Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Aangamize-Sodoma. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Aangamize-Sodoma. Onyesha machapisho yote

8/12/2018

Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili

Sura ya 5 Ukweli Kuhusu Mungu Kupata Mwili

5. Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili

Maneno Husika ya Mungu:
Kupata mwili mara ya kwanza kulikuwa kumkomboa mwanadamu kutoka katika dhambi kupitia mwili wa Yesu, hivyo, Aliokoa mwanadamu kutoka kwa msalaba, lakini tabia potovu ya kishetani ilibaki ndani ya mwanadamu. Kupata mwili mara ya pili si kwa ajili ya kuhudumu tena kama sadaka ya dhambi ila ni kuwaokoa kamilifu wale waliokombolewa kutoka kwa dhambi. Hii inafanyika ili wale waliosamehewa wakombolewe kutoka kwa dhambi zao, na kufanywa safi kabisa, na kupata mabadiliko ya tabia, hivyo kujikwamua kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza na kurudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu. Hivyo tu ndivyo mwanadamu ataweza kutakaswa kikamilifu. Mungu Alianza kazi ya wokovu katika Enzi ya Neema baada ya Enzi ya Sheria kufika mwisho.

4/03/2018

B. Mungu Lazima Aangamize Sodoma.


 Neno la Mwenyezi Mungu  | B. Mungu Lazima Aangamize Sodoma.

    (Mwa 18:26) Kisha BWANA akasema, Nikipata katika Sodoma wenye haki hamsini mjini, basi Nitapaacha mahali pote kwa ajili yao.
    (Mwa 18:29) Na akazungumza tena naye, akasema, Huenda wakapatikana humo arobaini. Akasema, Sitafanya hivyo.
    (Mwa 18:30) Akamwambia, labda watapatikana huko thelathini. Naye akasema, Sitafanya hivyo.
    (Mwa 18:31) Kisha akasema, huenda wakaonekana huko ishirini. Naye akasema, Sitauharibu.
    (Mwa 18:32) Naye akasema, huenda wakaonekana huko kumi. Naye akasema, Sitauharibu.
    Hizi ni dondoo chache Nilizochagua kutoka kwenye Biblia. Dondoo hizi si kamilifu, za matoleo ya awali. Kama mngependa kuziona hizo, mnaweza kuzitafuta kwenye Biblia nyinyi wenyewe; ili kuokoa muda, Nimeiacha sehemu ya maudhui asilia. Hapa Nimechagua tu vifungu na sentensi mbalimbali kuu, huku nikiziacha sentensi mbalimbali ambazo hazina umuhimu katika ushirika wetu wa leo.