12/05/2018

Kwa nini husemwa kuwa kupata mwili kwili kwa Mungu hukamilish umuhimu wa kupata mwili?

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kupata mwili

Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Kupata Mwili kwa Mungu

7. Kwa nini husemwa kuwa kupata mwili kwili kwa Mungu hukamilish umuhimu wa kupata mwili?

Aya za Biblia za Kurejelea:
"Kwa hiyo Kristo alitolewa mara moja kuzichukua dhambi za wengi; na kwa wale wamtazamiao ataonekana mara ya pili bila dhambi kwa wokovu" (EBR 9:28).
"Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu" (YN. 1:1).
Maneno Husika ya Mungu:
Kupata mwili mara ya kwanza kulikuwa kumkomboa mwanadamu kutoka katika dhambi kupitia mwili wa Yesu, hivyo, Aliokoa mwanadamu kutoka kwa msalaba, lakini tabia potovu ya kishetani ilibaki ndani ya mwanadamu. Kupata mwili mara ya pili si kwa ajili ya kuhudumu tena kama sadaka ya dhambi ila ni kuwaokoa kamilifu wale waliokombolewa kutoka kwa dhambi. Hii inafanyika ili wale waliosamehewa wakombolewe kutoka kwa dhambi zao, na kufanywa safi kabisa, na kupata mabadiliko ya tabia, hivyo kujikwamua kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza na kurudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu. Hivyo tu ndivyo mwanadamu ataweza kutakaswa kikamilifu. Mungu Alianza kazi ya wokovu katika Enzi ya Neema baada ya Enzi ya Sheria kufika mwisho. Ni mpaka siku za mwisho tu ambapo Mungu Ametakasa binadamu kikamilifu kwa kufanya kazi ya hukumu na kuadibu mwanadamu kwa kuwa muasi, ndipo Mungu atakamilisha kazi Yake ya wokovu na kupumzika. Kwa hivyo, katika hatua tatu za kazi, ni mara mbili tu ndipo Mungu Alikuwa mwili ili kufanya kazi Yake kati ya mwanadamu Mwenyewe. Hiyo ni kwa sababu moja tu kati ya hatua tatu za kazi ni kuwaongoza wanadamu katika maisha yao, ihali zingine mbili ni kazi ya wokovu. Mungu Anapokuwa mwili tu ndipo Atakapoishi pamoja na mwanadamu, kuzoea mateso ya dunia, na kuishi katika mwili wa kawaida. Katika hali hii tu ndipo Ataweza kumpatia mwanadamu wa uumbaji Wake neon la matendo wanalohitaji. Mwanadamu anapokea wokovu kamili kutoka kwa Mungu kwa sababu ya Mungu mwenye mwili, sio moja kwa moja kutoka kwa maombi yao kwenda mbinguni. Kwani mwanadamu ni mwenye mwili; mwanadamu hawezi kuona Roho wa Mungu na pia kutoweza kumkaribia. Kile tu mwanadamu anaweza kushiriki na mwili wa Mungu; kupitia Yeye tu ndipo mwanadamu ataweza kuelewa maneno yote, na ukweli wote, na kupokea wokovu kamili. Kupatikana kwa mwili mara ya pili kunatosha kumaliza dhambi za mwanadamu na kumtakasa mwanadamu. Hivyo, kupatikana kwa mwili mara ya pili kutafikisha tamati kazi yote ya Mungu mwenye mwili na kukamilisha umuhimu wa Mungu kupata mwili.
kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili (4)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Yesu Alipokuwa Akifanya kazi Yake, maarifa ya mwanadamu juu Yake yalikuwa bado hayakuwa bayana na hayakuwa wazi. Mwanadamu aliamini kila wakati kuwa Alikuwa Mwana wa Daudi na kumtangaza kuwa nabii mkuu na Bwana mwena Aliyezikomboa dhambi za mwanadamu. Wengine, wakiwa na msingi wa imani, wakaponywa tu kwa kugusa vazi Lake; vipofu wakaona na hata wafu kurejeshwa katika uhai. Hata hivyo, mwanadamu hangeweza kutambua tabia potovu za kishetani zilizokita mizizi ndani yake na pia mwanadamu hakujua jinsi ya kuitoa. Mwanadamu alipokea neema nyingi, kama amani na furaha ya mwili, baraka ya familia nzima juu ya imani ya mmoja, na kuponywa magonjwa, na mengine mengi. Yaliyobaki ni matendo mema ya mwanadamu na uonekano wa kiungu; kama mwanadamu angeishi katika huo msingi, alichukuliwa kama muumini mzuri. Waumini hao tu ndio wangeingia mbinguni baada ya kifo, hii ina maana kuwa walikuwa wameokolewa. Lakini katika maisha yao, hawakuelewa kamwe njia ya maisha. Walitenda tu dhambi, na kisha kukiri kila wakati bila njia ya kuielekea tabia iliyobadilika; hii ndiyo ilikuwa hali ya mwanadamu katika Enzi ya Neema. Je mwanadamu amepokea wokovu kamili? La! Kwa hivyo, hatua ilipokamilika, bado kuna kazi ya hukumu na kuadibu. Hatua hii inamfanya mwanadamu kuwa safi kupitia neno ili kumpatia mwanadamu njia ya kufuata. Hatua hii haingekuwa na matunda ama ya maana kama ingeendeleaa na kukemea mapepo, kwani msingi wa dhambi wa mwanadamu haungetupuwa mbali na mwanadamu angekoma tu baada ya msamaha wa dhambi. Kupitia kwa sadaka ya dhambi, mwanadamu amesamehewa dhambi zake, kwani kazi ya kusulubisha imefika mwisho na Mungu Ametawala juu ya Shetani. Lakini tabia potovu ya wanadamu bado imebaki ndani yao na mwanadamu anaweza kutenda dhambi na kumpinga Mungu; Mungu hajampata mwanadamu. Hiyo ndio sababu katika hatua hii ya kazi Mungu Anatumia neno kutangaza tabia potovu ya mwanadamu na kumuuliza mwanadamu kutenda kulingana na njia sahihi. Hatua hii ni ya maana zaidi kuliko zile za awali na pia yenye mafanikio zaidi, kwani wakati huu ni neno ambalo linatoa maisha moja kwa moja kwa mwanadamu na linawezesha tabia ya mwanadamu kubadilishwa kabisa; ni hatua ya kazi ya uhakika kabisa. Kwa hivyo, Mungu kupata mwili katika siku za mwisho imekamilisha umuhimu wa Mungu kupata mwili wa Mungu na kukamilisha usimamizi wa Mungu katika mpango wa kuokoa mwanadamu.
kutoka kwa "Fumbo la Kupata Mwili (4)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu mwenye mwili wa kwanza Hakukamilisha kazi ya kupata mwili; Alikamilisha tu hatua ya kwanza ya kazi iliyokuwa lazima kwa Mungu kuifanya katika mwili. Kwa hivyo, ili kuimaliza kazi ya kupata mwili, Mungu Amerudi katika mwili kwa mara nyingine tena, Akiishi kulingana na ukawaida na uhalisia wote wa mwili, yaani, kuifanya kazi ya Mungu ijitokeze katika mwili wa kawaida kabisa, na kwa njia hiyo Anahitimisha kazi Aliyoiacha bila kukamilisha katika mwili. Mwili wa pili uliopatikana kimsingi ni sawa na ule wa kwanza, lakini ni halisi zaidi, wa kawaida kabisa kuliko ule wa kwanza. Kwa sababu hiyo, mateso unayoyapitia mwili wa pili uliopatikana ni makubwa kuliko yale ya ule wa kwanza, ila mateso haya ni kwa sababu ya huduma Yake katika mwili, ambayo ni tofauti na mateso ya mwanadamu mwovu. Vilevile yanachipuka kutokana na ukawaida na uhalisi wa mwili Wake. Kwa kuwa Anatekeleza huduma Yake katika mwili wa kawida na halisi kabisa, mwili ni sharti upitie mateso mazito. Kadiri mwili ulivyo wa kawaida na halisi, ndivyo unateseka zaidi katika utekelezaji wa huduma Yake. Mungu Anafanya kazi katika mwili wa kawaida sana, mwili ambao si wa rohoni kamwe. Kwa kuwa mwili Wake ni wa kawaida, na ni lazima ubebe kazi ya kumwokoa mwanadamu, Anateseka hata zaidi kuliko ambavyo mwili wa rohoni unaweza kuteseka—mateso haya yote yanatokana na uhalisi na ukawaida wa mwili Wake. Kutokana na mateso yaliyopitiwa na hii miili miwili iliyopatikana wakati wa kutekeleza huduma Zao, mtu anaweza kuona kiini cha mwili uliopatikana. Kadiri mwili ulivyo wa kawaida, ndivyo Anapata mateso mazito Afanyapo kazi, na ndivyo maoni ya watu yanaendelea kuwa makali, na hatari zinazomkabili zinaendelea kuongezeka. Lakini, kadiri mwili ulivyo halisi, kadiri mwili unavyokuwa na hali kamili ya binadamu wa kawaida, ndivyo Anaweza zaidi kuifanya kazi ya Mungu katika mwili. Ulikuwa mwili wa Yesu ulioangikwa msalabani, mwili Wake Alioutoa kama kafara kwa dhambi; ni kupitia kwa mwili wenye ubinadamu wa kawaida ndipo Aliweza kumshinda Shetani na kumkomboa kabisa mwanadamu kutoka msalabani. Ni kupitia mwili kamili ndipo Mungu katika mwili mara ya pili Anatekeleza kazi ya ushindi na kumshinda Shetani. Ni mwili tu wa kawaida na halisi kabisa unaoweza kutekeleza kazi ya ushindi kwa ukamilifu wake na kutoa ushuhuda wa nguvu. Hii ni sawa na kusema kwamba kazi ya[a] kumshinda mwanadamu inafanywa kuwa bora kupitia uhalisia na ukawaida wa mwili wa Mungu, si kupitia miujiza mikuu na ufunuo. Huduma ya huyu Mungu mwenye mwili ni ya kunena na kwa njia hiyo inamshinda mwanadamu na kumfanya mkamilifu; kwa maneno mengine, kazi ya Roho Aliyejitokeza katika mwili, wajibu wa mwili, ni kunena na kupitia kwa hili kumshinda, kumfichua, kumfanya kuwa kamilifu, na kumwondoa mwanadamu kabisa. Kwa hivyo, ni katika kazi ya kushinda ambapo kazi ya Mungu katika mwili itatimiziwa kwa ukamilifu. Kazi ya ukombozi ya kwanza ilikuwa mwanzo tu wa kazi ya kupata mwili kwa Yesu; mwili unaofanya kazi ya kushindautaikamilisha kazi nzima ya kupata mwili kwa Yesu. Kijinsia, mmoja ni mwanamke na mwingine ni mwanamume; kwa hili, maana ya kupata mwili kwa Mungu imekamilishwa. Mawazo mabaya ya mwanadamu kumhusu Mungu yameondolewa: Mungu Anaweza kuwa mwanamke na mwanamume, na kimsingi Mungu mwenye mwili Hana jinsia. Mungu Alimuumba mwanamume na mwanamke, na Hatofautishi kati ya hizi jinsia. Katika hatua hii ya kazi Mungu Hafanyi ishara na miujiza, ili kwamba kazi iweze kutimiza matokeo yake kupitia kwa maneno. Aidha, mara hii kazi ya Mungu mwenye mwili si kuponya wagonjwa na kufukuza mapepo, ila kumshinda mwanadamu kupitia kunena, ikiwa na maana kwamba uwezo asili uliomo kwenye huu mwili uliopatikana wa Mungu ni kunena maneno na kumshinda mwanadamu, si kuponya wagonjwa na kufukuza mapepo. Kazi Yake katika ubinadamu wa kawaida si kutenda miujiza, si kuponya wagonjwa na kufukuza mapepo, ila ni kunena, na kwa hivyo Yesu kupata mwili kwa mara ya pili kunaonekana kwa watu kuwa kawaida zaidi ya mara ya kwanza. Watu wanaona kuwa Mungu kupata mwili si uongo; lakini huyu Mungu mwenye mwili ni tofauti na Yesu Aliyekuwa mwili, na japo wote ni Mungu wenye mwili, Hawako sawa kabisa. Yesu Alikuwa na ubinadamu wa kawaida, lakini Aliambatana na ishara nyingi na miujiza. Katika huyu Mungu mwenye mwili, macho ya mwanadamu hayataona ishara au miujiza, wala kuponya wagonjwa au kufukuza mapepo, wala kutembea juu ya bahari, wala kufunga kwa siku arobaini… Hafanyi kazi sawa na Aliyoifanya Yesu, si kwa kuwa mwili Wake kimsingi ni tofauti na ule wa Yesu, ila ni kwa sababu si huduma Yake kuponya wagonjwa na kufukuza mapepo. Haharibu kazi Yake mwenyewe, Havurugi kazi Yake mwenyewe. Kwa kuwa anamshinda mwanadamu kwa maneno Yake halisi, haina haja ya kumhini kwa miujiza, na kwa hivyo hii hatua ni kukamilisha kazi ya kupata mwili. Mungu mwenye mwili umwonaye leo ni mwili kabisa, na hana hali ya rohoni ndani yake. Anakuwa mgonjwa sawa tu na watu wengine, Anahitaji chakula na nguo sawa tu na watu wengine, kwani ni mwili kabisa. Ikiwa wakati huu Mungu mwenye mwili Angetekeleza ishara na miujiza mikuu, ikiwa Angeponya wagonjwa, kufukuza mapepo, au Angeweza kuua kwa neno moja tu, kazi ya kushinda ingefanywaje? Kazi ingeenezwa vipi miongoni mwa watu wa Mataifa? Kuponya wagonjwa na kufukuza mapepo ilikuwa kazi ya Enzi ya Neema, hatua ya kwanza katika kazi ya ukombozi, na sasa kwa kuwa Mungu Amemkomboa mwanadamu kutoka msalabani, Hatekelezi kazi hiyo kamwe. Ikiwa katika siku za mwisho "Mungu" sawa na Yesu Angeonekana, Ambaye Anaponya wagonjwa, Anafukuza mapepo na Anayesulubiwa kwa ajili ya wanadamu, "Mungu" huyo, japo Analingana na maelezo ya Mungu katika Biblia, na rahisi kwa mwanadamu kukubali, Hangeweza, katika kiini chake, kuwa mwili uliovaliwa na Roho wa Mungu, bali na roho mwovu. Kwani ni kanuni ya kazi ya Mungu kutorudia Alichokikamilisha. Hivyo basi kazi ya kupata mwili wa Mungu kwa mara ya pili ni tofauti na kule kwa kwanza. Katika siku za mwisho, Mungu Anafanikisha kazi ya kushinda katika mwili wa kawaida; Haponyi wagonjwa, Hatasulubishwa kwa ajili ya mwanadamu, ila tu Ananena maneno katika mwili, Anamshinda mwanadamu katika mwili. Ni mwili kama huo tu ndio mwili wa Mungu katika mwili; ni mwili kama huo tu ndio unaoweza kukamilisha Kazi ya Mungu katika mwili.
kutoka kwa "Kiini cha Mwili Ulio na Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kwa nini Ninasema kuwa maana ya kupata mwili haikukamilishwa katika kazi ya Yesu? Ni kwa sababu Neno halikuwa Mwili kikamilifu. Kilichofanywa na Yesu kilikuwa tu sehemu moja ya kazi ya Mungu katika mwili; Alifanya tu kazi ya ukombozi na Hakufanya kazi ya kumpata mwanadamu kikamilifu. Kwa sababu hii, Mungu Amekuwa mwili mara nyingine tena katika siku za mwisho. Hatua hii ya kazi, pia inafanywa katika mwili wa kawaida, ikifanywa na mwanadamu wa kawaida kabisa, ambaye ubinadamu wake haupiti mipaka ya ubinadamu. Kwa maneno mengine, Mungu Amekuwa mwanadamu kamili, na ni mtu ambaye utambulisho wake ni ule wa Mungu, mwanadamu kamili, mwili kamili, Ambaye Anatekeleza kazi. Katika jicho la mwanadamu, Yeye ni mwili tu ambao haujapita mipaka ya ubinadamu hata kidogo, mwanadamu wa kawaida kabisa Anayeweza kuzungumza lugha ya mbinguni, Ambaye Haonyeshi ishara za kimiujiza, Hafanyi miujiza, na hata kwa kiwango kidogo Haweka wazi ukweli wa ndani kuhusu dini katika kumbi kuu za mikutano. Kazi ya kupata mwili kwa mara ya pili inaonekana kwa wanadamu kuwa tofauti kabisa na ile ya kwanza, kiasi kwamba kazi hizi mbili zinaonekana kutokuwa na uhusiano wowote, na hakuna chochote katika kazi ya kwanza kinachoweza kuonekana wakati huu. Japo kazi ya kupata mwili kwa mara ya pili ni tofauti na ile ya kwanza, hili halithibitishi kuwa chanzo Chao si kimoja na sawa. Iwapo chanzo Chao ni kimoja inategemea aina ya kazi iliyofanywa na miili na si katika maumbo Yao ya nje. Katika hatua tatu za kazi Yake, Mungu Amekuwa mwili mara mbili, na mara zote kazi ya Mungu kuwa mwili inaanzisha enzi mpya, inaanzisha kazi mpya; kuwa mwili kwa mara ya kwanza na pili kunakamilishana. Macho ya wanadamu hayawezi kugundua kuwa hii miili miwili kwa kweli imetokana na chanzo kimoja. Ni wazi kwamba hili liko nje ya uwezo wa macho ya wanadamu au akili za wanadamu. Ila katika kiini Chao, ni miili sawa, kwani kazi Yao inatokana na Roho mmoja. Iwapo hii miili miwili inatokana na chanzo kimoja haiwezi kuamuliwa kutokana na enzi na sehemu Ilipozaliwa, au vigezo vingine kama hivyo, ila kwa kazi ya uungu iliyoonyeshwa Nayo. Kupata mwili wa pili hakufanyi kazi yoyote iliyofanywa na Yesu, kwani kazi ya Mungu haifuati makubaliano, lakini kila wakati inafungua njia mpya. Kupata mwili wa pili hakulengi kuongeza au kuimarisha maono ya kupata mwili wa kwanza katika akili za watu, ila kuutimiza na kuukamilisha, kuongeza kina cha wanadamu kumwelewa Mungu, kuvunja sheria zote ambazo zipo katika mioyo ya watu, na kufuta picha za uongo kuhusu Mungu mioyoni mwao. Ni wazi kuwa hakuna hatua yoyote ya kazi ya Mungu mwenyewe inaweza kumpa mwanadamu ufahamu kamili wa Mungu; kila mojawapo inatoa kwa sehemu tu, si ufahamu mzima. Japo Mungu Ameonyesha tabia Yake kikamilifu, kwa sababu ya upungufu wa ufahamu wa wanadamu, ufahamu wake kuhusu Mungu si kamili. Haiwezekani, kutumia lugha ya wanadamu, kueleza tabia nzima ya Mungu; basi hatua moja tu ya kazi yake itamwelezaje Mungu kikamilifu? Anafanya kazi katika mwili kwa kujisetiri katika ubinadamu wake wa kawaida, na mtu anaweza kumjua tu kupitia kwa maonyesho ya uungu Wake, si kupitia kwa umbo Lake la kimwili. Mungu Anakuja katika mwili kumruhusu mwanadamu Amjue kupitia kazi Zake mbalimbali, na hakuna hatua mbili za kazi Yake zinafanana. Ni kwa njia hii tu mwanadamu anaweza kuwa na ufahamu kamili wa kazi ya Mungu katika mwili, si kwa kujifunga katika kipengele kimoja tu.
kutoka kwa "Kiini cha Mwili Ulio na Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Yesu alifanya hatua ya kazi ambayo ilitimiza tu kiini cha "Neno alikuwako kwa Mungu": Ukweli wa Mungu ulikuwako kwa Mungu, na Roho wa Mungu alikuwa na mwili na alikuwa asiyetenganishwa kutoka Kwake, yaani, mwili wa Mungu mwenye mwili ulikuwa na Roho wa Mungu, ambalo ni thibitisho kuu zaidi kwamba Yesu mwenye mwili alikuwa aliyepata mwili wa kwanza wa Mungu. Hatua hii ya kazi ilitimiza maana ya ndani ya "Neno lapata mwili," ilichangia kwenye maana ya kina zaidi ya "naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu," na inakuruhusu wewe uamini kwa uthabiti maneno haya kwamba "Hapo mwanzo kulikuwako na Neno." Ambalo ni kusema, wakati wa uumbaji Mungu alikuwa na maneno, Maneno Yake yalikuwa na Yeye na yasiyotenganishwa kutoka Kwake, na enzi ya mwisho inafanya nguvu na mamlaka ya maneno Yake yawe hata wazi zaidi, na kumkubalia mwanadamu kuyaona maneno Yake yote—kuyasikia maneno Yake yote. Hiyo ndiyo kazi ya enzi ya mwisho. … Kwa sababu hii ni kazi ya kupata mwili kwa pili—na mara ya mwisho ambapo Mungu anapata mwili—inakamilisha kwa ukamilifu umuhimu wa kupata mwili, inatekeleza kabisa na kutoa kazi yote ya Mungu katika mwili, na kumaliza enzi ya Mungu kuwa katika mwili.
kutoka kwa "Utendaji (4)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Katika Enzi ya Neema, Mungu hakufanya kazi ya neno, lakini Alieleza tu usulubisho ili kuwakomboa binadamu wote. Bibilia inaelezea tu ni kwa nini Yesu alikuwa Asulubiwe, na mateso ambayo Alipitia kwenye msalaba, na jinsi mwanadamu anapaswa kusulubiwa kwa ajili ya Mungu. Katika enzi hiyo, kazi yote iliyofanywa na Mungu ilikuwa kuhusu usulubisho. Katika Enzi ya Ufalme, Mungu katika mwili Anazungumza maneno ili kushinda wale wote wanaomwamini. Huu ni, "Neno kuonekana katika mwili"; Mungu amekuja katika siku za mwisho ili kufanya kazi hii, ambayo ni kusema, Amekuja kutimiza umuhimu wenyewe wa Neno kuonekana katika mwili. Ananena tu maneno, na majilio ya ukweli ni chache. Hii ndiyo dutu kamili ya Neno kuonekana katika mwili, na wakati Mungu katika mwili Anaponena maneno Yake, huku ndiko kuonekana kwa Neno katika Mwili, na ni Neno kuja katika mwili. "Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu, na Neno likawa mwili." Hii (kazi ya kuonekana kwa Neno katika mwili) ni kazi ambayo Mungu atatimiza katika siku za mwisho, na ni sura ya mwisho ya mpango Wake mzima wa uongozi, kwa hivyo Mungu lazima Aje duniani na kudhihirisha maneno Yake katika mwili. Yale yanayofanywa leo, yale yatakayofanywa baadaye, yale yatakayotimizwa na Mungu, hatima ya mwisho mwanadamu, wale watakaookolewa, wale watakaoangamizwa, na mengine mengi—kazi hii ambayo lazima itimizwe mwishowe imesemwa wazi, na yote ni kwa ajili ya kutimiza umuhimu halisi wa Neno kuonekana kwa mwili. Amri za utawala na katiba ambayo ilipeanwa hapo awali, wale ambao wataangamizwa, wale watakaoingia katika mapunziko—maneno haya lazima yatimizwe. Hii ni kazi iliyotimizwa kimsingi na Mungu katika mwili katika siku za mwisho. Anawafanya watu waelewe kule ambako wale waliopangiwa na Mungu wanapaswa kuwa na wale wasiopangiwa na Mungu wanapaswa kuwa, jinsi ambavyo watu Wake na wana Wake watawekwa kwenye vikundi, ni nini kitaifanyikia Uyahudi, ni nini kitaifanyikia Misiri—katika siku za usoni, kila mojawapo ya maneno haya yatatimizwa. Hatua za kazi za Mungu zinaharakishwa. Mungu hutumia neno kama mbinu ya kumfichulia mwanadamu kinachopaswa kufanyika katika kila enzi, kinachopaswa kufanywa na Mungu katika mwili wa siku za mwisho, na huduma Yake ambayo inapaswa kufanywa, na maneno haya ni kwa ajili ya kutimiza umuhimu hasa wa Neno kuonekana kwa mwili.
kutoka kwa "Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu amekuja duniani kwa lengo la kukamilisha ukweli wa "Neno kufanyika mwili," ni sawa na kusema, Amekuja ili kwamba maneno Yake yaweze kutolewa kutoka katika mwili (sio kama wakati wa Musa katika Agano la Kale, ambapo Mungu alizungumza moja kwa moja kutoka mbinguni). Baada ya hapo, kila neno Lake litatimizwa wakati wa Enzi ya Ufalme wa Milenia, zitakuwa ni kweli ambazo zitaonekana katika macho ya watu, na watu watazitazama kwa kutumia macho bila tofauti hata kidogo. Hii ndiyo maana kuu ya Mungu kupata mwili. Ni sawa na kusema, kazi ya Roho imetimizwa kupitia mwili, na kupitia maneno. Hii ndiyo maana ya kweli ya "Neno kufanyika mwili" na "Neno Laonekana katika mwili." Ni Mungu pekee ndiye anayeweza kuzungumza mapenzi ya Roho, na ni Mungu pekee katika mwili ndiye anayeweza kuzungumza kwa niaba ya Roho; maneno ya Mungu yamewekwa wazi katika Mungu kupata mwili, na kila mtu anaongozwa nayo. Hakuna aliyeachwa, wote wanakuwa ndani ya mawanda haya. Ni kutoka tu katika matamshi haya ndipo watu wanaweza kujua; wale ambao hawatapata njia hii wanaota ndoto za mchana ikiwa wanadhani wanaweza kupata matamshi kutoka mbinguni. Hayo ndiyo mamlaka yaliyooneshwa katika mwili wa Mungu uliopata mwili: kuwafanya wote kuamini. Hata wataalamu wa kuheshimiwa sana na wachungaji hawawezi kuzungumza maneno haya. Wote ni lazima wajinyenyekeze chini yao, na hakuna anayeweza kuanza mwanzo mpya. Mungu atatumia maneno kuushinda ulimwengu. Atafanya hivi si kwa kupata kwake mwili, lakini kwa kutumia matamshi kutoka kwa Mungu katika mwili kushinda watu wote duniani; Namna hii tu ndiye Mungu katika mwili, na huu tu ndio kuonekana kwa Mungu katika mwili. Labda kwa watu, inaonekana kana kwamba Mungu hajafanya kazi kubwa—lakini Mungu analazimika kutamka maneno Yake ili watu washawishike kabisa, na wao kutishika kabisa. Bila kweli, watu wanapiga makelele na kupiga mayowe; kwa maneno ya Mungu, wote wananyamaza kimya. Mungu hakika atakamilisha ukweli huu, maana huu ni mpango ulioanzishwa na Mungu: kukamilisha ukweli wa Neno kuwasili duniani.
kutoka kwa "Ufalme wa Milenia Umewasili" katika Neno Laonekana katika Mwili
Huyu Aitwaye Mungu si Roho Mtakatifu pekee, huyo Roho, Roho Aliyoongezeka mara saba, Roho anayehusisha yote, bali pia mtu, mtu wa kawaida, mtu wa kipekee wa kawaida. Si wa kiume pekee bali pia kike. Wako sawa kwa namna kwamba wote kupata miili kwa Mungu hutenda kazi ya Baba yao, na kutofautiana kwa namna kwamba mmoja Anafanya kazi ya ukombozi na mwingine anafanya kazi ya ushindi. Wote wanamwakilisha Mungu Baba, lakini mmoja ni Bwana wa Ukombozi Aliyejaa upendo, ukarimu na huruma, na yule mwingine ni Mungu wa uhaki Aliyejaa hasira na hukumu. Mmoja ni Jemadari Mkuu Anayeanzisha kazi ya ukombozi na mwingine ni Mungu wa uhaki wa kukamilisha kazi ya kutamalaki. Mmoja ni Mwanzo na mwingine Mwisho. Mmoja ni mwili usio na dhambi na mwingine ni mwili unaokamilisha ukombozi, Anaendelea na kazi hiyo na kamwe hana dhambi hata. Wote ni Roho mmoja lakini wanaishi katika miili tofauti na walizaliwa katika sehemu tofauti. Na wametenganishwa na maelfu kadhaa ya miaka. Ilhali kazi Zao ni kijalizo kwa nyingine, hazina mgongano kamwe na zinaweza kuzungumziwa kwa wakati mmoja. Wote ni watu, lakini mmoja ni mtoto wa kiume na mwingine mtoto mchanga wa kike.
kutoka kwa "Inapofikia Mungu, Ufahamu Wako ni Upi?" katika Neno Laonekana katika Mwili
Ikiwa katika hii hatua Mungu mwenye mwili Anapitia ugumu au Anatekeleza huduma Yake, Anafanya hivyo ili kukamilisha maana ya kupata mwili, kwani huku ndiko Mungu kupata mwili kwa mara ya mwisho. Mungu Anaweza kuwa mwili mara mbili tu. Hakuwezi kuwepo mara ya tatu. Kuwa mwili kwa mara ya kwanza Alikuwa ni wa kiume, wa pili ni wa kike, na kwa hivyo sura ya mwili wa Mungu imekamilika katika akili za mwanadamu; aidha, huku kuwa mwili mara mbili tayari kumemaliza kazi ya Mungu katika mwili. Mara ya kwanza, Mungu mwenye mwili Alikuwa na ubinadamu wa kawaida, ili kukamilisha maana ya kupata mwili. Mara hii vilevile Ana ubinadamu wa kawaida ila maana ya huku kupata mwili ni tofauti: ni kwa kina, na kazi Yake ni ya umuhimu mkubwa. Sababu ya Mungu kuwa mwili tena ni kukamilisha maana ya kupata mwili. Mungu Akiikamilisha kabisa hii hatua ya kazi Yake, maana nzima ya kupata mwili, yaani, kazi ya Mungu katika mwili, itakuwa imekamilika, na hakutakuwa na kazi nyingine ya kufanywa katika mwili. Yaani, tangu sasa Mungu Hatawahi tena kuja katika mwili kufanya kazi Yake.
kutoka kwa "Kiini cha Mwili Ulio na Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
(Fungu Lililochaguliwa la Neno la Mungu)
Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili
Kila hatua ya kazi iliyofanywa na Mungu ina umuhimu mkubwa. Yesu alipokuja, Alikuwa mwanaume, na wakati huu Yeye ni mwanamke. Kutokana na hili, unaweza kuona kwamba Mungu aliwaumba mwanaume na mwanamke kwa ajili ya kazi Yake na Kwake hakuna tofauti ya jinsia. Roho Wake anapowasili, Anaweza kuchukua umbo la mwili wowote kwa matakwa Yake na mwili unamwakilisha Yeye. Awe mwanamume au mwanamke, wote wanamwakilisha Mungu ili mradi tu ni Mungu mwenye mwili. Kama Yesu angekuja na Angeonekana kama mwanamke, kwa maneno mengine, iwapo mtoto wa kike, sio wa kiume, angezaliwa kwa njia ya Roho Mtakatifu, hatua hiyo ya kazi ingeweza kukamilika pia. Kama hali ingekuwa hivyo, hatua hii ya kazi ingeweza kukamilishwa badala yake na mwanaume na kazi ingekuwa imekamilika pia. Kazi inayofanywa katika hatua zote ni muhimu sana; hakuna kazi inayojirudia au kupingana na nyingine. Wakati wa kazi Yake, Yesu alikuwa anaitwa Mwana wa pekee, ikiwa inaashiria jinsia ya kiume. Sasa kwa nini Mwana wa pekee hakutajwa katika hatua hii? Hii ni kwa sababu mahitaji ya kazi yamelazimisha badiliko la jinsia tofauti na ile ya Yesu. Kwa Mungu hakuna tofauti ya jinsia. Kazi Yake inafanywa kama Anavyotaka na haizuiliwi na kitu chochote kile, kimsingi ipo huru, lakini kila hatua ina umuhimu mkubwa. Mungu alifanyika mwili mara mbili, na ni dhahiri kwamba kupata mwili kwake katika siku za mwisho ni mara ya mwisho. Amekuja kufichua matendo Yake yote. Ikiwa katika hatua hii Hakufanyika mwili ili Yeye binafsi afanye kazi kwa ajili ya mwanadamu kushuhudia, mwanadamu milele angeshikilia fikra kwamba Mungu ni wa kuime tu, na sio wa kike. Kabla ya hili, wote waliamini kwamba Mungu anaweza kuwa tu mwanaume na kwamba mwanamke hawezi kuitwa Mungu, maana wote walichukulia kwamba mwanamume ana mamlaka juu ya mwanamke. Waliamini kwamba hakuna mwanamke anayeweza kuchukua mamlaka, bali ni mwanamume tu. Hata walisema kwamba mwanamume alikuwa ni kichwa cha mwanamke na kwamba mwanamke anapaswa kumheshimu mwanaume na asiweze kuwa juu yake. Iliposemwa hapo nyuma kwamba mwanamume alikuwa kichwa cha mwanamke, ilisemwa kwa kurejelea Adamu na Hawa ambao walidanganywa na yule nyoka, na wala sio mwanamume na mwanamke walioumbwa na Yehova hapo mwanzo. Kimsingi, mwanamke anapaswa kumtii na kumpenda mume wake, kama vile ambavyo mwanamume anapaswa kujifunza kuisaidia familia yake. Hizi ni sheria na kanuni zilizowekwa na Yehova ambazo kwazo mwanadamu anapaswa kuzifuata katika maisha yake ya hapa duniani. Yehova alimwambia mwanamke "tamaa yako itakuwa ni kwa mumeo, naye atatawala juu yako." Hii ilisemwa tu ili kwamba mwanadamu (yaani, mwanamume na mwanamke) waweze kuishi maisha ya kawaida chini ya utawala wa Yehova, ili kwamba maisha ya mwanadamu yawe na mfumo na yasipoteze mwelekeo. Kwa hivyo, Yehova alitengeneza kanuni zinazofaa kwa ajili ya namna ambavyo mwanamume na mwanamke wanavyopaswa kutenda, lakini kanuni hizi zilirejelea tu viumbe wote wanaoishi duniani, na sio kwa Mungu kupata mwili. Inawezekanaje Mungu awe sawa na uumbaji Wake? Maneno Yake yalielekezwa tu kwa mwanadamu wa uumbaji Wake; zilikuwa kanuni zilizowekwa kwa ajili ya mwanamume na mwanamke ili kwamba mwanadamu huyo aweze kuishi maisha ya kawaida. Hapo mwanzo, ambapo Yehova alimuumba mwanadamu, aliwaumba mwanamume na mwanamke; kwa hiyo, kupata Kwake mwili pia kulitofautishwa kuwa ama mwanamume au mwanamke. Hakuamua kazi Yake kulingana na maneno aliyozungumza kwa Adamu na Hawa. Kufanyika mwili mara mbili kuliamuliwa kabisa kwa kuzingatia mawazo Yake alipomuumba mwanadamu kwa mara ya kwanza. Yaani, alikamilisha kazi ya kupata kwake mwili mara mbili, kwa msingi wa mwanamke na mwanamume ambao hawakuwa wameharibiwa na dhambi. Ikiwa mwanadamu atatumia maneno yaliyozungumzwa na Yehova kwa Adamu na Hawa ambao walidanganywa na yule nyoka katika kazi ya Mungu katika mwili, je, si kwamba Yesu pia anapaswa kumpenda mke Wake kama Alivyotakiwa? Je, Mungu bado ni Mungu wakati huo tena? Ikiwa ni hivyo, je, Anaweza kukamilisha kazi Yake? Ikiwa ni vibaya kwa Mungu aliyepata mwili kuwa mwanamke, je, lisingekuwa kosa kubwa Mungu alipomuumba mwanamke? Ikiwa mwanadamu bado anaamini kwamba Mungu kupata mwili kama mwanamke ni vibaya, je, Yesu, ambaye hakuoa na hivyo hakuweza kumpenda mke Wake, hangekuwa na makosa kama kupata mwili kwa sasa? Kwa kuwa unatumia maneno yaliyozungumzwa na Mungu kwa Hawa ili kupima ukweli wa Mungu kupata mwili leo, unapaswa kutumia maneno ya Mungu kwa Adamu kumhukumu Bwana Yesu ambaye alikuwa mwili katika Enzi ya Neema. Je, hawa wawili sio sawa? Kwa kuwa unamhukumu Bwana Yesu kwa kumtumia mwanamume ambaye hakudanganywa na yule nyoka, huwezi kuhukumu ukweli wa kupata mwili leo hii kwa mwanamke ambaye alidanganywa na yule nyoka. Hiyo sio sawa kabisa! Ikiwa unafanya hukumu ya namna hiyo, basi hii inathibitisha kukosa urazini kwako. Yehova alipopata mwili mara mbili, jinsia ya mwili Wake ilikuwa inahusiana na mwanamume na mwanamke ambaye hakudanganywa na yule nyoka. Alipata mwili mara mbili kulingana na mwanamume na mwanamke ambaye hakudanganywa na yule nyoka. Usifikiri kwamba uanaume wa Yesu ulikuwa sawa na uanaume wa Adamu ambaye alidanganywa na yule nyoka. Hahusiani naye kabisa, na ni wanaume wawili wa asili tofauti. Hakika haiwezi kuwa kwamba uanaume wa Yesu unathibitisha yeye ni kichwa cha wanawake wote na sio kichwa cha wanaume wote? Je, yeye si Mfalme wa Wayahudi wote (ikiwa ni pamoja na wanaume na wanawake)? Ni Mungu Mwenyewe, sio tu kichwa cha mwanamke bali ni kichwa cha mwanamume pia. Ni Bwana wa viumbe vyote, na kichwa cha viumbe vyote. Unawezaje kuamua uanaume wa Yesu kuwa ishara ya kichwa cha mwanamke? Hii si kufuru? Yesu ni mwanamume ambaye hajapotoshwa. Yeye ni Mungu; ni Kristo; ni Bwana. Anawezaje kuwa mwanamume kama Adamu ambaye ameharibiwa na dhambi? Yesu ni mwili uliovaliwa na Roho wa Mungu aliye mtakatifu sana. Unawezaje kusema kuwa Yeye ni Mungu katika uanaume wa Adamu? Je, haingekuwa kwamba kazi yote ya Mungu ingekuwa na makosa? Je, Yehova angeweza kuuweka ndani ya Yesu uanaume wa Adamu ambaye alidanganywa? Sio kwamba kupata mwili kwa wakati huu ni kazi nyingine ya Mungu katika mwili tofauti kijinsia na Yesu lakini wanafanana katika asili? Bado unathubutu kusema kwamba Mungu aliyepata mwili hakuweza kuwa mwanamke kwa kuwa mwanamke ndiye aliyedanganywa kwanza na yule nyoka? Bado unathubutu kusema kwamba mwanamke ni najisi sana na ni chanzo cha upotovu wa mwanadamu, Mungu hawezi kufanyika mwili kama mwanamke? Bado unathubutu kusema kwamba "mwanamke siku zote atamtii mwanamume na hawezi kamwe kudhihirisha au kumwakilisha Mungu moja kwa moja"? Hukuelewa hapo nyuma; sasa bado unaweza kukufuru kazi ya Mungu, hususan Mungu aliyepata mwili? Kama huwezi kuona hili wazi wazi, ni vizuri zaidi ukawa makini na ulimi wako, la sivyo upumbavu na ujinga wako vitawekwa wazi na ubaya wako utadhihirishwa. Usidhani kwamba unaelewa kila kitu. Nakueleza kwamba yote uliyokwishayaona na kuyapitia hayatoshelezi kuelewa hata milenia ya mpango Wangu wa usimamizi. Sasa kwa nini basi unakuwa na kiburi? Talanta ndogo hiyo uliyonayo na maarifa kidogo hayo uliyonayo hayatoshelezi kutumika hata katika sekunde moja ya kazi ya Yesu! Je, una uzoefu mkubwa kiasi gani hasa? Yote uliyoyaona na yote uliyoyasikia katika maisha yako na yote uliyowahi kuyafikiria ni kidogo sana kulinganisha na kazi Ninayoifanya kwa muda mfupi sana! Ni bora usichambue chambue na kutafuta kosa. Haijalishi una kiburi kiasi gani, wewe bado ni kuimbe tu mdogo kuliko sisimizi! Vyote hivyo vilivyomo katika tumbo lako ni vichache zaidi ya vile vilivyomo katika tumbo la sisimizi! Usifikiri kwamba kwa kuwa umepitia mengi na umekuwa mkubwa, unaweza kuzungumza na kutenda kwa majivuno na ujeuri. Je, uzoefu wako na ukuu wako sio matokeo ya maneno Niliyoyazungumza? Je, unaamini kwamba umekuwa hivyo kwa sababu ya kufanya kwako kazi kwa bidii na kutokwa jasho? Siku hii, unaona kupata Kwangu mwili, na matokeo yake ni kwamba unakuwa na dhana nyingi hizo, kutoka kwazo unakuwa na fikira nyingi isiyohesabika. Ikiwa sio kwa kupata mwili Kwangu, bila kujali talanta zako ni za ajabu kiasi gani, usingeweza kuwa na dhana hizi nyingi. Sio kutokana na hili ndipo imeibuka fikira yako? Kama si kupata mwili kwa Yesu kwa mara ya kwanza, je, ungejua nini kuhusu kupata mwili? Je, si kwa sababu ya maarifa yako ya kupata mwili kwa mara ya kwanza ndio maana unathubutu kuhukumu kupata mwili kwa mara ya pili? Kwa nini uchunguze kwa makini badala ya kuwa mfuasi mtiifu? Umeingia katika mkondo huu na umekuja mbele ya Mungu aliyepata mwili. Ungewezaje kuruhusiwa kujifunza? Ni sawa kwako kujifunza historia ya familia yako, lakini ukichunguza "historia ya familia" ya Mungu, inawezekanaje Mungu wa leo akuruhusu kufanya hivyo? Je, wewe sio kipofu? Je, hujiletei dharau kwako mwenyewe?
Ikiwa tu kazi ya Yesu ingefanywa bila kitimizo cha hatua hii katika siku za mwisho, basi mwanadamu milele angeshikilia fikira kwamba Yesu pekee ndiye Mwana wa Mungu, yaani, Mungu ana mwana mmoja tu, na kwamba yeyote anayekuja baada yake akiwa na jina jingine hawezi kuwa Mwana pekee wa Mungu, wala Mungu Mwenyewe. Mwanadamu ana fikira kwamba Yule ambaye anajitoa sadaka kwa ajili ya dhambi au yule ambaye anachukua mamlaka kwa ajili ya Mungu na anayewakomboa wanadamu wote ni Mwana wa Mungu tu. Kuna baadhi ambao wanaamini kwamba ili mradi Yeye ni mwanamume ambaye anakuja, Anaweza kuchukuliwa kuwa ni Mwana wa Mungu wa pekee na mwakilishi wa Mungu. Na hata kuna wale wanaosema kwamba Yesu ni Mwana wa Yehova, Mwanaye wa pekee. Je, hii siyo fikira tu ya mwanadamu? Ikiwa hatua hii ya kazi haingefanywa katika enzi ya mwisho, basi wanadamu wote wangekuwa wamegubikwa katika kivuli suala la Mungu linapohusika. Ikiwa ni hivyo, mwanamume angejidhania kuwa ni mwenye hadhi ya juu kuliko mwanamke, na wanawake hawangeweza kuwa na uwezo wa kuinua vichwa vyao juu. Katika wakati kama huo, hakuna mwanamke angeweza kupokea wokovu. Watu siku zote wanaamini kwamba Mungu ni mwanamume, na siku zote Anawachukia wanawake na asingeweza kumpa mwanamke wokovu. Ikiwa ni hivyo, basi si kweli kwamba wanawake wote walioumbwa na Yehova na pia waovu wasingeweza kuwa na fursa ya kuokolewa? Je, ingekuwa na maana gani Yehova kumuumba mwanamke, yaani, kumuumba Hawa? Na je, mwanamke asingeangamia milele? Kwa hiyo, hatua hii ya kazi katika siku za mwisho ni kuwaokoa wanadamu wote, sio mwanamke tu bali wanadamu wote. Kazi hii ni kwa ajili ya wanadamu wote, na sio tu kwa ajili ya mwanamke. Ikiwa kuna watu wanaofikiria vinginevyo, basi ni wapumbavu kabisa!
Kazi inayofanywa kwa sasa imesukuma mbele kazi ya Enzi ya Neema; yaani, kazi katika mpango mzima wa usimamizi wa miaka elfu sita imesonga mbele. Ingawa Enzi ya Neema imekoma, kazi ya Mungu imeendelea sana. Kwa nini Ninazungumza mara kwa mara kwamba hatua hii ya kazi inajenga juu ya Enzi ya Neema na Enzi ya Sheria? Hii ina maana kwamba kazi ya wakati huu ni mwendelezo wa kazi iliyofanyika katika Enzi ya Neema na kuinua kazi ile iliyofanyika katika Enzi ya Sheria. Hatua hizi tatu zinaingiliana kwa karibu na kuunganika moja kwa inayofuata. Kwa nini pia Ninasema kwamba hatua hii ya kazi inajenga juu ya kile kilichofanywa na Yesu? Tuseme kwamba hatua hii haingeongezea juu ya kazi iliyofanywa na Yesu, ingebidi Asulubiwe tena katika hatua hii, na kazi ya ukombozi ya hatua iliyopita ingelazimika kufanywa upya tena. Hii isingekuwa na maana yoyote. Kwa hiyo, sio kwamba kazi imekamilika kabisa, bali ni kwamba enzi imesonga mbele, na kazi imekuwa ya juu kabisa kuliko ilivyokuwa kabla. Inaweza kusemwa kwamba hatua hii ya kazi imejengwa juu ya msingi wa Enzi ya Sheria na katika mwamba wa kazi ya Yesu. Kazi hii imejengwa hatua kwa hatua, na hatua hii sio mwanzo mpya. Ni muungano tu wa hatua tatu za kazi ndio unaweza kuchukuliwa kuwa mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita. Hatua hii inafanywa katika msingi wa kazi ya Enzi ya Neema. Ikiwa hatua hizi mbili za kazi hazihusiani, kwa nini hakuna msalaba katika hatua hii? Kwa nini Sibebi dhambi za wanadamu? Siji kupitia kuzaliwa kwa njia ya Roho Mtakatifu na wala Sitosulubiwa ili kubeba dhambi za wanadamu; badala yake, Nipo hapa moja kwa moja kumwadibu mwanadamu. Ikiwa Mimi kumwadibu mwanadamu na kuja Kwangu si kwa njia ya Roho Mtakatifu na hakukufuata usulubisho, basi Nisingekuwa na sifa zinazostahili kumwadibu mwanadamu. Ni hasa kwa sababu Mimi ni mmoja na Yesu ndiyo Nimekuja moja kwa moja kumwadibu na kumhukumu mwanadamu. Hatua hii ya kazi inajenga kwa ujumla juu ya hatua iliyotangulia. Hii ndiyo maana ni kazi kama hiyo tu inaweza ikamletea mwanadamu wokovu hatua kwa hatua. Yesu pamoja na Mimi tunatoka katika Roho Mmoja. Ingawa miili Yetu haina uhusiano, Roho Zetu ni moja; ingawa kile Tunachofanya na kazi Tulizonazo hazifanani, kwa asili Tunafanana; miili Yetu ina maumbo tofauti, na hii ni kwa sababu ya mabadiliko ya enzi na mahitaji ya kazi Yetu; huduma Zetu hazifanani, hivyo kazi Tunayoileta na tabia Tunayoifichua kwa mwanadamu pia ni tofauti. Ndio maana kile ambacho mwanadamu anakiona na kukipokea leo hii si kama kile cha wakati uliopita; hii ni kwa sababu ya mabadiliko ya enzi. Ingawa jinsia na maumbo ya miili Yao ni tofauti, na ingawa hawakuzaliwa kutoka katika familia moja, achilia mbali katika kipindi kimoja, Roho Zao ni moja. Ingawa miili Yao haina uhusiano wa damu au kimwili kwa namna yoyote ile, hii haipingi kwamba Wao ni Mungu kupata mwili katika vipindi viwili tofauti vya nyakati. Ni ukweli usiopingika kwamba Wao ni Mungu katika miili, ingawa hawatoki katika ukoo mmoja au hawatumii lugha moja ya binadamu (mmoja alikuwa mwanamume aliyezungumza lugha ya Kiyahudi na mwingine ni mwanamke anayezungumza Kichina pekee). Ni kwa sababu hizi ndiyo maana Wameishi katika nchi tofauti kufanya kazi ambayo inampasa kila mmoja kufanya, na katika nyakati tofauti vilevile. Licha ya ukweli kwamba ni Roho moja, wakiwa na asili inayofanana, hakuna mfanano wa wazi kabisa kati ya ngozi ya nje ya miili Yao. Wanashiriki tu ubinadamu sawa, lakini umbo na kuzaliwa kwa miili Yao hakufanani. Haya hayana athari katika kazi Zao au maarifa aliyonayo mwanadamu juu yao, maana, hata hivyo, ni Roho moja na hakuna anayeweza kuwatenganisha. Ingawa Hawana uhusiano wa damu, nafsi zao zinaongozwa na Roho Zao, ili kwamba waweze kufanya kazi tofauti katika nyakati tofauti, wakiwa na miili Yao isiyokuwa na undugu wa damu. Kwa namna ile ile, Roho wa Yehova sio baba wa Roho ya Yesu na Roho wa Yesu sio mwana wa Roho wa Yehova. Ni wa Roho moja. Kama tu Mungu katika mwili wa leo na Yesu. Ingawa Hawahusiani kwa damu, ni Wamoja; hii ni kwa sababu Roho Zao ni moja. Anaweza kufanya kazi ya rehema na wema, vilevile na ile kazi ya hukumu ya haki na kumwadibu mwanadamu, na ile ya kuleta laana kwa mwanadamu. Hatimaye, Anaweza kufanya kazi ya kuuharibu ulimwengu na kuwaadhibu waovu. Je, hafanyi haya yote Mwenyewe? Je, huu si ukuu wa Mungu? Angeweza kutangaza sheria kwa ajili ya mwanadamu na kutoa amri, na angeweza pia kuwaongoza Waisraeli wa awali katika maisha yao duniani na kuwaongoza kujenga hekalu na madhabahu, kutawala Israeli yote. Kwa sababu ya mamlaka Yake, Aliishi pamoja nao duniani kwa miaka elfu mbili. Waisraeli hawakuthubutu kuasi; wote walimheshimu sana Yehova na walifuata amri Zake. Kazi hii ilifanywa kwa sababu ya mamlaka Yake na ukuu Wake. Katika Enzi ya Neema, Yesu alikuja kuwakomboa wanadamu wote walioanguka (sio Waisraeli pekee). Alionyesha rehema na wema kwa mwanadamu. Yesu ambaye mwanadamu alimwona katika Enzi ya Neema Alikuwa amejazwa na wema na siku zote Alikuwa mwenye upendo, maana Alikuja kumkomboa mwanadamu kutoka dhambini. Angeweza kuwasamehe wanadamu dhambi zao hadi pale ambapo msalaba Wake ungeweza kumkomboa mwanadamu kutoka dhambini. Wakati huo, Mungu alionekana kwa mwanadamu katika rehema na wema; yaani, Alijitoa sadaka kwa ajili ya mwanadamu na Alisulubiwa kwa ajili ya dhambi za mwanadamu ili kwamba waweze kusamehewa milele. Alikuwa mwenye rehema, mwenye huruma, mwenye upendo na mstahimilivu. Na wale wote waliomfuata Yesu katika Enzi ya Neema nao pia walionekana kuwa wastahimilivu na wenye upendo katika mambo yote. Walistahimili mateso yote, na hawakuweza kulipiza kisasi hata walipopigwa, kulaaniwa au kupigwa mawe. Lakini haipo hivyo tena katika hatua hii ya mwisho, kama vile kazi ya Yesu na Yehova hazikufanana ingawa Roho Zao zilikuwa moja. Kazi ya Yehova haikuwa kwa ajili ya kukamilisha enzi bali kuiongoza na kuipeleka katika maisha ya mwanadamu duniani. Hata hivyo, kazi sasa ni kuwashinda wale wanadamu walioharibiwa sana katika nchi za Wamataifa na kuongoza sio tu familia ya China bali ulimwengu mzima. Unaona kazi hii ikifanywa sasa China pekee, lakini kwa kweli imekwishaanza kusambaa katika nchi za ughaibuni. Ni kwa nini wageni mara kwa mara wanatafuta njia ya kweli? Hiyo ni kwa sababu Roho tayari amekwishaanza kazi Yake, na maneno sasa yameelekezwa kwa watu wa ulimwengu mzima. Hii tayari ni nusu ya kazi. Roho wa Mungu amefanya kazi kubwa hiyo tangu dunia ilipoumbwa; Amefanya kazi tofauti katika enzi tofautitofauti, na katika mataifa tofauti. Watu wa kila enzi wanaiona tabia Yake tofauti, ambayo kwa asili inafichuliwa kupitia kazi tofauti Anazozifanya. Yeye ni Mungu, mwingi wa rehema na wema; Yeye ni sadaka ya dhambi kwa ajili ya mwanadamu na mchungaji wa mwanadamu, pia Yeye ni hukumu, kuadibu, na laana kwa mwanadamu. Angeweza kumwongoza mwanadamu kuishi duniani kwa miaka elfu mbili na pia kumwokoa mwanadamu aliyepotoka. Na siku hii, pia Anaweza kumshinda mwanadamu ambaye hamjui na kumfanya awe chini ya utawala Wake, ili kwamba wote wajinyenyekeze kwake kikamilifu. Mwishoni, Atachoma yote ambayo si safi na ambayo si ya haki ndani ya wanadamu katika ulimwengu mzima, kuwaonyesha kwamba Yeye si Mungu wa Rehema, wema, hekima, maajabu na utakatifu pekee, bali pia ni Mungu anayemhukumu mwanadamu. Kwa waovu miongoni mwa wanadamu wote, Yeye ni moto, hukumu na adhabu; kwa wale ambao wanapaswa kukamilishwa, Yeye ni mateso, usafishaji, na majaribu, vilevile faraja, ustahimilivu, kutoa maneno, kushughulika na kupogoa. Na kwa wale ambao wameondolewa, Yeye ni adhabu, vilevile mapatilizo. Niambie, je, Mungu si Mkuu? Anaweza kufanya kazi yote, sio tu kazi ya msalaba kama ulivyokuwa ukifikiri. Unamfikiria Mungu kuwa ni wa chini sana! Je, unaamini kwamba kila kitu kingefikia kikomo baada ya wokovu wa mwanadamu kupitia msalaba Wake? Na hivyo, kufuatia hii, ungeweza kumfuata mbinguni na kisha kula matunda kutoka katika mti wa uzima na kunywa kutoka katika mto wa uzima? ... Je, inaweza kuwa rahisi hivyo? Niambie, umekamilisha nini? Je, una maisha ya Yesu? Ni kweli umekombolewa Naye, lakini msalaba ulikuwa ni kazi ya Yesu Mwenyewe. Ni wajibu gani umeukamilisha kama mwanadamu? Una utauwa wa nje lakini huielewi njia Yake. Hivyo ndivyo unavyomdhihirisha? Ikiwa hujapokea maisha ya Mungu au kuona ujumla wa tabia Yake ya haki, basi huwezi kudai kuwa mmoja wa wale wenye maisha, na hufai kupitia katika lango la ufalme wa mbinguni.
Sio tu kwamba Mungu ni Roho bali Anaweza pia kuwa mwili; aidha, ni mwili wa utukufu. Yesu, ingawa hamjamwona, alishuhudiwa na Waisraeli, yaani, Wayahudi wa wakati huo. Mwanzoni alikuwa mwili, lakini baada ya kusulubiwa, alikuwa mwili wa utukufu. Yeye ni Roho anayezunguka mambo yote na Anaweza kufanya kazi katika maeneo yote. Anaweza kuwa Yehova, Yesu na Masihi; hatimaye, Anaweza kuwa Mwenyezi Mungu. Yeye ni haki, hukumu, na kuadibu, ni laana na ghadhabu, lakini pia mwenye rehema na wema. Kazi zote zinazofanywa Naye zinaweza kumwakilisha. Unasema Yeye ni Mungu ni wa namna gani? Wala huwezi kuelezea na unaweza kusema tu, "Siwezi elezea Mungu ni wa namna gani." Usihitimishe kwamba Mungu milele ni Mungu wa rehema na wema, kwa sababu tu Mungu alifanya kazi ya ukombozi katika hatua moja. Je, unaweza kuwa na uhakika kwamba Yeye ni Mungu wa namna hiyo tu? Ikiwa Yeye ni Mungu wa rehema na mwenye upendo, kwa nini Ataikomesha enzi hii katika siku za mwisho? Kwa nini Ataleta chini majanga mengi? Ikiwa ni kama unavyofikiri, kwamba Yeye ni Mungu wa rehema na mwema kwa mwanadamu hadi mwisho, hata hadi katika hatua ya mwisho, sasa kwa nini atatuma chini majanga kutoka mbinguni? Ikiwa Anampenda mwanadamu kama Yeye Mwenyewe na kama Anavyompenda Mwanawe wa pekee, kwa nini Atatuma chini mapigo na mvua ya mawe kutoka mbinguni? Kwa nini Anaruhusu mwanadamu kuteseka na njaa na ndwele ya kufisha? Kwa nini anaruhusu mwanadamu kuteseka na majanga haya? Hakuna mmoja wenu anayethubutu kusema Yeye ni Mungu wa namna gani, na hakuna anayeweza kuelezea. Je, unaweza kuwa na uhakika kwamba Yeye ni Roho? Je, unathubutu kusema kuwa Yeye ni mwili wa Yesu? Na unathubutu kusema kuwa Yeye ni Mungu ambaye milele atasulubiwa kwa ajili ya mwanadamu?
kutoka kwa "Neno Laonekana katika Mwili"
Masomo yanayohusiana: Neno la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni