Matamshi ya Mungu | "Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu"
Tatizo la kawaida lililo miongoni mwa binadamu wote ni kwamba wao huuelewa ukweli lakini hawawezi kuuweka katika matendo. Sababu moja ni kwamba binadamu hana nia ya kulipa gharama, na sababu nyingine ni kwamba utambuzi wa mwanadamu ni duni mno; hawezi kuona zaidi ya ugumu mwingi ulio katika hali halisi ya maisha na hajui jinsi ya kutenda kwa njia inayofaa. Kwa vile mtu ana tajriba ndogo sana, mwenye uwezo wa chini, mwenye ufahamu mdogo wa ukweli, yeye hawezi kutatua matatizo yanayomkabili maishani. Anaweza tu kupiga domo kuhusu imani yake kwa Mungu, ilhali hawezi kumhusisha Mungu katika maisha yake ya kila siku. Hii ni kusema, Mungu ni Mungu, na maisha ni maisha, kama kwamba binadamu hana uhusiano na Mungu katika maisha yake. Hayo ndiyo binadamu wote wanayaamini. Aina hii ya imani kwa Mungu haitaruhusu binadamu kupatwa na kukamilishwa Naye kwa uhakika. Kwa kweli, si kwamba neno la Mungu ni pungufu, badala yake uwezo wa binadamu wa kupokea neno Lake ni duni mno. Inaweza kusemwa karibu binadamu wote hutenda kulingana na nia za Mungu. Badala yake, imani yao kwa Mungu ni kwa mujibu wa nia zao wenyewe, fikra za kidini zilizowekwa, na desturi. Ni wachache wanaopitia mabadiliko baada ya kulikubali neno la Mungu na kuanza kutenda kwa mujibu wa mapenzi Yake. Badala yake, wanaendelea katika imani yao potovu. Wakati mwanadamu anaanza kuamini katika Mungu, anafanya hivyo kwa kuzingatia sheria za kawaida za dini, na anaishi na kuhusiana na wengine kwa misingi ya falsafa yake ya maisha. Hivyo ndivyo ilivyo kwa watu tisa kati ya kila watu kumi. Ni wachache sana wanaounda mpango mwingine na kuanza mwanzo mpya baada ya kuanza kumwamini Mungu. Hakuna anayeona au kuweka katika vitendo neno la Mungu kama ukweli.