9/06/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 33

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 33

Ufalme Wangu unawahitaji wale ambao ni waaminifu, wasio wanafiki, na wasio wadanganyifu. Je, si watu wenye moyo safi na waaminifu duniani hawapendwi na watu? Mimi ni kinyume kabisa cha jinsi ilivyo. Inakubalika kwa watu waaminifu kuja Kwangu; Nafurahia mtu wa aina hii, pia Ninamhitaji mtu wa aina hii. Hii ni haki Yangu hasa. Watu wengine ni wajinga; hawawezi kuhisi kazi ya Roho Mtakatifu na hawawezi kuyaelewa mapenzi Yangu. Hawawezi kuona familia yao na hali zinazowazingira kwa uwazi, wanafanya vitu bila kufikiri na kupoteza fursa nyingi za neema. Mara kwa mara wanajuta matendo yao na wanapokabiliwa na jambo, tena hawawezi kuliona kwa uwazi. Wakati mwingine wanaweza kumtegemea Mungu kupata ushindi, lakini wanapokabiliwa na jambo la aina hiyo tena baadaye, ugonjwa ule wa kitambo unarudi, na hawawezi kuyaelewa mapenzi Yangu. Lakini Siangalii mambo haya, na Sikumbuki dhambi zenu. Badala yake, Nataka kuwaokoa kutoka kwa nchi hii ya fujofujo na kuwaruhusu kuyafanya maisha yenu yawe mapya. Nimewasamehe mara kwa mara. Hata hivyo, sasa ni hatua muhimu zaidi. Hamwezi kuchanganyikiwa tena na hamwezi kusonga mbele namna hiyo tena—kusonga na kusimama. Mtaweza kufikia hatima lini? Ni lazima mfanye kadiri mwezavyo kukimbia kuelekea mwisho bila kusimama. Msizembee katika wakati muhimu zaidi, songeni mbele kwa ujasiri, na karamu karimu iko mbele yenu. Vaeni nguo zenu za harusi haraka na majoho ya haki na mhudhurie chajio cha harusi cha Kristo; furahieni raha ya familia milele! Hamtakuwa wenye huzuni, majonzi na kutanafusi tena kama awali. Wakati huo kila kitu kitakuwa kimetoweka kama moshi na uhai wa Kristo aliyefufuka tu ndio utakuwa na nguvu ndani yako. Litakuwa hekalu lililotakaswa na kusafishwa kwa ndani na uhai wa ufufuko ambao umepata utakuwa ndani yako milele hata milele!

Chanzo: Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 33

Endelea Kusoma: Neno la Mungu | "Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu"

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni