Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo kazi-ya-Roho-Mtakatifu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo kazi-ya-Roho-Mtakatifu. Onyesha machapisho yote

10/18/2019

Kuna tofauti ipi kati ya kazi ya wale wanaotumiwa na Mungu na kazi ya viongozi wa kidini?

VIII. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Kipengele cha Ukweli Kuhusu Tofauti Kati ya Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu

2. Kuna tofauti ipi kati ya kazi ya wale wanaotumiwa na Mungu na kazi ya viongozi wa kidini?

Aya za Biblia za Kurejelea:
“Naye akasema … Mtumishi wangu Musa hayuko hivyo, ambaye ni mwaminifu nyumbani mwangu mwote” (Hesabu 12:6-7).
“Na Yesu akajibu na kumwambia, … Na pia nakuambia, Kwamba wewe ni Petro, na nitalijenga kanisa langu juu ya mwamba huu; na milango ya jahanamu haitashinda dhidi ya kanisa hilo. Na nitakupa funguo za ufalme wa mbinguni: na chochote utakachofunga duniani kitafungwa mbinguni: na chochote utakachoweka huru duniani kitawekwa huru mbinguni” (Mathayo 16:17-19).
Ole wao wachungaji wa Israeli wajilishao! Wachungaji hawapaswi kuwalisha kondoo? Mnawala kondoo walio wanono, na kuvalia sufu zao, mnawaua wale ambao wamenona: lakini hamwalishi kondoo. Hamjawapa nguvu wagonjwa, wala hamjawaponya waliougua, wala hamjawafunga waliovunjika, wala hamjawarudisha wale waliofukuzwa, wala hamjawatafuta wale waliopotea; lakini mmewatawala kwa nguvu na ukatili.

9/24/2019

Neno la Mungu | Sura ya 12

Ikiwa una tabia ambayo si thabiti, nyepesi kuhamaki kama upepo au mvua, kama huwezi kuendelea kusonga mbele, basi fimbo Yangu haitakuwa mbali na wewe. Unaposhughulikiwa, kadiri hali ilivyo mbaya zaidi, na kadiri unavyoteswa zaidi, ndivyo upendo wako kwa Mungu unavyoongezeka, na unaacha kushikilia dunia. Bila njia nyingine, unakuja Kwangu, na unapata tena nguvu na imani yako. Ilhali, katika hali rahisi, ungeboronga. Ni lazima uingie ndani kwa mtazamo chanya, uwe mwenye vitendo na si baridi.

9/11/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 28

Unaona kwamba muda ni mfupi sana na kazi ya Roho Mtakatifu inavurumisha mbele, ikikusababisha kupata baraka kubwa hivi, kumpokea Mfalme wa ulimwengu, Mwenyezi Mungu, ambaye ni Jua ling’aalo, Mfalme wa ufalme—hii yote ni neema na huruma Yangu. Kuna nini kinachoweza kuwepo kinachoweza kukutoa kwa upendo Wangu? Tafakari kwa makini, usijaribu kuepa, subiri kwa ustahamilivu mbele Yangu kila wakati na usiwe ukizurura nje daima. 

9/06/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 33

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 33

Ufalme Wangu unawahitaji wale ambao ni waaminifu, wasio wanafiki, na wasio wadanganyifu. Je, si watu wenye moyo safi na waaminifu duniani hawapendwi na watu? Mimi ni kinyume kabisa cha jinsi ilivyo. Inakubalika kwa watu waaminifu kuja Kwangu; Nafurahia mtu wa aina hii, pia Ninamhitaji mtu wa aina hii. Hii ni haki Yangu hasa. Watu wengine ni wajinga; hawawezi kuhisi kazi ya Roho Mtakatifu na hawawezi kuyaelewa mapenzi Yangu. Hawawezi kuona familia yao na hali zinazowazingira kwa uwazi, wanafanya vitu bila kufikiri na kupoteza fursa nyingi za neema.