huu kuwasilisha mwanadamu na enzi mpya, kuwaambia wanadamu hatua inayofuata katika kazi Yake, ili waweze kutenda kwa mujibu wa njia iliyoelezwa na neno Lake. Na hapo Mungu Anakamilisha kazi Yake katika mwili. Anahitaji kuondoka mwanadamu, asiishi tena katika mwili wa binadamu wa kawaida, na badala yake kusonga mbali na mwanadamu kufanya sehemu nyingine ya kazi Yake. Yeye kisha Hutumia wanadamu wanaopendeza moyo Wake kuendeleza kazi Yake hapa duniani miongoni mwa kundi hili la wanadamu, lakini katika ubinadamu.
Mungu mwenye mwili hawezi kukaa na mwanadamu milele kwa sababu Mungu Ana kazi zingine nyingi za kufanya. Yeye hawezi kufungwa katika mwili; Yeye Anavua mwili ili Afanye kazi ambayo Anahitaji kufanya, ingawa yeye Anafanya kazi hiyo kwa mfano wa mwili. Wakati Mungu Anakuja duniani, Yeye hasubiri hadi Afike hali ambayo mwanadamu wa kawaida hufika maishani kabla ya kufa na kuondoka. Haijalishi mwili wake ni wa umri gani, wakati kazi Yake imemalizika, Anaondoka na kumwacha mwanadamu. Hana umri, yeye hahesabu siku zake kulingana na umri wa mwanadamu. Badala yake Yeye hukamilisha maisha Yake katika mwili kulingana na hatua ya kazi Yake. Baadhi ya wanadamu wanaweza kuhisi kwamba Mungu, ambaye Anakuja katika mwili, lazima akue mpaka afikie hatua fulani, Awe mwanadamu mzima, kufikia umri wa uzee, na kuondoka tu wakati mwili umeshindwa. Haya ni mawazo ya mwanadamu; Mungu Hafanyi kazi kwa namna hiyo. Yeye Anakuja katika mwili kufanya kazi Anayostahili kufanya, si kuishi maisha ya mwanadamu ya kuzaliwa kwa wazazi, kuwa mtu mzima, kutengeneza familia na kuanza kazi, kupata watoto, au kupitia panda shuka za maisha - hali ya maisha ya kawaida. Mungu kuja duniani ni Roho wa Mungu kuletwa katika mwili, na kuja katika mwili, bali Mungu Haishi maisha ya kawaida ya binadamu. Yeye Huja tu kukamilisha sehemu moja katika mpango wa usimamizi Wake. Baada ya hapo Atamwacha mwanadamu. Atakapokuja katika mwili, Roho wa Mungu hakamilishi ubinadamu wa kawaida wa mwili. Badala Yake, kwa wakati Alioweka, Uungu unafanya kazi moja kwa moja. Kisha, baada ya kufanya yote ambayo Yeye Anahitajika kufanya na kukamilisha huduma Yake, kazi ya Roho wa Mungu katika hatua hii imekamilika, na wakati huo maisha ya Mungu katika mwili yanaisha, haijalishi kama mwili Wake umefikia umri wa kifo au la. Hiyo ni, hatua ya maisha ambayo mwili unafika, muda ambao unaishi duniani, yote hutegemea kazi ya Roho. Haihusiani kwa vyovyote na kile mwanadamu anachoona kuwa ukawaida wa binadamu. Chukua Yesu kama mfano. Yeye Aliishi katika mwili kwa miaka thelathini na mitatu na nusu. Katika suala la urefu wa maisha ya mwili wa binadamu, Yeye Hakupaswa kufariki Akiwa na umri huo na Hakupaswa kuondoka. Lakini Roho wa Mungu hakujali kuhusu hayo yote. Wakati kazi Yake ilimalizika, mwili ulichukuliwa, ukatoweka na Roho. Hii ni kanuni ya jinsi Mungu Hufanya kazi katika mwili. Hivyo, kusema kwa kweli, Mungu katika mwili Hana ubinadamu wa kawaida. Tena, Yeye Haji duniani kuishi maisha ya kawaida ya binadamu. Yeye Haimarishi kwanza maisha ya kawaida ya binadamu kisha Aanze kufanya kazi. Badala Yake, mradi tu Amezaliwa katika familia ya kawaida ya binadamu, Yeye Ana uwezo wa kufanya kazi ya Mungu. Yeye Havuti mawazo ya mwanadamu hata kidogo; Yeye si wa mwili, na yeye hakika Hajihusishi na njia za jamii au kujihusisha katika mawazo ya mwanadamu au fikra, au kujiunga na falsafa ya maadili ya binadamu. Hii ni kazi ambayo Mungu mwenye mwili Anataka kufanya na umuhimu wa vitendo vya mwili wake. Mungu Anakuja katika mwili kimsingi kufanya hatua ya kazi inayohitaji kufanyika katika mwili. Yeye Hajihusishi na michakato isiyo na maana, na Yeye hapitii matukio ya kawaida ya mwanadamu. Kazi ambayo Mungu katika mwili Anahitaji kufanya haina hali ya kawaida ya binadamu. Hivyo, Mungu Anakuja katika mwili ili kutimiza kazi Anayohitaji kukamilisha katika mwili. Mengine yote Hayamhusu. Hafuati hatua zisizo za maana. Mara kazi Yake inapokamilika, umuhimu wa mwili Wake unaisha. Kumaliza hatua hii kuna maana kazi ambayo Yeye Anahitajika kufanya katika mwili imekamilika, huduma ya mwili Wake imekamilika. Lakini Yeye hawezi kuendelea kufanya kazi katika mwili kwa muda usiojulikana. Yeye lazima Aende mahali pengine kufanya kazi, mahali ambapo ni nje ya mwili. Ni kwa njia hii tu ndio anaweza kukamilisha na kupanua zaidi kazi Yake. Mungu hufanya kazi kulingana na mpango Wake wa awali. Yeye Anajua Anayohitaji kufanya na Aliyohitimisha kama kiganja cha mkono wake. Mungu Humwongoza kila mwanadamu kwenye njia ambayo Yeye tayari Amechagua. Hakuna anayeweza kuepuka hili. Ni wale tu ambao hufuata uongozi wa Roho wa Mungu ndio watakaokuwa na uwezo wa kuingia katika pumziko. Huenda ikawa katika kazi ya baadaye, sio Mungu Anayemwongoza mwanadamu kwa kuongea katika mwili, ila ni Roho anayeonekana ndiye anayeongoza maisha ya mwanadamu. Hapo tu ndipo mwanadamu atakuwa na uwezo wa uthabiti wa kugusa Mungu, kuona Mungu, na kwa kikamilifu zaidi kuingia katika hali halisi ambayo Mungu Anataka, ili aweze kukamilishwa na Mungu wa vitendo. Hii ndiyo kazi ambayo Mungu Anataka kukamilisha, Ambayo amepanga kwa muda mrefu. Kutokana na hili, mnapaswa nyote kuona njia ambayo mnapaswa kuchukua!
Maelezo ya Chini:
a. Nakala ya awali inaacha "Kwa mwanadamu."

kutoka kwa Neno Laonekana Katika Mwili

Kujua zaidi : Umeme wa Mashariki | Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni