Sura ya 6 Aina Mbalimbali za Utofautishaji Ambazo Unafaa Kumiliki katika Kusadiki Kwako kwa Mungu
6. Utofautishaji Kati ya Viongozi wa Kweli na wa Uongo, na Kati ya Wachungaji wa Kweli na wa Uongo
Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya mtenda kazi mwenye sifa inaweza kuwaleta watu katika njia sahihi na kuwaruhusu kuzama kwa kina katika ukweli. Kazi anayofanya inaweza kuwaleta watu mbele ya Mungu. Aidha, kazi anayofanya inaweza kutofautiana kutoka kwa mtu hadi mtu mwingine na wala haifungwi na kanuni, inawapa watu uhuru. Aidha, wanaweza kukua katika uzima kwa taratibu, wakiendelea kukua na kuzama ndani kabisa katika ukweli. Kazi ya mtenda kazi asiyehitimu haifikii kiwango hiki; kazi yake ni ya kipumbavu. Anaweza kuwaleta watu katika kanuni tu; kile anachowataka watu kufanya hakitofautiani kati ya mtu na mtu mwingine; hafanyi kazi kulingana na mahitaji halisi ya watu.
Katika kazi ya aina hii kunakuwa na kanuni nyingi sana na mafundisho mengi sana, na haiwezi kuwaleta watu katika uhalisia au katika hali ya kawaida ya kukua katika uzima. Inaweza kuwawezesha watu tu kusimama kwa kanuni chache zisizokuwa na maana. Uongozi wa namna hii unaweza tu kuwapotosha watu. Anakuongoza ili uwe kama yeye; anaweza kukuleta katika kile anacho na kile alicho. Kwa wafuasi kutambua endapo viongozi wana sifa, jambo la muhimu ni kuangalia njia wanayoiongoza na matokeo ya kazi yao, na kuangalia iwapo wafuasi wanapokea kanuni kulingana na ukweli, na kama wanapokea namna ya kutenda kunakowafaa wao ili waweze kubadilishwa. Unapaswa kutofautisha kati ya kazi tofauti za aina tofauti za watu; haupaswi kuwa mfuasi mpumbavu. Hili linaathiri suala la kuingia kwako. Kama huwezi kutofautisha ni uongozi wa mtu yupi una njia na upi hauna, utadanganywa kwa urahisi. Haya yote yana athari ya moja kwa moja katika maisha yako.
kutoka katika “Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Lazima uwe na ufahamu wa hali nyingi ambazo watu watakuwa ndani wakati Roho Mtakatifu anafanya kazi juu yao. Hasa, wale wanaofanya kazi kwa namna sawa kumtumikia Mungu lazima wawe na ufahamu bora zaidi wa hali nyingi zinazoletwa na kazi ambayo Roho Mtakatifu hutekeleza kwa wanadamu. Ikiwa unasema tu kuhusu uzoefu mwingi na njia nyingi za kuingia ndani, inaonyesha kwamba uzoefu wako unaegemea upande mmoja sana. Bila kujua hali yako ya kweli au kufahamu kanuni za ukweli, haiwezekani kufikia mabadiliko katika tabia. Bila kujua kanuni za kazi ya Roho Mtakatifu au kuelewa matokeo yatokayo hapo, itakuwa vigumu kutambua kazi ya pepo wabaya. Lazima ufunue kazi ya pepo wabaya na mawazo ya wanadamu na uende moja kwa moja kwenye kiini cha suala hili; lazima pia uonyeshe mikengeuko mingi katika utendaji wa watu au matatizo katika kumwamini Mungu ili waweze kuyatambua. Kwa kiwango cha kidogo sana, lazima usiwafanye kuhisi hasi au wasiojishughulisha. Hata hivyo, lazima uelewe shida ambazo zipo kwa watu wengi bila upendeleo, hupaswi kuwa bila busara au “ujaribu kumfunza nguruwe kuimba”; hiyo ni tabia ya upumbavu. Ili kutatua matatizo mengi ya wanadamu, lazima uelewe elimumwendo ya kazi ya Roho Mtakatifu, lazima uelewe jinsi Roho Mtakatifu anavyotekeleza kazi kwa watu tofauti, lazima uelewe matatizo ya wanadamu, upungufu wa wanadamu, ubaini masuala muhimu ya shida, na kufikia chanzo cha tatizo, bila mkengeuko au makosa. Ni mtu wa aina hii tu ndiye aliyestahiki kuratibu kumhudumia Mungu.
kutoka katika “Kile Ambacho Mchungaji wa Kutosha Anapaswa Kujiandaa Nacho” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wanaomhudumia Mungu wanapaswa kuwa marafiki wema wa Mungu, wanapaswa kumfurahisha Mungu, na kuwa na uaminifu wa hali ya juu kwa Mungu. Bila kujali iwapo unatenda bila kuonekana na watu, au mbele ya watu, unaweza kupata furaha ya Mungu mbele za Mungu, unaweza kusimama imara mbele za Mungu, na bila kujali jinsi watu wengine wanavyokutendea, wewe huifuata njia yako mwenyewe kila mara, na kuushughulikia kwa makini mzigo wa Mungu. Mtu wa aina hii pekee ndiye rafiki mwema wa Mungu. Marafiki wema wa Mungu wanaweza kumhudumia Yeye moja kwa moja kwa sababu wamepewa agizo kuu la Mungu, na mzigo wa Mungu, wao wanaweza kuuchukulia moyo wa Mungu kama moyo wao wenyewe, na mzigo wa Mungu kama mzigo wao wenyewe, na hawazingatii iwapo watafaidi au watapoteza matarajio: Hata wasipokuwa na matarajio, na hawatafaidi chochote, watamwamini Mungu daima kwa moyo wa upendo. Kwa hivyo, mtu wa aina hii ni rafiki mwema wa Mungu. Marafiki wema wa Mungu ni wasiri Wake pia; ni wasiri wa Mungu pekee ndio wanaoweza kushiriki katika kutotulia Kwake, matamanio Yake, na ingawa mwili wao una uchungu na ni mdhaifu, wanaweza kuvumilia uchungu na kuacha kile wanachokipenda ili kumridhisha Mungu. Mungu huwapa watu wa aina hii mizigo mingi, na kile ambacho Mungu atafanya hudhihirishwa kupitia kwa watu hawa. Yaani, watu hawa wanapendwa na Mungu, wao ni watumishi wa Mungu wanaoupendeza moyo Wake, na ni watu wa aina hii pekee ndio wanaoweza kutawala pamoja na Mungu.
kutoka katika “Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Mtu kama huyu daima anakuwa na mtazamo wa kikatili kwa kazi mpya ya Mungu, hajawahi kuonyesha nia hata ndogo ya kutii, na hajawahi kuonyesha utii ama kujinyenyekeza kwa furaha. Anajisifu mbele ya wengine na kamwe haonyeshi utii kwa mwingine. Mbele ya Mungu, anajiona kuwa hodari zaidi katika kuhubiri neno na mwenye ujuzi zaidi katika kufanya kazi kwa wengine. Kamwe hatupi “hazina” anazomiliki tayari, lakini anazichukua kama vitu vinavyorithiwa kwa familia vya kuabudiwa, vya kuhubiri kuhusu wengine, na huvitumia kuhutubia wale wapumbavu wanaomwabudu. Hakika kuna baadhi ya watu kama hawa kanisani. Inaweza kusemwa kwamba wao ni “mashujaa wasioshindwa,” kizazi baada ya kizazi kinachokaa kwa muda mfupi ndani ya nyumba ya Mungu. Wanachukua kuhubiri neno (mafundisho ya dini) kama wajibu wao wa juu zaidi. Mwaka baada ya mwaka na kizazi baada ya kizazi, wao huenenda kwa nguvu wakitekeleza wajibu wao “mtakatifu na usiokiukwa”. Hakuna anayethubutu kuwaguza na hakuna mtu hata mmoja anayethubutu kuwashutumu kwa uwazi. Wanakuwa “wafalme” katika nyumba ya Mungu, wakienea kote wakiwaonea wengine kutoka enzi hadi enzi.
kutoka katika “Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watapatwa na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi katika akili ya mwanadamu inafikiwa kwa urahisi sana na mwanadamu. Wachungaji na viongozi katika ulimwengu wa kidini, kwa mfano, wanategemea karama zao na nafasi zao katika kufanya kazi zao. Watu wanaowafuata kwa muda mrefu wataambukizwa na karama zao na kuvutwa na vile walivyo. Wanalenga karama za watu, uwezo na maarifa ya watu, na wanamakinikia mambo ya kimiujiza na mafundisho mengi yasiyokuwa na uhalisi (kimsingi, haya mafundisho ya kina hayawezi kutekelezeka). Hawalengi mabadiliko ya tabia za watu, badala yake wanalenga kuwafundisha watu uwezo wao wa kuhubiri na kufanya kazi, kuboresha maarifa ya watu na mafundisho makuu ya kidini. Hawalengi kuona ni kwa kiasi gani tabia ya watu imebadilika au ni kwa kiasi gani watu wanauelewa ukweli. Wala hawajali kuhusu viini vya watu, wala kujua hali za watu za kawaida na zisizo za kawaida. Hawapingi mitazamo ya watu au kufunua fikira zao, sembuse kurekebisha hali yao ya dhambi. Watu wengi wanaowafuata wanahudumia kwa karama zao za asili, na kile wanachokionyesha ni maarifa na ukweli wa kidini usioeleweka, ambao hauambatani na uhalisi na hauwezi kabisa kuwapa watu uzima. Kwa kweli, kiini cha kazi yao ni kulea talanta, kumlea mtu kuwa mhitimu mwenye talanta aliyemaliza mafunzo ya kidini ambaye baadaye anakwenda kufanya kazi na kuongoza.
kutoka katika “Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kumtumikia Mungu si kazi rahisi. Wale ambao tabia yao potovu haibadiliki hawawezi kamwe kumhudumia Mungu. Kama tabia yako haijahukumiwa na kuadibiwa na neno la Mungu, basi tabia yako bado inamwakilisha Shetani. Hii inatosha kuthibitisha kwamba huduma yako kwa Mungu ni kutokana na nia yako nzuri wewe binafsi. Ni huduma inayotokana na asili yako ya kishetani. Unamhudumia Mungu na hulka yako ya kiasili, na kulingana na mapendeleo yako ya kibinafsi; na zaidi, unaendelea kufikiria kwamba Mungu anapenda chochote kile unachopenda kufanya, na kwamba Mungu anachukia chochote kile ambacho hupendi kufanya, na unaongozwa kabisa na mapendeleo yako binafsi katika kazi yako. Je, huku kunaweza kuitwa kumhudumia Mungu? Hatimaye tabia yako ya maisha haitabadilishwa hata chembe; badala yake, utakuwa msumbufu hata zaidi kwa sababu umekuwa ukimhudumia Mungu, na hii itafanya tabia yako potovu kukita mizizi zaidi. Kwa njia hii, utaendeleza kwa ndani sheria kuhusu huduma kwa Mungu zitokanazo kimsingi na hulka yako binafsi, na uzoefu unaotokana na kuhudumu kwako kulingana na tabia yako binafsi. Hili ni funzo kutokana na uzoefu wa kibinadamu. Ni falsafa ya maisha ya binadamu. Watu kama hawa ni wa Mafarisayo na wale wajumbe wa kidini. Kama hawatawahi kuzinduka na kutubu, basi hatimaye watageuka na kuwa wale Makristo wa uwongo watakaoonekana katika siku za mwisho, na watu kuwa wanaowadanganya wanadamu. Makristo wa uwongo na wadanganyifu waliozungumziwa watatokana na mtu wa aina hii. Kama wale wanaomhudumia Mungu watafuata hulka yao na kutenda kulingana na mapenzi yao binafsi, basi wamo katika hatari ya kutupwa nje wakati wowote. Wale wanaotumia miaka yao mingi ya uzoefu kwa kumhudumia Mungu ili kutega mioyo ya watu, kuwasomea na lengo la kusimanga na kuwadhibiti na wale katu hawatubu, katu hawakiri dhambi zao, katu hawakatai manufaa ya cheo—watu hawa wataanguka mbele ya Mungu. Hawa ni watu walio kama Paulo, waliojaa majivuno ya vyeo vyao na wanaoonyesha ukubwa wao. Mungu hatawakamilisha watu kama hawa. Aina hii ya huduma huzuia kazi ya Mungu. Watu wanapenda kushikilia vitu vya kale. Wanashikilia fikira za kale, wanashikilia vitu vya kale. Hiki ni kizuizi kikuu katika huduma yao. Kama huwezi kuvitupa vitu hivi, vitu hivyo vitayakaba maisha yako yote. Mungu hatakupongeza, hata kidogo, hata kama utaivunja miguu yako au mgongo wako ukitia bidii, au hata ukifa katika “huduma” ya Mungu. Kinyume cha mambo ni kwamba: Atasema kwamba wewe ni mtenda maovu.
kutoka katika “Njia ya Huduma ya Kidini Lazima Ipigwe Marufuku” katika Neno Laonekana katika Mwili
Unadhani kwamba kuwa na maarifa ni sawa na kuwa na ukweli? Je, huo si mtazamo uliokanganywa? Unaweza kuzungumza maarifa mengi kama mchanga ulivyo ufuoni, lakini hakuna yaliyo na njia ya kweli. Katika hili, je huwadanganyi watu? Je, unafanya maonyesho matupu yasiyo na maana? Mienendo yote kama hii ni ya madhara kwa watu! Kadiri nadharia inavyokuwa ya juu, ndivyo inavyokosa uhalisi zaidi, na ndivyo inavyokosa zaidi uwezo wa kuwapeleka watu katika uhalisi; kadiri nadharia inavyokuwa ya juu, ndivyo inavyokufanya umuasi na kumpinga Mungu. Usizichukulie nadharia za kiwango cha juu kama hazina ya thamani; zina madhara, na hazina kazi yoyote! Pengine baadhi ya watu wanaweza kuzungumza juu ya nadharia za juu sana—lakini nadharia hizo hazina kitu chochote cha uhalisi, maana watu hawajazipitia wao binafsi, na kwa hiyo hawana njia ya kutenda. Watu kama hao hawawezi kumwongoza mwanadamu katika njia nzuri, na watawapotosha tu watu. Je, hii haileti madhara kwa watu? Angalau kabisa, unapaswa kuweza kutatua shida za sasa na kuwaruhusu watu kupata kuingia; hii tu ndiyo inachukuliwa kama ibada, na baada ya hapo ndipo utakuwa na sifa za kufaa kumfanyia Mungu kazi. Siku zote usizungumze maneno ya kifahari, ya ajabu, na usiwalazimishe watu kukutii wewe pamoja na vitendo vyako visivyofaa. Kufanya hivyo hakutaleta matokeo, na kunaweza kuongeza tu mkanganyiko wa watu. Kuwaongoza watu kwa namna hii kutaleta taratibu nyingi, ambazo zitafanya watu wakuchukie. Huu ni udhaifu wa wanadamu, na kwa kweli unadhalilisha.
kutoka katika “Sisitiza Uhalisi Zaidi” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wowote wasioelewa madhumuni ya kazi ya Mungu ni wale wanaompinga Mungu, na hata zaidi ya hayo ni wale waliofahamu madhumuni ya kazi ya Mungu lakini bado hawatafuti kumridhisha Mungu. Wale wanaosoma Biblia katika makanisa makubwa hukariri Biblia kila siku, lakini hakuna yeyote anayeelewa madhumuni ya kazi ya Mungu. Hakuna hata mmoja anayeweza kumwelewa Mungu; juu ya hayo, hakuna yeyote anayekubaliana na moyo wa Mungu. Wote hawana thamani, wanadamu waovu, kila mmoja akisimama juu kufundisha kuhusu Mungu. Ingawa wanalionyesha hadharani jina la Mungu, wanampinga kwa hiari. Ingawa wanajiita waumini wa Mungu, wao ni wale wanaokula mwili na kunywa damu ya mwanadamu. Wanadamu wote kama hao ni mashetani wanaoteketeza nafsi ya mwanadamu, pepo wakuu wanaowasumbua kimakusudi wanaojaribu kutembea katika njia iliyo sawa, na vizuizi vinavyozuia njia ya wanaomtafuta Mungu. Inagawa wao ni wenye “mwili imara,” wafuasi wao watajuaje kwamba wao ni wapinga Kristo wanaomwongoza mwanadamu katika upinzani kwa Mungu? Watajuaje kwamba hao ni mashetani hai wanaotafuta hasa nafsi za kuteketeza?
kutoka katika “Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kuhusu Sisi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni