Neno la Mwenyezi Mungu | Mamlaka ya Mungu (II)
Leo tutaendelea na ushirika wetu kuhusu mada ya “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee.” Tayari tumekuwa na ushirika mara mbili katika mada hii, wa kwanza kuhusiana na mamlaka ya Mungu na wa pili kuhusiana na tabia ya haki ya Mungu. Baada ya kusikiliza ushirika huu mara mbili, je, umepata ufahamu mpya wa utambulisho wa Mungu, hadhi, na hali halisi? Je, maono haya yamekusaidia kufikia maarifa mazito zaidi na uhakika wa ukweli kuuhusu uwepo wa Mungu? Leo Ninapanga kufafanua mada hii ya “Mamlaka ya Mungu.”Kuelewa Mamlaka ya Mungu Kutoka kwa Mitazamo Mikubwa na Midogo
Mamlaka ya Mungu ni ya kipekee. Ndiyo maonyesho ya sifa ya, na hali halisi maalum ya, utambulisho wa Mungu Mwenyewe. Hakuna kiumbe ambacho kiliumbwa wala kile ambacho hakikuumbwa kinachomiliki maonyesho ya sifa kama hizi na hali halisi maalum; Muumba tu ndiye anayemiliki aina hii ya mamlaka. Hivyo ni kusema kwamba, ni Muumba tu—Mungu Yule wa Kipekee—ambaye anaonyeshwa kwa njia hii na ndiye aliye na hali halisi hii. Kwa nini tuzungumzie mamlaka ya Mungu? Mamlaka ya Mungu Mwenyewe yanatofautiana vipi na mamlaka yaliyomo kwenye akili ya binadamu? Ni nini maalum sana kuyahusu? Na kunao umuhimu gani haswa kuyazungumzia hapa? Kila mmoja wenu lazima aweze kutilia maanani kwa umakinifu suala hili. Kwa watu wengi zaidi, “Mamlaka ya Mungu” ni fikira isiyoeleweka, ile ambayo ni ngumu sana kupata kuielewa, na mazungumzo yoyote kuihusu huenda yasizae matunda mazuri. Kwa hivyo lazima kutakuwepo na pengo kati ya maarifa ya mamlaka ya Mungu ambayo binadamu anaweza kumiliki, na hali halisi ya mamlaka ya Mungu. Ili kuliziba pengo hili, mtu lazima kwa utaratibu aweze kuelewa mamlaka ya Mungu kwa njia ya watu halisi-maishani, matukio, vitu au mambo muhimu yanayopatikana katika uwezo wa binadamu, na ambayo binadamu wanaweza kuyaelewa. Ingawaje kauli hii “Mamlaka ya Mungu” inaweza kuonekana kama isiyoeleweka, mamlaka ya Mungu kwa kweli si ya dhahania kamwe. Yeye yupo na binadamu kila dakika ya maisha yake, akimwongoza kila siku. Kwa hivyo, katika maisha ya kila siku ya kila mtu ataweza haswa kuona na kupitia dhana halisi ya mamlaka ya Mungu. Uhalisi huu ni ithibati tosha kwamba mamlaka ya Mungu kwa kweli yapo, na unakuruhusu kabisa kutambua na kuelewa hoja hii kwamba Mungu anamiliki mamlaka haya.Mungu aliumba kila kitu, na baada ya kukiumba, Anao utawala juu ya kila kitu. Kuongezea kuwa na utawala juu ya kila kitu, pia anadhibiti kila kitu. Wazo hili linamaanisha nini “Mungu anadhibiti kila kitu”? Hali hii inaweza kuelezewa vipi? Hali hii inatumika vipi katika maisha halisi? Unawezaje kuyajua mamlaka ya Mungu kwa kuelewa hoja hii kwamba “Mungu Anadhibiti kila kitu”? Kutoka kwenye kauli ile ile “Mungu anadhibiti kila kitu” tunafaa kuona kwamba kile ambacho Mungu anadhibiti si sehemu ya sayari, sehemu ya uumbaji, wala sehemu ya mwanadamu, lakini kila kitu: kuanzia kwa viumbe vile vikubwa hadi vile vidogovidogo, kuanzia kwa vile vinavyoonekana hadi visivyoonekana, kuanzia kwa nyota ulimwenguni hadi kwenye vitu vilivyo na uhai ulimwenguni, pamoja na viumbe vidogovidogo visivyoweza kuonekana kwa macho ya kawaida au viumbe vilivyo katika maumbo mengine. Huu ndio ufafanuzi hakika wa “kila kitu” ambacho Mungu “anadhibiti,” na ndio upana ambao Mungu anaonyesha ukuu Wake, urefu wa utawala na kanuni Yake.
Kabla ya ubinadamu huu kujitokeza, viumbe vyote—sayari zote, nyota zote kule mbinguni—tayari vilikuwepo. Kwenye kiwango cha vitu vikubwa, vyombo hivi vya mbinguni vimekuwa vikizunguka mara kwa mara chini ya udhibiti wa Mungu, kwa uwepo wavyo wote, hata hivyo miaka mingi imepita. Ni sayari gani inaenda wapi na wakati gani haswa; ni sayari gani inafanya kazi gani, na lini; ni sayari gani inazunguka katika mzingo gani, na ni lini inatoweka au inabadilishwa—vitu hivi vyote vinasonga mbele bila ya kosa lolote dogo. Nafasi za sayari na umbali kati yazo ni masuala yanayofuata ruwaza maalum, ni masuala ambayo yanaweza kufafanuliwa kwa data yenye uhakika; njia ambazo zinasafiria, kasi na ruwaza ya mizingo yao, nyakati ambapo zinapatikana kwenye nafasi mbalimbali zinaweza kufafanuliwa kwa hakika na kufafanuliwa kwa sheria maalum. Kwa miaka na mikaka sayari zimefuata sheria hizi na hazijawahi kupotoka hata chembe. Hakuna nguvu inaweza kubadilisha au kutatiza mizingo yazo au ruwaza zao ambazo zinafuata. Kwa sababu sheria maalum zinazotawala mzunguko wazo na data yenye uhakika inayozifafanua iliamuliwa kabla na mamlaka ya Muumba, zinatii sheria hizi zenyewe, kulingana na ukuu na udhibiti wa Muumba. Kwenye kiwango cha mambo makubwamakubwa, si vigumu kwa binadamu kujua zaidi kuhusu ruwaza fulani, data fulani, pamoja na sheria au matukio fulani yasiyoeleweka au yasiyoelezeka. Ingawaje ubinadamu haukubali kwamba Mungu yupo, haukubali hoja kwamba Muumba aliumba na anatawala kila kitu na zaidi ya yote hautambui uwepo wa mamlaka ya Muumba, wanasayansi wa kibinadamu, wanafalaki, nao wanafizikia wanachunguza na kugundua zaidi na zaidi kwamba uwepo wa kila kitu kwenye ulimwengu, na kanuni na ruwaza zinazoonyesha mzunguko wavyo, vinatawaliwa na kudhibitiwa na nishati nyeusi kubwa na isiyoonekana. Hoja hii inampa binadamu mshawasha wa kukubaliana na kutambua kwamba kunaye Mwenyezi aliye miongoni mwa ruwaza hizi za mzunguko, anayepangilia kila kitu. Nguvu zake si za kawaida, na ingawaje hakuna anayeweza kuona uso Wake wa kweli, Yeye hutawala na kudhibiti kila kitu kila dakika. Hakuna binadamu au nguvu zozote zile zinazoweza kuuzidi ukuu Wake. Huku binadamu akiwa amekabiliwa na hoja hii, lazima atambue kwamba sheria zinazotawala uwepo wa kila kitu haziwezi kudhibitiwa na binadamu, haziwezi kubadilishwa na yeyote; na wakati uo huo binadamu lazima akubali kwamba, binadamu hawezi kuelewa kikamilifu sheria hizi. Na hizi sheria hazitokei-kimaumbile lakini zinaamrishwa na Bwana na Mungu. Haya yote ni maonyesho na mamlaka ya Mungu yanayoonyesha kwamba mwanadamu anaweza kuelewa katika kiwango cha mambo makubwa.
Kwenye kiwango cha mambo madogomadogo, milima, mito, maziwa, bahari, na maeneo ya ardhi yote ambayo binadamu anatazama nchini, misimu yote ambayo yeye anapitia, mambo yote yanayopatikana kwenye ulimwengu, kukiwemo mimea, wanyama, vijiumbe na binadamu, vyote viko chini ya ukuu wa Mungu na vinadhibitiwa na Mungu Mwenyewe. Katika ukuu na udhibiti wa Mungu, vitu vyote vinakuwepo au vinatoweka kulingana na fikira Zake, maisha ya vitu hivi yanatawaliwa na sheria fulani, na vinakua na kuzaana kulingana nazo. Hakuna binadamu au kiumbe chochote kilicho juu ya sheria hizi. Kwa nini hali iko hivi? Jibu la pekee tu ni, kwa sababu ya mamlaka ya Mungu. Au, nikijibu kwa njia nyingine, kwa sababu ya fikira za Mungu na matamshi ya Mungu; kwa sababu Mungu Mwenyewe hufanya haya yote. Hivi ni kusema, ni mamlaka ya Mungu na ni akili ya Mungu ambayo iliunda sheria hizi; zitasonga na kubadilika kulingana na fikira Zake, na kusonga huku na mabadiliko haya yote yanafanyika au kutoweka kwa minajili ya mpango Wake. Hebu tuchukulie magonjwa ya mlipuko, kwa mfano. Yanazuka tu bila onyo, hakuna anayejua asili yake, au sababu maalum zinazoelezea ni kwa nini huwa yanafanyika, na kila wakati magonjwa ya mlipuko yanapofika mahali fulani, wale walio na bahati mbaya hawawezi kukwepa maafa. Sayansi ya binadamu inafafanua na kutuelewesha kwamba magonjwa ya mlipuko yanasababishwa na kuenea kwa vijiumbe maradhi vibaya au haribifu, na kasi yao, eneo lao, na mbinu ya kuenea kwake haiwezi kutabiriwa au kudhibitiwa na sayansi ya binadamu. Ingawaje ubinadamu huvipinga vijiumbe maradhi hivi kwa kila namna inayowezekana, huwa hauwezi kudhibiti ni watu gani au wanyama gani ambao wanaathiriwa kwa vyovyote vile wakati kunapokuwa na mkurupuko wa magonjwa mlipuko. Kitu cha pekee ambacho binadamu wanaweza kufanya ni kujaribu kuyazuia, kuyapinga, na kuyafanyia utafiti. Lakini hakuna anayejua chanzo asilia kinachoelezea mwanzo au mwisho wa magonjwa mlipuko yoyote ya kibinafsi, na hakuna anayeweza kuyadhibiti. Wakiwa wamekabiliwa na ongezeko na kuenea kwa magonjwa mlipuko, suala la kwanza ambalo binadamu hufanya ni kuunda chanjo, lakini mara nyingi magojwa mlipuko hayo hutoweka kabisa kabla ya hata chanjo kuwa tayari. Kwa nini magonjwa mlipuko hutoweka kabisa? Wengine husema kwamba viini vimeweza kudhibitiwa, wengine husema kwamba vimetoweka kabisa kwa sababu ya mabadiliko katika misimu…. Kuhusiana na ikiwa makisio haya ya kuchanganyikiwa ni kweli au la, sayansi haiwezi kutupa ufafanuzi wowote, na wala haitoi jibu lolote lenye uhakika. Kile ambacho ubinadamu unakabiliwa nacho si makisio haya tu lakini pia ukosefu wa mwanadamu katika kuelewa na woga wa magonjwa mlipuko haya. Hakuna anayejua, baada ya kila kitu kuchambuliwa, ni kwa nini magonjwa mlipuko haya huanza au ni kwa nini huisha. Kwa sababu ubinadamu unao imani tu katika sayansi, unategemea pakubwa kwa sayansi hiyo, lakini hautambui mamlaka ya Muumba au kuukubali ukuu Wake, hautawahi kuwa na jibu.
Katika ukuu wa Mungu, mambo yote yapo na huangamia kwa sababu ya mamlaka Yake, kwa sababu ya usimamizi Wake. Baadhi ya mambo huja na kwenda polepole, na binadamu hawezi kutambua ni wapi yalitokea au kung’amua sheria ambazo mambo haya hufuata, sisemi hata kuelewa sababu za mambo haya kuja na kwenda. Ingawaje binadamu anaweza kushuhudia, kusikia, au kupitia yote yanayokuja na kuisha miongoni mwa mambo yote; ingawaje mambo haya yanao mwelekeo kwa binadamu, na ingawaje binadamu hung'amua kupitia kwa yaliyofichika akilini mwake, hali isiyokuwa ya kawaida, hali ya mara kwa mara au hata hali ya ajabu ya mambo mbalimbali, bado hajui chochote kuhusu mapenzi ya Muumba na akili Yake ambavyo vinaelezea mambo hayo. Kunazo hadithi nyingi zinazotokana na haya mambo yote, ukweli mwingi uliofichwa. Kwa sababu binadamu amepotoka na kwenda mbali na Muumba, kwa sababu hakubali hoja hii kwamba Mamlaka ya Muumba ndiyo hutawala mambo yote, hatawahi kujua kila kitu kinachofanyika katika ukuu Wake. Kwa sehemu nyingi zaidi, udhibiti na ukuu wa Mungu huzidi mipaka ya fikra ya binadamu, maarifa ya binadamu, kuelewa kwa binadamu, kuhusu kile ambacho sayansi ya binadamu inaweza kutimiza; uwezo wa ubinadamu ulioundwa hauwezi kushindana nao. Baadhi ya watu husema “Kwa sababu hujashuhudia ukuu wa Mungu wewe mwenyewe, unawezaje kusadiki kwamba kila kitu kinatokana na mamlaka Yake?” Kuona si kuamini kila mara; kuona si kutambua na kuelewa kila mara. Kwa hivyo “sadiki” hutokea wapi? Ninaweza kusema kwa uhakika, “Sadiki inatokana na kiwango na kina cha kuelewa kwa watu kwa, na hali wanayopitia wao, uhalisi na chanzo kikuu cha mambo.” Kama unasadiki kwamba Mungu yupo, lakini huwezi kutambua, na wala huwezi kuelewa, hoja ya udhibiti wa Mungu na ukuu wa Mungu katika mambo yote, basi katika moyo wako hutawahi kukubali kwamba Mungu anayo mamlaka kama haya na kwamba mamlaka ya Mungu ni ya kipekee. Hutawahi kukubali kwa kweli Muumba kuwa Bwana wako, Mungu wako.
Hatima ya Binadamu na Hatima ya Ulimwengu Haviwezi Kutenganishwa na Ukuu wa Muumba
Nyinyi nyote ni watu wazima. Baadhi yenu ni wa umri wa kati; baadhi mmefikisha umri wa uzee. Kutoka kwa yule asiyesadiki hadi kwa yule anayesadiki, na kuanzia mwanzo wa kusadiki kwa Mungu hadi kukubali neno la Mungu na kuweza kupitia kazi ya Mungu, je, ni maarifa kiwango kipi uliyopata kuuhusu ukuu wa Mungu? Ni maono yapi uliyopata kwenye hatima yako ya kuwa binadamu? Je, mtu anaweza kutimiza kila kitu anachotamani katika maisha? Je, ni mambo mangapi kwenye miongo michache iliyopita katika kuwepo kwako uliyoweza kutimiza kama ulivyopenda? Ni mambo mangapi hayafanyiki kama yalivyotarajiwa? Ni mambo mangapi hutupata kwa mshangao mzuri? Ni mambo mangapi ambayo ungali unasubiri kutimia—unasubiri bila kufahamu muda sahihi, unasubiria mapenzi ya Mbinguni? Mambo mangapi yanakufanya uhisi kana kwamba huna wa kukusaidia na umezuiliwa? Watu wote wanayo matumaini kuhusu hatima yao, na hutarajia kwamba kila kitu katika maisha yao kitaenda sawa na wanavyopenda, kwamba hawatakosa chakula wala mavazi, kwamba utajiri wao utaongezeka pakubwa. Hakuna anayetaka maisha ya kimaskini na ya taabu, yaliyojaa ugumu, na kuandamwa na majanga. Lakini watu hawawezi kuona mbele au kudhibiti mambo haya. Pengine kwa baadhi ya watu, yaliyopita ni mchanganyiko tu wa yale mambo waliyoyapitia; hawajifunzi katu ni nini mapenzi ya Mbinguni, wala hawajali mapenzi hayo ni yapi. Wanaishi kwa kudhihirisha maisha yao bila kufikiria, kama wanyama, wakiishi siku baada ya siku, bila kujali kuhusu hatima ya binadamu ni nini, kuhusu ni kwa nini binadamu wako hai au vile wanavyostahili kuishi. Watu hawa hufikia umri wa uzee bila ya kufaidi ufahamu wowote wa hatima ya binadamu, na mpaka wakati ule wanapokufa hawana habari yoyote kuhusu maana ya maisha. Watu kama hao wamekufa; ni viumbe bila roho; wao ni wanyama. Ingawaje katika kuishi miongoni mwa mambo haya yote, watu hupata furaha kutoka kwa njia nyingi ambazo ulimwengu hutosheleza mahitaji yao ya anasa, ingawaje wanauona ulimwengu huu wa anasa ukiwa unapiga hatua bila kusita, hali yao binafsi waliyoipitia—kile ambacho mioyo yao na roho zao zinahisi na kupitia—hakina uhusiano wowote na mambo ya anasa, na hakuna kitu chochote cha anasa ambacho kinaweza kuchukua nafasi yake. Ni utambuzi ndani ya moyo wa mtu, kitu ambacho hakiwezi kuonekana kwa jicho vivyo hivyo tu. Utambuzi huu umo katika ufahamu wa mtu wa, na hisia za mtu za, maisha ya binadamu na hatima ya binadamu. Na mara nyingi humwongoza mtu katika kuelewa kwamba Bwana yule asiyeonekana anapanga vitu vyote, Anaunda kila kitu kwa ajili ya binadamu. Katikati ya haya yote, mtu hawezi kuepuka ila kukubali mipangilio na mipango ya hatima ya mambo; wakati uo huo, mtu hawezi kuepuka ila kukubali njia iliyo mbele ambayo Muumba amempangia, ukuu wa Muumba dhidi ya hatima ya mtu. Hii ndiyo hoja isiyopingika. Haijalishi ni maono na mtazamo gani ambao mtu anao kuhusu hatima yake, hakuna anayeweza kubadilisha hoja hii.Pale utakapoenda kila siku, kile utakachofanya, yule au kile utakachokumbana nacho, kile utakachosema, kile kitakachokufanyikia—je, kati ya vyote hivi kipo kinachoweza kutabirika? Watu hawawezi kutabiri matukio haya yote, sikutajii kudhibiti namna ambavyo yanavyoendelea. Katika maisha, matukio haya yasiyotabirika hufanyika kila wakati, na ni tukio la kila siku. Mabadiliko haya ya kila siku na njia ambazo yanajitokeza, au ruwaza ambazo yanajitokeza, ni vikumbusho vya kila wakati kwa ubinadamu kwamba hakuna kinachofanyika bila mpango, kwamba matukio ya mambo haya, na kutoepukika kwa mambo haya, haviwezi kubadilishwa na mapenzi ya binadamu. Kila tukio linaonyesha onyo kutoka kwa Muumba kwa mwanadamu, na pia linatuma ujumbe kwamba, binadamu hawawezi kudhibiti hatima zao wenyewe; na wakati uo huo kila tukio ni upingaji wa malengo yasiyo na mwelekeo, yasiyo na maana ya ubinadamu na tamanio la kuchukua hatima yake na kutaka kuidhibiti mwenyewe. Ni sawa na makofi yenye nguvu juu ya masikio ya binadamu moja baada ya jingine, yanayolazimisha binadamu kufikiria upya ni nani, hatimaye, atatawala na kudhibiti hatima yao. Na kama vile malengo na matamanio yao yanavyokiukwa mara kwa mara na kusambaratika, binadamu kwa kawaida huishia kukubali kwa nadharia yao bila kufahamu kile ambacho hatima yao imesheheni, kukubali kwa uhalisi, kwa mapenzi ya Mbinguni na ukuu wa Muumba. Kutokana na mabadiliko haya ya kila siku katika hatima za maisha yote ya binadamu, hakuna kitu ambacho hakifichui mipango ya Muumba na ukuu Wake; hakuna kile ambacho hakiutumi ujumbe huu kwamba “yale mamlaka ya Muumba hayawezi kupitwa,” ambacho hakionyeshi ukweli wa milele kwamba “mamlaka ya Muumba ni ya juu zaidi.”
Hatima za ubinadamu na zile za ulimwengu zimeingiliana kwa ndani na ukuu wa Muumba, zimefungamanishwa na haziwezi kutenganishwa na mipango ya Muumba; na hatimaye, haziwezi kutenganishwa na mamlaka ya Muumba. Kupitia kwenye sheria za mambo yote binadamu huja kuelewa mipango ya Muumba na ukuu Wake; kupitia kwenye sheria za namna ya kuishi ambazo anaona katika utawala wa Muumba; kutoka kwenye hatima za mambo yote anapata hitimisho kuhusu njia ambazo Muumba huonyesha ukuu Wake na kuvidhibiti; na kwenye mzunguko wa maisha ya binadamu na mambo yote ambayo binadamu kwa kweli hupitia ile mipango na mipangilio ya Muumba kwa mambo yote na kwa viumbe vyote vilivyo hai na anashuhudia kwa kweli namna ambavyo mipango na mipangilio hiyo inavyozidi sheria zote za nchi, kanuni, na taasisi, mamlaka na nguvu zote nyingine. Kwa mujibu wa haya, ubinadamu unashawishiwa kutambua kwamba, ukuu wa Muumba hauwezi kukiukwa na kiumbe chochote kilichoumbwa, kwamba hakuna nguvu zinazoweza kuharibu au kubadilisha matukio na mambo yaliyoamuliwa kabla na Muumba. Ni kupitia kwenye sheria na kanuni hizi takatifu ambapo binadamu na viumbe vyote wanaweza kuishi na kuzalisha, kizazi baada ya kizazi. Je, huu si mfano halisi wa mamlaka ya Muumba? Ingawaje binadamu huona, kwenye sheria zile za malengo, ukuu wa Muumba na utaratibu Wake wa matukio yote na mambo yote, ni watu wangapi wanaweza kung’amua kanuni ya ukuu wa Muumba juu ya ulimwengu? Ni watu wangapi wanaweza kujua, kutambua, kukubali kwa kweli na kujinyenyekeza kwa ukuu na mpangilio wa Muumba dhidi ya hatima zao wenyewe? Nani, ambaye baada ya kusadiki hoja ya ukuu wa Muumba juu ya viumbe vyote, ataweza kusadiki kwa kweli na kutambua kwamba Muumba pia anaamrisha hatima hii ya maisha ya binadamu? Ni nani anayeweza kuelewa kwa kweli hoja hii kwamba hatima ya binadamu imo kwenye kiganja cha mkono wa Muumba? Aina ya mtazamo ambao ubinadamu unafaa kuchukua katika ukuu wa Muumba, unapokabiliwa na hoja kwamba Anatawala na kudhibiti hatima ya binadamu, ni uamuzi ambao kila binadamu ambaye kwa sasa anakabiliwa na hoja hii lazima ajiamulie mwenyewe.
Awamu Sita katika Maisha ya Binadamu
Katika mkondo wa maisha ya mtu, kila mtu hufikia kwenye misururu ya awamu muhimu. Hizi ni hatua za kimsingi zaidi, na muhimu zaidi, zinazoamua hatima ya maisha ya mtu. Kile kinachofuata ni ufafanuzi mfupi kuhusu mafanikio haya ambayo kila mtu lazima apitie kwenye mkondo wa maisha yake.Kuzaliwa: Awamu ya Kwanza
Mahali ambapo mtu amezaliwa, amezaliwa katika familia ya aina gani, jinsia ya mtu, umbo la mtu, na wakati wa kuzaliwa: haya ndiyo maelezo ya awamu ya kwanza ya maisha ya binadamu.Hakuna yeyote aliye na chaguo kuhusu sehemu hizi za awamu hii; zote ziliamuliwa kabla, mapema kabisa na Muumba. Haziathiriwi na mazingira ya nje kwa vyovyote vile, na hakuna masuala yanayosababishwa na binadamu yanaweza kubadilisha hoja hizi ambazo Muumba aliamua kabla. Kwa mtu kuweza kuzaliwa inamaanisha kwamba Muumba tayari ametimiza hatua ya kwanza ya hatima ambayo Amempangilia mtu huyo. Kwa sababu Aliamua kabla maelezo haya yote tena mapema mno, hakuna aliye na nguvu za kubadilisha maelezo yoyote yale. Licha ya hatima ya baadaye ya mtu, hali za kuzaliwa kwa mtu ziliamuliwa kabla, na zinabakia kama zilivyo; haziathiriwi kwa njia yoyote ile na hatima ya mtu katika maisha, wala haziathiri kwa vyovyote vile ukuu wa Muumba juu yazo.
1. Maisha Mapya Yanazaliwa Kulingana na Mipango ya Muumba
Ni maelezo yapi ya awamu ya kwanza—mahali mtu anapozaliwa, familia ya mtu, jinsia ya mtu, umbo la mwili wa mtu, muda wa kuzaliwa kwa mtu—ambayo mtu anaweza kuchagua? Bila shaka, kuzaliwa kwa mtu ni tukio asiloweza kuchagua: Mtu anazaliwa bila hiari yake, katika mahali fulani, muda fulani, kwenye familia fulani, akiwa na umbo fulani la kimwili; mtu anakuwa mmojawapo wa familia fulani bila hiari, anarithi kizazi fulani cha familia. Mtu hana chaguo kwenye awamu hii ya kwanza ya maisha, lakini anazaliwa kwenye mazingira yanayochaguliwa kulingana na mipango ya Muumba, kwenye familia mahususi, na jinsia na umbo mahususi, kwenye wakati mahususi ambao unaunganishwa kwa undani na mkondo wa maisha ya mtu huyu. Mtu anaweza kufanya nini katika awamu hii muhimu? Yote yakisemwa, kwa kweli mtu hana chaguo kuhusu maelezo yoyote yale yanayohusu kuzaliwa kwake. Kama isingekuwa kuamua kabla kwa Muumba na mwongozo Wake, mtu aliyezaliwa upya kwenye ulimwengu huu asingejua ni wapi atakapoenda au ni wapi atakapoishi, asingekuwa na mahusiano yoyote, asingekuwa na popote na asingekuwa na maskani yoyote halisi. Lakini kwa sababu ya mipangilio makinifu ya Muumba, anaanza safari ya maisha yake akiwa na mahali pa kuishi, wazazi, na mahali anapoita nyumbani na watu wa ukoo. Kotekote kwenye mchakato huu, mwanzo wa maisha haya mapya unaamuliwa na mipango ya Muumba, na kila kitu ambacho mtu huyu atakuja kumiliki ataweza kukabidhiwa na Muumba. Kutoka kwenye kiumbe kinachoelea-kisichokuwa na jina lolote hadi kinapoanza kuwa na nyama–na–damu polepole, kinachoweza kuonekana, na hatimaye kuwa binadamu anayeweza kushikika, mojawapo ya viumbe vya Mungu, anayefikiria, anayepumua, anayehisi joto na baridi, anayeshiriki katika shughuli za kawaida za kiumbe kilichoumbwa kwenye ulimwengu yakinifu na ambaye atapitia mambo haya yote ambayo kiumbe kilichoumbwa lazima kipitie maishani. Kule Kuamuliwa kabla kwa kuzaliwa kwa mtu na Muumba kunamaanisha kwamba ataweza kumpa mtu huyu mambo yote yanayohitajika kwa kuishi kwake; na kwamba mtu anazaliwa vilevile inamaanisha kwamba yeye atapokea mambo yote yanayohitajika kutoka kwa Muumba, kwamba kuanzia wakati ule kwenda mbele yeye ataishi katika umbo jingine, linalotolewa na Muumba na linalotii ukuu wa Muumba.2. Kwa Nini Binadamu Tofauti Wanazaliwa Katika Hali Tofauti
Mara nyingi watu wanapenda kufikiria kwamba, kama wangezaliwa tena, wangezaliwa kwenye familia maarufu; kama wangekuwa wanawake, wangefanana na Binti wa Kifalme Anayependeza na wangependwa na kila mtu, na wangezaliwa wanaume, wangekuwa Kaka Mwenye Mvuto na Haiba, wasikose mahitaji yoyote, huku ulimwengu mzima ukiwaitikia mara moja kila unapoitwa na wao. Mara nyingi kuna wale walio na picha nyingi kuhusu kuzaliwa kwao na huwa hawajatosheka kabisa na huko kuzaliwa kwao, wanachukia familia zao, umbo lao, jinsia yao, na hata wakati wa kuzaliwa kwao. Ilhali watu hawajawahi kuelewa ni kwa nini wamezaliwa katika familia fulani au kwa nini wanafanana jinsi fulani. Hawajui kwamba, licha ya ni wapi wamezaliwa au ni vipi wanavyoonekana, wanafaa kuendeleza wajibu mbalimbali na kutimiza kazi maalum tofautitofauti katika usimamizi wa Muumba—kusudi hili halitawahi kubadilika. Ingawa katika macho ya Muumba, mahali anapozaliwa mtu, jinsia ya mtu, umbo la mwili wa mtu hivi vyote ni vitu vya muda. Ni misururu ya mambo madogomadogo katika kila awamu ya usimamizi Wake wa mwanadamu kwa ujumla. Na hatima halisi ya mtu na mwisho wake vyote haviamuliwi kutokana na wapi ambapo yeye amezaliwa katika awamu yoyote ile, lakini vinaamuliwa na kazi maalum ambayo yeye atatekeleza katika kila maisha, kwa hukumu ya Muumba kwao wakati ambapo usimamizi Wake wa mpango vitakamilika.Inasemekana kwamba kunayo sababu katika kila athari, na kwamba hakuna athari ambayo haina sababu. Na kwa hivyo kuzaliwa kwa mtu kumefungamanishwa haswa na maisha yake ya sasa na yale ya awali. Kama kifo cha mtu kinasitisha awamu yake ya sasa ya maisha, basi kuzaliwa kwa mtu ndio mwanzo wa mzunguko mpya; kama mzunguko wa kale unawakilisha maisha ya awali ya mtu, basi mzunguko huo mpya kwa kawaida ndio maisha yao ya sasa. Kwa sababu kuzaliwa kwa mtu kunaunganishwa na maisha ya kale ya mtu huyu pamoja na maisha ya sasa ya mtu huyu, mahali anapoishi, familia yake, jinsia, umbo na mambo mengine kama hayo, ambayo yanahusiana na kuzaliwa kwa mtu, vyote vinahusiana na mambo yote. Hii inamaanisha kwamba, mambo yanayoathiri kuzaliwa kwa mtu hayaathiriwi tu na maisha ya awali ya mtu, lakini yanaamuliwa na hatima ya mtu katika maisha ya sasa. Hii inaelezea mseto wa hali tofauti ambazo watu wanazaliwa: Baadhi wanazaliwa katika familia fukara, wengine katika familia tajiri. Baadhi wanazaliwa katika kundi la watu wa kawaida, wengine wanazaliwa katika ukoo wa kipekee. Baadhi wanazaliwa kusini, wengine wanazaliwa kaskazini. Baadhi wanazaliwa jangwani na wengine wanazaliwa katika ardhi zenye rotuba. Kuzaliwa kwa baadhi ya watu kunaandamana na vifijo, vicheko, na sherehe, wengine wanaleta machozi, janga, na matatizo. Baadhi wanazaliwa ili wathaminiwe, wengine wawekwe pembeni kama magugu. Baadhi wanazaliwa wakiwa na heshima na staha na wengine wanazaliwa wakiwa na mikosi na mikasa. Baadhi wanapendeza kuwatazama, na wengine wanatisha kuwatazama. Baadhi wanazaliwa usiku wa manane, wengine wanazaliwa chini ya jua kali la utosi. … Kuzaliwa kwa watu wa kila aina kunaamuliwa na hatima ambazo Muumba ameweka kwa ajili yao; kuzaliwa kwao kunaamua hatima zao pamoja na wajibu ambao wataendeleza na kazi maalum watakazotimiza. Yote haya yanategemea ukuu wa Muumba, ulioamuliwa kabla na Yeye; hakuna anayeweza kukimbia kundi hili lao lililoamuliwa kabla, hakuna anayeweza kubadilisha hali za[a] kuzaliwa kwao, na hakuna anayeweza kuchagua hatima yake binafsi.
Kukua: Awamu ya Pili
Kutegemea na aina gani ya familia ambayo wamezaliwa ndani, watu hukua katika mazingira tofauti ya nyumbani na wakajifunza mafunzo tofauti kutoka kwa wazazi wao. Hii huamua masharti ambayo mtu anafikisha umri wa kubaleghe na kukua[b]inawakilisha awamu ya pili muhimu ya maisha ya mtu. Inajulikana kwamba, watu hawana chaguo katika awamu hii, vilevile. Hii pia imepangwa, ilipangwa kabla.1. Hali Ambazo Mtu Hukulia Ndani Zimepangwa na Muumba
Mtu hawezi kuchagua watu au mambo ambayo yataweza kumhimiza na kumwathiri anapokua. Mtu hawezi kuchagua ni maarifa au mbinu gani atapata, ni mazoea gani ataishia kuwa nayo. Mtu hana kauli kuhusiana na wazazi na watu wake wa ukoo, aina ya mazingira ambayo atakulia ndani; mahusiano yake na watu, matukio, na mambo yaliyo katika mazingira yake na namna yanavyoathiri maendeleo yake, vyote ni zaidi ya udhibiti wake. Ni nani anayeamua mambo haya, basi? Ni nani anayeyapangilia? Kwa sababu watu hawana chaguo katika suala hili, kwa vile hawawezi kuamua mambo haya wao wenyewe, na kwa sababu bila shaka hayajipangi yenyewe kwa kawaida, ni wazi kabisa kwamba kuundwa kwa haya yote kunategemea mikono ya Muumba. Kama vile tu Muumba anavyopanga hali fulani za kuzaliwa kwa kila mtu, Yeye hupangilia pia hali mahususi ambazo mtu hukulia, bila shaka. Kama kuzaliwa kwa mtu kutaleta mabadiliko kwa watu, kwa matukio, na mambo yanayomzunguka yeye, basi kukua na maendeleo ya mtu huyo vyote vitaweza kuwaathiri vilevile. Kwa mfano, baadhi ya watu wanazaliwa katika familia fukara, lakini wanalelewa wakiwa wemezungukwa na utajiri; wengine wanazaliwa katika familia tajiri lakini husababisha utajiri wa familia zao kupungua, kiasi cha kwamba wanalelewa katika mazingira ya kimaskini. Hakuna kuzaliwa kwa yeyote kunatawaliwa na kanuni isiyobadilika, na hakuna anayelelewa katika hali zisizozuilika, na zisizobadilika. Haya si mambo ambayo binadamu anaweza kufikiria au kudhibiti; mambo haya yote ni mazao ya hatima ya mtu, na yanaamuliwa na hatima ya mtu. Bila shaka, kimsingi ni kwamba yote haya yaliamuliwa kabla katika hatima ya mtu na Muumba, yanaamuliwa na ukuu wa Muumba juu ya, na mipango Yake ya, hatima ya mtu huyu.2. Hali Mbalimbali Ambazo Watu Hukulia Ndani Husababisha Wajibu Tofauti
Hali za kuzaliwa kwa mtu huanzisha katika kiwango cha kimsingi mazingira na hali ambazo hukulia ndani, na hali ambazo mtu hukulia ndani vilevile ni zao la hali za kuzaliwa kwake. Kwenye wakati huu mtu anaanza kujifunza lugha, na akili za mtu zinaanza kukumbana na kuchanganua mambo mengi mapya, na katika mchakato huu mtu anakua bila kusita. Mambo ambayo mtu anasikia kwa masikio yake, anaona kwa macho yake, na anang’amua kwa akili zake huboresha na kuhuisha kwa utaratibu ulimwengu wa ndani wa mtu. Watu, matukio, na mambo ambayo mtu anakumbana nayo, maarifa ya kawaida, maarifa, na mbinu anazojifunza, na njia za kufikiria ambazo mtu anaathiriwa nazo, anaambiwa au kufunzwa, vyote vitamwongoza na kuathiri hatima ya maisha yake. Lugha anayojifunza mtu anapokua na njia yake ya kufikiria haviwezi kutenganishwa kutoka kwenye mazingira ambayo yeye analelewa katika ujana wake, na hayo mazingira yana wazazi, ndugu zake, na watu wengine, matukio, na mambo yanayomzunguka. Kwa hivyo mkondo wa maendeleo ya mtu unaamuliwa na mazingira ambayo yeye anakulia ndani, na pia unategemea watu, matukio, na mambo ambayo mtu anakumbana nayo kwenye kipindi hiki cha muda. Kwa sababu masharti ambayo mtu hukulia ndani yaliamuliwa kabla na tena mapema mno, mazingira anayoishi kwenye mchakato huu pia, kwa kawaida, yaliamuliwa kabla. Hayaamuliwi na chaguo na mapendeleo ya mtu, lakini yanaamuliwa kulingana na mipango ya Muumba, yanaamuliwa na mipangilio makinifu ya Muumba, na ukuu wa Muumba juu ya hatima ya mtu huyo katika maisha. Kwa hivyo watu ambao mtu yeyote hukumbana nao katika mkondo wa kukua, na mambo ambayo mtu hukutana nayo, vyote vimeunganishwa bila kuzuilika kwa mipango na mipangilio ya Muumba. Watu hawawezi kutabiri aina hizi za mahusiano mapevu, wala hawawezi kuyadhibiti au kuweza kuyaelewa. Mambo mengi tofauti na watu wengi tofauti wanao mwelekeo wa mazingira ambayo mtu hukulia, na hakuna binadamu anaweza kupangilia na kupanga mtandao mpana kama huo wa maunganisho. Hakuna mtu au kitu isipokuwa Muumba anaweza kudhibiti kujitokeza, kuwepo, na kutoweka kwa watu mbalimbali, matukio na mambo, na ni mtandao mpana ajabu wa maunganisho unaounda maendeleo ya mtu kama ilivyoamuliwa kabla na Muumba, na kuunda mazingira tofauti ambayo watu wanakulia ndani, na kuunda wajibu mbalimbali unaohitajika kwa minajili ya kazi ya Muumba ya usimamizi, kuweka misingi thabiti, yenye nguvu ili watu waweze kukamilisha kwa ufanisi kazi yao maalum.
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili
Kuhusu Sisi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni