4/28/2018

Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu kwa ajili ya Wokovu wa Mwanadamu

Mwenyezi Mungu alisema, Kama hatua ya mwisho ya kazi ya ushindi ingeanzia Israeli, basi kazi ya ushindi isingekuwa na maana. Kazi ni ya umuhimu zaidi wakati ikiwa inafanyika nchini humu, inapofanyika kwenu enyi watu. Ninyi ni watu wanyenyekevu zaidi, watu walio na hadhi ndogo zaidi. Ninyi ni watu katika ngazi ya chini kabisa ya jamii hii na ninyi ndio ambao walimtambua Mungu kwa kiwango cha chini sana mwanzoni . Ninyi ni watu ambao wamekwenda mbali zaidi na Mungu, na ni wale ambao wamejeruhiwa vibaya. Kwa sababu hatua hii ya kazi ni kwa ajili tu ya ushindi, je, haifai zaidi kuwachagua kuwa na ushuhuda ujao? Ikiwa hatua ya kwanza ya kazi ya ushindi haikufanyika kwenu, basi itakuwa vigumu kuendeleza kazi ya kushinda inayokuja, kwa sababu kazi ya ushindi ambayo itafuatia itafikia matokeo kulingana na ukweli kuwa hii Kazi inafanyika leo. Kazi ya ushindi leo ni mwanzo tu wa kazi nzima ya ushindi.Ninyi ni kundi la kwanza kushindwa; ninyi ni wawakilishi wa wanadamu wote ambao wanashindwa. Ikiwa kuna mtu yeyote aliye na ufahamu kweli, ataona kwamba kazi yote ambayo Mungu anafanya leo ni kubwa, kwamba Mungu hawaruhusu tu watu kujua uasi wao wenyewe, Yeye pia hufunua hali zenu. Madhumuni na maana ya maneno Yake sio kuwafanya watu kuwa wabaya, wala sio kusababisha watu kuanguka chini. Ni ili kwamba waweze kupata ufunuo na kuokolewa kupitia maneno Yake; ni kufufua roho ya mwanadamu kupitia maneno Yake. Kutoka wakati wa uumbaji wa dunia mpaka sasa, mwanadamu daima ameishi chini ya utawala wa Shetani, bila kujua kwamba kuna Mungu na kutoamini kuna Mungu. Kwamba watu hawa wanaweza kuingizwa katika wokovu mkuu wa Mungu na kuinuliwa sana na Mungu kwa kweli inaonyesha upendo wa Mungu; wale wanaoelewa kweli wote watafikiria kwa njia hii. Je, watu hao wasio na ufahamu watafikiria vipi? "Ah, Mungu anasema sisi ni uzao wa Moabu. Alisema Mwenyewe kuwa sisi ni wana wa Moabu. Je, tunaweza kuwa wazuri? Ni nani aliyetufanya sisi kuwa wana wa Moabu? Ni nani ambaye alitufanya hapo awali kumuasi Yeye sana? Mungu amekuja kutuhukumu; je, huoni jinsi Mungu alivyotuhukumu daima tangu mwanzo? Kwa kuwa tumemkataa Mungu tunapaswa kuadibiwa kwa njia hii.” "Je, maneno haya ni sahihi? Leo Mungu anawahukumu, na kuwaadibu, na kuwashutumu, lakini jueni kwamba shutuma yako ni ili kukufanya kuweza kujijua. Shutuma, laana, hukumu, kuadibu—haya yote ni ili kwamba uweze kujijua, ili tabia yako iweze kubadilika, na, zaidi ya hayo, ili uweze kujua thamani yako, na kutambua kwamba vitendo vyote vya Mungu ni vyenye haki, na kulingana na tabia Yake na mahitaji ya kazi Yake, kwamba Anafanya kazi kulingana na mpango Wake kwa wokovu wa mwanadamu, na kwamba Yeye ndiye Mungu mwenye haki anayempenda mwanadamu, na kumwokoa mwanadamu, na Anayemhukumu na kumwadibu mwanadamu. Kama utajua tu kwamba wewe ni mwenye hadhi ya chini, na kwamba umepotoka na hutii, lakini hujui kwamba Mungu angependa kuweka wazi wokovu Wake kupitia kwa hukumu na kuadibu ambako Anafanya ndani yako leo, basi huna njia yoyote ya kupitia haya, isitoshe huwezi kuendelea mbele. Mungu hajaja kuua, au kuangamiza, lakini kuhukumu, kulaani, kuadibu, na kuokoa. Kabla ya hitimisho ya mpango Wake wa usimamizi wa miaka 6,000—kabla ya Yeye kuweka wazi mwisho wa kila aina ya binadamu—kazi ya Mungu ulimwenguni ni kwa ajili ya wokovu, yote haya ni ili kuwafanya wale wanaompenda Yeye kukamilika kabisa, na kuwarejesha katika utawala Wake. (The sorce says “Please translate this part”) Kwenye macho ya mwanadamu, wokovu ni upendo wa Mungu, na upendo wa Mungu hauwezi kuwa kuadibu, kuhukumu, na kulaani; wokovu lazima uwe na upendo, huruma, na, zaidi ya hayo, maneno ya faraja, na lazima wokovu uwe na baraka zisizo na mipaka kutoka kwa Mungu. Watu husadiki kwamba wakati Mungu anapomwokoa mwanadamu Anafanya hivyo kwa kumgusa yeye na kumfanya yeye kuutoa moyo wake na kumpa Yeye kupitia kwa baraka na neema Zake. Hivyo ni kusema, Anapomgusa mwanadamu Anamwokoa yeye. Wokovu kama huu ni wokovu ambao shughuli ya biashara inafanywa. Pale tu ambapo Mungu atampa yeye mara mia ndipo mwanadamu anaponyenyekea kwa jina la Mungu, na kulenga kuwa na mienendo mizuri mbele ya Mungu na kumletea Yeye utukufu. Haya si mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu. Mungu amekuja kufanya kazi ulimwenguni ili kumwokoa mwanadamu aliyepotoka—hakuna uongo katika haya; kama upo, Asingefanya kazi Yake yeye Mwenyewe. Kitambo, mbinu Zake za wokovu zilikuwa kuonyesha upendo na huruma mkuu, kiasi cha kwamba Alijitolea Yake yote kwa Shetani ili naye aweze kuwapata wanadamu wote. Leo haifanani kamwe na kitambo: Leo, wokovu wako unatokea kwenye wakati wa siku za mwisho, wakati wa uainishaji wa kila mmoja kulingana na aina yake; mbinu za wokovu wako si upendo wala huruma, lakini kuadibu na hukumu ili mwanadamu aweze kuokolewa kabisa. Hivyo basi, kila kitu unachopokea ni kuadibu, hukumu, na kupiga bila huruma, lakini jua kwamba katika kupiga huku kusiko na huruma hakuna hata adhabu ndogo zaidi, jua kwamba licha ya namna ambavyo maneno haya yanavyoweza kuwa makali, kile kinachokupata ni maneno machache yanayoonekana kutokuwa na huruma kabisa kwako, na jua kwamba, licha ya namna ambavyo hasira Yangu itakavyokuwa, kile kitakachokujia bado ni maneno ya mafunzo, na sinuii kukudhuru, au kukuua. Je, haya yote ni ukweli, sivyo? Jua kwamba leo, haijalishi kama kutakuwa na kuhukumu kwa haki au utakasaji usio na huruma na kuadibu, yote haya ni kwa minajili ya wokovu. Haijalishi kama leo kunao uainishaji wa kila mmoja kulingana na aina yake, au uwekaji wazi wa aina za mwanadamu, matamko yote ya Mungu na kazi ni kwa ajili ya kuwaokoa wale wanaompenda Mungu kwa dhati. Kuhukumu kwa haki ni kwa ajili ya kumtakasa mwanadamu, utakasaji usio na huruma ni kwa ajili ya kumsafisha mwanadamu, maneno makali au kuadibu yote ni kwa ajili ya kutakasa, na kwa minajili ya wokovu. Na hivyo, mbinu ya leo ya wokovu haifanani na ya kitambo. Leo, kuhukumu kwa haki kunakuokoa wewe, na ni zana nzuri pia ya kumuainisha kila mmoja wenu kulingana na aina, na kuadibu kusiko na huruma kunawaletea wokovu mkubwa—na ni kipi ambacho unahitajika kusema mbele ya kuadibu na kuhukumu huku? Je, hujafurahia wokovu kutoka mwanzo hadi mwisho? Nyote mmeona Mungu mwenye mwili na kutambua kudura na hekima Yake; zaidi ya hayo, umepitia hali ya kupigwa na kufundishwa nidhamu mara kwa mara. Lakini je, hujapokea pia neema kubwa? Je, baraka zako si kubwa zaidi kuliko za mtu yeyote mwengine? Neema zako ni nyingi zaidi kuliko utukufu na utajiri ulioofurahiwa na Sulemani! Hebu fikiria: Kama nia Yangu ya kuja ulimwenguni ingekuwa ni kushutumu na kukuadhibu wewe, na wala si kukuokoa, je, siku zako zingedumu kwa muda mrefu? Mngeweza, enyi viumbe wenye dhambi wa mwili na damu, kuishi hadi leo? Kama ingekuwa tu ni kwa ajili ya kuwaadhibu nyinyi, kwa nini Nikawa mwili na kuanza kushughulikia shughuli kubwa kama hiyo? Je, lisingekuwa neno moja tu ambalo Ningetumia kuwaadhibu nyinyi viumbe wenye kufa tu? Ningekuwa bado na akili ya kukuangamiza baada ya kukushutumu? Je, bado husadiki maneno haya Yangu? Ningeweza kumwokoa mwanadamu kupitia tu kwa upendo na huruma? Au Ningetumia tu kusulubishwa kwa minajili ya kumwokoa mwanadamu? Je, tabia Yangu yenye haki si nzuri zaidi ya kumfanya mwanadamu kuwa mtiifu kabisa? Je, haiwezi kabisa kumwokoa mwanadamu zaidi?
Ingawa maneno Yangu yanaweza kuwa makali, yote yanasemwa kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu, kwa kuwa Ninazungumza tu maneno na sio kuuadhibu mwili wa mwanadamu. Maneno haya humsababisha mwanadamu kuishi katika nuru, kujua kwamba mwanga upo, kujua kwamba mwanga ni wa thamani, hata zaidi kujua jinsi maneno haya yalivyo na manufaa kwa mtu, na kujua kwamba Mungu ni wokovu. Ingawa Nimesema maneno mengi ya kuadibu na hukumu, hayajafanywa kwako katika vitendo. Nimekuja kufanya kazi Yangu, kuzungumza maneno Yangu na, ingawa maneno Yangu yanaweza kuwa magumu, yanasemwa kwa hukumu ya upotovu na uasi wako. Madhumuni Yangu ya kufanya hili yanabaki kumwokoa mtu kutoka kwa utawala wa Shetani, kutumia maneno Yangu ili kumwokoa mwanadamu; Kusudi Langu sio kumdhuru mwanadamu kwa maneno Yangu. Maneno Yangu ni makali ili matokeo yaweze kupatikana kutoka katika Kazi Yangu.Ni katika kufanya kazi kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kujijua na anaweza kujitenga mbali na tabia yake ya uasi. Umuhimu mkubwa zaidi wa kazi ya maneno ni kuwaruhusu watu kuweza kutia katika matendo ukweli baada ya kuuelewa ukweli, kutimiza mabadiliko katika tabia yao, na kutimiza maarifa kuhusu wao wenyewe na kazi ya Mungu. Mbinu za kufanya kazi tu kupitia kwa kuongea ndizo zinazoweza kuleta mawasiliano kuhusu uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu, maneno tu ndiyo yanayoweza kuelezea ukweli. Kufanya kazi kwa njia hii ndiyo mbinu bora zaidi ya kumshinda mwanadamu; mbali na matamko ya maneno, hakuna mbinu nyingine inayoweza kumpatia mwanadamu uelewa wa wazi zaidi wa ukweli na kazi ya Mungu, na hivyo basi katika awamu Yake ya mwisho ya kazi, Mungu anazungumza naye mwanadamu ili kuweza kuwa wazi kwa mwanadamu kuhusu ukweli na siri zote ambazo haelewi, na hivyo basi kumruhusu kufaidi njia ya kweli na uzima kutoka kwa Mungu na kisha kutosheleza mapenzi ya Mungu. Madhumuni ya kazi ya Mungu juu ya mwanadamu ni ili aweze kukidhi mapenzi ya Mungu na yote yamefanywa kumwokoa mwanadamu, kwa hivyo wakati wa wokovu wake wa mwanadamu Yeye hafanyi kazi ya kumwadibu mtu. Wakati wa wokovu wa mwanadamu, Mungu haadhibu maovu au kulipa mema, wala Yeye hafunui hatima ya aina zote za watu. Badala yake, ni baada tu ya hatua ya mwisho ya kazi Yake kukamilishwa ndipo basi Atafanya kazi ya kuadhibu maovu na kulipa mazuri, na kisha basi ndipo Atafunua mwisho wa aina zote za watu. Wale ambao wanaadhibiwa hakika hawataweza kuokolewa, wakati wale waliookolewa watakuwa wale ambao wamepata wokovu wa Mungu wakati wa wokovu Wake wa mwanadamu. Wakati wa kazi ya Mungu ya wokovu, wale wote ambao wanaweza kuokolewa wataokolewa kwa upeo wa juu zaidi, hakuna hata mmoja wao atakayeachwa, kwa kuwa kusudi la kazi ya Mungu ni kumwokoa mwanadamu. Wote ambao, wakati wa wokovu wa Mungu wa mwanadamu, hawawezi kufikia mabadiliko katika tabia zao, wote ambao hawawezi kumtii Mungu kabisa, wote watakuwa walengwa wa adhabu. Hatua hii ya kazi—kazi ya maneno—humwekea wazi mwanadamu njia na siri zote ambazo haelewi, ili mwanadamu aweze kuelewa mapenzi ya Mungu na mahitaji ya Mungu kwa mwanadamu, ili aweze kuwa katika ile hali ya kutia katika matendo maneno ya Mungu na kutimiza mabadiliko hayo katika tabia yake. Mungu huyatumia maneno tu kufanya kazi Yake, na hawaadhibu watu kwa sababu ni waasi kidogo, kwa sababu sasa ndio wakati wa kazi ya wokovu. Kama kila mtu ambaye alikuwa muasi angeadhibiwa, basi hakuna mtu ambaye angepata fursa ya kuokolewa; wote wangeadhibiwa na kuanguka kuzimuni. Kusudi la maneno ya yanayomhukumu mtu ni kumwezesha kujitambua na kumtii Mungu; sio kwao kuadhibiwa kwa njia ya hukumu ya maneno. Wakati wa kazi ya maneno, watu wengi watafunua uasi wao na kutotii kwao, na wataweka wazi kutotii kwao kwa Mungu mwenye mwili. Lakini Yeye hatawaadhibu watu hawa wote kwa sababu ya hili, badala yake Atawatupa kando wale ambao wamepotoka kabisa na ambao hawawezi kuokolewa. Atautoa mwili wao kwa Shetani, na katika hali kadhaa, kumaliza mwili wao. Wale ambao wanaachwa wataendelea kufuata na kupitia kushughulikiwa na kupogolewa. Ikiwa wanapofuata hawawezi kukubali kushughulikiwa na kupogolewa na wanazidi kupotoka, basi watu hawa watapoteza nafasi zao za wokovu. Kila mtu ambaye amekubali ushindi wa maneno atakuwa na nafasi nzuri ya wokovu. Wokovu wa Mungu wa kila mmoja wa watu hawa huwaonyesha upole Wake mkubwa, kumaanisha kwamba wanaonyeshwa uvumilivu mkubwa. Mradi watu warudi kutokakatika njia mbaya, mradi kama waweze kutubu, basi Mungu atawapa fursa ya kupata wokovu wake. Watu wanapoasi dhidi ya Mungu kwanza, Mungu hana hamu ya kuwaua, lakini badala yake Anafanya yote Anayoweza kuwaokoa. Ikiwa mtu kwa kweli hana nafasi ya wokovu, basi Mungu atamtupa pembeni. Kwamba Mungu si mwepesi wa kumwadhibu mtu ni kwa sababu Anataka kuwaokoa wale wote ambao wanaweza kuokolewa. Yeye huwahukumu, huwapa nuru na kuwaongoza watu tu kwa maneno, na Hatumii fimbo kuwaua. Kutumia maneno kuwaokoa watu ni kusudi na umuhimu wa hatua ya mwisho ya kazi.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni