Christian Video Swahili "Uaminifu ni wa Thamani Mno" | Wokovu wa Bwana
Zhen Cheng alikuwa mmiliki wa duka la urekebishaji wa vifaa vya stima. Alikuwa mkarimu, mwaminifu, na alifanya biashara inavyopasa kufanywa. Hangejaribu kumdanganya mtu, lakini alikuwa anachuma tu pesa za kutosha angalau kuimudu tu famillia yake. Baada ya muda, mmoja wa jamaa yake na mfanya biashara mwenza alimhimiza atende kulingana na sheria zisizoandikwa za biashara, na Zhen Cheng alianza kuamini katika misemo inayowakilisha falsafa ya kama vile: "Mwanaume bila kipato cha pili hawezi kamwe kuwa tajiri kama tu jinsi farasi aliyenyimwa nyasi kavu usiku hawezi kamwe kuongeza uzani,” “Wajasiri hufa kwa ajili ya tamaa; waoga hufa kwa njaa," "Pesa si kila kitu, lakini bila pesa, huwezi kufanya chochote," na "Pesa kwanza."
Zhen Cheng alipoteza dhamiri yake nzuri iliyokuwa imemwelekeza awali na akaanza kutumia mbinu za kisirisiri kupata pesa zaidi. Hata ingawa alipata pesa zaidi kuliko vile alivyopata awali, na hali ya maisha yake iliimarika, Zhen Cheng hata hivyo alihisi asiye na furaha na hali ya utupu ilimsumbua; maisha yalikuwa matupu na yaliyojaa mateso. Baada ya Zhen Chen kuikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, alikuja kuelewa kupitia neno la Mungu kwamba Mungu anawapenda watu waaminifu na Anawachukia walio wadanganyifu. Zhen Cheng pia alikuja kuelewa kwamba kuwa mtu mwaminifu ndiyo njia ya pekee ya kutenda kama mtu wa kweli na njia ya pekee ya kufanikisha sifa ya Mungu, na hivyo akaapa kuwa mtu mwaminifu. Hata hivyo, kuwa mtu mwaminifu katika maisha halisi kulidhihirika kuwa kugumu: Pamoja na ndugu kanisani, angeweza kuwa mnyoofu alivyopaswa kuwa, lakini angefanya hivyo katika ulimwengu wa biashara, angeweza kupata pesa? Hangeweza tu kwa matarajio ya kupata pesa chache zaidi, angeweza pia kupitia hasara kubwa na alikuwa katika hatari ya kupoteza duka lake. … Usoni pa mapambano kama hayo, je, Zhen Chen angeweza kuendesha biashara yake kwa uaminifu? Ni mabonde na milima ya aina gani yasiyotarajiwa yatatokea njiani? Thawabu yake kubwa itakuwa nini?…
Sikiliza zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, Chanzo cha Mafanikio ya Umeme wa Mashariki
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni