9/10/2018

Imani Katika Mungu Haipasi Kuwa kwa ajili ya Kutafuta Amani na Baraka Pekee

Sura ya 7 Vipengele Vingine vya Ukweli Ambavyo Unafaa Kueleweka Katika Imani Yako kwa Mungu

5. Imani Katika Mungu Haipasi Kuwa kwa ajili ya Kutafuta Amani na Baraka Pekee

Maneno Husika ya Mungu:
Ni kitu gani ambacho mwanadamu amepokea tangu alipomwamini Mungu mara ya kwanza? Umejua kitu gani kumhusu Mungu? Umebadilika kiasi gani kwa sababu ya imani yako kwa Mungu? Sasa mnajua nyote ya kwamba imani ya mwanadamu katika Mungu si kwa ajili ya wokovu wa roho na ustawi wa mwili tu, wala si kuimarisha maisha yake kwa njia ya upendo wa Mungu, na kadhalika. Kama ilivyo sasa, kama unampenda Mungu kwa ajili ya ustawi wa mwili au furaha ya muda, basi hata kama, mwishoni, upendo wako kwa Mungu utafikia kilele chake na wewe hutaulizia kitu chochote, upendo huu unaoutafuta ni upendo mchafu na haumpendezi Mungu.  Wale wanaotumia upendo kwa Mungu kusitawisha maisha yao yasiyopendeza na kujaza utupu katika mioyo yao ni wale ambao wanataka kuishi katika raha, si wale ambao kweli wanatafuta kumpenda Mungu. Upendo wa aina hii ni kinyume na matakwa ya mtu, harakati ya ridhaa ya hisia, na Mungu hahitaji upendo wa aina hii. Upendo wako, basi, ni upendo wa aina gani? Ni kwa ajili gani unampenda Mungu? Je, ni kiasi gani cha upendo wa kweli, ulicho nacho kwa Mungu sasa? Upendo wa watu wengi kati yenu ni kama uliotajwa hapo awali. Upendo wa aina hii unaweza tu kudumisha hali kama ilivyo; hauwezi kufikia uthabiti wa milele, wala kuchukua mizizi katika mtu. Aina hii ya upendo ni ule wa ua ambalo halizai matunda baada ya kuchanuka na hatimaye kunyauka. Kwa maneno mengine, baada ya wewe kumpenda Mungu mara moja kwa jinsi hii na hakuna mtu wa kukuongoza kwa njia ya mbele, basi utaanguka. Kama unaweza tu kumpenda Mungu katika nyakati za kumpenda Mungu na kutofanya mabadiliko katika tabia ya maisha yako baadaye, basi utaendelea kufunikwa na ushawishi wa giza, bila uwezo wa kutoroka, na bila uwezo wa kujinasua kwa kufungwa na kupumbazwa na Shetani. Hakuna mtu kama huyu anayeweza kukubaliwa na Mungu; mwishowe, roho zao, nafsi na mwili bado ni mali ya Shetani. Hili ni bila ya shaka. Wale wote ambao hawawezi kukubaliwa kikamilifu na Mungu watarudi mahali pao pa awali, yaani, kwa Shetani, na watakwenda chini kwa ziwa liwakalo moto wa jahanamu kukubali hatua ya pili ya adhabu kutoka kwa Mungu. Wale wanaokubaliwa na Mungu ni wale ambao wanamkataa shetani na kutoroka kutoka kwa miliki ya Shetani. Watu kama wale watahesabiwa rasmi miongoni mwa watu wa ufalme. Hivi ndivyo watu wa ufalme huja kuwa.
kutoka katika “Maoni Wanayopaswa Kushikilia Waumini” katika Neno Laonekana katika Mwili
Leo, lazima uwe katika njia sahihi kwani unaamini katika Mungu wa vitendo. Kwa kuwa una imani katika Mungu, hupaswi tu kutafuta baraka, lakini pia kutafuta kumpenda Mungu na kumjua Mungu. Kupitia kwa kupata nuru kutoka Kwake na harakati yako mwenyewe, unaweza kula na kunywa neno Lake, kukuza ufahamu wa kweli kuhusu Mungu, na kuwa na upendo wa kweli kwa Mungu unaotoka moyoni mwako. Kwa maneno mengine, upendo wako kwa Mungu ni wa kweli zaidi, ambapo hakuna yeyote anayeweza kuharibu au kukuzuia kuonyesha upendo wako Kwake. Basi uko kwa njia ya kweli ya imani kwa Mungu. Inathibitisha kwamba wewe unamilikiwa na Mungu, kwani moyo wako umemilikiwa na Mungu na wala huwezi kumilikiwa na kitu kingine. Kutokana na tajriba yako, malipo uliyolipa, na kazi ya Mungu, wewe una uwezo wa kuendeleza upendo usioamriwa kwa Mungu. Kisha unawekwa huru kutoka kwa ushawishi wa Shetani na kuishi katika mwanga wa neno la Mungu. Ni wakati tu ambao umekuwa huru kutoka kwa ushawishi wa giza ndipo unaweza kuchukuliwa kuwa umempata Mungu. Katika imani yako kwa Mungu, lazima utafute lengo hili. Huu ni wajibu wa kila mmoja wenu. Hakuna anayelazimika kutosheka na mambo jinsi yalivyo. Hamuwezi kuwa na fikira aina mbili kwa kazi ya Mungu au uichukulie kwa wepesi. Mnapaswa kumfikiria Mungu katika mambo yako yote na wakati wote, na kufanya mambo yote kwa ajili yake. Na wakati mnasema au kufanya mambo, mnapaswa kutilia maanani maslahi ya nyumba ya Mungu kwanza. Ni hii tu ndio inayolingana na mapenzi ya Mungu.
kutoka katika “Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Sasa, watu wote wameona kuwa mtu anayemtumikia Mungu lazima asijue jinsi ya kuteseka kwa ajili yake tu, lakini hata zaidi, anapaswa kuelewa kwamba kuamini katika Mungu ni kwa ajili ya kutafuta kumpenda. Mungu kukutumia wewe si kwa ajili ya kukusafisha wewe tu au kukufanya uteseke, lakini ni kukufanya ujue matendo Yake, kujua umuhimu halisi wa maisha ya binadamu, na hasa kukufanya ujue kwamba kumtumikia Mungu si kazi rahisi. Kupata uzoefu wa kazi ya Mungu hakuhusu kufurahia neema Yake, lakini zaidi kuhusu kuteseka kwa sababu ya upendo wako Kwake. Kwa kuwa unafurahia neema ya Mungu, lazima pia ufurahie kuadibu Kwake—lazima upitie haya mambo yote. Unaweza kupata uzoefu wa nuru ya Mungu ndani yako, na unaweza pia kupitia ushughulikiaji Wake kwako na hukumu Yake. Kwa njia hiyo, unakuwa na uzoefu wa pande zote. Mungu amefanya kazi ya hukumu kwako, na Yeye pia amefanya kazi ya kuadibu kwako. Neno la Mungu limekushughulikia, lakini pia limekupa nuru, limekuangazia. Wakati unataka kukimbia, mkono wa Mungu bado unakuvuta kwa nguvu. Hizi kazi zote ni kukufahamisha kwamba kila kitu kuhusu mwanadamu kinadhibitiwa na Mungu. Unaweza kufikiri kuamini katika Mungu ni kuhusu mateso, au kufanya mambo mengi kwa ajili Yake, au kwa ajili ya amani ya mwili wako, au ni kwa ajili ya kila jambo kwenda vyema kwako, kwa ajili ya kila jambo kuwa la kustarehesha—lakini hakuna kati ya haya ambayo ni madhumuni ambayo watu wanapaswa kuwa nayo kwa ajili ya kuamini katika Mungu. Kama hayo ndiyo unayoamini, basi mtazamo wako si sahihi na huwezi kukamilishwa kabisa. Matendo ya Mungu, tabia ya Mungu ya haki, hekima Yake, maneno Yake, na maajabu Yake na kutoeleweka kwa kina Kwake yote ni mambo ambayo watu wanapaswa kuelewa. Tumia uelewa huu kuachana na maombi ya kibinafsi na pia matumaini ya mtu binafsi na dhana zilizo moyoni mwako. Ni kwa kuondoa haya tu ndiyo unaweza kukidhi masharti yanayotakiwa na Mungu. Ni kwa njia hii tu ndio unaweza kuwa na uzima na kumridhisha Mungu. Kumwamini Mungu ni kwa ajili ya kumridhisha Yeye na kuishi kwa kudhihirisha tabia ambayo Yeye anahitaji, ili matendo na utukufu Wake viweze kudhihirishwa kupitia kundi hili la watu wasiostahili. Huo ndio mtazamo sahihi wa kuamini katika Mungu, na pia lengo unalopaswa kutafuta. Unapaswa kuwa na mtazamo sahihi wa kuamini katika Mungu na kutafuta kupata maneno ya Mungu. Unahitaji kula na kunywa maneno ya Mungu, na kuwa na uwezo wa kuishi kwa kudhihirisha ukweli, na hasa kuona matendo Yake ya utendaji, kuona matendo Yake ya ajabu kotekote katika ulimwengu mzima, pamoja na kazi ya vitendo Yeye hufanya katika mwili. Kwa njia ya uzoefu wao halisi, watu wanaweza kufahamu ni jinsi gani hasa Mungu hufanya kazi Yake kwao na mapenzi Yake kwao ni yapi. Haya yote ni ili kuondoa tabia yao potovu ya kishetani. Jiondolee uchafu na udhalimu ndani yako, ondoa nia zako mbaya, na unaweza kuendeleza imani ya kweli katika Mungu. Kwa kuwa tu na imani ya kweli ndiyo unaweza kweli kumpenda Mungu. Unaweza tu kweli kumpenda Mungu kwa msingi wa imani yako Kwake. Je, unaweza kufanikisha kumpenda Mungu bila kumwamini? Kwa kuwa unaamini katika Mungu, huwezi kukanganyika kuhusu jambo hilo. Baadhi ya watu hujawa na nguvu mara tu wanapoona kwamba imani katika Mungu itawaletea baraka, lakini hupoteza nguvu zote mara tu wanapoona wanafaa kupitia kusafishwa. Je, huko ni kuamini katika Mungu? Mwishowe, lazima upate utiifu kamili na mzima mbele ya Mungu katika imani yako. Unaamini katika Mungu lakini bado una madai Kwake, una mawazo mengi ya kidini ambayo huwezi kuyapuuza, maslahi ya kibinafsi huwezi kuacha, na bado unatafuta baraka za mwili na unataka Mungu auokoe mwili wako, kuiokoa nafsi yako—haya yote ni maonyesho ya watu wenye mtazamo usio sahihi. Hata kama watu wenye imani za kidini wana imani katika Mungu, hawatafuti mabadiliko ya tabia, hawafuatilii maarifa ya Mungu, na wanatafuta tu maslahi ya miili yao. Wengi kati yenu wana imani ambazo ni za kikundi cha kusadiki kidini. Hiyo siyo imani ya kweli katika Mungu. Kuamini katika Mungu lazima watu wamiliki moyo wa kuteseka kwa ajili Yake na radhi ya kujitoa wenyewe. Isipokuwa wakikidhi haya masharti mawili haihesabiki kama imani katika Mungu, na hawatakuwa na uwezo wa kufikia mabadiliko ya tabia. Ni watu tu wanaotafuta ukweli kwa kweli, wanaotafuta maarifa ya Mungu, na kufuatilia maisha ndio wale ambao kweli wanaamini katika Mungu.
kutoka katika “Ni Lazima Wale Wanaofaa Kukamilishwa Wapitie Usafishaji” katika Neno Laonekana katika Mwili
Je sasa mnaelewa imani kwa Mungu ni nini? Je kuamini Mungu ni kuona ishara na maajabu? Je ni kupanda mbinguni? Kuamini Mungu sio rahisi hata kidogo. Zile desturi za kidini lazima zitakaswe; kufuata uponyaji wa wagonjwa na kukemea mapepo, kusisitiza ishara na maajabu, kutamani zaidi neema, amani na furaha ya Mungu, kufuata mandhari na raha za mwili—haya ni matendo ya kidini, na matendo haya ya aina hii ya kidini ni aina ya imani isiyo dhahiri. Leo, imani ya kweli kwa Mungu ni nini? Ni kukubali neno la Mungu kama ukweli wa maisha yako na kumjua Mungu kutoka kwa neno Lake ili uufikie upendo wa kweli Kwake. Kuondoa tashwishi: Imani katika Mungu ni ili uweze kumtii Mungu, kumpenda Mungu, na kufanya majukumu ambayo kiumbe wa Mungu anapaswa kufanya. Hili ndilo lengo la kuamini katika Mungu. Lazima upate ufahamu wa upendo wa Mungu, jinsi Mungu anavyostahili heshima, jinsi, katika viumbe Vyake, Mungu anafanya kazi ya wokovu na kuwafanya wakamilifu—hicho ndicho kiasi cha chini zaidi unachopaswa kuwa nacho katika imani yako kwa Mungu. Imani kwa Mungu hasa ni mabadiliko kutoka kwa maisha katika mwili kwenda kwa maisha ya kumpenda Mungu, kutoka maisha ya kiasili kwenda kwa maisha katika nafsi ya Mungu, ni kutoka kumilikiwa na Shetani na kuishi chini ya utunzaji na ulinzi wa Mungu, ni kuweza kupata kumtii Mungu na sio kuutii mwili, ni kukubali Mungu kuupata moyo wako wote, kukubali Mungu akufanye mkamilifu, na kujitoa kutoka kwa tabia potovu ya kishetani. Imani kwa Mungu kimsingi ni kwa kuwezesha nguvu na sifa za Mungu kudhihirishwa kwako, ili uweze kufanya mapenzi ya Mungu, na kutimiza mpango wa Mungu, na uweze kutoa ushuhuda kwa Mungu mbele ya Shetani. Imani kwa Mungu haipaswi kuwa kwa ajili ya kuona ishara na maajabu, wala haipaswi kuwa kwa ajili ya mwili wako mwenyewe. Inapaswa kuwa kwa ajili ya kutafuta kumjua Mungu, na kuweza kumtii Mungu, na kama Petro, kumtii mpaka kifo. Hili ndilo imani hiyo inapaswa kupata. Kula na kunywa neno la Mungu ni kwa ajili ya kumjua Mungu na kumtosheleza Mungu. Kula na kunywa neno la Mungu kunakupa maarifa kubwa ya Mungu, na ndipo tu utakapoweza kumtii Mungu. Unapomjua tu Mungu ndipo unapoweza kupenda Mungu, na kupatikana kwa lengo hili ndilo lengo la pekee mwanadamu anapaswa kuwa nalo katika imani yake kwa Mungu. Iwapo katika imani yako kwa Mungu, unajaribu kila wakati kuona ishara na maajabu, basi mtazamo wa imani hii kwa Mungu si sahihi. Imani kwa Mungu ni hasa kukubali neno la Mungu kama ukweli wa maisha. Ni kuweka tu katika matendo maneno ya Mungu kutoka kwa kinywa Chake na kuyatekeleza mwenyewe ndiko kupatikana kwa lengo la Mungu. Katika kuamini Mungu, mwanadamu anapaswa kutafuta kufanywa mkamilifu na Mungu, kuweza kujiwasilisha kwa Mungu, na kumtii Mungu kikamilifu. Iwapo unaweza kumtii Mungu bila kulalamika, kuyajali mapenzi ya Mungu, kupata kimo cha Petro, na kuwa na mtindo wa Petro ilivyozungumziwa na Mungu, basi hapo ndipo utakuwa umefanikiwa katika imani kwa Mungu, na itadhihirisha kuwa umepatwa na Mungu.
kutoka katika “Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Unatumai kwamba imani yako kwa Mungu haitakuwa na changamoto ama dhiki, ama mateso yoyote. Unafuata vile vitu ambavyo havina maana, na huambatanishi faida yoyote kwa maisha, badala yake kuweka mawazo ya fujo kabla ya ukweli. Huna maana! Unaishi kama nguruwe—kuna tofauti gani kati yako, nguruwe na mbwa? Je, hao wasiofuata ukweli na badala yake wanafuata mapenzi ya kimwili, si wote ni wanyama? Hao waliokufa na bila roho si wafu wanaotembea? Maneno mangapi yamenenwa kati yenu? Je, kazi kidogo imefanywa kati yenu? Ni kiasi gani nimetoa kati yenu? Na mbona hujapata chochote? Una nini cha kulalamikia? Je, si ni kweli kuwa hujapata chochote kwa sababu unapenda mwili sana? Na ni kwa sababu mawazo yako ni ya fujo sana? Je, si kwa sababu wewe ni mpumbavu sana? Kama huna uwezo wa kupata baraka hizi, unaweza kumlaumu Mungu kwa kutokukuokoa? Unachofuata ni cha kukuwezesha kupata amani baada ya kumwamini Mungu—watoto wako wawe huru kutokana na magonjwa, ili mme wako apate kazi nzuri, ili mwana wako apate mke mwema, binti wako apate mme anayeheshimika, ili ndume na farasi wako walime shamba vizuri, kwa mwaka wa hali ya anga nzuri kwa mimea yako. Hili ndilo unalolitafuta. Harakati yako ni kuishi kwa starehe, ili ajali isipate familia yako, ili upepo ukupite, ili uso wako usiguswe na changarawe, ili mazao ya familia yako yasipate mafuriko, ili usiguswe na majanga yoyote, kuishi katika mikono ya Mungu, kuishi kwenye kiota chenye joto. Mwoga kama wewe, anafuata mwili kila wakati—je, una moyo, una roho? Si wewe ni mnyama? Nakupa njia ya ukweli bila kukuuliza chochote, ilhali hauifuati. Je, wewe ni wale wamwaminio Mungu? Nahifadhi uhai wa ukweli wa binadamu juu yako, ila hauufuati. Je, una tofauti kati ya nguruwe na mbwa? Nguruwe hawafuati maisha ya binadamu, hawafuati kutakaswa, na hawaelewi maana ya maisha. Kila siku wanapokula na kushiba, wanalala. Nimekupa njia ya ukweli, ila hujaipata: Wewe u mkono mtupu. Je, unakubali kuendelea na maisha haya, maisha ya nguruwe? Umuhimu wa watu hao kuwa hai ni nini? Maisha yako ni ya kudharauliwa na kutoheshimika, unaishi huku ukiwa na uchafu na uzinzi, na hufuati lengo lolote; je, si maisha yako ni ya kutoheshimika kwa yote? Je, una ujasiri wa kumtazamia Mungu? Ukiendelea kuwa na uzoefu wa haya, je, si utakosa kupata chochote? Umepewa njia ya ukweli, lakini kama utaipata ama hapana inategemea na kutafuta kwako.
kutoka katika “Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Unampenda Mungu kiasi gani hasa leo? Na unajua kiasi gani hasa kuhusu yote ambayo Mungu amefanya ndani yako? Haya ni mambo unayopaswa kujifunza. Mungu anapowasili duniani, yote ambayo Amefanya ndani ya mwanadamu na kumkubalia mwanadamu kuona ni ili mwanadamu atampenda na kumjua Yeye kweli. Kwamba mwanadamu anaweza kuteseka kwa ajili ya Mungu na ameweza kufikia umbali huu ni, kuhusiana na jambo moja, kwa sababu ya upendo wa Mungu, na kuhusiana na jambo lingine, ni kwa sababu ya wokovu wa Mungu; zaidi ya hayo, ni kwa sababu ya kazi ya hukumu na kuadibu ambayo Mungu ametekeleza ndani ya mwanadamu. Kama hamna hukumu, kuadibu, na majaribio ya Mungu, na kama Mungu hajawafanya mteseke, basi, kusema ukweli, ninyi hammpendi Mungu kweli. Kadri kazi ya Mungu ilivyo kuu zaidi ndani ya mwanadamu, na kadri mateso ya mwanadamu yalivyo makuu zaidi, ndivyo inavyoweza kuonyesha zaidi hasa vile kazi ya Mungu ilivyo ya maana, na ndivyo moyo wa mwanadamu unavyoweza kumpenda Mungu kweli zaidi. Unajifunzaje jinsi ya kumpenda Mungu? Bila mateso makali na usafishaji, bila majaribio ya kuumiza—na kama, zaidi ya hayo, yote ambayo Mungu alimpa mwanadamu ingekuwa neema, upendo, na rehema—je, ungeweza kufikia upendo wa kweli kwa Mungu? Kwa upande mmoja, wakati wa majaribio ya Mungu mwanadamu huja kujua kasoro zake, na huona kwamba yeye ni mdogo, wa kudharauliwa, na duni, kwamba hana chochote, na si kitu; kwa upande mwingine, wakati wa majaribio Yake Mungu humuumbia mwanadamu mazingira tofauti yanayomfanya mwanadamu aweze zaidi kupitia kupendeza kwa Mungu. Ingawa maumivu ni makubwa, na wakati mwingine yasiyoshindika—na hata hufikia kiwango cha huzuni ya kuseta—baada ya kuyapitia, mwanadamu huona vile kazi ya Mungu ndani yake ni ya kupendeza, na ni juu ya msingi huu tu ndiyo ndani ya mwanadamu huzaliwa upendo wa kweli kwa Mungu. Leo mwanadamu huona kwamba na neema, upendo na rehema ya Mungu pekee, hana uwezo wa kujijua mwenyewe kweli, sembuse kuweza kujua kiini cha mwanadamu. Ni kupitia tu usafishaji na hukumu ya Mungu, ni wakati tu wa usafishaji kama huo ndiyo mwanadamu anaweza kujua kasoro zake, na kujua kwamba hana chochote. Hivyo, upendo wa mwanadamu kwa Mungu umejengwa juu ya msingi wa usafishaji na hukumu ya Mungu. Kama wewe hufurahia tu neema ya Mungu, na maisha ya familia yenye amani au baraka yakinifu, basi hujampata Mungu, na imani yako kwa Mungu haijafaulu. Mungu tayari ametekeleza hatua moja ya kazi ya neema katika mwili, na tayari amempa mwanadamu baraka yakinifu—lakini mwanadamu hawezi kufanywa mkamilifu na neema, upendo, na rehema pekee. Katika uzoefu wa mwanadamu yeye hukabiliwa na baadhi ya upendo wa Mungu, na huuona upendo na rehema ya Mungu, lakini baada ya kupitia kwa kipindi fulani cha wakati, yeye huona kwamba neema ya Mungu na upendo na rehema Yake hayawezi kumfanya mwanadamu awe mkamilifu, na hayana uwezo wa kufichua kile ambacho ni potovu ndani ya mwanadamu, wala hayawezi kumwondolea mwanadamu tabia yake potovu, au kufanya kuwa kamilifu upendo na imani yake. Kazi ya Mungu ya neema ilikuwa kazi ya kipindi kimoja, na mwanadamu hawezi kutegemea kufurahia neema ya Mungu ili kumjua Mungu.
kutoka katika “Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wengi wa watu wanaomfuata Mungu wanashughulika tu na jinsi watakavyopata baraka nyingi na kuepuka majanga. Panapotajwa kazi na usimamizi wa Mungu, wanakaa kimya na kupoteza matamanio yao yote. Wanaamini kuwa kujua maswali ya kuchosha kama hayo hakutakuza maisha yao au kuwa na faida yoyote, na kwa hivyo hata kama wamezisikia habari kuhusu usimamizi wa Mungu, wanazichukulia kikawaida. Na hawazichukulii kama kitu cha thamani kukipokea, na hata kukikubali kama sehemu ya maisha yao. Watu kama hao wana nia sahili sana katika kumfuata Mungu: kupata baraka, na ni wazembe sana kuhudhuria chochote ambacho hakihusiani na nia hii. Kwao, kuamini kwa Mungu ili kupata baraka ndilo lengo halali na la thamani kwa imani yao. Hawaathiriwi na kitu chochote ambacho hakiwezi kutekeleza lengo hili. Hivyo ndivyo ilivyo na watu wengi wanaomfuata Mungu leo. Nia yao na motisha huonekana kuwa halali, kwa sababu wakati huo huo wa kumwamini Mungu, wanatumia rasilmali kwa ajili ya Mungu, wanajitolea kwa Mungu, na kutekeleza wajibu wao. Wanauacha ujana wao, wanajinyima kwa familia na kazi zao, na hata hukaa miaka mingi wakijishughulisha mbali na nyumbani kwao. Kwa ajili ya lengo lao kuu, wanabadili matamanio yao, wanabadili mtazamo wao wa nje wa maisha, hata kubadili njia wanayoitafuta, ila bado hawawezi kubadili nia ya imani yao kwa Mungu. Wanajishughulisha na usimamizi wa matamanio yao wenyewe; haijalishi njia iko mbali vipi, na ugumu na vikwazo vilivyo njiani, wanashikilia msimamo wao bila uoga hadi kifo. Ni nguvu zipi zinazowafanya wawe wa kujitolea kwa njia hii? Ni dhamiri yao? Ni sifa zao kubwa na nzuri? Ni kujitolea kwao kupigana na nguvu za maovu hadi mwisho? Ni imani yao wanayomshuhudia Mungu kwayo bila kutaka malipo? Ni utiifu wao ambao kwao wanajitolea kuacha kila kitu ili kutimiza mapenzi ya Mungu? Au ni roho yao ya kujitolea ambayo kwayo wanajinyima kila mara mahitaji badhirifu ya kibinafsi? Kwa watu ambao hawajawahi kujua kazi ya usimamizi wa Mungu kutoa zaidi, kwa hakika, ni muujiza wa ajabu! Hivi sasa, acha tusijadiliane kuhusu kiasi ambacho hawa watu wametoa. Tabia yao, hata hivyo, inastahili sana sisi kuichambua. Mbali na manufaa ambayo yanahusiana nao, je, kuna uwezekano wa kuweko kwa sababu nyingine ya wale hawajawahi kumfahamu Mungu kujitolea zaidi Kwake? Kwa hili, tunagundua tatizo ambalo halikutambuliwa hapo awali: Uhusiano wa mwanadamu na Mungu ni ule wa mahitaji ya kibinafsi yaliyo wazi. Ni uhusiano baina ya mpokeaji na mpaji wa baraka. Kwa kuiweka wazi, ni kama ule uhusiano baina ya mwajiriwa na mwajiri. Mwajiriwa hufanya kazi ili tu kupokea malipo yanayotolewa na mwajiri. Katika uhusiano kama huu, hakuna upendo, ila maafikiano tu, hakuna kupenda au kupendwa, ni fadhila na huruma tu; hakuna maelewano, ila kukubali na udanganyifu; hakuna mapenzi, ila ufa usioweza kuzibika. Mambo yanapofikia hapa, nani anaweza kubadilisha mwelekeo kama huu? Na ni watu wangapi ambao wanaweza kufahamu kwa kweli jinsi uhusiano huu ulivyokosa matumaini? Naamini kuwa watu wanapojitosa wenyewe kwenye raha ya kubarikiwa, hakuna anayeweza kukisia jinsi uhusiano na Mungu ulivyo wa aibu na usiopendeza.
Jambo la kusikitisha mno kuhusu imani ya wanadamu kwa Mungu ni kuwa wanadamu wanatekeleza usimamizi wao wenyewe katikati ya kazi ya Mungu na hawasikilizi usimamizi wa Mungu. Udhaifu mkubwa wa mwanadamu unaegemea katika jinsi, wakati huo huo anatafuta kujitoa kwa Mungu na kumwabudu, mwanadamu anaunda hatima yake kamilifu na kuhesabu jinsi ya kupokea baraka kubwa zaidi na hatima iliyo bora zaidi. Hata kama watu watafahamu jinsi walivyo wa kuhurumiwa, wenye chuki na walivyo ovyo, ni wangapi hapo ambao wanaweza kuachana na ukamilifu na matumaini yao? Na ni nani anayeweza kusimamisha hatua zake na kuacha kujifikiria yeye mwenyewe? Mungu Anawahitaji wale watakaojihusisha kwa karibu Naye kukamilisha usimamizi Wake. Anawahitaji wale ambao watatoa mawazo yao na mwili kwa ajili ya kazi Yake ya usimamizi ili kujitoa Kwake; Hawahitaji wale watakaoinua mikono yao na kuomba kutoka Kwake kila siku, na hata wale wanaotoa kidogo na kusubiri kulipwa kwa hilo tendo la kutoa. Mungu Anawadharau wale wanaotoa michango kidogo na kuridhika. Anawachukia wenye roho katili ambao hukataa kazi ya usimamizi Wake na hutaka tu kuongea kuhusu kwenda mbinguni na kupata baraka. Anachukia hata zaidi na wale ambao hufaidika na fursa inayowezeshwa na kazi Anayoifanya katika kuokoa wanadamu. Hii ni kwa sababu hawa watu hawajawahi kushughulishwa na Anachotarajia kupata Mungu kutokana na kazi Yake ya usimamizi. Wanashughulishwa tu na jinsi wanavyoweza kutumia hiyo fursa iliyowezeshwa na kazi ya Mungu ili kupata baraka. Hawajali roho Yake Mungu, kwa kuwa wanajishughulisha na mustakabali na hatima yao. Wale ambao wanakataa kazi ya usimamizi wa Mungu na hawana hata tamanio dogo katika jinsi Mungu Anavyowaokoa wanadamu na mapenzi Yake, wote wanafanya wapendavyo kando na kazi ya usimamizi wa Mungu. Tabia yao haikumbukwi na Mungu, na haikubaliwi na Mungu, na hata haiangaliwi kwa fadhila ya Mungu.
kutoka katika “Mwanadamu Anaweza Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu Pekee” katika Neno Laonekana katika Mwili
Je, ni nini unachopaswa kufuatilia sasa? Unachopaswa kufuatilia ni kama wewe una uwezo wa kuonyesha matendo ya Mungu, kama unaweza kuwa onyesho na udhihirisho wa Mungu, na kama wewe unastahili kutumiwa na Yeye. Ni kiasi gani cha kazi ambacho Mungu hakika amefanya kwako? Ni kiasi gani ambacho umeona, ni kiasi gani ambacho umegusa? Umepitia kiasi gani, na kuonja kiasi gani? Kama Mungu amekujaribu, kukushughulikia, au kukuadhibu—haijalishi chochote, matendo Yake na kazi Yake vimetekelezwa juu yako, lakini kama muumini katika Mungu, kama mtu ambaye ana nia ya kufuatilia kukamilishwa na Yeye, je, una uwezo wa kuonyesha matendo ya Mungu kwa njia ya uzoefu wako mwenyewe wa utendaji? Je, unaweza kuishi kwa kumdhihirisha Mungu kupitia kwa hili? Je, unaweza kuwakimu wengine kupitia uzoefu wako mwenyewe wa utendaji, na kugharimika mwenyewe kwa ajili ya kazi ya Mungu? Ili kuwa na ushuhuda kwa ajili ya matendo ya Mungu lazima uweze kueleza matendo Yake ni nini, na hili linafanywa kupitia uzoefu wako, maarifa, na mateso ambayo umevumilia. Je, wewe ni mtu ambaye huwa na ushuhuda kwa ajili ya matendo ya Mungu? Je, una matamanio haya? Kama unaweza kuwa na ushuhuda kwa ajili ya jina Lake, na hata zaidi, matendo Yake, pamoja na kuishi kwa kudhihirisha sura ambayo Yeye anataka kutoka kwa watu Wake, basi wewe ni shahidi wa Mungu. Je, unashuhudia kwa ajili ya Mungu vipi kwa hakika? Kutafuta na kuwa na hamu sana ya kuishi kwa kumdhihirisha Mungu, kuwa na ushahidi kupitia kwa maneno yako, kuwaruhusu watu kujua na kuona matendo Yake—kama kweli unatafuta yote haya, Mungu atakukamilisha. Ikiwa yote unayotafuta ni kukamilishwa na Mungu na kubarikiwa mwishoni kabisa, basi mtazamo wa imani yako katika Mungu si safi. Unapaswa kuwa ukifuatilia jinsi ya kuona matendo ya Mungu katika maisha ya kweli, jinsi ya kumridhisha Yeye wakati anafichua mapenzi Yake kwako, kutafuta jinsi ya kutoa ushuhuda kwa maajabu Yake na hekima, na jinsi ya kuonyesha nidhamu na ushughulikiaji Wake kwako. Haya yote ni mambo unayopaswa kuwa ukijaribu kuelewa sasa. Kama upendo wako kwa Mungu ni ili tu uweze kushiriki katika utukufu wa Mungu baada ya Yeye kukukamilisha, bado hautoshi na hauwezi kukidhi mahitaji ya Mungu. Unahitaji kuwa na uwezo wa kuwa na ushuhuda kwa matendo ya Mungu, kutosheleza mahitaji Yake, na kuwa na uzoefu wa kazi ambayo Amefanya kwa watu kwa njia ya utendaji. Iwe ni maumivu, machozi, au huzuni, lazima uyapitie yote kwa vitendo. Haya yote ni ili uweze kuwa shahidi wa Mungu. Je, ni chini ya utawala wa nini hasa sasa ndiyo unateseka na kutafuta ukamilifu? Je, ni kuwa na ushuhuda kwa ajili ya Mungu? Je, ni kwa ajili ya baraka za mwili au kwa ajili ya matarajio ya baadaye? Dhamira zako zote, motisha, na malengo ya kibinafsi ya kufuatilia lazima yarekebishwe na hayawezi kuongozwa na mapenzi yako mwenyewe.
kutoka katika “Ni Lazima Wale Wanaofaa Kukamilishwa Wapitie Usafishaji” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kuhusu Sisi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni