8/24/2018

Tofauti Kati Ya Kumfuata Mungu na Kuwafuata Watu

Sura ya 6 Aina Mbalimbali za Utofautishaji Ambazo Unafaa Kumiliki katika Kusadiki Kwako kwa Mungu

5. Tofauti Kati Ya Kumfuata Mungu na Kuwafuata Watu

Maneno Husika ya Mungu:
Kilicho na umuhimu mkuu katika kumfuata Mungu ni kwamba kila kitu kinapaswa kuwa kwa kadri ya maneno ya Mungu leo: Kama unafuatilia kuingia katika uzima au kutimiza mapenzi ya Mungu, kila kitu kinapaswa kulenga maneno ya Mungu leo. Kama kile ambacho unawasiliana kwa karibu na kufuatilia hakilengi maneno ya Mungu leo, basi wewe ni mgeni kwa maneno ya Mungu, na umeondolewa kabisa katika kazi ya Roho Mtakatifu. Kile ambacho Mungu hutaka ni watu ambao huzifuata nyayo Zake.  Haijalishi vile ulichoelewa awali ni cha ajabu na safi, Mungu hakitaki, na kama huwezi kuweka kando vitu hivyo, basi vitakuwa kizuizi kikubwa mno kwa kuingia kwako katika siku za baadaye. Wale wote ambao wanaweza kufuata nuru ya sasa ya Roho Mtakatifu wamebarikiwa. Watu wa enzi zilizopita pia walifuata nyayo za Mungu, ilhali hawangeweza kufuata mpaka leo; hii ndiyo baraka ya watu wa siku za mwisho. Wale ambao wanaweza kufuata kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu, na ambao wanaweza kuzifuata nyayo za Mungu, kiasi kwamba wamfuate Mungu popote Awaongozapo—hawa ni watu ambao wamebarikiwa na Mungu. Wale wasiofuata kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu hawajaingia katika kazi ya maneno ya Mungu, na haijalishi wanafanya kazi kiasi gani, au mateso yao ni makubwa vipi, au wanakimbia hapa na pale kiasi gani, hakuna linalomaanisha chochote kwa Mungu kati ya hayo, na Yeye hatawasifu.
kutoka katika “Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Fuata Nyayo za Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Watu wengi hawapati shangwe ndani ya ukweli, na vile vile katika hukumu. Badala yake, wao hupata furaha kwa nguvu na mali; watu kama hawa huchukuliwa kama wenye dharau. Wanatafuta tu madhehebu yaliyo na ushawishi duniani na wahubiri na waalimu wanaotoka katika seminari. Hata ingawa wameikubali njia ya ukweli, bado wako na shaka ndani yao na hawawezi kujitolea kikamilifu. Wanazungumzia kujinyima kwa sababu ya Mungu, lakini macho yao yamelenga tu wahubiri wakuu na waalimu, na Kristo anasukumwa pembeni. Mioyo yao imejaa umaarufu, mali na utukufu. Hawaamini kamwe kuwa mtu wa kawaida tu anaweza kuwashinda wengi vile, kwamba mtu asiye wa kutambulika kwa macho tu anaweza kukamilisha watu. Hawaamini kuwa hawa watu wasio na sifa, walio kwenye vumbi na vilima vya samadi ni watu waliochaguliwa na Mungu. Wanaamini kuwa kama watu wale wangekuwa vyombo vya wokovu Wake Mungu, basi mbingu na ardhi zitageuzwa juu na chini na watu wote watacheka kupindukia. Wanaamini kuwa iwapo Mungu atawachagua watu wasio na sifa yoyote wafanywe viumbe kamili, basi wao walio na sifa watakuwa Mungu Mwenyewe. Maoni yao yamechafuliwa na kutoamini; hakika, mbali na kutoamini, wao ni wanyama wasio na maana. Kwa maana wao wanathamini tu nyadhifa, hadhi kuu na mamlaka; wanachokithamini sana ni makundi makuu na madhehebu makuu. Hawana heshima hata kidogo kwa wale wanaoongozwa na Kristo; wao ni wasaliti tu waliomgeuka Kristo, kuugeuka ukweli na uhai.
Unachopendezwa nacho sio unyenyekevu wa Kristo, ila ni wale wachungaji wa uongo wenye umaarufu. Hupendi maarifa au kupendeza kwa Kristo, bali unapenda wale watukutu wanaojihusisha na ulimwengu mchafu. Unauchekelea uchungu wa Kristo asiyekuwa na pahali pa kulaza kichwa Chake, na badala yake unatamani maiti zinazokamata sadaka na kuishi katika uasherati. Hauko tayari kupokea mateso pamoja na Kristo, lakini unakimbilia mikononi mwa wapinzani wa Kristo hata ingawa wanakupa nyama za mwili pekee, barua na udhibiti pekee. Hata sasa, moyo wako bado unawaendea wao, sifa zao, hadhi zao, na ushawishi wao. Ilhali unazidi kuchukua mtazamo ambapo unaona kazi ya Kristo kuwa ngumu sana kukubali na huko tayari kuikubali. Hii ndiyo maana Ninasema hauna imani ya kumkubali Kristo. Sababu iliyokufanya Umfuate mpaka leo hii ni kuwa ulilazimishwa. Moyoni mwako milele mna picha nyingi refu; huwezi kusahau kila neno lao na matendo yao, au maneno yao ya ushawishi na mikono. Wao ni, katika moyo wenu, wakuu milele na tena mashujaa milele. Lakini hivi sivyo ilivyo na Kristo wa leo hii. Yeye moyoni mwako kamwe Hana umuhimu na kamwe Hastahili heshima. Kwa maana Yeye ni wa kawaida sana, mwenye ushawishi mdogo zaidi na Yuko mbali na ukuu.
kutoka katika “Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?” katika Neno Laonekana katika Mwili
Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:
Kumfuata Mungu humaanisha kumsikiliza Mungu katika kila kitu, kuitii mipango yote ya Mungu, kutenda kulingana na maneno ya Mungu, na kuyakubali yote yatokayo kwa Mungu. Kama unamwamini Mungu, basi unapaswa kumfuata Mungu; lakini, bila kulitambua, wakati wanapomwamini Mungu watu wengi huwafuata watu, ambalo ni jambo la mzaha na la kuhuzunisha. Kusema kwa kweli, yeyote watu wanayemfuata ni yule wanayemwamini. Ingawa watu wengine humwamini Mungu kwa jina tu, mioyoni mwao hakuna Mungu; katika mioyo yao, wao huwaabudu viongozi wao. Kuwasikiliza viongozi wa fulani, na kwenda hata kiasi cha kuikataa mipango ya Mungu, ni onyesho la kumwamini Mungu lakini kuwafuata watu. Kabla ya hawajapata ukweli, imani ya kila mtu imevurugika na kuchanganyikiwa kama hili. Wao hata hawajui kabisa maana ya kumfuata Mungu, na wanashindwa kusema tofauti kati ya kumfuata Mungu na kuwafuata watu. Wao huamini tu kwamba yeyote anayesema mafundisho mema, na ya juu, ni baba au mama yao; kwao, yeyote aliye na maziwa ni mama yao, na yeyote aliye na nguvu ni baba yao. Hivyo ndivyo jinsi wanavyosikitisha. Inaweza kusemwa kuwa, kwa hatua tofauti tofauti, hii ndiyo hali ya kiroho ya watu wengi.
Inamaanisha nini kumfuata Mungu? Na unawezaje kutia hilo katika vitendo? Kumfuata Mungu hakuhusishi tu kumwomba Mungu na kumsifu Mungu; kilicho muhimu zaidi ni kula na kunywa maneno ya Mungu na kuishi kulingana na maneno ya Mungu, kutenda kulingana na ukweli, kutafuta njia ya kupata uzoefu wa maisha katikati ya maneno ya Mungu, kukubali agizo la Mungu, kutekeleza kila moja ya wajibu wako vizuri, na kuitembea njia iliyo mbele yako kama unavyoongozwa na Roho Mtakatifu. Hasa, katika nyakati muhimu, wakati matatizo makuu yanapokufika, kuna hata haja kubwa zaidi ya kutafuta maana ya Mungu, kuwa na hadhari ya kudanganywa na mafundisho ya mwanadamu, na kutokuwa chini ya udhibiti wa mtu yeyote. “Kile kitokacho kwa Mungu mimi hukitii na kukifuata, lakini ikiwa kinatoka kwa mapenzi ya mwanadamu mimi hukikataa kwa uthabiti; wakati kile kinachohubiriwa na viongozi au wafanyakazi kina mgongano na mipango ya Mungu, basi mimi bila shaka humfuata Mungu na kuwakataa watu. Kama kina makubaliano kamili na mipango na mapenzi ya Mungu, basi naweza kukisikiliza.”
Inamaanisha nini kuwafuata watu? Kuwafuata watu inamaanisha mtu huwafuata wafanyakazi au viongozi anaowaabudu. Mungu hana nafasi kubwa katika mioyo yaomoyo wake; yeye hutundika kidokezo akisema anamwamini Mungu, na katika kila kitu anachofanya yeye ni kujifananisha na watu au kuwaiga. Hasa wakati ni jambo kuu, anawaacha watu kuamua, anawaacha watu waongoze jaala yao, yeye mwenyewe hatafuti maana ya Mungu, na anashindwa kutambua maneno yanayosemwa na watu. Mradi anachokisikia kinaonekana kuwa cha maana, basi bila kujali kama kinapatana na ukweli bado yeye hukikubali na kukisikiliza. Haya ni maonyesho ya kuwafuata watu. Imani ya watu kama hao katika Mungu haina kanuni, hakuna ukweli katika matendo yao, wao husikiliza mtu yeyote anayesema jambo la maana, na hata vijimungu vyao vikichukua njia mbaya, wao huvifuata mpaka mwisho. Mungu Akivilaani vijimungu vyao, basi watakuwa na dhana juu ya Mungu, na kushikilia kikiki vijimungu vyao. Sababu zao ni kwamba “tunapaswa kumsikiliza yeyote aliye na madaraka juu yetu; nguvu ya karibu ni bora kuliko nguvu ya juu.” Hii ni mantiki duni, upumbavu mtupu, lakini huo ndio upumbavu wa hao ambao huwafuata watu. Wale wanaowafuata watu hawana ukweli. Ni wale tu ambao humfuata Mungu wanaoamini kweli katika Mungu; Wale wanaowafuata watu huabudu sanamu, wamekuwa wakidanganywa na watu, na katika mioyo yao hakuna Mungu wala ukweli.
kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu
Watu wengi humwamini Mungu lakini hawajui ni nini maana ya kumtii Mungu, na hufikiri kwamba kuwasikiliza viongozi wao katika vitu vyote ni sawa na kumtii Mungu. Maoni kama haya ni ya upuuzi kabisa, kwa sababu chanzo cha utii wao si sahihi. Wao hudhukuru kuwasikiliza viongozi wao kuwa ni kumtii Mungu. Kumwamini Mungu kulingana na maoni haya ni kumwamini Mungu kwa jina tu; kwa uhakika, watu hawa huwaamini watu. …
Tunapomwamini Mungu, Mungu anapaswa kushikilia mahali pa kuongoza katika mioyo yetu, tunapaswa kusalimisha uongozi kwa Mungu katika mambo yote, tunapaswa kutafuta maana ya Mungu katika kila kitu, vitendo vyetu vinapaswa kulingana na maneno ya Mungu, na kwa mujibu wa mwongozo wa Roho Mtakatifu, na tunapaswa kutii yote yatokayo kwa Mungu. Ukiwasikiliza watu, basi hili linathibitisha kwamba Mungu hana mahali moyoni mwako, kwamba ni watu pekee walio na mahali katika moyo wako. Hakuna kilicho muhimu zaidi kwa watu kuliko kufuatilia ukweli na kuyaelewa mapenzi ya Mungu. Ikiwa huzingatii kuyatafuta malengo ya Mungu na kuyafahamu mapenzi ya Mungu, basi wako si utii wa kweli. Haijalishi ni sahihi jinsi gani wanavyosikika, ikiwa daima wewe huwasikiliza watu, basi kwa kiini wewe huwasikiliza watu–ambako si sawa na kumtii Mungu. Kwa kweli, kama wale wanaomwamini Mungu wanaweza kuelewa maana ya Mungu moja kwa moja kutoka kwa maneno Yake, ikiwa wanaweza kupata njia yao wenyewe ya kutenda katika maneno Yake, na huwasiliana ukweli kwa karibu, na kuuelewa ukweli, kwa maneno Yake, baada ya hayo wao waiweke katika vitendo, na ikiwa kwa wakati muhimu, wanaweza kuomba zaidi, na kutafuta uongozi wa Roho Mtakatifu, na kutii malengo ya Roho Mtakatifu, hivi kweli ni kumtii Mungu. Wale wanaomtii Mungu hutafuta njia katika maneno ya Mungu, matatizo yao hutatuliwa katika maneno ya Mungu, na wao hufanya kazi katikati ya uongozi wa Roho Mtakatifu; hivi kweli ni kumtii Mungu. Wale ambao husikiliza viongozi wao katika kila kitu wana hakika ya kupotea mbali na Mungu katika mioyo yao. Zaidi ya hayo, hawana amani mbele ya Mungu, sio wale wanaoishi mbele ya Mungu na kutafuta ukweli, hawana uhusiano na Mungu, na kanuni ya matendo yao ni kumsikiliza yeyote anayesema mambo halisi–mradi ni kiongozi, watatii. Vitendo kama hivyo ni vya dhihaka. Hawana ukweli wala uwezo wa kutofautisha, na wanaweza tu kudhibitisha kilicho sawa au kibaya kulingana na mawazo yao au akili, kwa hiyo jinsi gani wanaweza kujua kama kinafanana na ukweli? Kama wao huamini Mungu kulingana na maoni hayo, basi katika maisha yao yote hawatauelewa ukweli au kumjua Mungu. Aina hizo za imani zinaweza kusemwa kuwa kuamini katika ubongo wao wenyewe na kuitembea njia yao wenyewe, na hawana uhusiano na Mungu wa vitendo.
kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu
Yaliyopendekezwa: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi? Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni